+ All Categories
Home > Documents > Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta...

Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta...

Date post: 26-Feb-2020
Category:
Upload: others
View: 10 times
Download: 0 times
Share this document with a friend
31
Candidate session number Numéro de session du candidat Número de convocatoria del alumno N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q Swahili B – Higher level – Paper 1 Swahili B – Niveau supérieur – Épreuve 1 Swahili B – Nivel superior – Prueba 1 © International Baccalaureate Organization 2015 13 pages/páginas 8815 – 2315 Question and answer booklet – Instructions to candidates Write your session number in the boxes above. Do not open this booklet until instructed to do so. This booklet contains all the paper 1 questions. Refer to the text booklet which accompanies this booklet. Answer all of the questions in the boxes provided. Each question is allocated [1 mark] unless otherwise stated. The maximum mark for this examination paper is [60 marks]. Livret de questions et réponses – Instructions destinées aux candidats Écrivez votre numéro de session dans les cases ci-dessus. N’ouvrez pas ce livret avant d’y être autorisé(e). Ce livret contient toutes les questions de l’épreuve 1. Référez-vous au livret de textes qui accompagne ce livret. Répondez à toutes les questions dans les cases prévues à cet effet. Sauf indication contraire, chaque question vaut [1 point]. Le nombre maximum de points pour cette épreuve d’examen est de [60 points]. Cuaderno de preguntas y respuestas – Instrucciones para los alumnos Escriba su número de convocatoria en las casillas de arriba. No abra este cuaderno hasta que se lo autoricen. Este cuaderno contiene todas las preguntas de la prueba 1. Consulte el cuaderno de textos que acompaña a este cuaderno. Conteste todas las preguntas en las casillas provistas. Cada pregunta vale [1 punto] salvo que se indique lo contrario. La puntuación máxima para esta prueba de examen es [60 puntos]. 1 h 30 m Monday 9 November 2015 (afternoon) Lundi 9 novembre 2015 (après-midi) Lunes 9 de noviembre de 2015 (tarde) 16EP01 N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q – 2 – Kifungu A — Nyama ya Mbuzi ya Kukaanga Jibu maswali yafuatayo. Tumia aya ya kwa majibu yako. 1. Ni kifungu gani kinachoonyesha kuwa nyama ya mbuzi ni miongoni mwa vyakula vinayopendwa na watu wa pwani ya Kenya? .......................................................................... 2. Ni mawazo yapi mawili yametolewa kuhusu kuliwa kwa nyama ya mbuzi? [alama 2] (a) ..................................................................... (b) ..................................................................... 3. Aghalabu ni neno lipi husemwa kuhusiana na ulaji wa nyama ya mbuzi? .......................................................................... 4. Ni kwa nini aghalabu watoto hawali nyama ya mbuzi? .......................................................................... Chagua jibu muafaka. Andika herufi kwenye kisanduku ulichopewa. Tumia aya ya na kwa majibu yako. 5. Kulingana na kifungu hiki ni kauli gani iliyo sahihi kuhusu nyama ya mbuzi? A. Kuna njia moja tu ya kutayarisha myama ya mbuzi. B. Namna moja ya kutayarisha nyama ya mbuzi ni kutumia mafuta machache. C. Kukaanga ni namna moja ngumu ya kutayarisha nyama lakini ya haraka. D. Nyama ya kukaanga ni ngumu kwa watoto kuila. 6. Wakati wa kutayarisha nyama ya mbuzi… A. chumvi nyingi hutumiwa. B. chumvi kiasi kinachoridhisha hutumiwa. C. vitunguu saumu vilivyopondwa kijiko kimoja na nusu cha kulia hutumiwa. D. vitunguu saumu vilivyopondwa havitumiwi hata kidogo. 16EP02
Transcript
Page 1: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

Candidate session numberNuméro de session du candidat

Número de convocatoria del alumno

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

Swahili B – Higher level – Paper 1Swahili B – Niveau supérieur – Épreuve 1Swahili B – Nivel superior – Prueba 1

© International Baccalaureate Organization 201513 pages/páginas8815 – 2315

Question and answer booklet – Instructions to candidates

• Write your session number in the boxes above.• Do not open this booklet until instructed to do so.• This booklet contains all the paper 1 questions.• Refer to the text booklet which accompanies this booklet.• Answer all of the questions in the boxes provided. Each question is allocated [1 mark] unless

otherwise stated.• The maximum mark for this examination paper is [60 marks].

Livret de questions et réponses – Instructions destinées aux candidats

• Écrivez votre numéro de session dans les cases ci-dessus.• N’ouvrez pas ce livret avant d’y être autorisé(e).• Ce livret contient toutes les questions de l’épreuve 1.• Référez-vous au livret de textes qui accompagne ce livret.• Répondez à toutes les questions dans les cases prévues à cet effet. Sauf indication

contraire, chaque question vaut [1 point].• Le nombre maximum de points pour cette épreuve d’examen est de [60 points].

Cuaderno de preguntas y respuestas – Instrucciones para los alumnos

• Escriba su número de convocatoria en las casillas de arriba.• No abra este cuaderno hasta que se lo autoricen.• Este cuaderno contiene todas las preguntas de la prueba 1.• Consulte el cuaderno de textos que acompaña a este cuaderno.• Conteste todas las preguntas en las casillas provistas. Cada pregunta vale [1 punto] salvo que

se indique lo contrario.• La puntuación máxima para esta prueba de examen es [60 puntos].

1 h 30 m

Monday 9 November 2015 (afternoon)Lundi 9 novembre 2015 (après-midi)Lunes 9 de noviembre de 2015 (tarde)

16EP01

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 2 –

Kifungu A — Nyama ya Mbuzi ya Kukaanga

Jibu maswali yafuatayo. Tumia aya ya kwa majibu yako.

1. Ni kifungu gani kinachoonyesha kuwa nyama ya mbuzi ni miongoni mwa vyakula vinayopendwa na watu wa pwani ya Kenya?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

2. Ni mawazo yapi mawili yametolewa kuhusu kuliwa kwa nyama ya mbuzi? [alama 2]

(a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

3. Aghalabu ni neno lipi husemwa kuhusiana na ulaji wa nyama ya mbuzi?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

4. Ni kwa nini aghalabu watoto hawali nyama ya mbuzi?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Chagua jibu muafaka. Andika herufi kwenye kisanduku ulichopewa. Tumia aya ya na kwa majibu yako.

5. Kulingana na kifungu hiki ni kauli gani iliyo sahihi kuhusu nyama ya mbuzi?

A. Kuna njia moja tu ya kutayarisha myama ya mbuzi. B. Namna moja ya kutayarisha nyama ya mbuzi ni kutumia mafuta machache. C. Kukaanga ni namna moja ngumu ya kutayarisha nyama lakini ya haraka. D. Nyama ya kukaanga ni ngumu kwa watoto kuila.

6. Wakati wa kutayarisha nyama ya mbuzi…

A. chumvi nyingi hutumiwa. B. chumvi kiasi kinachoridhisha hutumiwa. C. vitunguu saumu vilivyopondwa kijiko kimoja na nusu cha kulia hutumiwa. D. vitunguu saumu vilivyopondwa havitumiwi hata kidogo.

16EP02

Page 2: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 3 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

7. Kutokana na kauli A hadi J, chagua kauli nne ambazo ni sahihi kulingana na kifungu hiki. Andika jibu mwafaka kwenye kisanduku ulichopewa. Tumia aya ya hadi kwa majibu yako. [alama 4]

Mfano: A

A. Baada ya kukata na kuosha nyama ya mbuzi weka kwenye sufuria utakayoipikia.

B. Unastahili kuchanganya vyema viungo ili vienee kwa nyama.

C. Ongeza maji ya kutosha kwenye nyama.

D. Usigeuze nyama punde inapoanza kuchemka.

E. Viungo vingi husaidia ladha ya awali ya nyama.

F. Viungo vya kutosha huchangia ladha ya awali ya nyama.

G. Ukitumia viungo vitasaidia kuondoa harufu ya mbuzi na kuimarisha ladha ya nyama.

H. Unastahili kutumia tangawizi iliyopondwa au ya unga.

I. Unaweza kuhepa kutafuna viungo iwapo utatumia tangawizi iliyopondwa au ya unga kwenye nyama.

J. Nyama ya mbuzi huweza kuliwa na chochote.

16EP03

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 4 –

Kifungu B — Maajabu Ya Dunia: Nyumbu Wathibitisha “Nyumbani” Kwao Ni Serengeti

Jibu maswali yafuatayo. Tumia aya hadi kwa majibu yako.

8. Kulingana na kifungu hiki, nyumbu walikuwa wakirudi wapi?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

9. Nyumbu walikuwa wameenda kufanya nini nchini Kenya?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

10. Ni kifungu gani kinamaanisha kuwa watalii wengi huvutiwa kuona nyumbu ana kwa ana?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

11. Ni kifungu gani cha maneno kinachoweza kutumiwa kuelezea kinyume cha: mtalii mmoja alikasirishwa na kile alichokitazama kwa macho yake?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

16EP04

Page 3: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 5 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

Kwa kutumia aya ya , ni maneno gani au vifungu gani vinamaanisha yafuatayo:

Mfano: sudi

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . bahati . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

12. kuona

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

13. kupendeza

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

14. inafahamika

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

15. miujiza

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

16EP05

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 6 –

Kauli zifuatazo zilizopo hapa chini ni kweli (K) au si kweli (S) kulingana na aya ya hadi . Chagua jibu mwafaka. Kama ni kweli andika [K] kama si kweli andika [S] kwenye kisanduku pembeni mwa kila sentensi. Thibitisha jibu lako kwa kunukuu sehemu mwafaka kutoka kwa kifungu. Majibu yote mawili yanatakikana kwa alama moja. Ya kwanza imetolewa kama mfano.

Kweli Si kweli

Mfano: Watalii walikuwa na nia ya kujiburudisha kwa kuona wanyama. K

Thibitisho: . . . . . . . . Walitaka kufurahisha nyoyo zao kwa kushuhudia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . makundi ya nyumbu yakihama. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

16. Kenya na Tanzania zimekuja pamoja katika shughuli ya kulinda mto Mara na mazingira yake.

Thibitisho: . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

17. Watalii huchukua wakati mwingi kuona namna nyumbu wanavyosaidiana mawazo ya kuvuka mto Mara.

Thibitisho: . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

18. Viboko ni tisho kubwa inayowapata nyumbu.

Thibitisho: . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

19. Wakati mwingine nyumbu wanapoona kuna hatari majini huendelea na safari yao.

Thibitisho: . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

16EP06

Page 4: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 7 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

Linganisha mwanzo na mwisho wa sentensi. Tumia aya ya kwa majibu yako.

Mfano: Meneja wa Uhusiano wa Shirika la Hifadhi ya Taifa E

20. Wanyama…

21. Mto Mara…

A. asema wageni wamekuja kuona mto Mara na wanyama.

B. ni pahali panapopendeza kwa wanyama.

C. huvuka mto Mara kuanzia asubuhi hadi jioni.

D. wanyama hawaachi kuvuka mto Mara.

E. alinena kuwa wageni wengi wamejitayarisha kuja kuwaona wanyama.

F. ni kikwazo kikuu kwa wanyama wanaovuka mto huo.

16EP07

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 8 –

Kifungu C — Hongera Kampuni Mashuhuri Kufadhili Mashindano Ya Ngoma Za Kisukuma

Linganisha kila mojawapo wa meneno yafuatayo kutoka kwenye kifungu na neno mwafaka linalokaribiana maana nalo. Andika herufi kwenye kisanduku ulichopewa. Umefanyiwa sentensi moja kama mfano. Zingatia: kuna majibu zaidi kuliko yale unayohitaji. Tumia aya ya kwa majibu yako.

Mfano: nikiyashutumu B

22. yamejikita

23. yamezagaa

24. tija

25. miradi

A. shughuli

B. nikiyalaumu

C. yameegemea

D. mali

E yamekuwa

F. yameenea

G. tangaza

H faida

I. maendeleo

J. nikiyashuku

Chagua jibu au kauli sahihi kutoka kwa kifungu itakayomaanisha yafuatayo. Zingatia aya ya hadi kwa majibu yako.

Mfano: Kwa wakati huu mambo yameanza kuwa tofauti…

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . kwa sasa hali hii imebadilika. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

26. Makampuni mengi yamekuwa yakitia juhudi sana katika kutoa fedha za shughuli za kimaendeleo pia.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

27. Tukishughulikia tu umaridadi na starehe hatutafua dafu.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

28. Mwandishi amechangamshwa mno na taarifa za mchango wa kampuni moja maarufu.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

16EP08

Page 5: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 9 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

29. Wengi wetu tumepuuza utamaduni na lugha zetu.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Chagua jibu muafaka. Andika herufi kwenye kisanduku ulichopewa. Tumia aya ya na kwa majibu yako.

30. Zitasaidia “japo kutukumbusha” ina maana gani?

A. Zitasaidia kutukumbusha angalau. B. Zitasaidia kwa kiasi kikubwa kutukumbusha. C. Zitasaidia kutukumbusha mengi. D. Zitasaidia kutukumbusha.

31. “Tulikuwa watu huru kifikira” ina maana gani?

A. Walikuwa wanafikiria juu ya uhuru wao. B. Walikuwa wanafanya mambo yao bila kuingiliwa. C. Walikuwa wanaingiliwa wanapofanya mambo yao. D. Walikuwa hawana uhuru wa kufikiria.

32. “Bila shaka makampuni mengine yataiga mfano wenu” ina maana gani?

A. Kwa hakika yatafuata na kutenda hivyo. B. Kuna wasiwasi kuwa yatafuata mfano wao. C. Yatakuwa na shida kuwafuata. D. Yatafuata kwa wasiwasi.

16EP09

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 10 –

Kifungu D — Msichana Aliyetoweka Kwa Sababu Ya Mahaba

Jibu maswali yafuatayo. Tumia aya ya hadi kwa majibu yako.

33. Ni nini kilimfanyikia Pili baada ya kuvuka mlango wa darasa?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

34. Taja yale Pili aliyatamka kimoyomoyo.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

35. Ni kifungu gani cha maneno kinachoonyesha kuwa maisha ya mji atakaoenda Pili ni wa kipekee ikilinganishwa na miji mingine licha ya kuwa mdogo?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

36. Ni kifungu kipi cha maneno kinaonyesha kuwa Pili alikuwa amebakia mwenyewe chuoni?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Chagua jibu muafaka. Andika herufi kwenye kisanduku ulichopewa. Tumia aya ya na kwa majibu yako.

37. Ni kwa nini Pili alikazia macho ya udadisi maktaba?

A. Alikuwa na fikira tele. B. Alitaka tu kufanya hivyo. C. Alitaka kuona maktaba. D. Alitaka kitu kutoka kwa maktaba.

38. Baada ya kutoa picha ya mpenziye ukutani, Pili alifanya nini?

A. Aliichanachana. B. Aliibandua. C. Aliweka vizuri katika mkoba wake. D. Aliweka juu ya meza nzuri.

16EP10

Page 6: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 11 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

39. “Lilifutika haraka na kurejesha usumbufu wa awali” ina maana gani?

A. Liliondolewa na mambo mengi ya kusisimua. B. Lilishindwa na vitu vya kawaida. C. Hakukuwa na mashindano ya mambo. D. Liliondolewa haraka na kurudia hali ya mashaka.

Linganisha kila mojawapo wa meneno yafuatayo kutoka kwenye kifungu na neno mwafaka linalokaribiana maana nalo. Andika herufi kwenye kisanduku ulichopewa. Zingatia: kuna majibu zaidi kuliko yale unayohitaji. Tumia aya ya hadi kwa majibu yako.

40. alipowasili

41. mawazo

42. hamu

43. hakuchelewa

44. tulivu

45. hususan

A. shwari

B. haja

C. alipofika

D. hasa

E. upendo

F. anakutafuta

G. fikira

I. ilimlazimu

J. hakukawia

K. hakufika

16EP11

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 12 –

Kifungu E — Ati, Mila Hii Ni Unyanyasaji Wa Kijinsia? Wanawake Mnasemaje?

46. Kutokana na kauli A hadi H, chagua kauli nne ambazo ni sahihi kulingana na kifungu hiki. Andika jibu mwafaka kwenye kisanduku ulichopewa. Tumia aya ya hadi kwa majibu yako. [alama 4]

A. Ni mazoea wanawake wa Kiafrika kupiga magoti wanapowasalimia wanaowazidi kwa umri.

B. Hakuna tofauti ya namna ya kupiga magoti kwa makabila yote Afrika.

C. Kwa Wasukuma mwanamke anapaswa kupiga magoti hadi chini kabisa.

D. Upigaji wa magoti ni dalili ya ulezi bora.

E. Upigaji wa magoti ni dharau.

F. Mwanamke pia anaweza kupigiwa magoti.

G. Wavulana au wanaume hawastahili kupiga magoti.

H. Shule ya upili ya Kahororo haiwafundishi vijana adabu njema.

Chagua jibu muafaka. Andika herufi kwenye kisanduku ulichopewa. Tumia aya ya kwa majibu yako.

47. Kulingana na msimulizi ni nini kinastahili kuweko katika utamaduni wetu?

A. Maelewano na utamaduni. B. Heshima. C. Maelewano na utangamano. D. Maelewano na heshima.

48. Kulingana na aya hii, ni nini cha kustaajabisha?

A. Tunatupilia mbali utamaduni wetu. B. Kuna utandawazi mwingi. C. Tunaiga utamaduni wa kigeni. D. Wale tunaoiga wana mila kama zetu tunazopuuza.

16EP12

Page 7: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 13 –

Ni maneno yapi yanaweza kujaza mapengo katika aya ya ? Chagua maneno kwenye orodha uliyopewa na kisha uyaandike hapo chini.

ishara mila nzuri tabia wasio

matumaini muhali potofu utamaduni utu

Mfano: [ – X – ] . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .mila . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

49. [ – 49 – ] . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

50. [ – 50 – ] . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

51. [ – 51 – ] . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

52. [ – 52 – ] . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Jibu maswali yafuatayo. Tumia aya ya kwa jibu lako.

53. Ni sentensi gani humaamisha kuwa msimulizi alitaka wanawake watoe kauli zao juu ya dhana ya kupiga magoti?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

16EP13

Please do not write on this page.

Answers written on this page will not be marked.

Veuillez ne pas écrire sur cette page.

Les réponses rédigées sur cette page ne seront pas corrigées.

No escriba en esta página.

Las respuestas que se escriban en esta página no serán corregidas.

16EP14

Page 8: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

Please do not write on this page.

Answers written on this page will not be marked.

Veuillez ne pas écrire sur cette page.

Les réponses rédigées sur cette page ne seront pas corrigées.

No escriba en esta página.

Las respuestas que se escriban en esta página no serán corregidas.

16EP15

16EP16

Page 9: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T

Swahili B – Higher level – Paper 1Swahili B – Niveau supérieur – Épreuve 1Swahili B – Nivel superior – Prueba 1

© International Baccalaureate Organization 20158 pages/páginas8815 – 2316

Text booklet – Instructions to candidates

• Do not open this booklet until instructed to do so.• This booklet contains all of the texts required for paper 1.• Answer the questions in the question and answer booklet provided.

Livret de textes – Instructions destinées aux candidats

• N’ouvrez pas ce livret avant d’y être autorisé(e).• Ce livret contient tous les textes nécessaires à l’épreuve 1.• Répondez à toutes les questions dans le livret de questions et réponses fourni.

Cuaderno de textos – Instrucciones para los alumnos

• No abra este cuaderno hasta que se lo autoricen.• Este cuaderno contiene todos los textos para la prueba 1.• Conteste todas las preguntas en el cuaderno de preguntas y respuestas.

1 h 30 m

Monday 9 November 2015 (afternoon)Lundi 9 novembre 2015 (après-midi)Lunes 9 de noviembre de 2015 (tarde)

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 2 –

Blank pagePage vierge

Página en blanco

Page 10: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N15 /2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 3 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

Kifungu A

Nyama ya Mbuzi ya Kukaanga

Nyama ya mbuzi ni moja kati ya vile vyakula ambavyo watu wengi au familia nyingi za pwani ya Kenya hula hasa wakati wa sherehe kama vile harusi kwa hamu sana. Kwa sababu mbuzi hula majani tofauti, hudhaniwa hutibu magonjwa tele. Ni moja kati ya vile vyakula ambavyo watu hupania kula. Sasa hivi imekuwa ni dhana kuwa nyama ya mbuzi ni lazima ichomwe na wengi wamezoea kwamba nyama hii huliwa kwa baa. Mara nyingi ukisikia watu wanaongelea juu ya kula nyama ya mbuzi, utasikia jina la baa au mahali fulani pa nyama choma pakitajwa. Mara nyingi watoto wamekosa kula nyama ya mbuzi kwa sababu mama na baba zao huila kwa baa.

Nyama ya mbuzi kama ilivyo ya ng’ombe au kuku huweza kuandaliwa na kupikwa nyumbani kwa ajili ya mlo wa familia. Kuna namna nyingi sana za kuandaa na kupika nyama ya mbuzi na mojawapo ni kukaanga kwa mafuta machache. Namna hii ya upishi wa nyama ya mbuzi ingawa ni rahisi na ya haraka, ina ladha nzuri na ni rahisi kula hata kwa watoto ukilinganisha na nyama ya kuchoma.

Mahitaji

Nyama ya mbuzi kilo moja. Chumvi kwa ladha uipendayo. Vitunguu saumu iliyopondwa/sagwa

kijiko kimoja na nusu cha chai. Tangawizi vijiko vitatu vya chakula. Mafuta ya kupikia nusu kikombe. Vijiko vitatu vya chakula vya limau.

Njia

Baada ya kukata na kuosha nyama ya mbuzi, toa maji yote kwenye nyama kisha weka kwenye sufuria utakayopikia. Ongeza chumvi, limau, vitunguu saumu na maji ya tangawizi katika nyama, kisha changanya vizuri ili viungo visambae kwenye nyama.Weka jikoni na uchemshe huku ukiwa umefunika. Usiweke maji kwenye nyama kwani nyama huwa na maji mengi ya asili. Pale tu nyama inapoanza kuchemka, igeuze na uendelee kuigeuza kila baada ya dakika mbili ili iive yote kwa pamoja na pia ili viungo viendelee kusambaa.

Maelezo ya ziada

Usiweke viungo vingi kwani vitapoteza ile ladha ya mbuzi. Lengo la kuweka vitunguu saumu, maji ya tangawizi na limau ni kuondoa harufu ya mbuzi na pili ni kuboresha ladha ya nyama.

Zingatia utumiaji wa maji au mchuzi wa tangawizi, usiweke tangawizi iliyopondwa au kusagwa na wala usitumie tangawizi ya unga. Lengo hapa ni kuepuka kutafuna kiungo unapokula. Viungo vyote vinatakiwa kupotelea ndani ya nyama. Mpaka hapo, nyama ya mbuzi ya kukaanga iko tayari na inaweza kusindikizwa na chakula chochote. Mimi napenda zaidi kusindikiza na ugali na mboga ya majani.

Imetoholewa kutoka, www.tollyzkitchen.wordpress.com (2013)

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 4 –

Kifungu B

Maajabu Ya Dunia: Nyumbu Wathibitisha “Nyumbani” Kwao Ni Serengeti

Maelfu ya maelefu ya makundi ya wanyama aina ya nyumbu, wanaokadiriwa kufika zaidi ya milioni 1.5 wameanza kurejea nyumbani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakitokea mbuga ya wanyama ya Masai Mara nchini Kenya walikoenda kwa mapumziko ya muda mfupi.

Tukio la kurejea nyumbani kwa nyumbu hao huwavutia watalii wengi mno kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kujionea kwa macho yao wenyewe badala ya kuangalia kwenye runinga.

“Sina maneno ya kuelezea furaha yangu kuhusu hiki nilichokiona moja kwa moja kwa macho yangu… nimepata tu kuona makundi ya nyumbu hawa wakivuka mto huu kupitia kwa mkanda wa picha uliorekodiwa, lakini sasa imekuwa ni maajabu kweli kushuhudia hali hii”, anasema mtalii mmoja kutoka Uholanzi akiwa na mumewe. Yeye na mumewe wakiwa ni miongoni tu mwa watalii wengi wanaotembelea Serengeti kujionea maajabu hayo, anasema amekaa kwenye mbuga hiyo kwa siku ya tano akisubiri kuona jinsi makundi ya nyumbu yanavyovuka mto huo kwa pamoja.

“Nafikiri nimekuwa mwanamke mwenye bahati sana kushuhudia uhamaji wa makundi ya nyumbu yakivuka mto […] hakika sina maneno zaidi ila haya ni maajabu ya dunia”. Anasema Serengeti ni mbuga nzuri yenye kuvutia ndiyo maana inatambuliwa kama ni moja ya Maajabu Saba ya Dunia.

Anasema walianza safari yao katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ambayo imejaa wanyama wengi wakiwemo tembo na walitaka kufurahisha nyoyo zao kwa kushuhudia makundi ya nyumbu yakihama na jinsi yanavyovuka mto huo.

Mto Mara umeanzia Kenya na kupita katika hifadhi ya Serengeti hadi ziwa Victoria ambako humwaga maji yake. Ili kutunza mto huo ambao ni muhimu kwa maisha ya wanyama, mradi wa kuutunza umeanzishwa kwa ushirikiano wa nchi mbili hizi, mradi ambao huangalia maeneo mbalimbali ya mto huo ili mazingira yake yasiharibiwe.

Wawapo Serengeti, watalii wengi wanapenda kuangalia makundi ya wanyama hao wanapochukua muda mrefu kujishauri namna ya kuvuka mto Mara, wenye viboko wengi lakini hofu kubwa inayowakumba nyumbu ni mamba ambao wamekuwa hatari kwao.

Ukiwasikiliza wanyama hao, sauti yao hutoa burudani ya aina yake ambayo utapenda kuendelea kusikiliza. Wakati fulani nyumbu watoto huanza kujaribu kuvuka na kufuatiwa na wakubwa lakini wagusapo maji na kuhisi kwamba kuna mamba, basi kundi zima hurudi nyuma kwa kukimbia ovyo.

Baada ya kurudi nyuma, huwachukua tena muda mrefu na wakati mwingine hukimbilia eneo lingine mbali kujaribu kuvuka na kufanikiwa kufanya hivyo kwa hata baada ya saa zaidi ya tano. Meneja wa Uhusiano wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), anasema watalii wengi wamekuwa wakipanga safari za kutembelea hifadhi hiyo ikiwa ni pamoja na kujionea makundi ya wanyama wakiwa wanarejea nyumbani na namna wanavyovuka mto. Wanyama hao hufanya hivyo wakati wowote kuanzia macheo hadi magharibi wanapoacha shughuli hiyo. Asema mto Mara ni kizuizi kikuu kwa wanyama na wafikapo ukingoni, huchukua muda mwingi kuvuka.

John Ngunge, Nipashe (2012)

Page 11: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 5 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

Kifungu C

Hongera Kampuni Mashuhuri Kufadhili MashindanoYa Ngoma Za Kisukuma

Kundi la ngoma la Makilikili kutoka Shinyanga

Kwa muda sasa nimekuwa nikiyashutumu makampuni mbalimbali hapa nchini kwa kuwa maajenti wa utandawazi. Kwa mfano, nimekuwa nikijiuliza: ni kwa nini makampuni haya yamejikita zaidi katika kudhamini mashindano ya urembo ambayo yamezagaa katika kila kona ya nchi badala ya kujikita katika mambo yenye tija zaidi kwa jamii kama ujenzi wa madarasa, ununuzi wa madawati, uchimbaji wa visima vya maji huko vijijini na miradi mingine ya kimaendeleo?

Inabidi niseme hapa kwamba sasa hali hii imebadilika na makampuni mengi, japo bado yamemakinikia shughuli za burudani ili kujitangaza zaidi, yamejibidiisha sana kudhamini shughuli za kimaendeleo pia.

Makampuni mengi sana yamekuwa yakijenga madarasa na ofisi za walimu, kununua madawati, kuchimba visima, kusaidia vituo vya kulea watoto yatima na miradi mingineyo. Hili ni jambo njema kwani kama tukishupalia tu mashindano ya urembo na burudani basi ni wazi kuwa hatutafika popote.

Ni katika mtazamo huu, ambapo nimefurahishwa sana na taarifa kuwa kampuni moja mashuhuri imetoa shilingi milioni 12 ili kudhamini mashindano ya ngoma za Kisukuma kule Mwanza. Hili ni jambo la umuhimu, si kwa sababu mimi ni Msukuma, bali kutokana na ukweli kwamba wengi wetu sasa tumefunikwa na kungu la utandawazi na usasa kiasi kwamba hatujali tena utamaduni na lugha zetu za mama zilizotulea na kutukuza.

Shughuli hizi za kitamaduni zikiendelea kuimarishwa na makampuni binafsi kama tunavyoshuhudia katika mashindano ya urembo, zitasaidia japo kutukumbusha kuwa sisi ni watu wenye utamaduni wetu wenyewe na kwamba kabla ujio wa watawala wetu kutoka huko walikotoka, tulikuwa watu huru kifikira, kisaikolojia na kitamaduni.

Hongera kampuni hii mashuhuri na Mkurugenzi wenu wa Masoko kwa hatua yenu hii ya kimapinduzi kufadhili shughuli hizi za kitamaduni. Bila shaka makampuni mengine yataiga mfano wenu. Nina hakika tukifanya hivi tutapata kuonja maendeleo ya kutosha.

Imetoholewa kutoka, http://matondo.blogspot.com (2012)

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 6 –

Kifungu D

Msichana Aliyetoweka Kwa Sababu Ya Mahaba

Baada ya Pili kuvuta hatua mbili tatu kuvuka mlango wa darasa lake lililoelekeana na ofisi ya Msarifu, alirudiwa na kumbukumbu ya kuwa kesho yake jioni ndiyo ilikuwa nafasi yake ya mwisho kwa kipindi hicho kuiona sura ya chuo cha Tabora muhula huo. “Nakumbuka nilimtumia mpenzi wangu Moddy barua ikimfahamisha kuwasili kwangu hapo Musoma”, Pili aliyatamka kimoyomoyo.

Pindi Pili alipomaliza kujifungulia baraza la binafsi alirejea bwenini akaanza kusafisha karibu kila kilichomhusu katika safari yake. Muhula wa mchana akapiga pasi nguo zake na kuzipanga barabara ndani ya sanduku lake. Jioni hiyo Pili aliporejea kutoka mjini kuagana na baadhi ya rafiki zake mbalimbali aliufikia uwanja wa chuo akajifungulia kumbukumbu tele.

Uwanja wa chuo uliozoea kuwaweka wanafunzi wengi huku na huko, siku hiyo ulionekana mweupe kasoro Pili ambaye alikuwa amesimama kando ya maktaba akifikiria jinsi atakavyoyatambua maisha ya Musoma; maisha ya mji mdogo uliofanikiwa starehe za pekee ukilinganishwa na miji mingine iliyovuma miaka nenda miaka rudi. Mwili mzima wa Pili ulisisimka na kuchemka kila alivyouvuta akilini mwake mji wa Musoma kwa jumla.

Bila ya kujifahamu, Pili aliiutulizia macho ya udadisi maktaba, baadaye akatoa sauti nzito, “unh”. Papo hapo akaongoza ujia uliokuwa unaelekea bwenini. Chumbani mwa Pili alikwishapabadilisha muundo wake wa nyuma. Mapambo yaliyokuwa ukutani alikwishayabandua. Picha ya mpenzi wake Moddy ambayo ilikuwa ikionekana kila alipokuwa akifungua kabati lake, alikwishaibandua na kuibana sawasawa ndani ya mkoba wake wa hali ya juu.

Pili akakamilisha maandalizi yake ya safari yake, akatulia kunako kitanda hali akipanga na kupangua mahali atakapofikia huko Musoma. Utashi wa moyo wakati mwingine ulihitaji afikie kwa shangazi wake na mvutano wa mahaba vilevile ulipigania nafasi katika kupata haki yake. Fikira zake zilijaribu kuvuruga ushindani huo kichwani mwake na kila alipojaribu kuvumbua wazo jingine, lilifutika haraka na kurejesha usumbufu wa awali. Mawingu ya mvua huweza kufukuzwa kwa upepo mkali lakini kwa upande wa Pili hapakuwa na kitu ambacho kingeliweza kubadili au kumpatia uamuzi wa mkato.

Page 12: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 7 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

“Nitakata shauri pindi nifikapo huko mbele”, Pili alitoa jawabu huku akiinua sanduku lake tayari kukivuka kizingiti cha mlango. Naye akaendelea kuhesabu hatua kuelekea kwenye kituo cha magari, alimkuta dada yake Justina amefika mbele kutoka chuoni.

Uchochoro alioufuata Pili ulikwishaingia giza na ilimbidi auache na kufuata mtaa uliojaa nuru ya taa. Alipowasili kwenye kituo cha gari, alimkuta dadake Justina pale muda mfupi akiwa na wanafunzi wenzake ambao wengi wao walikuwa wanaelekea Morogoro kupitia njia panda ya Dodoma.

Justina alipokuwa hapo kituoni mawazo yalikuwa hayamweki pamoja kutokana na hamu ya kuwaona wazazi wake kwa sababu kipindi kilichopita alikikilikizia kwa shangazi wake. Hakika maelezo yote yalikuwa sawa.

Magharibi hiyo, chombo kilifika kituoni halafu dereva akaweka kizuio kuwapa abiria nafasi ya kupanda na kushuka. Pili hakuchelewa kupanda ndani ya gari moshi tayari kuelekea Musoma. Safari ilikuwa tulivu; abiria hawakusongamana au kukosa nafasi. Kwa kweli nafasi hii ilimpa Pili wasaa wa kutosha kumudu kufunua picha kamili juu ya shangazi wake, na hususan mpenzi wake aliyetarajia kukutana naye baada ya wakati mrefu kupita pasipo kuonana.

PC Geranija na AS Muwanga, Doa la Mauti (1976)

N15/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 8 –

Kifungu E

Ati, Mila Hii Ni Unyanyasaji Wa Kijinsia? Wanawake Mnasemaje?

Katika makabila mengi ya Kiafrika, wanawake kupiga magoti wanapowasalimia wanaume au watu wanaowazidi kwa umri ni jambo la kawaida. Upigaji huu wa magoti hutofautiana kutoka kabila moja hadi jingine. Kwa Wasukuma kwa mfano, mwanamke alitegemewa kupiga magoti mpaka chini kabisa hasa anaposalimiana na wazee; na upigaji huu wa magoti ulikuwa bado ni ishara mojawapo ya kuonyesha kwamba binti amelelewa vyema na ana sifa za kuolewa!

Wazo la upigaji magoti limezua maswali kuhusu mila hii kongwe. Je, ni heshima au udhalilishaji? Inabidi tukumbuke pia wanaopigiwa magoti si wanaume pekee bali, mwanamke anaweza kumpigia mwanamke mwenzake anayemzidi umri au anayetaka kumwonyesha kwamba anamheshimu. Na katika jamii nyingine wavulana na hata wanaume ndio hupiga magoti.

Nakumbuka wakati nikisoma katika shule ya sekondari ya Kahororo kule Bukoba, vijana wa Kihaya ndio walikuwa wakipiga magoti walipokuwa wakiwapa watu wazima vitu na jambo hili lilitugutusha sana sisi “Banyamahanga” wa kutoka mikoa ya Shinyanga na Mara.

Kuna njia nyingi za kuonyesha heshima kwa watu wazima au watu wenye mamlaka katika jamii mbalimbali duniani. Lakini mimi nadhani kinachohitajika ni maelewano na utangamano wa kitamaduni. Kwa wakati huu wa dot.com, wakati wa usasa na utandawazi ni rahisi sana kutupilia mbali mila zetu kwa kudai kwamba zimepitwa na wakati. Na wakati mwingine tunaweza kushangaa baadaye tunapokuja kugundua kwamba hata hao “wakubwa wetu” tunaojaribu kuwaiga kumbe hata nao wana mila zinazofanana na zetu tunazojaribu kuzitupilia mbali.

Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba ni lazima tuwe waangalifu kwani si kila [ – X – ] yetu ni mbaya na si kila mila ya kimagharibi ni nzuri! Mila ikionekana ni [ – 49 – ] basi ni lazima tutupilie mbali na kama ni nzuri, ni lazima tuishikilie. Vinginevyo tutapoteza utambulisho wetu na kuwa watu [ – 50 – ] na chao hapa duniani! Ni dhahiri shahiri kuwa hakuna kitu kibaya sana duniani kushinda mtu asiye na [ – 51 – ] wake. Najua si [ – 52 – ] kukosa watu kama hao katika jamii yetu.

Na kama kupiga magoti kwa nia ya kuonyesha heshima ni unyanyasaji, basi inatubidi tutafute njia nyingine ya kuonyesha heshima. Na kwa jambo hili la kupiga magoti, ningeomba hasa wanawake watupe maoni yao. Wanajisikiaje wanapofanya hivyo? Ni kweli wanahisi kuwa wananyanyaswa?

http://matondo.blogspot.com (2010)

Page 13: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N15/2/ABSWA/HP2/SWA/TZ0/XX

Swahili B – Higher level – Paper 2Swahili B – Niveau supérieur – Épreuve 2Swahili B – Nivel superior – Prueba 2

© International Baccalaureate Organization 20153 pages/páginas8815 – 2317

Instructions to candidates

• Do not open this examination paper until instructed to do so.• Section A: choose one task. Each task is worth [25 marks].• Section B: write a personal response to the stimulus provided. The task is worth [20 marks].• The maximum mark for this examination paper is [45 marks].

Instructions destinées aux candidats

• N’ouvrez pas cette épreuve avant d’y être autorisé(e).• Section A : choisissez une tâche. Chaque tâche vaut [25 points].• Section B : exprimez votre opinion personnelle sur la réflexion fournie. La tâche vaut [20 points].• Le nombre maximum de points pour cette épreuve d’examen est de [45 points].

Instrucciones para los alumnos

• No abra esta prueba hasta que se lo autoricen.• Sección A: elija una tarea. Cada tarea vale [25 puntos].• Sección B: escriba una opinión personal al estímulo provisto. La tarea vale [20 puntos].• La puntuación máxima para esta prueba de examen es [45 puntos].

1 h 30 m

Tuesday 10 November 2015 (morning)Mardi 10 novembre 2015 (matin)Martes 10 de noviembre de 2015 (mañana)

N15/2/ABSWA/HP2/SWA/TZ0/XX– 2 –

Sehemu A

Kamilisha mojawapo wa kazi zifuatazo. Andika maneno 250 hadi 400.

1. Utofauti wa tamaduni

Lugha nyingi ulimwenguni huzungumzwa na idadi ndogo ya watu, baadhi yazo ziko katika hatari ya kuangamia. Andika makala itakayochapishswa katika jarida la shule kwa nini na vipi lugha zinazozungumzwa na watu wachache zinavyoweza kulindwa.

2. Mila na desturi

Shule yako imeandaa Siku ua Utamaduni ambapo wanafunzi kutoka tamaduni tofauti walisherehekea mila zao, mazoea na/au desturi zao. Andika kipeperushi kwa wanafunzi ukiwajulisha kuhusu tukio hili kabla halijatendeka.

3. Afya

Makala ya hivi majuzi katika gazeti la kitaifa imemulika jambo kuwa vijana wengi sana wana matatizo ya afya kwa sababu wanatumia muda wao mwingi kwenye tarakilishi. Andika barua kwa mhariri wa gazeti ambapo unaelezea mawazo yako kuhusu jambo hili.

4. Burudani

Wewe na wanafunzi wenzako hivi karibuni mlitazama filamu ya kihistoria. Kwa kuwa wengi wa wanafunzi wenzako hawakuhudhuria, mwalimu wako amekuomba uandike maoni yako kuhusu filamu hiyo kwa blogu yako. Andika blogu yako.

5. Sayansi na teknolojia

Shule yako inaandaa mjadala juu ya swali: “Je, maendeleo ya teknolojia yanatishia maisha ya kibinafsi?” Kwa mjadala huu, unaenda kuweka wazi mawazo yako ya kupinga au kuunga mkono mjadala huu. Andika hotuba yako utakayotoa mbele ya wanafunzi wenzako.

Page 14: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N15/2/ABSWA/HP2/SWA/TZ0/XX– 3 –

Sehemu B

Kulingana na kichocheo kifuatacho, toa jibu lako binafsi na ulithibitishe. Chagua maandiko yoyote uliyoyasoma darasani. Andika maneno kati ya 150 na 250.

6. Uhusiano wa mapema unachangiwa mno na shinikizo la hirimu hata hivyo mitandao ya kijamiii inastahili kulaumiwa pia.

N16

/2/A

BS

WA

/HP

1/S

WA

/TZ0

/XX

/M

8 pa

ges/

pági

nas

Mar

ksch

eme

Bar

ème

de n

otat

ion

Esqu

ema

de c

alifi

caci

ón

Nov

embe

r / N

ovem

bre

/ Nov

iem

bre

2016

Swah

ili /

Swah

ili /

Swah

ili B

Hig

her l

evel

N

ivea

u su

périe

ur

Niv

el s

uper

ior

Pape

r / É

preu

ve /

Prue

ba 1

Page 15: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

2 –

N16

/2/A

BS

WA

/HP

1/S

WA

/TZ0

/XX

/M

Th

is m

arks

chem

e is

con

fiden

tial a

nd fo

r the

exc

lusi

ve u

se o

f exa

min

ers

in th

is e

xam

inat

ion

sess

ion.

It

is th

e pr

oper

ty o

f the

Inte

rnat

iona

l Bac

cala

urea

te a

nd m

ust n

ot b

e re

prod

uced

or d

istri

bute

d to

any

oth

er p

erso

n w

ithou

t the

aut

horiz

atio

n of

the

IB A

sses

smen

t Cen

tre.

Ce

barè

me

de n

otat

ion

est c

onfid

entie

l. S

on u

sage

est

rése

rvé

excl

usiv

emen

t aux

exa

min

ateu

rs p

artic

ipan

t à c

ette

ses

sion

. C

e ba

rèm

e de

not

atio

n es

t la

prop

riété

de

l’Org

anis

atio

n du

B

acca

laur

éat I

nter

natio

nal.

Tout

e re

prod

uctio

n ou

dis

tribu

tion

à de

tie

rces

per

sonn

es s

ans

l’aut

oris

atio

n pr

éala

ble

du c

entre

de

l’éva

luat

ion

de l’

IB e

st in

terd

ite.

Est

e es

quem

a de

cal

ifica

ción

es

conf

iden

cial

y p

ara

uso

excl

usiv

o de

lo

s ex

amin

ador

es e

n es

ta c

onvo

cato

ria d

e ex

ámen

es.

Es

prop

ieda

d de

l Bac

hille

rato

Inte

rnac

iona

l y n

o de

be s

er re

prod

ucid

o ni

di

strib

uido

a n

ingu

na o

tra p

erso

na s

in la

aut

oriz

ació

n de

l cen

tro d

e ev

alua

ción

del

IB.

3 –

N16

/2/A

BS

WA

/HP

1/S

WA

/TZ0

/XX

/M

1. F

or q

uest

ions

whe

re s

hort

answ

ers

are

requ

ired,

the

answ

er m

ust b

e cl

ear.

Do

not a

war

d th

e m

ark

if th

e an

swer

doe

s no

t mak

e se

nse

or if

the

addi

tiona

l inf

orm

atio

n m

akes

the

answ

er a

mbi

guou

s, in

corr

ect o

r inc

ompr

ehen

sibl

e.

2. A

llow

spe

lling

mis

take

s so

long

as

they

do

not h

inde

r com

preh

ensi

on o

r do

not c

hang

e th

e se

nse

of th

e ph

rase

. 3.

For

true

or f

alse

que

stio

ns, c

andi

date

s m

ay u

se a

tick

or a

cro

ss to

indi

cate

thei

r int

ende

d re

spon

se b

ut u

sage

mus

t be

cons

iste

nt. I

f a c

andi

date

writ

es

two

ticks

or t

wo

cros

ses

for t

he s

ame

answ

er a

war

d [0

]. If

a c

andi

date

ans

wer

s w

ith a

cro

ss a

nd a

tick

for t

he s

ame

answ

er, m

ark

the

tick

and

igno

re

the

cros

s.

4. F

or q

uest

ions

whe

re th

e ca

ndid

ate

has

to w

rite

a le

tter i

n a

box

(for e

xam

ple,

mul

tiple

cho

ice

ques

tions

), if

a ca

ndid

ate

has

writ

ten

two

answ

ers

– on

e in

th

e bo

x an

d on

e ou

tsid

e –

only

mar

k th

e an

swer

insi

de th

e bo

x.

5. T

he to

tal n

umbe

r of m

arks

for t

he q

uest

ion

pape

r is

[60]

. 1.

En

ce q

ui c

once

rne

les

ques

tions

pou

r les

quel

les

des

répo

nses

brè

ves

sont

atte

ndue

s, la

répo

nse

donn

ée d

oit ê

tre c

laire

. N

’attr

ibue

z pa

s de

poi

nts

si

la ré

pons

e n’

a au

cun

sens

ou

si le

s in

form

atio

ns s

uppl

émen

taire

s qu

’elle

con

tient

la re

nden

t am

bigu

ë, in

corr

ecte

ou

inco

mpr

éhen

sibl

e.

2. V

ous

pouv

ez a

utor

iser

les

faut

es d

’orth

ogra

phe

tant

qu’

elle

s ne

nui

sent

pas

à la

com

préh

ensi

on o

u qu

’elle

s ne

cha

ngen

t pas

le s

ens

de la

phr

ase.

3.

En

ce q

ui c

once

rne

les

ques

tions

de

type

vra

i ou

faux

, les

can

dida

ts p

euve

nt c

oche

r ou

mar

quer

d’u

ne c

roix

la ré

pons

e de

leur

cho

ix, m

ais

ils d

oive

nt

rest

er c

ohér

ents

. S

i un

cand

idat

a u

tilis

é de

ux c

oche

s ou

deu

x cr

oix

pour

la m

ême

répo

nse,

attr

ibue

z [0

]. S

i un

cand

idat

a ré

pond

u pa

r une

cro

ix e

t un

e co

che

à la

mêm

e qu

estio

n, p

rene

z en

com

pte

la c

oche

et i

gnor

ez la

cro

ix.

4. E

n ce

qui

con

cern

e le

s qu

estio

ns p

our l

esqu

elle

s le

can

dida

t doi

t écr

ire u

ne le

ttre

dans

une

cas

e (p

ar e

xem

ple,

dan

s le

cas

de

ques

tions

à c

hoix

m

ultip

le),

s’il

a do

nné

deux

répo

nses

diff

éren

tes,

l’un

e à

l’int

érie

ur d

e la

cas

e et

l’au

tre e

n-de

hors

, ne

pren

ez e

n co

mpt

e qu

e la

répo

nse

qui s

e si

tue

dans

la c

ase.

5. L

e no

mbr

e to

tal d

e po

ints

pou

r l’é

preu

ve d

’exa

men

est

de

[60]

. 1.

Las

pre

gunt

as q

ue re

quie

ran

una

resp

uest

a co

rta d

eben

resp

onde

rse

con

clar

idad

. N

o ot

orgu

e la

pun

tuac

ión

si la

resp

uest

a no

tien

e se

ntid

o o

si la

in

form

ació

n ad

icio

nal h

ace

que

la re

spue

sta

sea

ambi

gua,

inco

rrec

ta o

inco

mpr

ensi

ble.

2.

Per

mita

err

ores

de

orto

graf

ía s

iem

pre

y cu

ando

no

dific

ulte

n la

com

pren

sión

ni c

ambi

en e

l sen

tido

de la

ora

ción

. 3.

En

las

preg

unta

s de

ver

dade

ro o

fals

o, lo

s al

umno

s po

drán

indi

car l

a re

spue

sta

eleg

ida

con

un ti

c o

una

cruz

, per

o el

uso

de

los

sign

os d

ebe

ser

cohe

rent

e. S

i el a

lum

no m

arca

dos

tics

o d

os c

ruce

s en

la m

ism

a re

spue

sta,

oto

rgue

la p

untu

ació

n [0

]. S

i el a

lum

no re

spon

de m

arca

ndo

una

cruz

y

un ti

c en

la m

ism

a re

spue

sta,

pun

túe

el ti

c e

igno

re la

cru

z.

4. E

n la

s pr

egun

tas

que

requ

iera

n es

crib

ir un

a le

tra e

n un

a ca

silla

(por

eje

mpl

o, e

n la

s pr

egun

tas

de o

pció

n m

últip

le),

si e

l alu

mno

ha

escr

ito d

os

resp

uest

as (u

na d

entro

de

la c

asill

a y

la o

tra fu

era)

, pun

túe

únic

amen

te la

resp

uest

a m

arca

da d

entro

de

la c

asill

a.

5. E

l núm

ero

tota

l de

punt

os a

sign

ados

al c

uest

iona

rio d

e ex

amen

es

[60]

.

Page 16: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

4 –

N16

/2/A

BS

WA

/HP

1/S

WA

/TZ0

/XX

/M

Kifu

ngu

A —

Kan

ga, v

azi l

inal

owak

ilish

a ut

amad

uni w

a K

itanz

ania

Swal

i Ji

bu le

ngw

a K

ubal

i U

siku

bali

Ala

ma

1.

lin

atum

iwa

takr

iban

i na

mak

abila

yot

e

Huw

akili

sha

utam

adun

i wa

wat

anza

nia

1

2.

ki

tam

baa

kilic

hore

mbw

a na

mau

a / r

angi

mba

limba

li /

kuch

apis

hwa

man

eno

M

ojaw

apo

1

3.

ut

amad

uni w

a ja

mii

husi

ka

“U

tam

adun

i” pe

kee

“Jam

ii hu

sika

” pek

ee

1

4.

C

1

5.

D

1

6.

A

1

7.

B

1

8.

S

iku

ya h

arus

i (kw

a w

anaw

ake)

/ w

akat

i wa

sala

(k

wa

wan

awak

e w

a K

iisla

mu)

M

ojaw

apo

1

9.

H

utum

ika

kam

a ta

ulo

ya k

ufut

a m

aji (

baad

a ya

kuo

ga)

Kam

a ta

ulo/

kufu

ta m

aji (

baad

a ya

ku

oga)

1

10.

C

1

11.

D

1

12.

F

1

13.

G

1

1.

Ju

mla

13

5 –

N16

/2/A

BS

WA

/HP

1/S

WA

/TZ0

/XX

/M

Kifu

ngu

B —

Fur

sa y

a el

imu

– Za

nzib

ar

Sw

ali

Jibu

leng

wa

Kub

ali

Usi

kuba

li A

lam

a

14.

Map

indu

zi m

atuk

ufu

(ya

wat

u w

a Za

nzib

ar)

map

indu

zi

1

15.

elim

u ya

wen

gi /

(yam

ewap

atia

furs

a ya

) kup

ata

elim

u kw

a w

atot

o w

a w

afan

yaka

zi n

a w

akul

ima

moj

awap

o

1

16.

yatu

pasa

tutu

pie

jicho

(uta

ratib

u w

a el

imu

ulio

tole

wa

mia

ka

ya n

yum

a)

1

17.

kwa

nadr

a zi

litol

ewa

kwa

wat

oto

wa

wan

yong

e

1

18.

w

alio

kuw

a na

vip

awa

maa

lum

vi

paw

a m

aalu

m

Vip

awa

peke

e 1

19.

el

imu

ya m

uda

mfu

pi

Elim

u nd

ogo

1

20.

m

azin

gira

1

21.

ki

paw

a

1

22.

S

i kw

eli

unat

oa fu

rsa

za e

limu

kwa

wot

e U

tara

tibu

huu

ulije

ngw

a ju

u ya

us

awa

Si k

wel

i pek

ee

Thib

itish

o pe

kee

1

23.

K

wel

i ili

ondo

a ad

a za

shu

le

K

wel

i pek

ee

Thib

itish

o pe

kee

1

24.

S

kuli

1

25.

M

adar

asa

1

26.

E

limu

(ya

msi

ngi)

1

2.

Ju

mla

13

Page 17: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

6 –

N16

/2/A

BS

WA

/HP

1/S

WA

/TZ0

/XX

/M

Kifu

ngu

C —

Maz

ingi

ra m

acha

fu n

a at

hari

zake

Swal

i Ji

bu le

ngw

a K

ubal

i U

siku

bali

Ala

ma

27.

Kuw

a na

afy

a bo

ra/k

uend

elea

kuw

a na

afy

a bo

ra

moj

awap

o “A

fya

bora

” pek

ee

1

28.

Tuw

eze

kuen

dele

a na

shu

ghul

i zet

u (z

a ki

la s

iku

katik

a uj

enzi

wa

Taifa

)

1

29.

usaf

i wa

maz

ingi

ra n

i dun

i ha

mna

viw

ango

maa

lum

vi

livyo

wek

wa

katik

a ku

yaw

eka

maz

ingi

ra s

afi

1

30.

shug

huli

1

31.

gh

aram

a

1

32.

uh

arib

ifu

1

33.

hi

fadh

i

1

34.

ha

tuna

maz

oea

ya k

utup

a na

kuh

arib

u ta

ka k

atik

a nj

ia il

iyo

sahi

hi

1

35.

ha

rufu

kal

i su

mu

mba

limba

li (z

inaz

owaa

thiri

ki

afya

wak

azi)

1

36.

a)/b

) up

epo

unao

vum

a / w

adud

u ka

ma

inzi

na

men

de /

njia

ya

upum

uaji

/ Vim

elea

vya

mag

onjw

a vy

awez

a pi

a ku

ingi

a ka

tika

viny

waj

i vis

ivyo

funi

kwa,

vya

kula

vili

vyoa

chw

a w

azi

Maj

ibu

yoyo

te 2

2

37.

tu

tapu

nguz

a gh

aram

a ku

bwa

zitu

mik

azo

katik

a m

atib

abu

ya m

agon

jwa

1

3.

Ju

mla

12

7 –

N16

/2/A

BS

WA

/HP

1/S

WA

/TZ0

/XX

/M

Kifu

ngu

D —

Tek

nolo

jia n

a M

tindo

wa

Mai

sha

Sw

ali

Jibu

leng

wa

Kub

ali

Usi

kuba

li A

lam

a

38.

C, E

K

atik

a m

pang

ilio

wow

ote.

A

lam

a [1

] kw

a ki

la h

eruf

i

2

39.

kisa

ikol

ojia

sa

ikol

ojia

1

40.

kuw

epo

uwez

o w

a ku

chag

ua

1

41.

kum

ekuw

epo

na c

hang

amot

o ny

ingi

(kat

ika

kuch

ungu

za

kadh

ia y

a “M

tindo

wa

Mai

sha”

)

chan

gam

oto

nyin

gi p

ekee

1

42.

ku

ibuk

a te

knol

ojia

mpy

a (k

atik

a m

aish

a ya

mw

anad

amu)

1

43.

ku

pitia

uhu

sian

o na

mai

ngili

ano

yake

na

wat

u al

ioku

wa

akiis

hi k

arib

u na

o

1

44.

w

alio

kuw

a na

uhu

sian

o na

dun

ia y

a nj

e ya

miji

au

vijij

i vya

o

1

45.

na

fasi

ya

eneo

si m

uhim

u sa

na (k

atik

a ku

unda

uta

mbu

lisho

w

a m

tu b

inaf

si)

1

46.

C

1

4.

Ju

mla

10

Page 18: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

8 –

N16

/2/A

BS

WA

/HP

1/S

WA

/TZ0

/XX

/M

Kifu

ngu

E —

Tum

bom

bele

Mla

Mis

itu

Sw

ali

Jibu

leng

wa

Kub

ali

Usi

kuba

li A

lam

a

47.

a) /

b) /

c)

Miti

ilifu

rahi

a am

ani (

isiy

o na

kip

imo)

/ m

iti il

isha

ngili

a he

wa

mw

anan

a (il

iyov

uma

vuu

vuu!

) / (K

uteu

liwa

kwa

Tum

bom

bele

) hak

ukup

okel

ewa

kwa

fura

ha n

a m

iti/ k

uliz

ua

kilio

na

huzu

ni

Kat

ika

mpa

ngili

o w

owot

e.

Ala

ma

[1] k

wa

kila

jibu

3

48.

C

1

49.

D

1

50.

kujif

aham

isha

hal

i ya

mis

itu il

ivyo

kuw

a nc

hini

hum

o

kum

karib

isha

nyu

mba

ni b

aada

ya

kute

uliw

a 1

51.

M

iti h

utup

atia

hew

a sa

fi (in

ayov

uma

kuto

ka k

usin

i kue

leke

a ka

skaz

ini)

1

52.

ku

ozea

jela

Kuf

ungw

a je

la

kuoz

a 1

53.

W

atu

wal

ifum

ukan

a

1

54.

m

apat

o

1

55.

w

izar

a

1

56.

ki

u

1

5.

Ju

mla

12

Candidate session numberNuméro de session du candidat

Número de convocatoria del alumno

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q

Swahili B – Higher level – Paper 1Swahili B – Niveau supérieur – Épreuve 1Swahili B – Nivel superior – Prueba 1

© International Baccalaureate Organization 201612 pages/páginas8816 – 2315

Question and answer booklet – Instructions to candidates

• Write your session number in the boxes above.• Do not open this booklet until instructed to do so.• This booklet contains all the paper 1 questions.• Refer to the text booklet which accompanies this booklet.• Answer all of the questions in the boxes provided. Each question is allocated [1 mark] unless

otherwise stated.• The maximum mark for this examination paper is [60 marks].

Livret de questions et réponses – Instructions destinées aux candidats

• Écrivez votre numéro de session dans les cases ci-dessus.• N’ouvrez pas ce livret avant d’y être autorisé(e).• Ce livret contient toutes les questions de l’épreuve 1.• Référez-vous au livret de textes qui accompagne ce livret.• Répondez à toutes les questions dans les cases prévues à cet effet. Sauf indication

contraire, chaque question vaut [1 point].• Le nombre maximum de points pour cette épreuve d’examen est de [60 points].

Cuaderno de preguntas y respuestas – Instrucciones para los alumnos

• Escriba su número de convocatoria en las casillas de arriba.• No abra este cuaderno hasta que se lo autoricen.• Este cuaderno contiene todas las preguntas de la prueba 1.• Consulte el cuaderno de textos que acompaña a este cuaderno.• Conteste todas las preguntas en las casillas provistas. Cada pregunta vale [1 punto] salvo que

se indique lo contrario.• La puntuación máxima para esta prueba de examen es [60 puntos].

1 h 30 m

Friday 4 November 2016 (afternoon)Vendredi 4 novembre 2016 (après-midi)Viernes 4 de noviembre de 2016 (tarde)

12EP01

Page 19: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 2 –

Kifungu A — Kanga, vazi linalowakilisha utamaduni wa Kitanzania

Jibu maswali yafuatayo. Tumia aya ya hadi kwa majibu yako.

1. Kwa nini kanga ni vazi linalotambulisha utamaduni wa Watanzania?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

2. Taja sifa moja ya kanga.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

3. Maana ya maandishi yaliyochapishwa kwenye kanga inategemea nini?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Chagua jibu sahihi kutoka kwa A, B, C, D. Andika herufi ya uchaguzi wako katika kisanduku. Tumia aya ya hadi kwa majibu yako.

4. Kifungu cha maneno “Vazi la kanga ni maarufu zaidi kwa Waswahili” kina maana gani?

A. Kanga ndilo vazi pekee linalojulikana na Waswahili. B. Vazi pekee linalokubalika kwa Waswahili ni kanga. C. Kanga ni mashuhuri sana Uswahilini kuliko kwingine. D. Kanga ni vazi la heshima zaidi miongoni mwa Waswahili.

5. Kulingana na kifungu hiki, ni kauli gani iliyo ya kweli kuhusu kanga?

A. Uvaaji wa kanga ulipata umaarufu karne 19 zilizopita. B. Kanga zilikuwa zimeenea kabla ya karne ya 19. C. Wanawake kutoka sehemu zenye joto hawakuvaa kanga. D. Ni katika sehemu zenye joto wanawake walivaa kanga sana.

6. Kuenea kwa vazi la kanga ukanda wa pwani kulisababisha nini?

A. Watu kutoka bara walivutiwa na kuanza kuvaa kanga. B. Wageni kutoka bara walianza kutembelea ukanda wa Afrika Mashariki. C. Watu wa makabila mbalimbali walianza kuvutiwa na wageni. D. Wageni waliotembelea Afrika Mashariki walianza kuvaa kanga kwa

njia mbalimbali.

12EP02

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 3 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

7. Tafsiri tofauti zinazotolewa na uvaaji wa kanga zina sifa gani?

A. Zinalingana na kimo cha kanga. B. Zinalingana na mahitaji ya anayevaa. C. Zinategemea makabila na dini. D. Zinalingana na kanga yenyewe.

Jibu maswali yafuatayo. Tumia aya ya hadi kwa majibu yako.

8. Taja tukio moja ambapo kanga huvaliwa kama vazi mahususi.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

9. Kanga inatumiwa kwa njia gani nyingine isipokuwa kuvaliwa?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Linganisha kila mojawapo ya maneno yafuatayo kutoka kwa kifungu na neno mwafaka linalokaribiana maana nalo. Andika herufi kwenye kisanduku ulichopewa.

Mfano: kimo (mstari 13) A

10. umaarufu (mstari 17)

11. ukanda (mstari 19)

12. haja (mstari 22)

13. sala (mstari 29)

A. kipimo

B. nyanda

C. umashuhuri

D. eneo

E. umahiri

F. matakwa

G. maombi

H. urefu

I. shida

J. kafara

12EP03

Page 20: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 4 –

Kifungu B — Fursa ya elimu – Zanzibar

Jibu maswali yafuatayo. Tumia aya ya hadi kwa majibu yako.

14. Jambo gani limeleta mabadiliko katika fursa za elimu Zanzibar?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

15. Taja tokeo moja la mabadiliko ya mfumo wa elimu Zanzibar.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

16. Ni usemi gani katika kifungu unamaanisha kuwa hatuna budi kuangazia kwa undani mfumo wa elimu wa hapo awali?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

17. Ni kifungu gani cha maneno kinadhihirisha kuwa nafasi za elimu kwa watoto wa maskini zilikuwa chache?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

18. Ni sifa gani iliyopelekea watoto wa tabaka la chini kupata nafasi ya kwenda shuleni?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

19. Ni kwa nini ilikuwa vigumu kwa tabaka la chini kupata kazi muhimu?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

12EP04

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 5 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

Tafuta maneno kutoka kwenye kifungu yenye maana hizi. Tumia aya ya kwa majibu yako.

Mfano: Mpangilio wa kufanya kitu.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . mfumo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

20. Mambo yanayozunguka mtu anapokaa.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

21. Uwezo wa mtu wa kufanya kitu fulani.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Sentensi zilizopo hapa chini ni kweli au si kweli kulingana na aya ya . Weka alama [] kwenye jibu lililo sahihi na kisha uthibitishe jibu lako kwa kuandika nukuu mwafaka kutoka kwenye kifungu. Alama [] pamoja na nukuu zinahitajika kwa alama moja.

Kweli Si kweliMfano: Mfumo mpya wa elimu unalenga kuwatoa wananchi

kutoka ukandamizwaji.

Thibitisho: . . . lengo la mpango mpya wa elimu ni kuwakomboa wananchi. . . . . . . .

22. Mpangilio wa elimu uliopo unawezesha baadhi kupata elimu.

Thibitisho: . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

23. Ili kuwa na nafasi sawa za elimu, malipo ya karo yalisitishwa.

Thibitisho: . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

12EP05

Page 21: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 6 –

Kamilisha jedwali lifuatalo kwa kuonyesha ni nani au nini neno/maneno yaliyopigiwa mstari yanarejelea. Tumia aya ya kwa majibu yako.

Katika kifungu… neno/ maneno… li/yanarejelea…

Mfano: …ikaamua kutoa fursa… (mstari 30) “ikaamua” . . . . . . . . . . . . . .serikali . . . . . . . . . . . .

24. …ilikuwa moja tu… (mstari 32) “ilikuwa” . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

25. …yanayotoa elimu ya… (mstari 33) “yanayotoa” . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

26. …ya msingi ambayo… (mstari 35) “ambayo” . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

12EP06

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 7 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

Kifungu C — Mazingira machafu na athari zake

Jibu maswali yafuatayo. Tumia aya ya kwa majibu yako.

27. Taja jukumu moja kila mtu anapaswa kuhakikisha analo?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

28. Ni kwa nini tunafaa kudumisha uzima wetu?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

29. Ni tishio gani kubwa kwa afya mijini na vijini?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Tafuta maneno kutoka kwenye kifungu yenye maana hizi. Tumia aya ya hadi kwa majibu yako.

30. Mambo au kazi zinazofanywa.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

31. Hasara au matumizi ya matendo fulani.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

32. Tabia ya kuvuruga kitu au jambo.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

33. Mahali vitu huwekwa na kutunzwa ili viwe salama.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

12EP07

Page 22: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 8 –

Jibu maswali yafuatayo. Tumia aya ya hadi kwa majibu yako.

34. Kwa nini ni kawaida sana kuona taka nyingi kila mahali?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

35. Taja athari moja ya kuishi katika maeneo yenye taka nyingi.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

36. Taja njia mbili ambazo magonjwa mbalimbali husambazwa kutokana na taka zisizotupwa au kuharibiwa vizuri. [alama 2]

(a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

37. Ni kifungu gani cha maneno kinaonyesha kuwa matumizi mengi yatokanayo na maradhi yataenda chini?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

12EP08

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 9 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

Kifungu D — Teknolojia na mtindo wa maisha

38. Kutokana na kauli A hadi F, chagua kauli mbili ambazo ni sahihi kulingana na kifungu hiki. Andika jibu mwafaka kwenye kisanduku ulichopewa. Tumia aya ya kwa majibu yako. [alama 2]

Mfano: B

A. Intaneti imekuwa ikifikia kila mtu tangu mwanzo.

B. Watu wote kwa jumla wanaweza kupata intaneti.

C. Mifumo ya mawasiliano ya zamani imebadilishwa na intaneti.

D. Mtindo wa maisha unabadilika kwa nadra sana kwa sababu ya teknolojia mpya.

E. Mtindo wa maisha umebadilishwa kwa kiasi kikubwa na teknolojia mpya.

F. Mawasiliano ya zamani yanapendelewa na watu wengi zaidi.

Jibu maswali yafuatayo. Tumia aya ya kwa majibu yako.

39. Ni mwelekeo gani Alfred Adler alichukua alipoibuka na dhana ya mtindo wa maisha?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

40. Taja sifa moja kuu ya mtindo wa maisha.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

41. Ni kifungu gani cha maneno kinachodhihirisha kuwa bado kuna shida nyingi katika kutafiti mtindo wa maisha?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

42. Swali kuhusu mojawapo ya sifa za mtindo wa maisha limetokea kutokana na nini?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

12EP09

Page 23: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 10 –

Chagua kifungu sahihi cha maneno kutoka katika kifungu hiki kumalizia sentensi zifuatazo. Tumia aya ya kwa majibu yako..

Mfano: Walikoishi watu kulisaidia…

. . . . . . . . . . . . . . . . kuunda utambulisho wa kijamii wa mwanadamu. . . . . . . . . . . . . . . . .

43. Kukaa katika eneo ndogo kulisababisha mtu kujulikana…

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

44. Sio watu wengi…

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

45. Kutokana na kuvumbuliwa kwa teknolojia mpya…

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Chagua jibu sahihi kutoka kwa A, B, C, D. Andika herufi ya uchaguzi wako katika kisanduku.

46. Makala hii ina umuhimu gani?

A. Kuimarisha matumizi ya teknolojia katika maisha ya kila siku. B. Kuelimisha jamii kuhusu teknolojia ya kisasa. C. Kujadili athari za teknolojia ya sasa kwa maisha. D. Kujadili changamoto za maisha ya teknolojia mpya.

12EP10

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 11 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

Kifungu E — Tumbombele mla misitu

Jibu swali lifuatalo. Tumia aya ya kwa majibu yako.

47. Andika vifungu vitatu vya maneno ambavyo mwandishi ametumia kuipa miti hisia za binadamu au mnyama. [alama 3]

(a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(c) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Chagua jibu sahihi kutoka kwa A, B, C, D. Andika herufi ya uchaguzi wako katika kisanduku. Tumia aya ya hadi kwa majibu yako.

48. Chagua kauli isiyo ya kweli kulingana na kifungu.

A. Tumbombele alikuwa na elimu ya kiwango cha chini. B. Majina ya miti yalimtatiza Tumbombele. C. Masomo ya Tumbombele yalikuwa wazi kwa kila mtu. D. Ilikuwa vigumu kuelewa masomo ya Tumbombele.

49. Ni kwa njia gani wambunge kama Tumbombele waliteuliwa kama mawaziri?

A. Kutokana na kimbunga kikali cha kisiasa. B. Kwa sababu walikuwa wambunge wa Bumbi. C. Walikuwa mbumbumbu wenye elimu duni. D. Walikuwa wafuasi wa chama kilichokuwa kinatawala.

12EP11

Page 24: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/Q– 12 –

Jibu maswali yafuatayo. Tumia aya ya hadi kwa majibu yako.

50. Taja sababu ya waziri Tumbombele kutembelea msitu wa Mvule baada ya kuteuliwa.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

51. Taja sababu moja ya miti kusemekana kuwa ni uhai.

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

52. Ni adhabu gani ilipendekezwa na waziri kuhusu ukiukaji wa amri ya kutokata miti ya kiasili?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

53. Ni maneno gani katika kifungu yanamaanisha umma ulitawanyika?

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Ni maneno yapi yanaweza kujaza mapengo katika aya ya ? Chagua maneno kwenye orodha uliyopewa na kisha uyaandike hapo chini.

hotuba kivuli shule wizara

kiu mapato waziri ziara

Mfano: [ – X – ] . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .ziara . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

54. [ – 54 – ] . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

55. [ – 55 – ] . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

56. [ – 56 – ] . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

12EP12

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T

Swahili B – Higher level – Paper 1Swahili B – Niveau supérieur – Épreuve 1Swahili B – Nivel superior – Prueba 1

© International Baccalaureate Organization 20168 pages/páginas8816 – 2316

Text booklet – Instructions to candidates

• Do not open this booklet until instructed to do so.• This booklet contains all of the texts required for paper 1.• Answer the questions in the question and answer booklet provided.

Livret de textes – Instructions destinées aux candidats

• N’ouvrez pas ce livret avant d’y être autorisé(e).• Ce livret contient tous les textes nécessaires à l’épreuve 1.• Répondez à toutes les questions dans le livret de questions et réponses fourni.

Cuaderno de textos – Instrucciones para los alumnos

• No abra este cuaderno hasta que se lo autoricen.• Este cuaderno contiene todos los textos para la prueba 1.• Conteste todas las preguntas en el cuaderno de preguntas y respuestas.

1 h 30 m

Friday 4 November 2016 (afternoon)Vendredi 4 novembre 2016 (après-midi)Viernes 4 de noviembre de 2016 (tarde)

Page 25: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 2 –

Blank pagePage vierge

Página en blanco

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 3 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

Kifungu A

Kanga, vazi linalowakilisha utamaduni wa Kitanzania

5

10

15

20

25

30

Ingawa Tanzania kuna makabila zaidi ya 120 yenye mavazi tofauti kanga ni miongoni mwa mavazi yanayowakilisha utamaduni wa Watanzania kwa kuwa linatumiwa takribani na makabila yote.

Kanga ni kipande cha kitambaa kilichorembwa kwa maua, rangi mbalimbali na kuchapishwa maneno. Maneno haya hutoa tafsiri kulingana na utamaduni wa jamii husika. Doti moja ya kanga ni kipande cha kitambaa chenye upana usiozidi mita moja na urefu usiozidi mita nne ambacho hukatwa katikati na kupata vipande viwili vyenye kimo sawa.

Vazi la kanga ni maarufu zaidi kwa Waswahili wa maeneo ya mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki hasa Tanzania katika pwani ya Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar, Kilwa, Bagamoyo na Kenya hasa Mombasa na Malindi. Kwa mujibu wa historia ya uvaaji wa kanga, vazi hilo lilianza kutumika na kupata umaarufu tangu karne ya 19 ambapo kanga zilivaliwa zaidi na wanawake katika sehemu zenye joto.

Kuenea kwa vazi hilo katika ukanda wa pwani kuliwavutia pia watu wa bara ambao walianza kutumia kanga kama vazi la ziada na kuwafanya wageni wanaotembelea Afrika Mashariki kuvutiwa na jinsi kanga inavyotumiwa na watu wa makabila mbalimbali kwa matumizi mbalimbali. Uvaaji wa kanga hutoa tafsiri tofauti kulingana na haja ya wavaaji wenyewe.

Kuna wale wanaoona kuwa kanga ni vazi la ziada kwa mwanamke ambapo huvaa nguo kisha juu hujitanda kanga kama nguo ya ziada. Wengine husema kuwa ni vazi maalum la siku ya harusi kwa wanawake, yaani Bibi harusi. Tafsiri ya wengi husema kuwa kanga ni nguo au vazi la kwanza kwa mtoto mchanga siku anayokuja duniani. Hata hivyo matumizi ya kanga ni mengi na baadhi ya makabila wanatumia kanga kama vazi maalum hususani wakati wa sala kwa wanawake wa Kiislamu.

Pia joto linapokithiri baadhi ya watu huvaa kanga kwa kuwa ni vazi jepesi kwa ajili ya kupunguza joto. Kanga pia hutumika kama taulo ya kufuta maji baada ya kuoga. Vilevile, kanga hutumika kama sare maalum ya harusi kwa koo mbili zinazoungana ambapo sare ya kanga hutumika kama ishara ya kujenga umoja, upendo na mshikamano.

Lucy Lyatuu, HabariLeo (2015)

Page 26: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 4 –

Kifungu B

Fursa ya elimu – Zanzibar

5

10

15

20

25

30

35

Tangu yafanyike mapinduzi matukufu ya watu wa Zanzibar, kumekuwa na mabadiliko katika fursa za elimu. Mahali pa elimu ya wachache pamechukuliwa na elimu ya wengi. Kabla hatujayachunguza mabadiliko haya vipi yamewapatia fursa za kupata elimu watoto wa wafanyakazi na wakulima, yatupasa tutupie jicho utaratibu wa elimu uliotolewa miaka ya nyuma.

Zanzibar ilipokuwa chini ya utawala wa wachache fursa nyingi za elimu zilitolewa kwa tabaka. Ama kwa tabaka la mabwanashamba au kwa tabaka tawala na kwa nadra zilitolewa kwa watoto wa wanyonge waliokuwa na vipawa maalum ambavyo watoto wa matabaka ya mwanzo na ya pili hawakuwa navyo. Watoto wa tabaka la chini walipata elimu ya muda mfupi. Elimu waliyopata haikuwawezesha kushika dhamana muhimu za serikali. Nafasi walizoweza kushika ni za chini ambazo malipo yake pia yalikuwa ni madogo. Hata hizo nafasi walizozishika, mathalan, kusomesha shule za msingi, kusaidia kuuguza wagonjwa hospitalini au ukarani wa daraja la chini, zilikuwa chache mno. Kwa hivyo, ililazimu vijana wengi wakomee darasa la 7 au 8.

Kukosa nafasi za kuendelea na masomo au kuajiriwa serikalini kuliwafanya vijana warudi vijijini ambako mfumo mbaya wa elimu ya kikoloni ulikwisha kuwatenga na wakulima. Elimu ya miaka saba au minane waliyoipata haikuweza kuwafanya wawe wakulima, kwani haikuwatayarisha kwa maisha ya baadaye. Mengi kati ya yale waliyojifunza hayakuhusu mazingira yao. Kwa hivyo, wanafunzi walibaki bado wageni katika nchi yao. Watoto wa wachache, wa matabaka tawala pamoja na waliomiliki mashamba na idadi ndogo mno ya watoto wa wanyonge wenye kipawa cha kupigiwa mfano, ndio walioweza kuendelea na skuli za sekondari na hata Chuo cha Makerere, Uganda na mwishowe Ulaya.

Sasa Zanzibar ina utaratibu mpya wa elimu, utaratibu huu umeanzishwa baada ya mapinduzi. Lengo la mpango mpya wa elimu ni kuwakomboa wananchi kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Utaratibu huu uliojengwa juu ya usawa – bila kujali rangi au dini ya mtu unatoa fursa za elimu kwa wote ili kuwaunganisha watu na hatimaye kujenga jamii ya kijamaa. Katika kutayarisha mpango wa kuzigawa fursa za elimu, serikali ya wafanyakazi na wakulima ilichukua hatua zifuatazo; kwanza iliondoa ada za shule, pili, skuli zote zilizokuwa zikiendeshwa na makabaila zilichukuliwa na serikali.

Serikali mpya haikutosheka na mabadiliko hayo; ikaamua kutoa fursa zaidi. Kabla ya mapinduzi kulikuwa na skuli tatu hapa Zanzibar zilizotoa elimu ya sekondari. Huko Pemba ilikuwa moja tu. Leo kuna shule kadhaa zinazotoa elimu ya sekondari ya kidato cha 1 hadi 3 na kuna madarasa yasiyopungua 40 yanayotoa elimu ya kidato cha 4. Vyuo navyo vimeongezeka. Kwa mfano, kuna vyuo vinavyowatayarisha wanafunzi kwa kilimo, uvuvi na ufundi. Lakini, mabadiliko makubwa kabisa yanaonekana katika elimu ya msingi ambayo imekusudiwa kuwapatia nafasi watoto wote waliofikia umri wa kuingia shule.

Haji Ameir, Mazoezi ya Ufahamu (1981)

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 5 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

Kifungu C

Mazingira machafu na athari zake

Kuwa na afya bora, pamoja na kuendelea kuwa na afya bora ni wajibu wa kila binadamu. Tunahitaji kuwa na miili yenye afya bora na nguvu ili tuweze kuendelea na shughuli zetu za kila siku katika ujenzi wa taifa. Mtakubaliana na mimi kuwa ili taifa lipate maendeleo ya haraka, halina budi kuwa taifa la watu wenye afya njema. Ni wazi kabisa katika nyakati hizi, na katika jamii tunayoishi, na katika vijiji, miji na majiji, kiwango cha usafi wa mazingira ni duni sana na hamna viwango maalum vilivyowekwa katika kuyaweka mazingira safi.

Nadhani kinachotufanya tuwe hivi na kutojali kuyaweka mazingira yetu yawe safi, ni mazoea tuliyokuwa nayo na tumekulia katika mazingira yasiyo safi hali iliyotufanya tuzoee mazingira yasiyo safi. Ona vyakula viuzwavyo mtaani bila kufunikwa katika vumbi jingi na moshi mzito utokanao na magari na shughuli nyingine, lakini tunanunua na kula. Ni kweli kuwa ulaji huo hupelekea kupata magonjwa ambayo hutufanya tujikute katika hospitali mbalimbali tukihangaika kuokoa maisha yetu. Ni gharama kwetu na gharama kwa taifa.

Tazama wasafiri wa vyombo mbalimbali vya majini, mijini, katika mikoa na hata nje ya nchi watupavyo taka katika mazingira bila kujali uharibifu, bila kujali kama ni mbuga ya wanyama, kama ni chanzo cha maji na hata bila kujali kama ni msitu wa hifadhi.

Kwa kuwa hatuna mazoea ya kutupa na kuharibu taka katika njia iliyo sahihi, siyo ajabu kuona taka za majumbani na hata viwandani zikiwa zimetupwa ovyo mitaani, barabarani, katika majengo ambayo hayatumiki, katika mitaro, mtoni, chini ya madaraja, fukwe za bahari na maziwa, mbuga za wanyama na hata katika misitu. Taka hizi hutoa harufu mbaya na kali hata kama mtu anapita mita kadhaa mbali na taka hizo. Pia ni kero kubwa kuishi katika baadhi ya makazi kutokana na rundo kubwa la taka katika maeneo hayo zitoazo harufu kali na sumu mbalimbali zinazowaathiri kiafya wakazi hao.

Taka zinazozalishwa na familia zaweza kuwa hatari zisipotupwa na kuharibiwa katika njia iliyo sahihi. Taka hizi zaweza kupelekea milipuko ya magonjwa hatari, na zinapoachwa wazi zinaweza kuchafua mazingira, na kusambaza magonjwa kupitia upepo unaovuma, wadudu kama nzi na mende, na pia uambukizo wa magonjwa waweza kusambazwa kupitia njia ya upumuaji. Vimelea vya magonjwa vyaweza pia kuingia katika vinywaji visivyofunikwa, vyakula vilivyoachwa wazi barabarani na kusababisha magonjwa kama kuhara damu, kipindupindu, homa ya tumbo, minyoo, kichefuchefu na kutapika.

Kwa hiyo basi, kuyaweka mazingira yetu katika hali ya usafi, kutatuepusha na matatizo mengi yakiwemo magonjwa mbali mbali. Pia tutapunguza gharama kubwa zitumikazo katika matibabu ya magonjwa hayo. Nchi yenye watu wenye afya ni nchi yenye mazingira mazuri na safi kwa ukuaji wa uchumi wake.

https://sayansiyaafya.blogspot.co.uk (2015)

Page 27: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 6 –

Kifungu D

Teknolojia na mtindo wa maisha

Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kujiunga nami katika makala hii ambayo huangazia taathira za teknolojia mpya za mawasiliano na habari na hasa intaneti katika mtindo wa maisha ya mwanadamu. Katika miaka ya awali ya utumizi wake, intaneti ilikuwa ikitumika na watu wachache tu lakini sasa watu wote wa dunia wanaweza kutumia intaneti. Mtandao huu uliojaa maelezo na ambao pia una uwezo wa mawasiliano ambao hutumiwa na watu wa matabaka yote sasa umekuwa kitu cha kawaida katika dunia ya leo. Kustawi kwa kasi kwa utumizi wa intaneti ni nukta ambayo haiwezi kupingika. Kwa upande mwingine, mabadiliko katika vifaa vya mawasiliano ya kisasa ni jambo ambalo limepelekea kutikisika misingi ya suhula za zamani za mawasiliano. Wataalamu na wanafikra wanaweza kuchangia pakubwa katika teknolojia za kisasa kwa kuvumbua mambo ambayo yanaweza kuwa na faida kwa jamii. Hivi sasa kufuatia ustawi wa kasi wa intaneti tunashuhudia kuongezeka kwa idadi ya watumizi wake kiasi kwamba masuala mengi zaidi ya mtindo wa maisha yanaathiriwa na teknolojia hii.

Dhana ya "mtindo wa maisha" ilitumiwa kwa mara ya kwanza katika karne ya 20 na Alfred Adler mwanasaikolojia au mtaalamu wa elimu ya nafsi kutoka Ujerumani. Hata hivyo, mtazamo wake kuhusu "mtindo wa maisha" ulikuwa wenye muelekeo wa kisaikolojia tu na hivyo haukuangazia mielekeo mingine kama vile ya kijamii. Hivi sasa nadharia ya "mtindo wa maisha" ina uhusiano wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja na taaluma za saikolojia, tabia, uchumi, usimamizi, mauzo, soshiolojia, utamaduni na sayansi ya mawasiliano. Moja ya sifa maalumu za "mtindo wa maisha" ni kuwepo uwezo wa kuchagua na kuwa chaguo hili hugeuka na kuwa simulizi ya mtu binafsi ambayo huweza kumuarifisha miongoni mwa wengine. Kuna mielekeo miwili katika kuarifisha au kubainisha maana ya "mtindo wa maisha". Muelekeo wa kwanza ni kuhusu tabia au mwenendo na pili ni thamani za kimaisha. Pamoja na hayo, kumekuwepo na changamoto nyingi katika kuchunguza kadhia ya "mtindo wa maisha" na hivyo bado kunahitajika utafiti zaidi na wa kina. Pamoja na hayo, kuibuka kwa teknolojia mpya katika maisha ya mwanadamu kumepelekea kujitokeza swali kuhusu "uwezo wa kuchagua" kama moja ya sifa za "mtindo wa maisha".

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 7 –

Turn over / Tournez la page / Véase al dorso

Siku za nyuma, eneo la kuishi, kufanya kazi na kadhalika lilikuwa na nafasi ya kimsingi katika kuunda utambulisho wa kijamii wa mwanadamu. Hii ni kwa sababu mwanadamu alikuwa akiishi katika eneo dogo na hivyo utambulisho wake wa kijamii ulibainika kupitia uhusiano na maingiliano yake na watu aliokuwa akiishi karibu nao. Ni watu wachache tu waliokuwa na uhusiano na dunia ya nje ya miji au vijiji vyao na kwa msingi huo mila na desturi za kikaumu au kikabila zilikuwa na nafasi muhimu katika utambulisho wa watu. Kufuatia kuibuka kwa teknolojia mpya ya habari na mawasiliano, nafasi ya eneo si muhimu sana katika kuunda utambulisho wa mtu binafsi.

http://kiswahili.irib.ir (2015)

Page 28: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N16/2/ABSWA/HP1/SWA/TZ0/XX/T– 8 –

Kifungu E

Tumbombele mla misitu

Miti ilifurahia amani isiyo na kipimo hadi siku ambayo Tumbombele aliteuliwa kuwa waziri wa misitu katika nchi ya Mbalungi. Tumbombele alikuwa amechaguliwa na wakazi wa eneo bunge la Bumbi katika uchaguzi wa mwaka uliotangulia. Kabla ya hapo, miti ilishangilia hewa mwanana iliyovuma vuu vuu! Kutoka mti mmoja kuelekea mwingine. Kuteuliwa kwa Tumbombele hakukupokelewa kwa furaha na miti. Badala yake kulizua kilio na huzuni.

Tumbombele alikuwa mbumbumbu mwenye elimu duni. Ungemuuliza majina ya miti ya kiasili hangeweza kukutajia hata mmoja. Historia yake ya elimu iligubikwa kwenye giza totoro. Ilisemekana mara alifika hadi kidato cha kwanza. Wakati mwingine ilisemekana kuwa hajawahi kuona mlango wa shule ya upili. Masomo yake yaligubikwa na utata.

Kimbunga kikali cha kisiasa kilichovuma nchini humo mwaka uliotangulia kilipeperusha hata wasiokuwa na ajenda yoyote hadi wakaingia bungeni. Hatimaye waliteuliwa kuwa mawaziri mradi tu wawe wakereketwa wa chama tawala licha ya elimu yao pungufu. Mmoja wa wale waliofaidika kutokana na vuguvugu hilo alikuwa Tumbombele.

Mara tu baada ya kuteuliwa waziri wa misitu, Tumbombele alifanya ziara ya kujifahamisha hali ya misitu ilivyokuwa nchini humo. Kwanza alitembelea msitu wa Mvule. Maafisa wa misitu, walinzi wa misitu, machifu na manaibu wao na wananchi walikuja kumsikiliza waziri mpya wa misitu. Hii pia ilikuwa sherehe ya kumkaribisha nyumbani baada ya kuteuliwa kuwa waziri.

Tumbombele alisimama mbele ya uwanja akaanza kuhutubu: “Serikali yetu inatambua umuhimu wa misitu. Inatambua miti ni uhai. Miti hutupatia hewa safi inayovuma kutoka kusini kuelekea kaskazini. misitu ni uhai. Asiyehifadhi miti hana nafasi katika Bumbi na nchini kwa jumla.” Wananchi walimpigia makofi na ukemi kumshangilia. “Kuanzia sasa ni marufuku kukata miti hasa ya kiasili kwa shughuli zozote zile. Anayetaka kuozea jela ajaribu kukata miti ya kiasili ovyoovyo”. Watu walimshangilia zaidi. Aliendelea kuzungumzia manufaa ya kuhifadhi mazingira na hasara ya kutofanya hivyo. Kisha mkutano ukafika mwisho wake. Watu walifumukana kuelekea makwao. Hotuba ya waziri Tumbombele ilijaa matumaini. Iliwapa watu wa Bumbi na nchi nzima ya Mbalungi uhai na mwamko mpya.

Baada ya [ – X – ] yake ya kujifahamisha na hali ya misitu, Tumbombele alirudi jijini. Aliwaza na kuwazua kuhusu utajiri wa nchi ya Mbalungi. Alijisemea kimoyomoyo, “Mimi ni waziri wa misitu. Mtu huvuna apandacho. Si walisema kuwa mtu hujipatia [ – 54 – ] kutokana na kazi aifanyayo? Kwa nini nisijifaidi kutokana na [ – 55 – ] ninayosimamia? Nitafanya mipango”. Kutoka siku, hiyo [ – 56 – ] cha kupata pesa kwa njia za mkato kilimwingia hadi mishipani.

Kobia John, Kurudi Nyumbani na Hadithi Nyingine (2007)

N16/2/ABSWA/HP2/SWA/TZ0/XX

Swahili B – Higher level – Paper 2Swahili B – Niveau supérieur – Épreuve 2Swahili B – Nivel superior – Prueba 2

© International Baccalaureate Organization 20163 pages/páginas8816 – 2317

Instructions to candidates

• Do not open this examination paper until instructed to do so.• Section A: choose one task. Each task is worth [25 marks].• Section B: write a personal response to the stimulus provided. The task is worth [20 marks].• The maximum mark for this examination paper is [45 marks].

Instructions destinées aux candidats

• N’ouvrez pas cette épreuve avant d’y être autorisé(e).• Section A : choisissez une tâche. Chaque tâche vaut [25 points].• Section B : exprimez votre opinion personnelle sur la réflexion fournie. La tâche vaut [20 points].• Le nombre maximum de points pour cette épreuve d’examen est de [45 points].

Instrucciones para los alumnos

• No abra esta prueba hasta que se lo autoricen.• Sección A: elija una tarea. Cada tarea vale [25 puntos].• Sección B: escriba una opinión personal al estímulo provisto. La tarea vale [20 puntos].• La puntuación máxima para esta prueba de examen es [45 puntos].

1 h 30 m

Monday 7 November 2016 (afternoon)Lundi 7 novembre 2016 (après-midi)Lunes 7 de noviembre de 2016 (tarde)

Page 29: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

N16/2/ABSWA/HP2/SWA/TZ0/XX– 2 –

Sehemu A

Kamilisha mojawapo wa kazi zifuatazo. Andika maneno 250 hadi 400.

1. Utofauti wa tamaduni

Lugha ya sheng imesambaa na kuwa maarufu miongoni mwa wanafunzi. Katika darasa lako la lugha mtajadili mada hii: “Sheng inaathiri wanafunzi kujieleza kwa lugha sanifu”. Andika makala ya kufungua hotuba yako kukataa au kukubaliana na mada hii.

2. Mila na desturi

Katika gazeti moja la taifa, mwandishi mmoja ameandika kuhusu kusitisha sherehe zote za kidini na za kitaifa ili watu wote wawe sawa. Andika barua kwa mhariri wa gazeti hili huku ukitoa mawazo yako kuhusu jambo hili.

3. Afya

Katika shule jirani, kumetokea mkurupuko wa ugonjwa wa kuambukiza sana. Kama mwakilishi wa wanafunzi, utaandika maagizo katika tovuti ya shule kuhusu jinsi ya kujikinga, hatua za kuchukua mtu akiambukizwa, na mapendekezo ya kuepuka kuusambaza.

4. Burudani

Unataka kujua ni shughuli gani vijana hufurahia kufanya siku hizi. Umeamua kufanya utafiti miongoni mwa marafiki zako ukitumia mitandao ya kijamii kuhusu shughuli wanazopendelea zaidi. Andika ripoti kuhusu matokeo ya utafiti huo na utoe maoni yako kuyahusu.

5. Sayansi na teknolojia

Mkurugenzi mkuu wa kampuni moja ya simu nchini amealikwa shuleni kuongea kuhusu faida na umuhimu wa teknolojia katika jamii. Umeteuliwa kuongoza mahojiano baina yako na yeye kwa niaba ya wanafunzi wengine. Andika mahojiano yatakayochapishwa katika jarida la shule.

N16/2/ABSWA/HP2/SWA/TZ0/XX– 3 –

Sehemu B

Kulingana na kichocheo kifuatacho, toa jibu lako binafsi na ulithibitishe. Chagua maandiko yoyote uliyoyasoma darasani. Andika maneno kati ya 150 na 250.

6. Licha ya juhudi kabambe na hatua anuwai kuchukuliwa ili kuyatunza na kuyahifadhi mazingira, athari za uharibifu wa mazingira zinajidhihirisha kila mahali na kila siku.

Page 30: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

Instructions to candidates

• Do not open this examination paper until instructed to do so.• Section A: choose one task. Each task is worth [25 marks].• Section B: write a personal response to the stimulus provided. The task is worth [20 marks].• The maximum mark for this examination paper is [45 marks].

Instructions destinées aux candidats

• N’ouvrez pas cette épreuve avant d’y être autorisé(e).• Section A : choisissez une tâche. Chaque tâche vaut [25 points].• Section B : exprimez votre opinion personnelle sur la réflexion fournie. La tâche vaut [20 points].• Le nombre maximum de points pour cette épreuve d’examen est de [45 points].

Instrucciones para los alumnos

• No abra esta prueba hasta que se lo autoricen.• Sección A: elija una tarea. Cada tarea vale [25 puntos].• Sección B: escriba una opinión personal al estímulo provisto. La tarea vale [20 puntos].• La puntuación máxima para esta prueba de examen es [45 puntos].

1 h 30 m

Swahili B – Higher level – Paper 2Swahili B – Niveau supérieur – Épreuve 2Swahili B – Nivel superior – Prueba 2

Tuesday 7 November 2017 (morning)Mardi 7 novembre 2017 (matin)Martes 7 de noviembre de 2017 (mañana)

3 pages/páginas © International Baccalaureate Organization 2017

N17/2/ABSWA/HP2/SWA/TZ0/XX

8817 – 2317

Sehemu A

Kamilisha mojawapo wa kazi zifuatazo. Andika maneno 250 hadi 400.

1. Utofauti wa tamaduni

Unaishi katika nchi inayozungumzwa Kiswahili na mji wako umewavutia wahamiaji wengi wageni, suala ambalo limesababisha utofauti wa tamaduni. Andika katika blogu ambapo utajadili faida na changamoto za utofauti wa tamaduni katika jamii.

2. Mila na desturi

Unaishi katika nchi inayozungumzwa Kiswahili kwa mara ya kwanza ambapo familia moja imekukaribisha uishi nayo na baadhi ya mila na desturi ni ngeni kwako. Jana, uliaibika kwa sababu ulikosa kufuata jambo moja la kitamaduni katika nchi hiyo bila kukusudia. Andika kwenye shajara ukieleza kilichotokea, na kile ulichosoma kutokana na tukio hilo.

3. Afya

Marafiki zako wengi wamefanya maamuzi fulani ya chakula (kama vile kuepuka nyama, maziwa na mafuta). Uliwahoji wawili wao kuhusu sababu za uamuzi wao. Andika mahojiano hayo, yatakayochapishwa katika sehemu ya ‘Afya’ ya jarida la shule yako.

4. Burudani

Pesa ina jukumu muhimu katika michezo siku hizi. Umeombwa utoe hotuba kwa wanafunzi wenzako kuhusu upande chanya wa hali hii. Andika hotuba yako.

5. Sayansi na teknolojia

Kampuni nyingi za usafiri wa umma zinaanza kuwapa wasafiri wao huduma za bure za Wi-Fi. Hata hivyo, kampuni ya mabasi katika eneo unaloishi bado haina huduma hii. Andika barua kwa mkurugenzi wa kampuni hiyo ukieleza umuhimu na faida ambazo huduma ya bure ya intaneti inaweza kuwa nazo kwa kampuni hiyo.

– 2 – N17/2/ABSWA/HP2/SWA/TZ0/XX

Page 31: Swahili B Higher level Paper 1 Swahili B Niveau supérieur Épreuve … · 2019-10-23 · y Mafuta ya kupikia nusu kikombe. y ijiko vitatu vya chakula vya limau. Njia Baada ya kukata

Sehemu B

Kulingana na kichocheo kifuatacho, toa jibu lako binafsi na ulithibitishe. Chagua maandiko yoyote uliyoyasoma darasani. Andika maneno kati ya 150 na 250.

6. Katika dunia yetu, vijana wanastahili kujifunza lugha zinazozungumzwa na wengi pekee.

– 3 – N17/2/ABSWA/HP2/SWA/TZ0/XX

Recommended