+ All Categories
Home > Documents > Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa...

Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa...

Date post: 30-May-2019
Category:
Upload: buinhan
View: 237 times
Download: 0 times
Share this document with a friend
12
Historia ya Ukombozi Ujumbe wa Biblia katika vipindi 10 Diocese-Based Leadership Training Program Mennonite Churches of East Africa (KMC/KMT) Yameandaliwa na Joseph & Gloria Bontrager Theological Education Coordinators, 2015
Transcript
Page 1: Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala. Adamu na Hawa walivutwa na tamaa

Historia ya Ukombozi Ujumbe wa Biblia katika vipindi 10

Diocese-Based Leadership Training Program Mennonite Churches of East Africa (KMC/KMT)

Yameandaliwa na

Joseph & Gloria Bontrager Theological Education Coordinators, 2015

Page 2: Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala. Adamu na Hawa walivutwa na tamaa

Historia ya Ukombozi, uk.2

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2015 Joseph Bontrager

Yaliyomo

Utangulizi 2

1. Kuumbwa kwa dunia 3

2. Wanadamu wamwasi Mungu 4

3. Abramu – wito na agano 5

4. Mungu awaokoa Waisraeli kutoka Misri na kufanya agano nao 6

5. Waisraeli waingia nchi ya ahadi 7

6. Waisraeli wachukuliwa mateka 8

7. Waisraeli warudi katika nchi 9

8. Yesu Mkombozi 10

9. Kanisa 11

10. Yerusalemu mpya 12

Utangulizi

Biblia ni historia. Inatoa habari za Mungu alivyoumba vitu vyote na kuvibariki, na akaumba binadamu kwa mfano wake na kumbariki na walikuwa na ushirikiano mzuri. Ila binadamu alichagua kumwasi Mungu na kutegemea nguvu zake mwenyewe.

Tangu uasi wa wanadamu, Mungu alifanya mpango wa kuwakomboa na kujenga tena uhusiano nasi. Ujumbe wa Biblia ni historia ya ukombozi huo, jinsi Mungu alivyoagana na watu aliowachagua, atakuwa mfalme wao, na kupitia watu hao kuleta Mkombozi wa ulimwengu wote.

Lakini ukombozi haukumalizika kwa mara moja, Mungu alichagua kijifunua kwa hatua na kufanya ukombozi kwa hatua, kuanzia Bustani ya Edeni hadi Yerusalemu Mpya, ukombozi utakapokamilika. Alianza kujifunua katika kuumba mwanadamu kwa mfano wake, na ufunuo kamili ni Yesu Kristo.

Page 3: Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala. Adamu na Hawa walivutwa na tamaa

Historia ya Ukombozi, uk.3

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2015 Joseph Bontrager

1. Kuumbwa kwa dunia Ukamilifu; dunia ilivyokusudiwa na Mungu

Hapo mwanzoni Mungu akaumba mbingu na nchi. Alitenga bahari na nchi kavu, alifanya miti na maua, alifanya wanyama wote. Mwisho alimfanya bindamu, naye alimfanya kwa mfano wake Mungu – alimfanya awe na roho, na akili, na tabia ya upendo na ushirikiano, naye alimfanya mwanaume na mwanamke.

Halafu Mungu alitayarisha bustani na kuwaweka wanadamu ili kuitunza na kwa chakula. Katika bustani Mungu aliweka miti miwili. Mti wa uzima kwa ajili ya uhai wao, na mti wa ujuzi kwa ajili ya kupima utii na uaminifu. Mungu aliwaambia waweza kula kwa kila mti ili mti wa ujuzi wa mema na mabaya wasile. Na Mungu aliona kila kitu alichoumba akasema ni chema sana.

1. Mwanzo 1:1. Hapo mwanzo Mungu akaziumba mbingu na nchi.

Hapo mwanzo alikuwa nani? (Mungu)

Na huyo Mungu alifanya nini? (aliziumba mbingu na nchi)

2. Mwanzo 1:27. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Je, mfano wa Mungu katika mwanadamu ni nini? o Mungu hana mwili kama mwanadamu, ni roho o Utakatifu – usafi, kutengwa kwa makusudi ya Mungu tu o Nafsi hai (Mwanzo 2:7) – akili, hisi, uchaguzi, kujifahamu, ubunifu, kuwajibika o Roho (Warumi 8:16) – kumfahamu Mungu na kuhusiana naye o Upendo (1 Yohana 3:16) o Ushirikiano –si vema huyu mtu awe peke yake (Mwanzo 2:18); Mungu

alitembea na kuongea nao bustanini (Mwanzo 3:8) o Utawala, kuitiisha, kujaza nchi

Yesu ni mfano kamili wa Mungu (Wakolosai 1:15; 2:9)

3. Mwanzo 2:16-17. Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile,….

Mungu alifanyaje kumpatia mwanadamu mahitaji yake? (Mwanzo 2:9)

Mungu alitoa mwanadamu agizo gani? (Mwanzo 2:16-17))

4. Mwanzo 1:31. Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana.

Wanadamu kwa mfano wake

Mwanaume na mwanamke kusaidiana

Dunia kwa furaha na uzima ya wanadamu

Ushirikiano kati ya Mungu na wanadamu, na mwanadamu kwa mwanadamu

Kujadiliana:

1) Kwa nini ni muhimu tumtambue Mungu kama Muumbaji?

2) Mfano wa Mungu katika binadamu ni hali na tabia gani?

3) Kwa nini Mungu aliweka mti wa ujuzi wa mema na mabaya?

4) Tunda la mti huo lilikuwa tunda gani?

5) Kwa nini Mungu aliweza kupendezwa na kila kitu alichokifanya?

6) Eleza uhusiano kati ya Mungu na wanadamu hapo mwanzoni ulikuwaje?

Page 4: Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala. Adamu na Hawa walivutwa na tamaa

Historia ya Ukombozi, uk.4

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2015 Joseph Bontrager

2. Wanadamu wamwasi Mungu Kusudi ya Mungu kuvunjwa; ardhi kulaaniwa; binadamu kuteswa

Shetani aliingia katika bustani katika mwili wa nyoka akawashawishi wanadamu kula kutoka mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Aliwadanganya na kutia mashaka kuhusu agizo la Mungu kuwakataza kula kwa mti huo. Waliona tunda la mti lafaa kwa chakula, na kupendeza macho, na kuleta maarifa, na wakala.

Mara moja walitambua kwamba ni uchi, na walijificha mbele ya Mungu. Uasi wao ulileta aibu na hofu. Uasi wao ulileta laana juu ya nchi, na kusababisha uchungu katika maisha yao. Na waliondolewa katika bustani.

1. Mwanzo 3:1. Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu.

Nyoka alikuwa nani katika mwili wa nyoka?

Soma Isaya 14:12-15 na Ezekieli 28:11-17. Yanahusu mfalme maadui wa Israeli, lakini wengine wanaamini hao wafalme ni mifano wa ibilisi shetani. Je, ibilisi aliumbwa na sifa gani? Ni dhambi gani ilimsababisha kutolewa mbinguni?

Biblia inamweleza shetani kuwa na tabia gani sasa? Soma Yohana 8:44, 2 Wakorintho 11:14, Ufunuo 12:9, Ufunuo 12:10, 1 Petro 5:8.

2. Nyoka akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile…? Shetani alimdanganya mwanadamu na kutia mashaka kuhusu mambo gani? Mwanzo 3:4-5.

3. Mwanzo 3:6. Mwanamke alipona ya kuwa ule mtu wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala.

Adamu na Hawa walivutwa na tamaa za kimwili kuliko maagizo ya nani?

Wanadamu waliamini tunda la mti litawapatia faida gani?

Soma 1 Yohana 2:15-17. Kwa nini hatuwezi kupenda mambo ya dunia na kumpenda Mungu pia?

4. Mwanzo 3:8-10. Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini…, wakajificha. Kwa nini Adamu na Hawa walijificha waliposikia sauti ya Mungu?

5. Mwanzo 3:14. Bwana Mungu alimwambia nyoka, Kwa sababu umefanya hayo, umelaaniwa….

6. Mwanzo 3:16-19. Akamwambia mwanamke, Nitazidisha uchungu wako…, na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Akamwambia Adamu, …ardhi imelaaniwa kwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake….

Kujadiliana:

1) Asili ya dhambi ya wanadamu ilikuwa ni nini hasa?

2) Taja matokeo ya kumwuasi Mungu kwa nyoka (mst.14-15). Matokeo kwa mwanamke (mst.16). Kwa ardhi (mst.17). Kwa mwanaume? (mst.17-19). Je, tunaona matokeo hayo hata sasa?

3) Soma Mwanzo 3:15. Kuna ahadi gani ya ukombozi? Uzao wako ni nani?

4) Je, ukombozi wa Mungu utahusu mambo gani na vitu gani? Soma mistari kuhusu ukombozi: Waefeso 1:7; Tito 2:14; Warumi 8:19-23; 1 Petro 1:18-19.

Page 5: Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala. Adamu na Hawa walivutwa na tamaa

Historia ya Ukombozi, uk.5

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2015 Joseph Bontrager

3. Abramu – Wito na Agano Ahadi na agano kati ya Mungu na Abramu

Baada ya uumbaji na uasi wa binadamu, Mungu alikusudia kukomboa wanadamu, na kuleta mkombozi kupitia watu wateule. Mungu akawachagua Abramu na Sarai na kuahidi kuwafanya kuwa taifa kubwa, atawabariki na kuwafanya kuwa baraka kwa watu wote duniani. Abramu aliacha nyumba ya baba yake alichukua mkewe Sarai na kufuata ongozi wa Mungu wakaingia katika nchi ya Kanaani. Kila alipoenda Abramu alijenga madhabahu na kumwabudu Mungu, akiwa mwaminifu na kumtii Mungu. Kufuatana na uaminifu wao, Mungu alifanya agano na Abramu na Sarai. Aliahidi kuwapa nchi yote ya Kanaani, na uzao watakuwa wengi kama mavumbi na nyota ni nyingi.

Abramu and Sarai wakamzaa Isaka; Isaka na mkewe Rebekah wakamzaa Yakobo na Esau; Yakobo na mkewe Raheli wakawazaa wana 12. Kati ya wana alikuwa ni Yusufu, aliyeuzwa na ndugu zake kuwa mtumwa na kupelekwa Misri. Baadaye akapewa cheo cha juu katika nchi ya Misri kwa sababu alitafsiri ndoto ya Farao na kuokoa nchi ya Misri katika miaka ya njaa.

Yakobo, aliyeitwa Israeli, na jamaa zake walienda Misri kwa sababu ya njaa ili kupata chakula, na Waisraeli walikaa Misri zaidi ya miaka 400. Walizidi kuongezeka wakawa taifa kubwa.

1. Mwanzo 12:1-3. Toka wewe katika nchi yako.

Wito wa Mungu kwa Abramu na Sarai ulikuwa kuacha nini na kwenda wapi?

Mungu aliwaahidi baraka gani?

2. Mwanzo 13:14-17. Nchi hii yote uionayo nitakupa wewe na uzao wako.

Mungu alirudia ahadi yake ya kuwabariki, kwa kuwapa nini?

3. Mwanzo 15:7-21. Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu.

Mungu alirudia ahadi na kufanya agano na Abramu na Sarai.

Mungu aliagiza vitu gani kwa kufanya agano na Abramu? (mst.9)

Mungu alimwonya Abramu kwamba uzao watakuwa wageni katika nchi isiyo yao kama watumwa, baadaye watatoka (mst.13-14). Nchi hiyo ni nchi gani?

4. Mwanzo 17:1-22. Nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.

Mungu aliimarisha agano na Abramu na Sarai. Ishara ya agano ni nini? (mst.10).

Mungu alibadilisha majina yao. o Abramu, baba mtukufu, ataitwa Ibrahimu, baba wa mataifa (mst.5) o Sarai, binti wa kifalme, ataitwa Sarah, mama wa mataifa (mst. 16)

5. Soma Mwanzo 17:7 na Wagalatia 3:16.

Mungu aliahidi kuiimarisha agano na uzao wa Ibrahimu. Kufuatana na Wagalatia 3:16, je, uzao huo ni nani?

Kujadiliana:

1) Je, uzao wa Ibrahimu na Sarai watabariki watu wote wa dunia kwa njia gani?

2) Kwa sababu gani Mungu alibadilisha majina ya Abramu na Sarai?

3) Soma Wagalatia 3:29. Eleza jinsi sisi pia tunavyobarikiwa katika ahadi kwa Abramu.

4) Eleza jinsi habari hizo zinavyoonyesha upendo na uaminifu wa Mungu.

Page 6: Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala. Adamu na Hawa walivutwa na tamaa

Historia ya Ukombozi, uk.6

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2015 Joseph Bontrager

4. Mungu aokoa Waisraeli kutoka Misri na kufanya Agano nao Agano kati ya Mungu na Waisraeli; sheria ni kivuli cha ukombozi kamili

Wakati wa njaa katika Kanaani, Yakobo na jamaa yake walienda Misri kupata chakula. Yusufu, mwana wa Yakobo, alikuwa amepelekwa Misri kwa hila za ndugu zake na aliokoa Misri kwa kutafsiri ndoto ya mfalme Farao. Kwa hiyo Waisraeli walikaribishwa kukaa Misri.

Baada ya miaka zaidi ya 400, Waisraeli waliongezeka kuwa wengi. Mfalme wa Misri Farao alianza kuwatesa Waisraeli kwa sababu walizidi, hadi Mungu alimwita Musa kuwatoa Waisraeli katika nchi ya Misri. Mungu aliwatoa kwa matendo makuu na miujiza yaliyoleta hukumu juu ya watu wa Misri, waliingia jangwa la Sinai. Hapo jangwani Mungu aliwatunza, aliwaongoza, na kuwapa sheria kuhusu ibada na maisha yao. Hayo yote yalikuwa kama kivuli cha wokovu na ukombozi wa Yesu Kristo, na kuonyesha upendo wa Mungu kwa watu wake.

1. Waisraeli katika Misri

Kutoka 1:6-14. Kwa nini mfalme wa Misri aliweka wasimamizi na kuwawatesa? (11)

Kutoka 3:7-10. Mungu alikusudia kufanya nini alipoona na kusikia mateso ya watu? (7)

Mungu alileta mapigo juu ya Misri: Kutoka 7:16-18, mto kuwa damu; 8:1-4, vyura; 8:16, chawa; 8:20-21, mainzi; 9:1-3, tauni juu ya mifugo; 9:8-9, majipu; 9:18, mvua ya mawe; 10:3-6, nzige; 11:1-10, kifo cha mzaliwa wa kwanza.

Kutoka 12:1-13. Mungu aliokoa Waisraeli kwa kuwaagiza nini? (ni pasaka ya Bwana – maana ya pasaka ni kupita juu… mst. 11,13)

2. Waisraeli watoka Misri

Kutoka 13:17-18; 14:21-31. Waisraeli walipita Bahari ya Shamu kwa njia gani? (21)

3. Mungu afanya Agano na Waisraeli

Kutoka 19:1-6. Mungu alidai nini kwa Waisraeli? Mungu aliahidi nini kwa Waisraeli?

Kutoka 24:1-8. Eleza jinsi walivyoimarisha agano kati ya Mungu na Waisraeli.

4. Agano Jipya

Wagalatia 3:24. Kusudi ya Torati (Sheria za Waisraeli) ni nini?

Waebrania 8:5-6. Hema takatifu na taratibu za ibada zilikuwa nini kwa injili ya Yesu?

Waebrania 10:1. Torati inaandaaje kuja kwake Yesu? Eleza maana ya kivuli.

Kujadiliana:

1) Eleza jinsi wokovu kutoka Misri ni kivuli cha wokovu kamili katika Agano Jipya:

2) Utumwa wa Waisraeli katika Misri ni kivuli cha hali gani ya watu leo?

3) Eleza kwa vipi Pasaka ya Waisraeli inatuelekeza kwa Yesu.

4) Eleza jinsi habari hizo zinavyoonyesha upendo na uaminifu wa Mungu.

Page 7: Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala. Adamu na Hawa walivutwa na tamaa

Historia ya Ukombozi, uk.7

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2015 Joseph Bontrager

5. Waisraeli Waingia katika Nchi ya Ahadi Ahadi ya nchi yatimizwa

Baada ya kifo cha Musa, Mungu alimchagua Yoshua kuongoza Waisraeli kuingia katika nchi ya Kanaani. Mungu alitoa Wakanaani kwa sababu ya dhambi zao, naye aliwaonya Waisraeli wanaweza kuondolewa pia wakimwasi Mungu (Kumbukumbu 9:4-5; 28:58-63). Mungu aliwafanya Waisraeli kuwa taifa ili kuonyesha sifa za Mungu mbele ya mataifa (Yoshua 4:24).

Kuna vipindi 3 katika historia ya Waisraeli katika nchi. 1) Waamuzi - Mungu aliweka waamuzi kuwashauri na kuwaongoza; 2) Ufalme mmoja Israeli – Sauli, Daudi, na Sulemani walitawala Israeli na kupanua mipaka yake; 3) Falme mbili za Israeli na Yuda. Wakati wa wafalme Mungu alituma manabii kuwaonya Waisraeli juu ya dhambi zao.

1. Mungu anamwita Yoshua. Yoshua 1:1-9

Mungu alimwagiza Yoshua nini?

Mungu alimwahidi Yoshua nini?

2. Waisraeli wavuka Mto Yordani. Yoshua 3:1-17

Waisraeli walivuka mtu Yordani kwa kufuata taratibu gani?

Eleza umuhimu wa Sanduku la Ushuhuda.

Sanduku la Ushuhuda lilikuwa mahali Mungu alipokutana na watu wake. Ndani ilikuwa sheria ya Mungu, na juu yake Kiti cha Rehema. Soma maelezo yake katika Kutoka 25:10-22

3. Ushindi juu ya wafalme wa Kanaani. Yoshua 10:40-42

Kwa nini Waisraeli waliweza kushinda maadui yao? (42)

Nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuketi humo. (Hesabu 33:53)

4. Viongozi wa Israeli – Vipindi vitatu (3)

Waamuzi. Waamuzi 2:6-16

Ufalme (1 Samweli 8:1-9); Sauli (1 Samweli 10:1); Daudi (2 Samweli 5:1-5); Suleman (1 Wafalme 1:38-40)

Falme mbili – Yuda na Israeli (1 Wafalme 12:1, 16-17, 20-21)

5. Watu wa Mungu katika Agano Jipya. 1 Petro 2:9-10. Tazama jinsi Waisraeli ni mfano wa kanisa; na hali ya watu wa Mungu inatimiza mfano wa Waisraeli.

Mzao mteule – Mungu ametuchagua

Ukuhani wa kifalme – Mungu ametoa sheria zake na kufanya agano nasi

Taifa takatifu – Mungu anatukusanya ili tufanye kazi yake

Watu wa milki ya Mungu – watu wa Mungu ni makao ya Roho Mtakatifu

Kuzitangaza fadhili zake Mungu – Mungu ametutuma ili kushuhudia matendo ya Mungu

Taifa la rehema – tumepokea fadhili za Mungu

Kujadiliana:

1) Je, Mungu alikuwa na kusudi gani kufanya Waisraeli kuwa taifa?

2) Soma 2 Petro 1:4. Sisi kama watu wa Mungu, je, tumepokea ahadi na baraka gani kutoka kwa Mungu?

3) Soma Warumi 8:31-32,38. Eleza jinsi ushindi wa Waisraeli ni mfano wa ushindi wetu.

4) Eleza jinsi habari hizo zinavyoonyesha upendo na uaminifu wa Mungu.

Page 8: Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala. Adamu na Hawa walivutwa na tamaa

Historia ya Ukombozi, uk.8

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2015 Joseph Bontrager

6. Waisraeli Wachukuliwa Mateka Uasi na Hukumu

Mungu aliwahukumu Waisraeli kwa sababu ya uasi wao na ibada ya sanamu, walichukuliwa mateka na nchi jirani wapagani. Kwanza mfalme wa Ashuru alishinda taifa ya kaskazini Israeli, baadaye mfalme wa Babeli alishinda taifa la kusini Yuda. Wafalme hao waliwapeleka sehemu ya Waisraeli katika nchi yao. Katika hali hiyo ya shida, Mungu alituma manabii kuwaonya na kutabiri kuja kwa Mtiwa Mafuta atakayeshinda maadui na kuwakusanya Waisraeli tena kuwa watu wake. Atafanya agano jipya nao na kuwapa moyo mpya ya utii (Yeremia 31:31-34). Na atawafanya kuwa ufalme wa amani na wataleta baraka kwa dunia nzima kupitia Mtiwa Mafuta (Isaya 9:2-7), ambaye ni Masiya, Yesu Kristo.

Ibada katika masinagogi ilianza wakati wa mateka. Walikuwa mbali na Yerusalemu na hekalu, kwa hiyo walianza kujikusanya katika makundi kwa mafundisho. Walimu walioitwa marabi, walifafanua na kufundisha sheria za Mungu.

1. Mungu aliwaonya Waisraeli kuhusu utii na uasi

Kumbukumbu 28:1-9. Mungu aliahidi nini wakisikia sauti yake?

Kumbukumbu 28:15-19,36,49. Mungu alitoa onyo gani wasipotii maagizo yake?

Kumbukumbu 30:1-3. Wakimwasi Mungu na kutawanyika, halafu kumrudia, Mungu alitoa ahadi gani?

2. Wafalme wa Israeli na Yuda

Wafalme wengine walifanya maovu. Mfalme gani anatajwa katika 1 Wafalme 15:25-26? 1 Wafalme 16:25? 1 Wafalme 16:33?

Wafalme wengine walifanya yaliyo mema. Mfalme gani anatajwa katika 1 Wafalme 15:11? 1 Wafalme 22:42-43? 2 Wafalme 12:2?

3. Watu wa Mungu wachukuliwa mateka na nchi pagani

2 Wafalme 17:5-8. Ni nchi gani ilishinda na kuteka Taifa la Kaskazini, Israeli?

2 Wafalme 25:8-12. Ni nchi gani ilishinda na kuteka Taifa la Kusini, Yuda?

4. Manabii wa kipindi cha mateka walitabiri Agano Jipya

Isaya 7:14. Mungu atatoa ishara gani? Soma Mathayo 1:22-23, neno la nabii lilitimia.

Isaya 9:1-7. Yesu ataleta nuru kuu gani (2)? Atakuwa mfalme wa namna gani (6-7)?

Isaya 53:3-6. Mateso ya Yesu yanatusaidiaje?

Yeremia 31:31-34. Sheria ya Agano Jipya itaandikwa wapi?

Kujadiliana:

1) Je, kwa sababu gani Mungu aliruhusu Waisraeli kuchukuliwa mateka na nchi pagani?

2) Tunajifunza nini kuhusu Mungu katika kutekwa na kurudishwa katika nchi?

3) Eleza jinsi Agano Jipya ilivyo bora kulika Agano la Kale. (Soma Yeremia 31:31-34)

4) Eleza jinsi habari hizo zinavyoonyesha upendo na uaminifu wa Mungu.

Page 9: Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala. Adamu na Hawa walivutwa na tamaa

Historia ya Ukombozi, uk.9

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2015 Joseph Bontrager

7. Waisraeli Warudi katika Nchi Ufufuo na ukombozi

Kipindi cha mateka kilileta mabadiliko katika nia na imani ya Waisraeli. Walitambua kwamba walitekwa kwa sababu ya kuabudu miungu ya wapagani na kutofuata njia za haki na ukweli. Kwa mambo yaliyowatokea, Waisraeli walianza kuelewa kwamba ufalme wa Mungu si taifa la dunia hii, bali ni ufalme wa kiroho. Pili, waliona kwamba Mungu hakai katika hekalu bali katika roho ya mtu. Tatu, waliona kuwa haki ya kweli si kwa matendo ya ibada bali ni kumpenda Mungu na jirani.

Walipopewa ruhusa kurudi katika nchi yao, kazi ya kwanzi ilikuwa kujenga hekalu na kutoa dhabihu. Walianza kushika sikukuu za Mungu na kusafisha maisha yao. Kazi ya pili ilikuwa kujenga ukuta na malango ya Yerusalemu ili kulinda usalama.

Taifa la Israeli halikurudi kwa hali yake ya heshima na nguvu kama wakati wa wafalme, lakini walianza kushika na kutii sheria za Mungu zaidi. Kurudi katika nchi ni wakati wa ufufuo na kumrudia Mungu wao. Hayo yote ni mifano na “kivuli” cha ukweli wa agano jipya, kwamba inatubidi kuwa waaminifu. Mungu alikuwa anawaandaa kumpokea Masiya na kufanya nao agano jipya litakalofanywa na damu ya Yesu na maagizo yake kuandikwa katika mioyo yao.

1. Waisraeli walirudi Yerusalemu na kujenga hekalu (Ezra 1-6)

Waisraeli waruhusiwa kurudi kwa agizo la mfalme Koreshi (1:1-3). Walivumilia upinzani na kumaliza hekalu (6:15).

Walirejesha ibada ya hekalu. Walisherehekea sikukuu gani? (6:19)

2. Ezra alifika Yerusalemu na kufundisha (Ezra 7-10)

Kuhani Ezra aliwafundisha nini? (7:10)

Walitambua kwamba shida yao ilisababishwa na nini? (9:13)

Wakatubu dhambi gani? (10:2). Kwa nini dhambi hiyo ni hatari kwa watu wa Mungu?

3. Nehemia alijenga ukuta wa Yerusalemu na kurekebisha maisha yao (Nehemia 1-13)

Nehamia aliposikia hali mbaya ya watu wa Yerusalemu, alifanya nini? (1:1-11)

Nehemia alirudi Yerusalemu kwa kufanya nini? (2:1-20; 6:15)

Alirekebisha udhalimu gani juu ya maskini? (5:1-13)

Ezra, Nehemia, na Walawi walisoma na kufundisha nini? (8:1-3,7-9)

Kuna dalili gani kwamba Waisraeli walianza kushika agano na Mungu? (9:1-3)

4. Mafundisho na Uamsho wa Kiroho

Watu wa Mungu wakifuata njia za wapagani wanaleta matokeo gani? (Ezra 9:10-14)

Uhai wa kiroho hutokana na kuabudu. Walijenga nini kwanza katika Ezra 3:2?

Maisha ya roho huhitaji ulinzi na utaratibu. Nehemia alijenga nini kwa kulinda mji na kuwezesha utaratibu wa maisha? (Nehemia 2:17)

Walioamshwa waliahidi kufanya nini? (Nehemia 10:28-29)

Kujadiliana:

1) Je, wakati walipokaa katika mateko, Waisraeli walijifunza nini kuhusu Mungu na ukombozi wake?

2) Eleza kwa nini ni muhimu watu kufundishwa neno la Mungu.

3) Je, dhambi inaweza kuleta hukumu na dhiki hata leo? Eleza jibu yako.

4) Je, ni dhambi gani leo inashika watu, na wangetubu ili kupate uzima na baraka?

Page 10: Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala. Adamu na Hawa walivutwa na tamaa

Historia ya Ukombozi, uk.10

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2015 Joseph Bontrager

8. Yesu Mkombozi Kutimiza Ukombozi

Hata uliowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana (Wagalatia 4:4-5).

Wakati ulipotimia, Yesu alizaliwa. Aliitwa Imanueli, yaani Mungu pamoja nasi. Yesu alianza kazi ya ukombozi akawaita wanafunzi 12 na kuwafundisha kuhusu Ufalme wa Mungu, ambao ni ufalme wa kiroho, si ufalme wa siasa wala si ufalme wa dunia hii (Yohana 18:36). Alifanya miujiza akaponya wagonjwa na kutoa mapepo kama ishara za Ufalme wa Mungu. Yesu alifundisha upendo kwa watu wote, na unyenyekevu katika huduma, na maisha yake yalikuwa mfano wa tabia hizo. Yote yalikuwa mifano wa maisha katika Ufalme wa Mungu.

Yesu alishtakiwa na wakuu wa Wayahudi kuwa amemwasi Mungu. Walisema anataka kuwa mfalme na kupindua serikali. Hivyo alisulubishwa hapo Yerusalemu, lakini siku ya tatu Yesu alifufuka kutoka wafu, akionyesha mamlaka yake juu ya mauti na maovu.

Sheria (agano la kale) ni kivuli cha mema itakayokuwa, wala si sura yenyewe (Waebrania 10:1). Maisha ya Yesu yalitimiza sheria za maadili kwa jinsi alivyofuata nia ya sheria, wala si maneno yake tu (Mathayo 5:17,20-22,27-28). Maisha yake yalionyesha namna ya maisha katika ufalme wa Mungu. Kwa kifo chake Yesu alitimiza sheria za dhabihu kwa kujitoa dhabihu iliyotimiza dhabihu zote kwa ajili ya dhambi zetu (Waebrania 9:11-15). Ufufuo wa Yesu ulionyesha ushindi wa Yesu juu ya mauti na unawezesha ushirikiano wetu na Mungu.

Yesu alitimiza madhumuni ya Mungu kukomboa binadamu na dunia kutoka vifungo vya maovu na mauti yaliyotutega na kututenga na Mungu. Yesu alifanya agano jipya kwa kujitoa kuwa sadaka kamilifu na kutupatanisha na Mungu.

1. Yesu alimshinda Mwovu aliyefunga binadamu na kumfanya kumwasi Mungu

Mwanzo 3:15. Mungu alisema na nani? Eleza maana ya huo utakuponda kichwa.

Yohana 12:31. Mkuu wa ulimwengu ni nani? Atafanywaje?

Luka 10:18. Yesu aliongea na nani? Alimwona Shetani anakuwaje?

Waebrania 2:14-15. Mauti ya Yesu yalileta matokeo gani?

2. Yesu alitimiza sheria za Agano la Kale na kuleta uzima

Mathayo 5:17. Yesu alikuja kufanyaje sheria za Agano la Kale? (ona pia Mathayo 5:21-22, 27-28, 33-34)

Yohana 10:10. Yesu alikuja ili tuwe na nini

Warumi 6:4. Kama Kristo alivyofufuka, na sisi tuwe na maisha gani?

Warumi 12:2. Je, tunabadilishwa kwa vipi tunapojitoa kwa Mungu?

3. Yesu alitupatanisha na Mungu na kufanya agano jipya kati ya Mungu na wanadamu

Warumi 5:10. Tulipatanishwa na Mungu kwa _____________________________.

Waebrania 8:6. Yesu ni mjumbe wa __________________. (ona Yeremia 31:31-33)

Luka 22:20. Kikombe cha mesa ya Bwana ni mfano wa _____________________.

Kujadiliana:

1) Eleza jinsi Yesus alivyotimiza madhumuni ya Mungu ya ukombozi.

2) Kwa vipi agano jipya ni bora kuliko agano la kale?

3) Eleza tofauti kati ya Ufalme wa Mungu na falme za dunia.

Page 11: Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala. Adamu na Hawa walivutwa na tamaa

Historia ya Ukombozi, uk.11

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2015 Joseph Bontrager

9. Kanisa Maisha ya Ukombozi

Kazi kuu ya kanisa ni kuunganisha ukombozi wa Yesu Kristo na maisha ya wanadamu. Ukombozi ulitimizwa kwa kifo na ufufuo wa Yesu, hakuna kuongeza ili binadamu kupatanishwa na Mungu. Lakini wanadamu wanapaswa kukubali kazi ya Roho Mtakatifu katika roho zao, kuwabadilisha na kuwafanya kuwa wana wa Mungu. Yesu ameponda kichwa cha nyoka Shetani, lakini bado anazunguka kama simba na kutafuta wale anaoweza kuwaangamiza (1 Petro 5:8).

Kanisa linakaa katika kipindi kati ya ukombozi kutimizwa na Yesu, na ukombozi kukamilika, mwovu atakaposhindwa na kufungwa. Ukombozi ni kamili, lakini haijakamilika.

Kanisani tunatakiwa kuishi jinsi maisha yalivyo katika Ufalme wa Mungu. Tabia ya kanisa ni upendo, kazi ya kanisa ni utumishi, hali ya kanisa ni uzima na amani. Kanisa ni ushirikiano wa wanadamu wanaoishi kwa sheria ya upendo na kujitoa kusaidiana na kujengana, wakiongozwa na kuwezeshwa na Roho Mtakatifu. Katika kanisa waumini wanaungana kumsifu na kumshukuru Mungu kwa matendo yake makuu. Na wanatawanyika kuleta neno la uzima, yaani injili, kwa dunia iliyo bado chini ya utumwa wa mwovu na mauti.

1. Kanisa linakiri kwamba Yesu ni Bwana.

Matendo 2:36. Mitume walihubiri neno gani kuu?

Wagalatia 5:16-25. Yesu kuwa Bwana wa mwenendo wetu, ni mwenendo gani?

2. Kanisa ni jamii ya wale waliokombolewa na kupatanishwa na Mungu.

2 Wakorintho 5:18. Yesu ametupatanisha na nani?

Waefeso 2:13-16. Yesu alibomoa nini ili kutuunganisha kama ndugu?

3. Kanisa hueneza habari ya ukombozi katika dunia yote.

2 Wakorintho 5:20. Kanisa ni wajumbe wa Kristo kuleta neno gani?

Mathayo 28:18-20. Kanisa limepewa amri na mamlaka kufanya nini?

4. Kanisa ni nyumba ya Mungu, mwili wa Kristo, na makao ya Roho Mtakatifu.

1 Wakorintho 12:27. Eleza maana ya kuwa mwili wa Kristo na viungo.

Waefeso 2:19. Eleza maana ya watu wa nuyumbani mwake Mungu.

Waefeso 2:21-22. Kanisa linaitwa hekalu takatifu na maskani ya Mungu katika Roho. Maneno hayo yanaeleza nini kuhusu hali ya kanisa?

Kujadiliana:

1) Katika dunia yetu, unaona dalili gani kwamba Shetani bado anazungukazunguka na ukombozi haujakamilika?

2) Eleza maana ya maneno haya: Ukombozi ni kamili, lakini haijakamilika.

3) Mungu aliagiza Adamu na Hawa, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha (Mwanzo 1:28). Yesu alituagiza enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi (Mathayo 28:19). Ongea jinsi maagizo hayo yanavyofanana.

4) Je, kwa maneno yako, ujumbe wetu wa ukombozi na upatanisho tunaopeleka kwa dunia ni ujumbe gani?

Page 12: Historia ya Ukomboziequip4change.org/pdf/swahili/level1/Historia-ya-Ukombozi.pdfmacho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa…alitwaa tunda akala. Adamu na Hawa walivutwa na tamaa

Historia ya Ukombozi, uk.12

Diocese-Based TEE, Kenya Mennonite Church, Kanisa la Mennonite Tanzania ©2015 Joseph Bontrager

10. Yerusalemu Mpya Kukamilisha Ukombozi

Ukombozi utakuwa umekamilika katika Yerusalemu Mpya, baada ya mwovu Shetani kufungwa na kutupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 20:10). Wanaomwamini Yesu watakusanyika, pasipo na machozi, wala kifo, wala kilio, wala maumivu. Mungu mwenyewe atakaa kati ya watu wake (Ufunuo 21:2-4). Kuna mto wa maji ya uzima utokao katika kiti cha enzi cha Mungu. Mti wa uzima unatoa matunda yake kila mwezi na majani yake ni ya kuwaponya mataifa. Wala hakuna laana wala usiku (Ufunuo 22:1-5).

Kitabu cha Ufunuo kinaonyesha ushindi wa Yesu juu ya mwovu, ushindi huo ukielezwa kwa njia ya mifano na ishara zinazohitaji ufafanuzi ili kuelewa. Wataalamu wanatoa mawazo mbalimbali kuhusu maana ya ishara hizo. Lakini ujumbe mkuu wa kitabu cha Ufunuo ni kwamba Yesu ameshinda na atashinda na kukamilisha ukombozi.

Yesu Mkombozi ni Mshindi. Kusudi ya Mungu tangu mwanzo ni kuleta uzima na ushirikiano na wanadamu. Katika Yerusalemu mpya, mpango wa Mungu utatimilizwa na kukamilishwa.

1. Ushindi juu ya Mwovu Shetani

Ufunuo 5:9. Walionunuliwa kwa damu ya Yesu ni watu gani?

Ufunuo 12:10-11. Mwovu alishindwa kwa nguvu ya nini?

Ufunuo 20:10. Mwisho wa Ibilisi Shetani utakuwaje?

2. Uzima tele, pasipo laana wala mauti

Ufunuo 21:1-4. Eleza hali ya Yerusalemu Mpya inavyoelezwa katika mistari hiyo.

Ufunuo 22:1. Mto wa maji ya uzima unatoka wapi?

Ufunuo 22:2. Mti wa uzima unatoa matunda na majani gani? Kwa kusudi gani?

3. Mungu kati ya watu wake

Yohana 14:2-3. Yesu alitoa ahadi gani kwa wanafunzi wake?

Ufunuo 21:3. Kwa nini ni muhimu Mungu kukaa na wanadamu?

Ufunuo 21:22. Katika Yerusalemu Mpya hekalu ni namna gani?

4. Waingiao katika Yerusalemu mpya

Ufunuo 2:7. Atakayerithi na kupokea maji ya uzima na mti wa uzima ni nani?

Ufunuo 21:27. Watakaoingia katika Yerusalemu Mpya ni watu gani?

Ufunuo 22:14. Watakaoingia Yerusalemu Mpya ni waliofanya nini?

Ufunuo 22:17. Ni nani atakayekaribishwa kupokea maji hayo ya uzima?

Kujadiliana:

1) Fananisha hali ya Yerusalemu mpya na hali ya Bustani ya Edeni kabla wanadamu hajamwasi Mungu. Kuna nini inafanana? Kuna nini ni tofauti?

2) Mti wa uzima upo Yerusalemu mpya, kama ulivyokuwa katika Edeni. Unavyofikiri, kwa nini hakuna mti wa ujuzi wa mema na mabaya katika Yerusalemu mpya?

3) Je, maji ya uzima yanayotoka katika kiti cha enzi ni mfano wa nini, kwa jinsi unavyofikiri?

4) Eleza jinsi habari hizo zinavyoonyesha upendo na uaminifu wa Mungu.


Recommended