+ All Categories
Home > Documents > Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf ·...

Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf ·...

Date post: 02-Mar-2019
Category:
Upload: truongngoc
View: 385 times
Download: 2 times
Share this document with a friend
22
Maisha ya Uzima Diocese-Based Leadership Training Program Mennonite Churches of East Africa (KMC/KMT) Joseph and Gloria Bontrager Theological Education Coordinators, 2014
Transcript
Page 1: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

Maisha ya Uzima

Diocese-Based Leadership Training Program

Mennonite Churches of East Africa (KMC/KMT)

Joseph and Gloria Bontrager Theological Education Coordinators, 2014

Page 2: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

2

Yaliyomo

Soma la 1 Mpango wa Mungu ni Uzima 3

Somo la 2 Dhambi na Magonjwa 5

Somo la 3 Shalom – Kurudisha Hali ya Uzima 7

Somo la 4 Mwonekano Kamilifu wa Kibiblia 9

Somo la 5 Roho, Nafsi, Mwili – Mtu Mzima 10

Somo la 6 Kujitunza Mtu Binafsi 12

Somo la 7 Jinsia na Ngono 14

Somo la 8 Ndoa 16

Somo la 9 Uzima katika Jamii 18

Somo la 10 Kutunza Uumbaji – Uzima wa Mazingira 21

Page 3: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

3

Somo la 1. Mpango wa Mungu ni Uzima

Tangia mwanzo, Mungu alidhamiria mpango wake kuwa uumbaji uwe mkamilifu katika nyanja zote, na kuwa mzima ndani yake. Mungu aliumba nchi, anga, wanyama na akaweka kila kitu mahali pake. Akatangaza kila alichoumba kuwa ni “chema” (Mwanzo 1:25). Ndipo Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, na akasema ni “chema sana” (Mwanzo 1:27-30). Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi (mwili wake), ndipo Mungu akampulizia puani pumzi ya uhai (roho yake), mtu akawa nafsi hai (nafsi yake). Mungu akamwumba binadamu kama mwili, roho, na nafsi (Mwanzo 2:7).

Mfano wa Mungu katika binadamu si mfano wa kimwili, kwa sababu Mungu hana mwili kama binadamu, ni roho. Mfano wa Mungu unahusu tabia yake, kama vifuatavyo:

Haki na utakatifu (Waefeso 4:24)

Ufahamu (Wakolosai 3:10)

Utukufu na heshima (Zaburi 8:4-5)

Madaraka na mamlaka (Zaburi 8:6-8).

Mungu aliwabariki Adamu na Hawa na vyote walivyohitaji. Mungu aliwaandalia Bustani ya Edeni (Mwanzo 2:8-9) na kuwaweka katika bustani (Mwanzo 2:15-17). Katika bustani hiyo binadamu alibarikiwa na vifuatavyo:

Uzuri – “unaotamanika kwa macho” (mst.9)

Chakula – “kufaa kwa kuliwa” (mst.9)

Uchaguzi – “mti wa ujuzi wa mema na mabaya” (mst.9)

Kazi na shughuli – “ailime na kuitunza” (mst.15)

Ushirikiano – “si vema mtu awe peke yake, nitamfanyia masaidizi wa kufanana naye” (mst.18)

Ilikuwemo miti miwili maalum kati ya miti yote katika Bustani, mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya (Mwanzo 2:9). Mungu alimwagiza Adamu kwamba waweza kula matunda ya kila mti katika bustani isipokuwa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya (Mwanzo 2:16-17). Mti wa uzima ni mfano wa kumtegemea Mungu, kwa sababu uzima na uhai hutoka kwa Mungu. Lakini mti wa ujuzi wa mema na mabaya ni mfano wa binadamu kutegemea hekima yake na uwezo wake mwenyewe. Adamu na Hawa waliagizwa wasile kutoka mti huo “kwa maana siku unapokula matunda yam ti huo utakufa hakika” (Mwanzo 2:17).

Mungu aliwatembelea na kusema nao Adamu na Hawa (Mwanzo3:8). Na jinsi walivyomtii Mungu walizidi kufurahia uhusiano na Mungu na maisha na kazi zao katika paradiso ya bustani. Walikuwa na uzima tele na hawakuhitaji cho chote. Walikuwa na afya katika mwili, akili, na roho.

Katika somo linalofuata tutaona jinsi amani na ushirikiano ziliharibika kufuatana na uchaguzi wa Adamu na Hawa, na zilitokeza uchungu, ugumu, na mashindano.

Page 4: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

4

Maswali ya kujadaliana:

1. Soma Mwanzo 2:15-23. Eleza hali ha maisha katika Bustani ya Edeni. Mungu aliwapatia Adamu na Hawa baraka zipi?

2. Kwa mawazo yako, eleza uhusiano kati ya Mungu na Adamu na Hawa katika Mwanzo 1-2. Andika maneno machache yanayoeleza hali ya uhusiano yao.

3. Mungu aliwatunzia Adamu na Hawa uzima katika kila sehemu ya maisha yao. Je, Mungu alifanya nini kutunza:

a. Uzima wa kimwili _________________________________________

b. Uzima wa kiakili __________________________________________

c. Uzima wa ki-mahusiano ____________________________________

d. Uzima wa kiroho __________________________________________

4. Je, umewahi kuona watu wakifanya uchaguzi uletao kifo? Au je, umewahi kuona watu wakifanya uchaguzi uletao uzima? Taja mifano.

5. Je, uzima wa aina gani unakosa zaidi katika eneo lako la nyumbani?

Page 5: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

5

Somo la 2. Dhambi na Magonjwa

Je, nini ilitokea ili kuharibu afya na uzima wa dunia na binadamu?

Shetani alileta majaribu ya mashaka kuhusu maneno aliyosema Mungu. Adamu na Hawa wakachagua kutosikiliza maagizo ya Mungu, na kutotii kile alichosema Mungu. Uasi wa Adamu na Hawa uliharibu uhusiano baina yao na Mungu, na kusababisha matokeo ya kazi ngumu, uchungu na hatimaye kifo (Mwanzo 2:17; 3:1-19). Watu waliugua katika miili yao, na uhusiano wao, na katika roho na fikira zao.

Kupitia dhambi ya Adamu na Hawa, wote tulirithi hali ya dhambi, na matokeo ni kifo (Warumi 6:12; 1 Yohana 3:4; Warumi 5:12,19). Dhambi iliharibu mpango wa Mungu wa kwanza, na kuleta udhaifu katika miili yetu, fikira na roho, na kuleta uharibifu katika nchi na wanyama waliomo. Isipokuwa uwepo upatanisho kati ya Mungu na binadamu, dhambi hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu, na kuvunja haki na usawa ulimwenguni.

Afya mbaya ina maanisha, kuishi nje ya neema ya Mungu, na nje ya uhusiano naye Mungu na kwa wenzetu, na nje ya uhusiano mzuri na uumbaji. Kuishi nje ya neema ya Mungu inaweza kusababisha ugonjwa wa kimwili, wa kihisia, wa kijamii au wa kiroho. Wafuasi wa dini za kiasili wanaamini kuwa afya mbaya husababishwa na mizimu au uchawi. Endapo mtu aliacha kutii desturi na mila, au alifanya jambo la kuudhi waliokufa, na hao mizimu walikasirika na kusababisha ugonjwa au laana dhidi yake. Wengine huamini kuwa ugonjwa husababishwa na shida, uhalifu au dhambi. Lakini Biblia inatuambia wazi kwamba dhambi na magonjwa yalianza na uasi wa Adamu na Hawa uliotufarakisha na Mungu, na yakaenea kufuatana na dhambi za watu wote (Warumi 5:12). Inawezekana ugonjwa umefuatana na dhambi za watu wengi (Walawi 26:14-17), au hata uasi wa mtu mmjoja (Daudi – 2 Samweli 11:2-5, 14-17,27; na Akani – Yoshua 7:1-12). Lakini, hata hivyo, si sababu peke yake tu.

Kwa nini Mungu anaruhusu magonjwa?

1. Ili kutukumbusha juu ya upeo wetu mdogo na kwamba tunamtegemea Mungu (Danieli 4:30-33).

2. Ili kuleta utukufu kwa Mungu (Yohana 9:1-3).

3. Ili kutuongoza, kama alivyomwongoza Yusufu (Mwanzo 41:37-45; 50:20; 2 Wakorintho 1:9).

4. Ili kutufanya kufanana kama Mungu alivyo (Warumi 8:28-29; 2 Wakorintho 12:7-10; Yakobo 1:2-3)

Kwa sababu gani Mungu haponyi kila mara?

Kama magonjwa ni matokeo ya dhambi ya Adamu, je, sivyo vema kama Mungu ataponya tukimrudia na kutubu katika imani? Hapa sababu 2:

Ili “tusipate kujivuna kupita kiasi,” bali “uwezo wa Kristo ukae juu yetu” (2 Wakorinto 12:7-10).

Kwa maana viumbe vyote na hata sisi tunaugua pamoja wakati tukisubiri ukombozi kamili (Warumi 8:22-23).

Page 6: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

6

Maswali ya kujadaliana:

1. Mungu alimwumba Adamu na Hawa kwa mfano wake. Baada ya kumwasi Mungu je, bado walikuwa wanabeba mfano wa Mungu? Mfano wake Mungu ulipotea au kuchafuka tu?

Taja tabia za mfano wa Mungu walizopoteza.

Taja tabia za mfano wa Mungu walizobaki nazo.

2. Je, dhambi ya Adamu na Hawa inatuhusu maisha yetu bado leo kwa jinsi gani?

3. Waonaje, uchungu wa dhambi tunaosikia leo ni kwa ajili ya dhambi ile ya Adamu, au ni kwa ajili ya dhambi zetu wenyewe tu?

4. Kwenu nyumbani, je, watu wenge hudhani kwamba magonjwa husababishwa na nini?

5. Tafuta mistari ya Biblia inayoeleza hali na umuhimu wa mizimu. Je, wazee waliokufa na mizimu wanajihusisha kwa njia gani katika maisha yetu leo? Kwa njia gani tuonyeshe heshima kwa watu waliokufa?

Page 7: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

7

Somo la 3. Shalom – Kurudisha Hali ya Uzima

Lugha ya kiasili ya Agano la Kale ni Kiebrania. Neno la Kiebrania “shalom” hutafsiriwa “amani.” Shalom ni tarajio la Mungu kwamba uumbaji wake uwe mkamilifu na mzima. Shalom ni hali ya umoja na utulivu, amani ndani yetu, tena kati yetu na wenzetu, na wengine duniani (Marko 12:30-31; Luka 10:25-37). Inajumlisha pia utunzaji wa vyote vilivyoumbwa (Mwanzo 1:28-30; Isaya 32:16-20) na ushirikiano wetu na Mungu (Mwanzo 3:8-9; Ezekieli 37:26-27; Malaki 2:5-6).

Hivyo, uzima (shalom) ni kuishi kwa amani katika nafsi yako, amani na Mungu, amani na umoja kua watu wengine na kwa uumbaji wake Mungu. Mungu hukusudisa afya na uzima kwetu katika mwili, na nafsi, na roho. Lazima sehemu hizo zote ziwe na uzima ili mtu awe mzima. Paulo aliwaombea waamini kwamba Mungu “awatakase kabisa” katika nafsi, na roho, na mwili (1 Wathesalonike 5:23). Ndiye Mungu atakasaye na Mungu ni mwaminifu. Yesu alipomponya mtu mwenye kupooza alimponya kiroho – “umesamehewa dhambi zako” – na kimwili – “ondoka uende” (Marko 2:1-12). Uzima ni kurudisha uzima katika mwili, akili, roho, na mahusiano.

Yesu alieliza kwamba uzima wa milele ni kumpenda Mungu kwa moyo wote (kupenda), na roho yote (motisha), na nguvu zote (mwili), na akili yote (fikira), na kumpenda jirani kama nafsi yetu (mahusiano). Yesu alisema “Fanya hivi nawe utaishi” (Luka 10:25-28).

Neno “wokovu” katika lugha ya asili latoka kwa neno lenye maana “kufanywa mzima.” Wokovu ni kurejesha au kukomboa kile kilichoharibika. Mungu alifanya mpango na njia ya kupantanisha na kurudisha wanadamu walioanguka kwa njia ya Mwana wake Yesu (Warumi 5: 15-17). Yesu alieleza kazi yake ya wokovu alipokuwa akianza huduma yake hapa duniani akisema, “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa” (Luka 4:18-19). Wakati mwingini Yesu alieleza kusudi lake kwamba, “Nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” (Yohana 10:10). Wokovu ni kurudisha hali ya uzima katika roho, akili, na mwili, hali iliyopotea kwa ajili ya dhambi. Agano Jipya lafundisha kwamba waamini wa Kikristo “wafananishwe na mfano wa Mwana wake” (Warumi 8:29) na mwisho “tutafanana naye” (1 Yohana 3:2).

Shalom ni kutengeneza upya uhusiano wetu na Mungu (yaani wokovu wetu). Waraka kwa Waefeso hueleza yafuataho:

Kurejesha uumbaji, “kuvijumlisha vitu vyote” (Waefeso 1:10)

Wokovu ni neema ya Mungu kwetu, ukombozi na msamaha (Waefeso 1:7; 2:5)

Umoja katii ya Wakristo ni “maskani ya Mungu” (Waefeso 2:22)

“Kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu” (Waefeso 3:19)

Umoja ni kipawa cha Roho (Waefeso 4:3)

“Kuwa mtu mkamilifu” na kufikia “utimilifu wa Kristo” (Waefeso 4:13)

Kuwa “wafuasi na Mungu” (Waefeso 5:1)

Kupenda kama Yesu alivyotupenda (Waefeso 5:2).

Page 8: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

8

Maswali ya kujadaliana:

1. Katika maneno yako, eleza maana ya Shalom.

2. Soma 1 Wathesalonike 5:213-24. Maneno “Mungu wa amani” ni sawa na kusema “Mungu wa Shalom.” Ni nani anayetoa Shalom?

3. Soma Yohana 10:7-10. Yesu alikuju ili tuwe na “uzima tele.” Je, “uzima tele” ni nini?

4. Je, mtu maskini au mtu mgonjwa anaweza kuona ule “uzima tele” Yesu alioahidi?

5. Rudia maelezo kutoka Waefeso yaliyoandikwa katika aya ya Shalom ni kutengeneza upya uhusiano wetu na Mungu. Jinsi unavyojua wokovu katika maisha yako, je, inafanana na maelezo hayo? Au je, hayo yanafanana na hali ya kanisa lako? Eleza jibu lako.

Page 9: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

9

Somo la 4. Mwonekano Kamilifu wa Kibiblia

Tumeumbwa ili tuishi katika hali ya amani na Mungu, na wengine, na ulimwengu, na katika roho zetu. Kujifahamu na kukubali hali yetu jinsi tulivyo ni muhimu ikiwa tutakuwa na uzima. Mungu alituumba kwa mfano wake, kila mmoja tofauti, ili tumletee Mungu sifa. Jinsi tunavyotambua na kukubali tulivyo, na sehemu zote za maisha yetu, na kujitoa kwa Mungu, tunakuwa na uzima. Mungu hufurahia tukiwa na uhusiano naye na tukijitoa kwa kutimiza makusudi yake. Uzima ni kujifahamu ni nani, na kujua kusudi letu, na kujua tabia yetu.

Kujifahamu: Nani Wewe?

Binadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu, mwanamume na mwanamke, Mungu akawathamini sawa, aliona ni “vizuri sana” (Mwanzo 1:27).

Binadamu ni sababu ya upendo wa Mungu wa kuleta ukombozi (Wakolosai 1:19,20; Yohana 3:16).

Binadamu alistahili kuokolewa na kupatanishwa na kupokea baraka na urithi kutoka kwa Mungu (Warumi 6:12-19; 1 Yohana 3:4; Warumi 5:19).

Kusudi: Kwa nini Wewe?

Binadamu aliumbwa kwa utukufu wa Mungu (Isaya 43:7,21; Wakolosai 1:10, 2:9; Waefeso 1:4-6). Tunabeba mfano wa Mungu Baba, kiumbe cha maana kuliko viumbe vyote, wenye thamani na heshima.

Binadamu aliumbwa ili awe na uhusiano na Mungu, yaani kutembea na Mungu (Mika 6:8) na kumpenda Mungu (Luka 10:27).

Biandamu aliumbwa ili awe na uhusiano na binadamu wengine (Mathayo 27: 37-39). Mahusiano wa maana na wengine hutokana na uhusiano wetu na Mungu.

Tabia: Nini Wewe?

Sisi ni hekalu la Mungu, kila mtu binafsi sawa na ushirika wa watu, ni makao yake Mungu (1 Wakorintho 3:16-17).

Sisi ni viungo vya wa mwili wa Kristo (1 Korintho 6:15), tukiendeleza kazi ya Yesu na kumwakilisha Yesu kwa wengine.

Sisi ni dhabihu ya kumpendeza Mungu (Warumi 12:1), tukitoa mwili, fikira, roho na nafsi, kama ibada takatifu kwake.

Maswali ya kujadaliana:

1. Katika habari ya uumbaji wa ulimwengu, Adamu na Hawa waliumba wote kwa mfano wake Mungu. Neno hilo lasemaje kuhusu thamani yao mbele ya Mungu? Je, kuna tofauti kati ya thamani ya mwanaume na thamani ya mwanamke, au mmoja alipewa thamani kuliko mwenzake?

2. Je, Mungu alikuwa na kusudi gani katika kuumba binadamu?

3. Soma 1 Wakorintho 3:16-17. Ikiwa mwili wetu ni hekalu la Mungu, tuishije?

4. Kwa njia gani tunaweza kuleta sifa na heshima kwa Mungu Baba?

5. Kama kiti cha miguu mitatu, uzima na ukamilifu ni kujifahamu wewe ni nani, na kujifahamu kusudi lako, na kujifahamu tabia yako. Kama mchungaji au kiongozi, je, ni ipi kati ya hizo tatu una mashaka au udhaifu zaidi nayo?

6. Kwa sababu gani watu katika kanisa lako wanaona ni vigumu kuelewa hayo matatu? Kwa njia gani untaweza kuwasaidia?

Page 10: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

10

Somo la 5. Roho, Nafsi, Mwili – Mtu Mzima

Imani ya Kikristo siyo dini ya kiroho tu. Inajumlisha kila sehemu ya binadamu na jamii anamoishi. Ni namna gani tunaweza kufuatilia na kudumisha Shalom ile (uzima) ambao Mungu anadhamiria kwetu? Uzima unategemea jinsi tunavyotunza uhusiano wetu na Mungu, na jinsi tunavyotunza mwili wetu, na jinsi tunavyotunza mahusiano na watu wenzetu, na jinsi tunavyotunza mazingira yetu. Utunzaji wa mwili ni muhima kama ulivyo utunzaji wa nafsi zetu. Mwili, nafsi, na akili haviwezi kutenganishwa. Mwili ni mtyu wa nje, ni jinsi tunavyohusiana na viumbe vyote. Nafsi ni mtu wa ndani, akili yetu na uchaguzi na hisia. Roho ni kinachotuunganisha na Mungu na dunia ya kiroho. Kila sehemu inaathiri nyingine, hivyo hutegemeana. Angalia uhusiano uliopo, kati ya afya ya mwili, fikira na nafsi katika Zaburi 38: 3,5,7,10,11,17.

Afya ya akili na nafsi inategemea uhusiano wetu yetu na Mungu, na uhusiano wetu na watu wengine. Tunapolea na kuutunza mahusiano hayo, hata mwili inakuwa na hali nzuri. Katika Biblia yote, upendo wa Mungu ni amri ya kwanza nao ni msingi wa uzima (Kutoka 20:3-6; Marko 12:30; Zaburi 16:11; Zaburi 37:5). Afya ya roho zetu inategemea uhusiano wetu na Baba yetu wa Mbinguni, kwani tuliumbwa kwa mfano wake, tuliumbwa kuwa na ushirika Naye, alirejesha ushirika nasi kupitia Mwana wake. Afya na ukamilifu hujengwa jinsi tunavyomruhusu Roho wa Mungu kuishi ndani yetu. Tunakuwa wazima na kujazwa na utimilifu wa Mungu, jinsi Kristo aishivyo ndani yetu, nasi tunaishi katika upendo wake (Waefeso 3:16-19; Waebrania 12:12-16). Wakati tunapokosa uhusiano na Mungu, au hatumpendi kama tunavyopaswa, tunaharibu mawasiliano naye. Tunapoasi amri alizotupa, kama mwongozo wa maisha yetu, tunavunja uhusiano naye. Uvunjifu wa uhusiano na Mungu, Muumba wetu na Baba yetu, husababisha nafsi zetu ziwe na hamu sana ya kuponywa.

Nafsi yetu ni mtu wa ndani, ni fikira, imani, hisia. Inajengwa na desturi na mazingira yetu, na matokeo yalitupata katika maisha yetu ya nyuma. Na jinsi tunavyojibua mambo mazuri au mabaya yanayotukabili katika maisha, na mwenendo wetu unaofuata, hutegemea uzima ya nafsi yetu, kama tunajibu kwa njia inayojenga au kuharibu mahusiano. Anayeweza kujibu matukio kwa njia ya uzima huwa na mahusiano mazuri na wenzake. Asiyeweza kujibu kwa njia ya uzima huharibu mahusiano yake na wengine na kupunguza uzima wa nafsi yake.

Mara nyingi mtu huyu hugeukia mambo mengine ili kujaza utupu wa nafsi yake. Anaweza kugeukia mahusiano mabaya yasiyo halali, akitegemea kusaidiwa. Au anaweza kugeukia ulevi, madawa, fedha, au ngono ili kujaza utupu wa nafsi yake. Tabia za aina hii, mara nyingi, husababisha maradhi ya nafsi, kama vile, wasiwasi, shida, msongo wa mawazo, lawama, mashaka, na ukiwa. Upo uwezekano wa kupata maradhi ya kimwili, kama vile, shinikizo la damu, vidonda vya tumbo, uzito wa ziada au uzito pungufu. Uhusiano duni au utegemezi katika madawa na ulevi, unaweza pia kusababisha magonjwa ya zinaa au matatizo ya akili.

Page 11: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

11

Maswali ya kujadaliana:

1. Je, unaweza kueleza hali ya kila sehemu 3, yaani mwili, nafsi, roho. Andika elezo fupi juu ya kila sehemu.

2. Mtu anapopokea wokovu kwa Imani, je, ni sehemu gani itabadilika zaidi, mwili wake, au nafsi yake, au roho yake? Au ni sehemu zote tatu zitabadilika? Eleza jibu lako.

3. Kwa nini ni muhimu sisi kutunza mwili wetu na kulinda afya yake, ina faida gani?

4. Soma Marko 12:28-30. Yesus alisema tumpende Mungu kwa moyo wote, na akili yote na nguvu zote. Je, inatosha ikiwa tunampenda na moyo wetu, lakine siyo kwa akili yetu? Je, tutaweza kumpenda Mungu kwa akili yetu, lakini siyo kwa nguvu yetu? Eleza jibu lako.

Page 12: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

12

Somo la 6. Kujitunza Mtu Binafsi

Ni jinsi gani tunaweza kufanikiwa au kufanya kazi ili kuufikia uzima? Kabla ya yote ni lazima tukumbuke kuwa, uzima wetu hujengwa juu ya uhusiano imara na Mungu. Na hatutakuwa na afya ya ya kiroho, wakati tunapuuza au kuharibu miili yetu. Roho zetu zitafute kwanza, uzima katika Mungu, aliyetuumba, na anayejua mapungufu na kushindwa kwetu. Lakini, anajua pia uwezo uliomo ndani yetu. Kupitia nia yetu, tunaweza kufanywa upya, tukabadilishwa tufanane na Kristo, ili tuweze kujua mapenzi yake na kumpendeza Mungu (Warumi 12:2; Waefeso 4:23; Yakabo 5:13-16). Kukiri juu ya mahitaji yetu, udhaifu wetu, dhambi na kushindwa kwetu, ni muhimu sana katika kufuatilia uzima (Mithali 3:5-7; Zaburi 6:2-9; Zaburi 38:1-11; Isaya 53:5; Isaya 32:17-18; Yakobo 5:16). Tunatafuta ushirika na Mungu kupitia imani, na kutegemea neema ya Mungu kuishi maisha yanayolingana na mapenzi yake. Ushirika huo na Mungu huhitaji muda utengwe kwa kusoma Neno lake, kuutumia muda kuwasiliana na Mungu katika maombi, na kukubali uwepo na mwongozo wake. Anapojidhihirisha kwetu, tunaitikia na kukiri dhambi zetu, kupokea msamaha wake, kutoa nafsi zetu katika mapenzi yake, na kutembea ndani ya utii wake. Hii inaruhusu Roho wa Mungu kuishi ndani yetu na kujenga afya na uzima (Waefeso 3:19; Waebrania 12:12-16).

Afya ya roho hutusaidia tabia na mwenendo, na kutuwekea msingi imara katika maamuzi na mawazo yetu (Tito 2:3-14). Pia, inatupa uhuru kutoka katika makosa na wasiwasi, tunakuwa na amani mioyoni mwetu. Uzima wa kiroho hutokana na uhusiano imara na Mungu, kupitia maisha na mwenendo ya utakatifu na utii kwa mafundisho ya Yesu. Tukiishi katika hali ya ushirikiano na Baba, twapata usalama na utayari wa kufanya mapenzi yake (Yohana 13:3-5).

Tunapokuwa na mahangaiko na wasiwasi ndani ya nafsi zetu, tunarudi kwake yeye atupaye nguvu, “na kumtwika Yeye mizigo yetu” (Zaburi 55:22; Mathayo 11:30). Ndipo Mungu hutupatia amani na furaha. Hatuwezi kujiponya sisi wenyewe. Shida na majaribu yanapotupata twajifunza kutegemea upendo wake na uwezo wake. Tunaposongwa na mambo ya maisha, tujaze mawaza yetu na sala na shukrani (Wafilipi 4:6-8). Na tuweke tumaini letu ndani ya Mungu (Zaburi 42:5; Zaburi 33:18,22), na kuwa na furaha (Mithali 15:13; 17:22; 18:14). Kuchukuliana mizigo na ndugu zetu hupunguza uzito wa mizigo (Wagalatia 6:2; Waefeso 4:25). Roho zetu hupata uzima na kuponywa jinsi tunapotambua mambo yaliyotuumiza rohoni na kusamehe, pamoja na kupokea msamaha kwa yale tuliyofanya tulipoumiza wengine. Tunaweza kuburudisha nafsi zetu tukichukua muda kwa kufanya upya nia yetu kwa njia ya kusoma, na kutakafari, na na kutathmini maisha na mawazo yetu.

Upande mwingine wa kutunza uzima ni kutunza mwili wetu. Kupitia mwili tunakutana sisi kwa sisi tena tunakutana na Mungu. Na jinsi tunapojitoa mwili kwa Mungu, hivyo tunasaidiana na kuwa vyombo vya neema kwa kila mmoja wetu (Warumi 6:13-14; Warumi 12:1). Kwa njia ya mwili, maisha ya Yesu yanadhihirika wazi kwa wengine (2 Wakorintho 4:10). Ndani ya mwili wa Kristo ulikaa utimilifu wa Mungu (Wakolosai 1:19-20; 2:9-10). Kristo anaishi ndani ya mwili wetu akitupatia imani na nguvu za ufufuo (Wagalatia 2:20). Mungu amekusudia kukaa ndani ya mwili wetu na hivyo kuonyesha upendo wake na nguvu yake kwa wengine.

Kwa vile mwili ni “hekalu la Mungu” (1 Wakorintho 3:16; 6:19; 2 Wakorintho 6:16; Waefeso 2:21), na kwa sababu tunapaswa kumheshimu Mungu kwa mwili wetu, inatubidi tuwe makini katika utunzaji wa mwili ili uwe na hali bora. Tunahitaji chakula bora, tukidhibiti aina na kiasi cha chakula. Kama tutakula kwa ulafi au tutaunyima mwili chakula, tunaharibu

Page 13: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

13

uwezo wa mwili kuwa na afya bora. Kuachana na mambo ya starehe-binafsi, kama vile, dhambi za zinaa, na ulevi na madawa, pia utalinda mwili kutokuwa na magonjwa (1 Wakorintho 6:18-20; 1 Wakorintho 10:31). Mwili pia unahitaji kipindo cha kufanya kazi, na kipindi cha kupumzika ili uwe na afya. Mungu alipanga kazi kwa Adamu na Hawa katika bustani, ikiwa ni sehemu ya maisha yao ya kila siku (Mwanzo 2:15). Lakini, hata baada ya kuanguka, Mungu alimwagiza mwanadamu, kuwa na muda wa kupumzika, ili kuurejeshea mwili nguvu (Kutoka 20:8-11). Kufanya kazi nyingi na ukosefu wa mipaka ya uzito wa kazi, mara nyingi ni mwanzo wa afya duni, kwa viongozi walio wengi. Ili kuwa na ufanisi katika huduma, ni lazima kutathmini na kuweka vipaumbele katika shughuli na kuweka uwiano mzuri ambao utaendelea kutunza afya zetu.

Maswali ya kujadaliana:

1. Kwa njia gani tunaweza kuimarisha uhusiano wetu na Mungu, yaani kutunza uzima wa roho yetu?

2. Kwa njia gani tunaweza kuimarisha nafsi yetu, yaani kuimarisha akili na nia yetu?

3. Kuna mambo gani yatadhoofisha roho yetu?

4. Kuna mambo gani yatadhoofisha akili yetu?

5. Je, tunaweze kusema kwamba dhambi za kingono, na ulevi, na utegemezi wa madawa ni dhambi za kiroho, sawa na kuwa dhambi za kimwili? Eleza jibu lako.k

6. Je, mwenendo na matendo yako yalibadilika ulipopokea wokovu? Toa mfano wa badiliko lilitokea.

7. Taja na kuandika njia tunazoweza kutunza mwili wetu ili tuwe na uzima.

Page 14: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

14

Somo la 7. Jinsia na Ngono

Hali ya jinsia ni mpango mzuri wa Mungu. Ni jinsi tulivyoumbwa na jinsi tunavyoishi duniani kama mwanaume na mwanamke. Ni nia yetu juu ya mwili wetu na mwili wa mwingine. Jinsia inahusu jinsi tunavyoingiliana na kuhusiana kama wanaume na wanawake katika maisha yote. Uzima wa kijinsia ni kuhusiana kwa heshima na usafi. Uzima wa kijinsia unatambua kwamba tunahitaji wote, wanaume kwa wanawake, ili tuwe na ukamilifu, hakuna uzima kwa moja bila mwingine. Ngono ni matendo na mahusiano ya kimwili ambayo yanastahili tu katika uhusiano wa ndoa halali. Dunia yetu inafuata mila na nia kuhusu jinsia na ngono isiyo halali wala haileti uzima. Mifano ni wanaume wanaotafuta kutawala wanawake, au wanaofanya ngono na mwingine nje ya uhusiano wa ndoa halali.

Biblia inazungumzia jinsia kwamba ni mpango wake katika uumbaji (Mwanzo 1:26-31). Mungu alitangaza kila kitu chema, mpaka hapo alipoona kwamba, Adamu hakupata miongoni mwa wanyama, ye yote wa kuwa msaidizi au mwenzi kwake. Mungu akasema “Si vema huyo mtu awe peke yake” (Mwanzo 2:18-20). Adamu alikuwa si mzima wala hajakamilika. Hakuna aliyekidhi mahitaji ya Adamu, kutoka katika ufalme wa wanyama,lakini mpango wa Mungu ulikuwa Adamu asikae peke yake. Kwa hiyo Mungu alimwumba mwanamke kutoka kwa ubavu mmoja wa Adamu (Mwanzo 2:21-22). Na Mwanamke alipoletwa kwake, akasema, “Ah! Nyama katika nyama yangu, anafanana nami!” Hakuumbwa kwa ajili ya kazi ya ngono tu, lakini alikuwa binadamu mwenzake, ambaye angeweza kusema naye, wanaweza kushirikiana na kufanya kazi pamoja. Mungu aliuuita huu uumbaji wa mwisho, kuwa ni “vema sana”. Miili yetu ya kiume na kike, iliumbwa kwa ajili ya starehe na kuzaliana katika ukamilifu wa ndoa (Mwanzo 1:24-25). Biblia hukiri kwamba upendo kati ya watu wawili ni “mzuri kupita divai” (Wimbo ulio Bora 4:10).

Mwanaume na Mwanamke pamoja waliumbwa kwa mfano wa Mungu na mwonekano wa sifa zake. Waliumbwa washirika wawe na usawa, na kupewa kazi wote sawa, ya kuwa mawakili katika dunia. Tabia na sifa za mwanamke za kuzaa, kulea, kutunza, na kujitolea kwa upendo, huonyesha sifa za Mungu (Isaya 66:9, 13). Tabia na sifa za mwanaume kama kupatia, na kuwa na nguvu, heshima na uwezo, huonyesha sifa tofauti za Mungu. Ingawaje, jamii wakati mwingine huzoea kutoa umuhimu zaidi kwa kazi za mwanaume, hali hii siyo ya kibiblia. Mithali 31 inamwonyesha mwanamke anayeshiriki kwa uaminifu na mumewe, na siyo tu mzazi na mlezi wa watoto. Katika Agano la Kale wanawake walitambuliwa kama ni washiriki kamili katika maisha ya mkutano wa agano (Kumbukumbu 29:10-11). Katika Israeli, mkutano ulijumuisha familia zote (aangalia maagizo ya Pasaka, Kutoka 12:3-4). Wanawake pia walitegemewa kuleta sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya ibada na utakaso (Walawi 12:6; 15:28-29).

Agano Jipya linakiri kuwa, mwili wa kibinadamu ni mzuri, na kiumbe cha Munge cha kupendeza, unaostahili heshima na utunzaji. Yesu Kristo ni mfano wa ukomavu wa mwanadamu katika mambo ya jinsia, yaani mahusiano ya wanaume kwa wanawake. Yesu alijikubali hali yake mwenyewe na mahali pake katika mpango wa Mungu. Alijenga mahusiano ya uzima na wote, wanaume kwa wanawake na watoto, kupitia matendo yake ya upole, lakini ya nguvu, na upendo na huduma. Aliwaponya wanawake (Luka 8:43-48), aliwaruhusu wakasema naye, walimfuata, wakamsaidia na kufanya kazi naye (Luka 10:38-42). Haya yalikuwa ni kunyime cha utaratibu wa jamii ya wakati ule walivyoishi. Yesu alihusiana na wanawake kwa sababu ni wanadamu na siyo vyombo vya ngono. Uhusiano wake kwa wanawake ulikuwa wa uzima na usafi, alijali zaidi wawe na uzima kuliko sifa zake,

Page 15: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

15

hata kama wengine walikuwa na mashaka juu ya usafi wake (Yohana 4:7; Yohana 12:3). Mara nyingi aliwaendea watu waliodharaulika katika jamii, wanawake na wanaume, na uhusiano wake na watu haukuwa na upendeleo wa hali ama cheo, bali ulikuwa sawa kwa wote. Yesu alitoa ujumbe wa Mungu wa uumbaji, msamaha, uponyaji na upendo kwa watu wote. Katika mafundisho yake, na katika mifano na hadithi na miujiza, aliyonyesha kwamba anawajali wanawake (Luka 21:1-4; Mathayo 25:1-13; Luka 18:1-8; Luka 11:27-28).

Maswali ya kujadaliana:

1. Kwa sababu gani Mungu aliwaumba binadamu mwanaume na mwanamke?

2. Baada ya Mungu kuumba binadamu kwa mfano wake, mwanaume na mwanamke, aliona kwamba “ni chema sana” (Mwanzo 1:31). Je, unakubali kuwa ni “chema sana”?

3. Wakati mwingine mtu anaweza kufikiri kwamba mwili wake ni kitu cha aibu. Unavyoona, kuna sababu gani?

4. Toa mifano katika maisha ya Yesu jinsi alivyokuwa na nia nzuri kuhusu jinsia.

5. Taja mifano unavyoona katika dunia yetu ya nia isiyo nzuri kuhusu jinsia.

6. Utawezaje kufundisha na kujenga nia bora kuhusu jinsia katika kanisa lako?

7. Tunawezaje kujenga nia ya heshima na usawa kati ya wanaume na wanawake katika makanisa yetu?

Page 16: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

16

Somo la 8. Ndoa

Mahusiano kati ya wanaume na wanawake yanakuwa ya aina nyingi. Wakati mwingine uhusiano ni urafiki tu, wakati mwingine ni wa uchumba, wakati mwengine ni wa kuonana, wakati mwingine ni wa kujamiiana tu. Uhusiano wa kujamiiana ni maalum, hufanyika katika mazingira na hali fulani, na hivyo hufahamika kuwa ni “uhusiano wa ukaribu.” Lakini ukaribu huo si tendo la kimwili tu, ukaribu ni kufahamiana katika roho zetu, kumfahamu mwenzako kwa ndani na katika moyo wake. Ngono ni tendo la kimwili, lakini inagusa roho ya mtu kwa ndani zaidi. Huo ukaribu wa kweli unajumuisha kushirikishana, kuaminiana, kupendana, kuelewana, kukubaliana na kuwekana wazi, katika mambo kati yao wawili.

Mungu alituumba na hitaji la ukaribu wa kweli. Tatizo ni kwamba watu wengi wanaelezea ukaribu wa aina moja tu, ukaribu wa kujamiiana. Lakini tamanio la ukaribu hauwezi kuridhishwa kwa njia ya mahusiano la kimwili tu. Ukaribu usio na heshima kwa mwingine ni ukaribu uliopotoka. Ukaribu wa kujamiiana unaridhisha tu kama ni juu ya msingi wa ukaribu wa roho na moyo. Hakika, mara nyingi uhusiano utachafuka na roho ya mtu kuharibika endapo hali ya kujamiiana ilitokea nje ya uwenza katika ndoa.

Ni muhimu kuweka mipaka ya kuongoza mahusiano kati ya wanaume na wanawake katika mambo ya ukaribu. Kwa maneno au kwa matendo yetu, tunaweza kutuma ujumbe wa kijinsia, kwa kusudi au si kwa kusudi, lakini unatuingiza katika ukaribu na matendo yasiyo sahihi wala ya uzima. Hivyo Wanaume na wanawake wanajenga uhusiano juu ya msingi wa uzuri na mvuto wa mwili tu unaowaingiza katika ukaribu wa kingono bila ukaribu wa kweli wa roho. Ni wajibu wa kanisa kufundisha na kutoa mifano ya mipaka katika mambo ya kijinsia inayoleta uzima. Kwa njia ya mawasiliano yaliyo wazi na kweli kuhusu mambo ya jinsia na ngono, tutajenga uzima katika jamii na jamaa zetu.

Maandiko yafuatyo yanaweka misingi ya kibiblia juu ya hali na tabia za ukaribu, inatuongoza kuhusu mahusiano yetu:

Mwanzo 2:24. Ndoa ni kuacha, kuambatana, na kuwa mwili mmoja.

Mithali 5:18-21. Baraka ya uaminifu katika ndoa.

Mithali 18:22. Apataye mke apata kitu chema, naye ajipatia kibali kwa Mungu.

Wimbo ulio Bora 4:10. Upendo wa kweli na halali hupendeza na kuridhisha.

1 Wakorintho 6:13,15-20. Mwili ni wa Bwana na ni hekala la Roho Mtakatifu, wala si kwa zinaa wala uasherati.

Waefeso 5:28-33. Uhusiano wa upendo kati ya mume na mke ni mfano wa uhusiano wa Kristo na Kanisa.

Wagalatia 5:16-24; 6:8. Epuka matendo ya mwili, panda tunda la Roho.

2 Wakorintho 6:14-15. Epuka fungamano lisilo sahihi, yaani ukaribu wa ndani kati ya anayeamini na asiyeamini.

Mithali 2:16-19; 5:3-9; 7:1-27; 1 Wakorintho 10:7-8 Maonyo dhidi ya uasherati.

Kanuni tatu za kibiblia kuhusu ndoa zenye afya:

Ujifunze na kumfahamu mtu kiroho, kiakili, na kimoyo kabla ya kuoana. Oana na mtu ambaye mnashabihiana, katika fikira na malengo yenu. Kuza ukaribu wa kiroho na kimoyo kabla ya ukaribu wa kimwili.

Usioane na asiyeamini (2 Wakorintho 6:14-15).

Page 17: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

17

Usijamiiane kabla ya ndoa (Mwanzo 2:18). Kuacha nyumba ya wazazi bora kutangulia kujamiiana. Kujamiiana kwanza, kabla ya ndoa, huweka mkazo juu ya uhusiano wa kimwili baadala ya ukaribu wa kiroho na kimoyo.

Uaminifu katika ndoa hutia hali ya usalama iliyo msingi wa ndoa yenya afya. Kukosa uaminifu katika uhusiano wa ndoa ni sababu kubwa ya ndoa isiyo imara na isiyoridhisha

Maswali ya kujadaliana:

1. Je, toa mifano katika maisha yetu ya kawaida tunapohusiana wanaume kwa wanawake. Katika kila mfano, ni ukaribu wa aina gani unastahili na kufaa?

2. Kwa nini ni hatari kujenga uhusiano juu ya mvuto wa kimwili tu?

3. Je, nini msingi wa ukaribu wa kingono wenye uzima na kuridhisha?

4. Kwa nini Biblia inaonya juu ya ndoa kati ya mwamini na asiyeamini?

5. Wanaovunja ndoa yao kwa uzinzi au uasherati, je, wanatoa sababu gani? Na kufuatana na Biblia, je, sababu hizo ni za haki?

6. Ongea kuhusu njia kanisa lako linaweza kutoa mafundisho juu ya ndoa na mahusiano yanayoleta uzima.

Page 18: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

18

Somo la 9. Uzima katika Jamii – Kutunzana

Mungu anatuita, tukulete uzima na ukamilifu, yaani Shalom, katika dunia yetu. Alituumba tuwe na hamu ya uhusiano na wengine, kuwajali na kuwapenda wengine – ni sehemu ya mfano na sura ya Mungu ndani yetu. Hatuishi katika upweke mbali na wengine, bali katika mahusiano na familia, marafiki, na watu wengineo nyumbani, kazini, na katika maisha yetu ya kila siku. Tunaishi katika jamii.

Katika Agano la Kale, Mungu aliweka miongozo kwa ajili ya watu wake, ili kuijenga na kutunza afya na uzima katika jamii zao. Mahusiano kati yao na utii kwa sheria za Mungu yalikuwa msingi wa afya yao. Sheria kwa Waisraeli zinazoitwa Amri Kumi zilikuwa miongozi ya kimsingi kwa maisha yao ya kijamii (Kutoka 20:1-17). Mungu alisema kama wataisikia sauti ya Bwana, atawaepusha na magonjua ya Wamisri (Kutoka 15:26). Alisema atawabariki Israeli, ikiwa watamtii, na kuwaadhibu wasipomtii (Walawi 26:1-39; Kumbukumbu 28:1-68). Mungu pia alitoa maagizo kwa watu wake, waangalie mahitaji ya maskini, yatima, wajane na wageni (Kumbukumbu 10:17-19; 14:28-29). Hadithi ya Ruthu na Boazi katika kitabu cha Ruthu ni mfano halisi wa jinsi sheria hizi zilivyotekelezwa katika jamii yao (Ruthu 2:1-23).

Mpango wa Mungu wa kutunza uzima miongoni mwa watu, umeelezwa vizuri katika maagizo ya Mika, kwa wana wa Israeli, “Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na Bwana anatake nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako” (Mika 6:8). Mungu hupendezwa zaidi na huduma yetu kwa maskini, kwa wanaoonewa, na kwa wanaokataliwa, kuliko jitihada zetu za ibada ya unyenyekevu na fufunga (Isaya 58:6-14). Mungu anaheshimu hudumua yetu kwa wengine, kuwa ni aina ya ibada iliyo ya hali ya juu, iliyokamilika.

Mafundisho ya Yesu. Yesu alithibitisha Agano la Kale katika jibu lake la swali la Mfarisayo alilyeuliza kuhusu amri iliyo kuu. Akawaambia, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri kuu, tena ni ya kwanza, na ya pili yanafanana nayo, nayo ni hii: mpende jirani yako kama nafsi yako” (Mathayo 22: 35-40). Upendo wa Yesu kwa Mungu ulimvuta kupenda na kutumikia wenye shida. Yesu aliwakuta watu hapo walipohitaji, kama ya kimwili, ya kiroho au ya kijamii. Aliwahudumia akiwaponya na kuwapa uzima (Marko 1:21-27; Marko 2:1-12; Yohana 4:7-26; Yohana 5:5-9). Aliwaruhusu watu wakaja kwake, wakamgusa na kumwuliza maswali. Aliwasikiliza, akasikia na kuwajali juu ya mahitaji yao. Aliwakubali na kuwaona wastahili muda wake. Hivyo watu wanapohisi kuwa usalama upo, na kwamba wanakubalika na wanapendwa, wanaachana na vikwazo vya woga na kutoaminiana, ambavyo husababisha ukosefu wa uhusiano mzuri na wengine. Hivyo wanakuwa huru na kujiweka wazi kwa uponyaji wa mwili na wa roho. Hivyo, Kristo ni mfano wetu.

Jamii ya Mungu. Sisi tulio wafuasi wake, tunatakiwa pia kufuata wito wake na kuleta uzima kwa wengine – kuwaponya waliovunjika moyo, kuwaacha huru waliosetwa, na kuwahubiri maskini habari njema (Luka 4:18-19). Sisi wenyewe tukifanywa wazima kupitia uhusiano wetu na Kristo, tunawaendea wengine na kuwaletea neon la uzima. Pamoja twaunda ushirikiano wa watu wenye uhusiano sisi kwa sisi, na pia kwa Mungu (Waefeso 4: 14-16). Wakati mwingine, ushirika huo huitwa “familia ya Mungu.” Tunakuwa viungo katika mwili wa Kristo (Waefeso 4:25). Ikiwa tumeunganishwa na imani yetu katika Yesu, wajibu wetu ni zaidi ya uhusiano wa kiroho na Mungu tu. Tumeagizwa kuwapenda na kuwahudumia wengine (Wagalatia 5:13-14). Imani yetu inaonekana hata katika kuonyesha upendo kwa maadui yetu (Mathayo 5:43-48; Warumi 12:20).

Page 19: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

19

Maisha ya uzima hufuata uvumilivu, wema na upole kwa wote, wanaopendeka, na wasiopendeka. Mungu anataka tuwapende wengine wote, kama tuanvyojipenda nafsi zetu (Marko 12:31; Wafilipi 2:4; Waefeso 4:23-5:2). Hii inawezekana tu, kama kila mara tutafanya roho zetu upya katika ushirika na Mungu, Baba yetu. Tunapokuwa na uzoefu wa neema ya Mungu, msamaha na upendo, tunaweza pia kishi na kufanana na Mungu, katika haki ya kweli na utakatifu (Waefeso 4:24). Wakati Mungu anatuvuta kwake, nasi tunamkubali na kukubaliana sisi kwa sisi, ndipo Mungu huishi ndani ya uhusiano wetu. “Sisi tunajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho” (Waefeso 2:22). Upendo wa Mungu uliomo ndani yetu ni ushuhuda kwa wale wote wanaotuzunguka, na huvuta wengine kuingia katika familia ya Mungu.

Angalia mistari ifuatayo kuhusu injili na jinsi inavyojenga mahusiano:

Katika kanisa la mitume, watu walikula pamoja na kushirikisha vitu vyao, kwa manufaa ya wengine (Matendo 2:44-47; 4:32-34).

Kuwa mvumilivu kwa maoni ya wengine, kwa utamaduni na desturi tofauti, na kutafuta kuwa na amani na watu wote (Warumi 14:4-21).

Kristo ndani yetu anatutaka tuishi kwa heshima, kufarijiana na shukurani (1 Wathesalonike 5:12), na kuridhika (Wafilipi 4:11; 1 Timotheo 6:7), na kutenda mema kwa kutoa mali zetu (1 Timotheo 6:18; Mathayo 6:19).

Mahusiano duni au mabaya ni aina ya ugonjwa, ambao mara nyingi, huleta afya duni kwa watu binafsi,kwa jamaa na jamii. Paulo aliwaambia Wagalatia, “Lakini mkiumana na kulana, angalieni, msije mkaangamizana” (Wagalatia 5:15). Ugomvi, vita, wivu, na uchoyo ni mifano ya maradhi ya kijamii, yanayoharibu uhusiano wetu, na kuangamiza dhamira ya Mungu ya Shalom na uzima katika uumbaji wake. Angalia madhara hayo katika hadithi ya Kaini na Habili (Mwanzo 4:8-12). Mahusiano duni husababisha kutokuajibika katika kazi za nyumbani, kama vile, ukosefu wa utunzaji wa watoto na wazee. Pia yanaweza kuwa chanzo cha vurugu na mvutano katika ndoa, kazini, katika mashirika na hata kanisa makanisa. Endapo watu wataishi kwa faida yao na kudai haki zao tu, na wakichukua mali ya wengine bila kujali mahitaji ya wengine, matokeo yake ni mgawanyo wa vitu na shughuli usio wa haki. Wakati watu watahesabu wengine kuwa na thamani au heshima kuliko wengine, haya yote husababisha umaskini, njaa, na utumwa.

Uzima wa Milele. Ni lazima tukumbuke kuwa, njia za maisha tunazoishi sasa, zinatoa mwelekeo wa maisha ya baadaye (baada ya kifo). Soma na kufikiria hadithi ya tajiri na Lazaro (Luka 16:19-31). Tajiri hakujali mahitaji ya maskini aliyekaa langoni kwake wakati wa maisha yake duniani, hali hii ilimpeleka kuzimu. Katika hukumu ya mataifa (Mathayo 25:31-46), Yesu anaelezea huduma iliyotolewa kwa wengineo, kama kuwalisha wenye njaa, kuwakarimu wageni, kuwatembelea wagonjwa na walio magerezani, wakahesabiwa kuwa na haki na kupewa thawabu.

Uzima wa milele, au uzima tele, huanza sasa katika uhusiano wetu kati yetu na Mungu. Kumpenda Mungu kwa moyo, roho, akili, na nguvu, na kupenda jirani kama mwenyewe, ni uzima wa milele. Wale wasiofuata makusudi ya Mungu wataadhibiwa milele (Yohana 3:16; Yohana 5:24-29; Warumi 6:23; 1Timothei 2:5-6; Ufunuo 20:12-15; Ufunuo 21:27).

Page 20: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

20

Maswali ya kujadaliana:

1. Je, Agizo Kumi bado zinaweza kuleta faida tukizifuata katika mahusiano ya dunia yetu leo?

2. Soma Mika 6:8 na Isaya 58:6-14. Je, Mungu anadai nini kwetu wakati tunapoona mtu mwenye shida? Je, huduma yetu kwa wengeni inaweza kuwa kipimo cha hali yetu ya kiroho?

3. Je, Yesu alionyesha upendo wake kwa wenye shida kwa njia zipi? Taja mifano.

4. Taja mambo machache yanayoharibu uzima ya kijamii katika dunia ya leo.

5. Ongea kuhusu jinsi kanisa lako linaonyesha upendo kwa Mungu na kwa wenye shida.

Page 21: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

21

Somo la 10. Kutunza Uumbaji – Uzima wa Mazingira

Kama tunaelewa kwamba, Mungu aliumba nchi na vitu vyote vilivyomo, ikiwemo nchi, manyasi na miti, wanyama na wanadamu, tutakiri pia, kama Mungu ni Mmiliki Mkuu wa vyote alivyoumba. Wanadamu tuliumbwa kama sehemu ya asilia kwani tulumbwa kutoka ardhini na kupewa kazi na Mungu ya kuitunza ardhi, kuijaza nchi na kuitiisha (Mwanzo 1:28; Mwanzo 2:15). Maagizo ya kwanza kwa mwanadamu yalikuwa: “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha, mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi (Mwanzo 1:28). Mwanadamu alipokabidhiwa utawala juu ya nchi hakupewa haki ya kutumia uumbaji kwa malengo yake binafsi. Alipewa wajibu wa kuithamini na kuitunza. Binadamu alwajibika kwa Mungu kuhusu nchi. Alipewa kumwakilishi Mungu kuutunza na kuupenda ulimwengu ulioumbwa na Mungu. Mungu alimweka mwanadamu katika Bustani ya Edeni, ailime na kuitunza (Mwanzo 2:15). Alipewa kila mche na mti kwa ajili ya chakula, yeye na wanyama (Mwanzo 1:29-30), isipokuwa alikatazwa kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya (Mwanzo 2:16-17). Sheria iliwekwa kuhusu mti huo, kwa sababu Mungu alijua matokeo yake yangekuwa mabaya. Wakati Adamu na Hawa walipojaribiwa na nyoka na kuasi maagizo ya Mungu, ndipo uhusiano ulivunjika na Mungu. Walifukuzwa kutoka katika bustani, laana ikawekwa juu ya nchi na kwa wanyama. Ulimaji wa ardhi ukawa ni mgumu na wa kitatanisha, baada ya dhambi kuingia ulimweguni, Adamu akaambiwa, atakula chakula kwa jasho lake. (Mwanzo 3:14-19).

Dhambi ile ya Adamu na Hawa pia iligusa jamaa yao. Kaini alilima ardhi na kuleta sadaka kutoka kazi yaka badala ya sadaka iliyotakiwa na Mungu. Mungu alikataa sadaka ya Kaini na Kaini akamkasirikia nduguye, naye akamuua. Kaini alimwaga damu isiyo na hatia katika ardhi, na hivyo kuichafua ardhi, na “haitakupa mazao yake” (Mwanzo 4:12). Jinsi wanadamu walivyozaaliana na kuongezeka, ndivyo dhambi zao zilileta dhuluma zaidi juu ya nchi, mpaka Mugu akaamua kuiangamiza nchi kwa gharika. Mungu akamwokoa Nuhu na jamaa yake tu, na viumbe hai vyenye mwili, viwili vya kila namna (Mwanzo 6:1-8:19). Mungu akafanya agano na Nuhu baada gharikas hiyo akaahidi kutoangamiza kamwe dunia kwa gharika tena. Agano hilo lilithibitisha upendo wa Mungu kwa uumbaji wake na mpango wake wa kuukomboa. Hadi leo hii, Mungu bado anaendeleza na kutekeleza kazi yake ya ukombozi wa uumbaji wake wote, wa dunia na wa mwanadamu (Warumi 8:22-23).

Baada ya gharika, ardhi ilikuwa ni muhimu sana kwa watu wa Mungu. Ahadi ya Mungu kwa Ibrahamu ilihusu suala la ardhi. Kanaani ilikuwa “ni nchi ya ahadi” kwa Waisraeli baada ya kutoka Misri na kutembea jangwani. Mungu altoa maagizo maalum kwao, juu ya kuishi katika nchi, na jinsi ya kuitumia, na kukumbuka kuwa, Mungu ndiye mmiliki wa ardi. Katika Agano la Kale, Mungu alijali sana mahitaji ya watu wake, aliwapa chakula. Kwa mfano, Yusufu katika Misri (Mwanzo 47:12) na alitoa mana kwa Waisraeli jangwani (Kutoka 16:1-31). Mungu aliwapa walichohitaji, aliwaonya wasihodhi wala kula wa ulafi. Aliwapatia maji jangwani (Kutoka 15:22-25). Na Mungu aliwapa sheria kuhusu chakula ili kuwalinda afya yao (Walawi 11:1-47).

Mungu alidhamiria mwanadamu aishi kwa amani na mali-asili, kama kwa mfano mimea, wanyama, ardhi na maji, na kwamba ardhi izalishe kutosheleza watu wote ulimwenguni. Katika karne zilizopita, sisi wandamu tumetumia vibaya utawala tuliopewa juu ya uumbaji. Tumeona wajibu wetu kama kibali cha kufanya lolote tunalopenda juu ya rasilimali zilizopo. Ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa na ujenzi, bila kupanda miti mingine. Bila miti,

Page 22: Maisha ya Uzima - equip4change.orgequip4change.org/pdf/swahili/level2/Maisha-ya-Uzima.pdf · hutawala dunia yetu, ikisababisha magonjwa, na kuharibu maelewano kati yetu na wenzetu,

MAISHA YA UZIMA

Diocese-Based TEE, Kanisa la Mennonite Tanzania, Kenya Mennonite Church ©2014 Joseph Bontrager

22

ardhi inachukuliwa na mvua mzito, na mashamba yanageuka kuwa jangwa. Tumechafua maji na mito na hivyo kusambaza magongwa. Matatizo hayo yanazidi hali idadi ya watu inavyoongezeka.

Mfano mwingine wa matumizi mabaya ya rasilimali in kutumia ngano kwa kutengeneza vinywaji kama pombe na tumbako kwa sigara. Hizo huharibu afya ya kimwili na kiroho na kusababisha matatizo mengi katika jamii (Mwanzo 9:20-22; Kutoka 32:6).

Mara nyingi usimamizi mbaya wa mali asili ya ardhi na maji, ni chanzo cha upugufu na ukosefu wa rasilmali hizo, ambao huleta ugawaji usio wa usawa kati ya wenye uwezo na maskini.

Matokeo ya umaskini ni uonevu na urejeshaji usio wa haki wa ruzuku ya bidhaa na huduma. Agano Jipya linatutaka Wakristo kuwajibika katika suala la ugawaji sawa wa rasilmali na kushirikishana katika jamii zetu (2 Wakorintho 8:13-15). Hili limejadiliwa hapo juu katika somo la 9.

Sisi ni mawakili wa uumbaji wa Mungu. Mtazamo sahihi wa uwakili pamoja na kujua mahitaji ya dunia, ungetuamsha na kujenga uwajibikaji wa rasilimali zilizopo,na kujiunga na Mungu katika ukombozi na uzima uliopangwa na Mungu kwa ajili ya uumbaji wake.

Maswali ya kujadaliana:

1. Je, Mungu alikuwa na mpango gani kwa binadamu ili awe na uhusiano gani na uumbaji wake?

2. Mungu alipoumba dunia aliona “ni vema.” Je, ilitokea nini uumbaji uligeuka kuwa si vema?

3. Mungu aliumba dunia tuwe na vyote tunavyohitaji. Kwa nini dunia yetu inakosa haki na umaskini umezidi?

4. Eleza jinsi Mungu anataka leo tutunze dunia yetu na uumbaji wote.

5. Taja mifano ya matatizo yaliyotokea kwa sababu ya uwakili mbaya ya dunia.

6. Je, sisi wa kanisa tunfanye nini kuongeza nguvu na kutia moya watu wetu ili tutunze dunia na rasilimali tuliyo nayo?


Recommended