+ All Categories
Home > Documents > CHRISTIAN ETHICS/MAADILI YA KIKRISTO

CHRISTIAN ETHICS/MAADILI YA KIKRISTO

Date post: 03-Feb-2023
Category:
Upload: udsm
View: 0 times
Download: 0 times
Share this document with a friend
19
Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania 1 MAADILI YA KIKRISTO Maadili ni nini? Maadili ni “Ni mpangilio wa kanuni bora zinazotawala mwenendo wa kundi maalum la watu. 1 ” Fasili hii inamaanisha kwamba maadili ni: Kwa mujibu wa maana hii kumbe kila kundi la watu lina kanuni zake zinazotawala mwenendo mzima wa kundi hilo. Kwa maana hiyo ni sahihi kusema kuna maadili ya kikristo, maadili ya kiualimu, maadili ya kiuongozi nk. 2 maadili ni “maelekezo yanayofaa ambayo hutolewa kupitia wasilisho fulani.” Ukiangalia vizuri zaidi fasiri hii utagundua kuwa mwandishi anakaza juu ya maelekezo yanayofaa, kwa maana hiyo yale maelekezo yasiyofaa hayo siyo maadili. Watu wengine hutumia neno ‘maadili’ kumaanisha mafundisho kuhusu ‘ukweli na uongo’ uzuri na wema. Wengine wanasema kwamba maadili yanahusika na tabia za watu zilizo nzuri au mbaya. Kulingana na fasili hii tunaweza kupata maana moja ya maadili kwamba ni mpangilio wa kanuni bora ambazo zimelenga kutoa maelekezo yanayofaa kwa ajili ya kundi fulani la watu katika jamii husika. Maadili ya kikristo ni mpangilio wa kanuni bora ambazo zimelenga kutoa maelekezo yanayofaa kwa ajili ya wakristo. Wataalam wengine hudai kuwa Maadili ya Kikristo muhtasari wake umetolewa na Wakolosai 3:1-6 : "Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkon wa kuum wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maan mlikufa na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu 3 . Huku zaidi ya orodha ya "kufanya" na ya "kutofanya ," Biblia inatupa maelekezo ya kina juu ya namna tunapaswa kuishi. Biblia ndio kila kitu tunahitaji kujua kuhusu jinsi ya kuishi maisha ya 1 Kunhiyop, S.Y. (2008:). African Christian Ethics. Nairobi: Wordalive Publishers 2 Ndallu na wenzake (2014). Kamusi Teule ya Kiswahili Sanifu. NairobiL: EEP 3 www.gotquestions.org/Kiswahili/Maadili-ya-Kikristo.html Na. mch. Daniel John Seni Utangulizi Maadili ya kikristo yamefupishwa katika kitabu cha Wakolosai 3:1- 6. Si kila kitu kiko wazi katika Biblia bali tunahitaji kusoma kwa makini na kuweza kutumia katika maisha yetu ya kila siku. Kwa mfano suala la madawa ya kulevya halijazungumziwa katika biblia lakini tukiangalia madhara ya madawa ya kulevya tunaweza kujua kwamba ni hatari kwa afya na hivyo kuharibu hekalu la Roho Mtakatifu (1 Kor 6:19-20). Lakini pia Roho Mtakatifu aliye ndani yetu aliye mafuta ndiye anatufundisha na hivyo tunaweza kujua
Transcript

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

1

MAADILI YA KIKRISTO Maadili ni nini?

Maadili ni “Ni mpangilio wa kanuni bora

zinazotawala mwenendo wa kundi

maalum la watu.1” Fasili hii inamaanisha

kwamba maadili ni:

Kwa mujibu wa maana hii kumbe kila

kundi la watu lina kanuni zake

zinazotawala mwenendo mzima wa

kundi hilo. Kwa maana hiyo ni sahihi

kusema kuna maadili ya kikristo, maadili

ya kiualimu, maadili ya kiuongozi nk.

2maadili ni “maelekezo yanayofaa ambayo hutolewa kupitia wasilisho fulani.” Ukiangalia vizuri

zaidi fasiri hii utagundua kuwa mwandishi anakaza juu ya maelekezo yanayofaa, kwa maana

hiyo yale maelekezo yasiyofaa hayo siyo maadili.

Watu wengine hutumia neno ‘maadili’ kumaanisha mafundisho kuhusu ‘ukweli na uongo’ uzuri

na wema. Wengine wanasema kwamba maadili yanahusika na tabia za watu zilizo nzuri au

mbaya.

Kulingana na fasili hii tunaweza kupata maana moja ya maadili kwamba ni mpangilio wa kanuni

bora ambazo zimelenga kutoa maelekezo yanayofaa kwa ajili ya kundi fulani la watu katika

jamii husika.

Maadili ya kikristo ni mpangilio wa kanuni bora ambazo zimelenga kutoa maelekezo yanayofaa

kwa ajili ya wakristo. Wataalam wengine hudai kuwa Maadili ya Kikristo muhtasari wake

umetolewa na Wakolosai 3:1-6 : "Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo

juu Kristo aliko, ameketi mkon wa kuum wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.

Kwa maan mlikufa na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo

atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. Basi,

vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na

kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu3.

Huku zaidi ya orodha ya "kufanya" na ya "kutofanya ," Biblia inatupa maelekezo ya kina juu ya

namna tunapaswa kuishi. Biblia ndio kila kitu tunahitaji kujua kuhusu jinsi ya kuishi maisha ya

1 Kunhiyop, S.Y. (2008:). African Christian Ethics. Nairobi: Wordalive Publishers

2 Ndallu na wenzake (2014). Kamusi Teule ya Kiswahili Sanifu. NairobiL: EEP

3 www.gotquestions.org/Kiswahili/Maadili-ya-Kikristo.html

Na. mch. Daniel John Seni

Utangulizi

Maadili ya kikristo yamefupishwa katika kitabu cha Wakolosai 3:1-

6. Si kila kitu kiko wazi katika Biblia bali tunahitaji kusoma kwa

makini na kuweza kutumia katika maisha yetu ya kila siku. Kwa

mfano suala la madawa ya kulevya halijazungumziwa katika biblia

lakini tukiangalia madhara ya madawa ya kulevya tunaweza kujua

kwamba ni hatari kwa afya na hivyo kuharibu hekalu la Roho

Mtakatifu (1 Kor 6:19-20). Lakini pia Roho Mtakatifu aliye ndani

yetu aliye mafuta ndiye anatufundisha na hivyo tunaweza kujua

zaidi masuala ya kimaadili (1 John 2:27).

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

2

Kikristo. Hata hivyo, Biblia haifundishi kila hali ambayo sisi hukumbana nayo katika maisha

yetu. Ni jinsi gani sasa tunaweza kuamua hali kama hizo ambazo Biblia haiko wazi kihivyo

katika kuamua mambo? Hapa ndipo maamzi ya kikristo yanapokuja sasa kutumika!

Sayansi hudai maadili ni "seti ya kanuni za maadili, utafiti wa maadili." Kwa hiyo, maadili ya

Kikristo itakuwa kanuni inayotokana na imani ya Kikristo ambayo sisi hutenda. Wakati neno la

Mungu linaweza kukosa kuangazia kila hali sisi hupitia katika maisha yetu, kanuni zake

hutupatia viwango vya kujiendesha katika hali hizo ambapo hamna maelekezo ya wazi.

Kwa mfano, Biblia haisemi chochote kwa wazi kuhusu matumizi ya dawa za kulevya, lakini

kulingana na kanuni sisi hujifunza kwa njia ya maandiko, tunaweza kujua kwamba ni makosa.

Kwani Biblia inatuambia kwamba mwili ni hekalu la Roho Mtakatifu na kwamba tunapaswa

kumheshimu Mungu nao (1 Wakorintho 6:19-20).

Tunahitaji kujua wazi kwamba neno la Mungu halitoi kila hali ambayo sisi tunakumbana nayo

katika maisha yetu, Katika mambo mengi, tunaweza tu kuona ni nini Biblia inasema na kufuata

mwendo sahihi kwa kuzingatia kanuni hizo. Katika maswali ya kimaadili ambapo maandiko

hayatoi mwelekeo wa wazi, sisi tunapaswa kuangalia kanuni ambayo inaweza kutumika katika

hali hiyo. Tunapaswa kuomba juu ya neno lake, na kujiachilia sisi wenyewe kwa Roho wake.

Roho atatufundisha na kutuongoza katika Biblia kupata kanuni ambazo sisi tunahitaji kusimama

kwayo ili tuweze kuishi kama iwapasavyo Wakristo.

Maadili binafsi

Haya ni maadili yanayohusu mtu binafsi kwa kile ambacho anatakiwa kukifanya katika jamii.

Inahusu hasa na namna mtu anavyotakiwa kufanya kwa upande wake yeye kama yeye.

Maadili ya kijamii

Maadili haya yanahusu mwenendo mzima katika jamii. Katika nchi kama Tanzania mara nyingi

mkazo uko katika maadili ya kijamii kuliko maadili ya kibinafsi. Katika kufunza maadili

tunahitaji pia kujua maana ya maneno haya ili ya yatusaidie kujua zaidi mila na desturi za jamii

husika. Mara nyingi jamii zetu zinaongozwa na maadili ambayo yametawala kama mila na

desturi. Lakini swali la kujiuliza, je mila na desturi hizo ni nzuri? Tusichanganye maana ya

maadili na mila na desturi.

Tamaduni/Utamaduni: Ni desturi fulani za maisha zilizozoelewa au mila au ustaarabu.

Desturi ni kawaida ambazo jamii fulani inaona kuwa ni za lazima au ni jambo la kawaida

litendwalo na watu kila siku au ni ile hali ya mazoea. Desturi zinaweza kuwa nzuri au mbaya ili

mradi watu wamezoea hivyo!

Mila ni mambo yanayofanywa kulingana na chanzo na mazoea ya jamii asili.

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

3

Mila na desturi mara nyingi sana zinapingana na maadili ya kikristo. Wakati mwingine watu

unaweza kuwauliza kwa nini mnafanya hivi? Jibu watakalokwambia ni kwamba kwa sababu

tumekuta wazazi wetu wakifanya hivi, yaani mazoea! Mara nyingi mazoea yanaenda kinyume na

mwenendo wa kikristo. Wakristo wanaongozwa na neno la Mungu. Lakini hata katika neno la

Mungu wakati mwingine watu wanapofasili tofauti baadhi ya vifungu vya Biblia wanaibuka na

maana mpya na kupelekea kuwa na maadili tofauti tofauti ya kikristo. Kwa hiyo tunahitaji kujua

maana halisi katika kufasili baadhi ya vifungu vya kibiblia ili tuweze kufuata kile ambacho Neno

la Mungu limeagiza kuhusu maisha yetu kwa ujumla.

Kila jamii ina maadili yake lakini maadili ya kikristo ya pote! Si kwa watu wa sehemu fulani tu.

Kwa mfano hapa Tanzania tuna makabila zaidi ya 125 lakini ukiangalia kila kabila lina maadili

yake fulani ambayo yanaambatana na mila na desturi (ndani yake kuna miiko kadha wa kadha)

ndani yake lakini maadili ya kikristo yanahitaji kutumika katika hali zote katika makabila haya.

Tunahitaji pia kujua kwamba Biblia kama mwongozo wetu iliandikwa katika utamaduni wa watu

fulani, hata hivyo yapo mambo ya kitamaduni na mambo ambayo Biblia imekaza kama

mwongozo kwa kanisa. Jambo fulani inaweza kuliona jamii totauti na jinsi Biblia inavyolijadili.

Kwa mfano suala la kuacha mke/mume katika jamii nyingi za kiulimwengu ni jambo la kawaida

kabisa lakini Biblia inalijadili kwa upana zaidi.

Chanzo cha maadili ya Kikristo

Maadili ya kikristo chanzo chake kikuu Biblia. Biblia ndiyo kiongozi mkuu katika maadili ya

kikristo. Jamii inaweza kuliona jambo fulani kuwa ni zuri lakini Biblia ikaliona kuwa ni baya.

Kwa mfano suala la kuwa na Boy/Girl Friend na mkawa mnashiriki kimwili ni suala la kawaida

kabisa katika jamii yetu kwa leo lakini jambo hili kibilia linahesabika kama uasherati! Nadhani

katika jambo hili hakuna mjadala sana kwa sababu hakuna andiko lolote linashadidia dai kama

hilo katika maandiko. Kwa hiyo tunahitaji kujua Biblia inasema nini hasa katika jambo fulani

kuliko kuangalia jamii inasema nini.

Chanzo cha maadili yote ni Mungu mwenyewe. Kwa hiyo Mungu ndiye chanzo kikubwa cha

maadili. Mungu ameyafunua maadili hayo kupitia ufunuo wake. Tunajua wazi kwamba Mungu

amejifunua kwa mwanadamu kwa namna mbili; ufunuo wa kawaida/ujumla na ufunuo maalum.

1. Ufunuo wa Kawaida

Ufunuo wa kawaida ni ule ufunuo ambapo Mungu amejifunua mwenyewe kupitia asili, historia

na dhamira za watu. Zab. 19:1 inasema Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, na anga

laitangaza kazi ya mikono yake. Soma pia maandiko haya.Zaburi 147:8-9, Mdo 14:15-17, Rum

2:14-15, Rum 1:21. Nadhani baada ya kusoma mafungu haya umepata kitu pale kwamba Mungu

amejifunua kwa watu kwa namna ya jinsi alivyoumba vitu vyote duniani na kwa dhamira ndani

ya kila mtu. Ni dhahiri kwamba kila mtu anao ufahamu wa ndani kuhusu Mungu. Hakuna mtu

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

4

anayeweza kusema kwamba hakumjua Mungu kwa sababu Mungu ameweka ufahamu wake

ndani yako.

2. Ufunuo maalum

Mungu amejifunua katika ufunuo huu kwa njia ya Neno. Kwa nini ni ufunuo maalum? Kwa

sababu ni njia ya pekee kabisa ambayo Mungu ameitumia ili kujifunua kwa wanadamu, yaani

njia hii inaonyesha suluhisho la dhambi za mwanadamu kwa kumtuma Yesu KRISTO kama

Neno la Mungu halisi yaani lililo hai na kuwa kuwa mwili (Yn 1:14) “Neno akafanyika mwili,

akakaa kwetu” Ufunuo wa Mungu kwa njia ya Neno umegawanyika katika aina mbili:

2.1.Neno lililo hai

Neno lililo hai ni Yesu KRISTO mwenyewe aliyekuja kwa jinsi ya Mwili huku akiwa Neno

halisi yaani akiwa Mungu. Yohana 1:1,14. “hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno

alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu…naye Neno akafanyika mwili akakaa

kwetu”

2.2.Neno kama Biblia. Maandiko yote yameandikwa kwa msaada wa Roho Mtakatifu

(2Petro1:20-21) yaani wanadamu waliandika yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho

Mtakatifu (2Tim 3:16).

Katika kutafuta maarifa katika neno la Mungu tunahitaji kusoma kwa makini, kwa kuzingatia

kanuni za kisarufi na tafsiri ya neno la Mungu kwa wakati huo na wakati wa leo. Inashauriwa

unaporejelea Biblia uwe na usuli wa Biblia nzima. Huwezi kupata usuli huo bila ya kusoma

Biblia nzima. Inashauriwa kusoma Biblia yote ili kujua jambo fulani katika maandiko. Kwa

mfano ukisoma katika Agano la Kale peke yake unaweza kujikuta ukakubaliana na hoja

kwamba kuoa wake wengi ni sawa kwa sababu Biblia inasema hivyo jambo ambalo

linatakiwa liangaliwe katika Biblia nzima. Kwa hiyo kuwa makini kusoma fungu au mstari

mmoja katika Biblia na kutoa mahitimisho yake kwa haraka haraka. Hitimisho lolote lile

linalohusiana na masuala ya kimaadili lazima yafikiwe kama tu Neno la Mungu limeshadidia

suala hilo katika mawanda yake.

Kila unaposoma neno la Mungu lazima ukusudie kulitii na wala sio kwa kufuata mawazo

yako. Watu wengi sana hufuata mawazo yao badala ya neno la Mungu. Biblia katika Zaburi

119:11 inasema Moyoni mwako nimeliweka Neno lako nisije nikakutenda dhambi. Kwenda

kinyume na kile ambacho neno la Mungu linasema inaweza kusababisha wewe kutenda

dhambi hivyo unapolisoma uwe na lengo la kutii na kukubali matokeo yoyote yale

yatakayotokea.

Hata hivyo katika kutatua masuala ya kimaadili tunahitaji kuwa makini zaidi. Kwa mfano

katika maadili ya kikristo kutoa mimba ni kitendo kiovu ambacho ni dhambi kwa mtoaji

lakini je itakuwaje kama ujauzito huo ukiendelea kuwepo tumboni mwa mama inaweza

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

5

kupelekea kifo chake? Je atoe mimba ili kutunza mama

au mama afe na mtoto abaki? Haya ni baadhi tu ya

mambo ambayo yanahitaji kujadiliwa kwa makini sana

kabla ya kutolewa maamzi sahihi huku maadili ya

kikristo yakizingatiwa.

CHANGAMOTO ZA KIMAADILI

ZINAZOKABILI UKRISTO SIKU HIZI

Kuna changamoto za kimaadili nyingi sana ambazo

katika kitabu hiki hatuwezi kuzijadili kila moja. Ni

kweli kwamba katika Ukristo kila siku changamoto

mpya inazaliwa/inajitokeza. Sasa ni vigumu sana

kushughulikia changamoto hizi kwa muda wa siku nne

na hata kama tungepata muda wa kutosha si rahisi sana

kuzimaliza. Nadhani watu wanaoshughulika na masuala

ya ushauri wanajua ni mambo gani wanapambana nayo

kila siku. Unaweza kushangaa kila siku watu wanakuja

kupokea ushauri lakini kila mtu ana hoja yake ya pekee

kabisa. Hivyo basi kwa minajili ya kozi ya Biblia

nimechagua baadhi ya changamoto tu. Zifuatazo ni

changamoto za kimaadili kwa kanisa la leo

1. Masuala ya Siasa

Hatuwezi kujua zaidi kuhusu masuala ya siasa bila kujua kuhusu serikali. Serikali ni watu

waliochanguliwa kwa ajili ya kuwaongoza watu wengine. Kunhiyop (khj)4 anafafanua kuwa kazi

kubwa ya serikali ni kuwaadhibu wale ambao wanavunja sheria za nchi fulani. Sheria hizo

zinakuwa zimeandaliwa kwa ajili ya kuwaongoza watu wa makundi yote katika nchi. Yaani

hakuna cha dini fulani bali watu wa dini zote huunganishwa na kuwa wamoja kwa kutii sheria

moja. Serikali imetawaliwa na wanasiasa. Wanasiasa ndio wanaoshika nchi kwa sasa, bila siasa

hakuna serikali. Sasa kanisa linajikuta likiwa katikati ya siasa na kushindwa cha kufanya.

1.1. Kanisa na siasa

Kanisa wakati mwingine limekuwa katika changamoto katika siasa. Baadhi ya marais

wamekuwa wakitangaza hadharani upande wa dini wanaoushadidia. Katika historia kwa

mfano,mwaka 1991 raisi wa Zambia Fredrick Chiluba alitangaza kuwa Zambia ni taifa la

4 Khj-kirefu chake ni kama hapo juu au keshatajwa

Kanisa kwa sasa liko katika

hali ngumu kwa upande wa

maadili. Maadili

yanaendelea kumomonyoka.

Mfumko wa makanisa

duniani unatishia usalama

wa maadili ya Kikristo kwani

si jambo rahisi kwa sasa

kuamua katika hali ya

maadili. Hata hivyo sisi

kama watumishi wa Mungu

tunahitaji kujua masuala

mbalimbali ya kimaadili

ambayo yanatishia maadili

ya kikristo. Kwa ajili ya kozi

hii tutaangalia masuala

yafuatayo:

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

6

Kikristo.5 Huku akitubu kwa ajili ya uovu ambao umewahi kufanywa na watu wa taifa la

Zambia. Mfano mwingine ni raisi wa Nigeria, Obasanjo alidai kuokoka baada ya kufungwa kwa

makosa ya kijeshi. Katika kipindi cha uchaguzi alitangaza

kwamba yeye atakuwa raisi wa kikristo jambo ambalo

lilisababisha wakristo wengi kumpigia kura.

inawezekana kabisa mchungaji ukawa na kanisa halafu

ukaingia katika siasa? Je kanisa linaweza kutoa

mwongozo wa jinsi ya kuchagua kiongozi anayefaa katika

serikali?6Haya ni baadhi ya maswali ya msingi

tunapoendelea kujadili suala la siasa katika maadili ya

kikristo.

Katika maandiko serikali imeelezwa katika mazingira

kadha wa kadha. Ukianzia katika agano la Kale wakati wa

utawala wa Wafalme inadhihilisha wazi kwamba Mungu

alikubali tawala za wanadamu katika mazingira hayo.

kuna makundi mawili yanayozungumzia ujihusishaji wa

kanisa katika siasa. Kuna kundi la kwanza linadai kuwa ni

kanisa linapaswa kujihusisha kikamilifu katika siasa na

wale wanaokataa kwamba kanisa halipaswi kujihusisha na

siasa.

Hoja kwa wale wanaokubali

kujihusisha na siasa.

Wanaoshadidia upande huu

wanadai kuwa kila mkristo

lazima awe hai katika mambo

ya kiulimwengu. Wanadai

kuwa kanisa haliwezi kukaa

nje ya ulimwengu kwa sababu

linahitaji kuonyesha upendo

wa Mungu kwa watu wa

ulimwengu. Wanadai kuwa

bila kanisa kujihusisha na siasa

na pamoja na serikali wakristo

5 Paul Freston (2001). Evangelicals and Politics in Asia, Africa and Latin America. Cambridge: Cambridge University

press, Uk 158 6 Mwaka 2010 kanisa Katoliki liliandika ilani kwa washirika wake kuonyesha aina gani yakiongozi aweze

kuchaguliwa

Katika kipindi cha nyuma,

watumishi wengi wa Mungu

walikuwa wakiogopa sana

kuingia katika siasa kwa sababu

ya uovu ulio ndani ya siasa.

Huku wengine wakiwa na

misemo kwamba ‘siasa ni

mchezo mchafu’ swali la msingi

je wakristo wajihusishe na

mambo ya siasa?

Hoja za wanakataa kujihusisha

na siasa

Wale wanaoshadidia upande huu

wanadai kuwa kanisa limetengwa

kabisa na Yesu Kristo na hivyo

lenyewe si la ulimwengu huu.

Katika Yohana 17:16 “ninyi si wa

ulimwengu huu.” Warumi 12:2

inasema “wala msiifuatishe

namna ya dunia hii bali mgeuzwe

upya nia zenu mpate kujua hakika

yaliyo mapenzi ya Mungu yaliyo

mema ya kumpendeza na

ukamilifu.” Pia katika 2Kor 6:17

inasema “tokeni kati yao

mkatengwe nao asema Bwana.”

Kulingana na maandiko haya

wanaoshadidia upande huu

wanadai kuwa kanisa haliwezi

kujihusisha na mambo ya siasa

wala watumishi wake kuhusika

katika siasa kwa sababu wao ni

watu tofauti katika ulimwengu

huu.

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

7

hawawezi kuishawishi jamii kubadilika.kwa mfano katika Biblia akina Mordekai na Danieli

waliweza kubadilisha serikali zikawa za kumtii Mungu. Kwa upande mwingine wanakaza

kwamba kanisa halingii kichwa kichwa tu katika siasa bali linahusika na mambo ya siasa kwa

namna ifuatayo:-

i. Kuombea serikali na watu wake kwa ujumla

ii. Kuikosoa serikali kama inaenda kinyume na maadili yanayotakikana

iii. Kushirikiana na serikali katika kuondoa maovu katika nchi

Kambi hii pia ina misingi mingine kutoka katika maandiko ikidai kwamba:

i. Serikali inaanzia kwa Mungu Mwenyewe. Rom 13:1

ii. Serikali hufanya kazi kwa niaba ya Mungu. Rom 13:4

iii. Serikali ipo kwa ajili ya kuhamasisha mazuri kufanyika. Rum13:4-5.

Kwa minajili ya kozi hii nakubaliana na kambi pili kwamba kanisa linaweza kujihusisha na

siasa. Kanisa lijihusisha katika siasa ili kupata nafasi katika masuala ya kiuchumi, kijamii na

kiafya. Kama kanisa likipata nafasi kama hizo ndani ya kanisa basi ufalme wa Mungu hapa

duniani utaendelea kuinuliwa zaidi na zaidi.

Maswali la mjadala:

1. Je mchungaji anaweza kugombea uongozi katika siasa, kwa mfano ubunge huku akiendelea

kuongoza kanisa? Kubali au kataa kwa hoja kuntu.

2. Tunawezaje kukemea viongozi wanaofanya maovu zaidi katika nchi zetu zinazoendelea? Je

unaweza kumkabili raisi kama amefanya ubaya?

3. Kama tukikubaliana kwamba serikali zote zinatoka kwa Mungu, je unasema nini kuhusu

serikali za kijeshi ambazo wakati mwingine huua umati wa raia wasio na lawama?

4. Msimamo wako ni upi kuhusu kanisa na siasa? (hakikisha unatumia maandiko)

1.2.Vita na maasi

Suala la vita na maasi linahitaji mjadala mkubwa sana. Kuna watu wengine wanaodai

kwamba mkristo haruhusiwi kujihusisha na vita vya aina yoyote ile isipokuwa vita vya

kiroho tu. Lakini wengine wanadai kwamba wakristo wanaweza kwenda kwenye vita ili

kusaidia kukomboa katika vita.

1.2.1. Vita katika agano la kale

1.2.1.1.Waisrael waliagizwa kuwafukuza Wakanaani kwa vita ( Hes 33:50-56)

1.2.1.2. Mfalme Sauli aliagizwa kuwaua Waamaleki kwa vita (Isam.15:2-3)

1.2.1.3. Mungu ni mtu wa vita nk

1.2.2. Vita katika agano jipya

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

8

1.2.2.1.Kununua panga. Luka 22:36-38

1.2.2.2.Ufalme wa Yesu sio wa dunia hii ( Yoh. 18:36)

Kanuni za kutumia kunapotokea vita kati ya wakristo na wasio wakristo

1.2.3. kutafuta suluhu kila inapowezekana. Math 26:52

1.2.4. kuhamasisha haki duniani

1.2.5. Kuondoa ukabila ndani ya kanisa (Gal 3:28)

1.2.6. Upendo na msamha kwa maadui

Swali la mjadala

Je mkristo anaweza kwenda katika vita? Kama anaweza kwenda ni kwa namna gani

anaweza akatunza amri inayosema usiue? Jadili kwa hoja maridhawa.

B. Masuala ya Kiuchumi

Uchumi ni kipengele kingine muhimu katika kanisa la leo. Kuna mambo mengi yanayohusiana

na masuala ya kiuchumi ambayo yaliyo mengi yanahitaji mwongozo wa kimaadili. Yafutayo ni

baadhi ya mambo hayo:-

2.1. Umaskini

Suala la umasikini katika jamii nyingi za kiafrika ni suala tete. Watu wengi wengi wanahangaika

kwa sababu ya maisha magumu. Wakati mwingine wanakosa hata mavazi, malazi na hata

chakula. Lakini je ni mapenzi ya Mungu watu kuwa maskini? Nafikiri sio mapenzi ya Mungu

bali ni matokeo ya dhambi, na kwa sababu hiyo Mungu aliamua kuweka utaratibu wa namna ya

kutoka katika hali ya umasikini. Wakati Mungu alipomuumba mwanadamu alikusudia aishi

maisha tele lakini anguko limesababisha matatizo makubwa sana katika jamii zetu. Lakini swali

la msingi,je kwa nini nchi nyingi za kiafrika ni maskini sana kuliko za Ulaya? Je madhara ya

anguko yako kwetu tu? Kwa nini hali ya maisha ni tofauti kiasi hicho? Je matajiri wamewaibia

maskini mali zao? Je nini maadili ya kikristo katika jambo hili?

Je Mungu amepanga umaskini kwa watumishi wake? kwa nini tunahangaika na

umaskini? jadili

2.3.Rushwa

Siku hizi watu hujaribu kupunguza ukali wa neno ‘rushwa’ ‘hongo’ kwa kusema; zawadi,

hongera, maji, chai nk. Watu wengi hutoa na kupokea rushwa kwa namna tofauti tofauti.

Wengine hudai ni shukrani tu, wengine hudai ni mshahara kwa kazi yangu na wengine hudai ni

haki yangu kupokea rushwa. Ili rushwa iitwe rushwa mazingira ya utoaji wake yanahitaji

yaangaliwe. Kazi ya rushwa ni kununua haki

Biblia imekataza kupokea rushwa ya aina yoyote ile na kwa mazingira yoyote yale. (soma

mafungu haya Kumb. 10:16-18, 2Nyak 19:7, Mhub. 7:7, Zab 62:10) nk

Swali la mjadala: 1. Je unakubaliana na msemo kwamba “rushwa haiepukiki katika jamii

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

9

yetu?”

Tuchukulie unaendesha gari, unasimamishwa na trafiki na gari lako linaonekana lina kosa

dogo tu la rangi kuchubuka. Na asikari anakuomba faini ya shilingi 30.000/= hapo hapo

anakwambia ‘hebu naomba unipe ya maji nikuache uende na safari zako, leta 2000/- ‘ je

utakubali kumpa? Kama utakubali toa hoja madhubuti na kama hautakubali toa hoja kuntu.

1.3. Harambee/fund rising

Harambee au kwa lugha nyingine ‘changizo’ ina asili yake. Jamii nyingi za kiafrika zina

utamaduni wa kusaidiana kwa pamoja kama kazi inahitaji watu wengi. Hiyo nayo tunaweza

kusema kuwa ni aina fulani ya harambee. Kila kabila lina aina yake ya kufanya harambee; kwa

mfano katika jamii ya wasukuma kuna maneno maalum yanayotumika kuelezea harambee ya

aina hiyo kwa mfano ‘lubili’ ‘buyobe’ ‘ikhuma lya busiga’ nk. Kwa Wakulya wanasema’irika.’

Kwa hiyo suala la harambee si suala geni katika jamii nyingi za kiafrika. Watanzania wana

msemo ‘umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu’

Changizo au kufanya kitu katika hali ya umoja ni jambo la kawaida katika ukristo. Katika biblia

kuna sehemu nyingi ambapo changizo liliweza kufanyika kwa ajili ya kuinua huduma fulani

iendelee kwa nguvu.

a) Musa alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa hema. Kut. 20-34

b) Mfalme Daudi alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa hekalu. INyak. 28:12, 19. 29:2-9

c) Nehemia alifanya harambee kwa ajili ya kurekebisha mji wa Yerusalemu. Neh. 1:4-11,

2:1-18; 3:1-5 nk (au soma kitabu chote cha Nehemia)

d) Ezra alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa hekalu. Ezra 2:68-69

e) Hagai naye katika huduma yake alifundisha watu kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu.

Hag. 1:1-14

f) Yesu pia alihudumiwa katika huduma yake na wanawake kadha wa kadha. Luka 8:1-3

g) Mitume nao walihitaji fedha kwa ajili ya kuendeleza huduma yao. Mdo. 4:32-5:11

h) Mtume Paul alifanya changizo kwa ajili ya huduma. I Kor 16:1-3, 2Kor 8:1-24

Swali la msingi ni kwamba kwa nini suala hili liko katika maadili ya kikristo?

Kwa kuwa ni muhimu katika huduma ya BWANA kuwa na changizo la watu wengi, au mtu

mmoja/supporter, au kanisa maalumu linaweza kukusapoti lakini bado kuna mambo ya kimaadili

ambayo yanahitaji kuzingatiwa katika upataji wa huduma hizo. Mambo yafuatayo yanahitaji

kuangaliwa kwa makini sana katika huduma

a) Kuomba msaada kwa wasio wakristo

Swali ambalo mara nyingi tunapaswa kujiuliza ni je tunaweza kwenda kuomba msaada

wa kifedha labda kwa ajili ya kujenga kanisa kwa watu wasio waamini? Je mtu ambaye

pengine tunajua wazi kwamba labda amepata fedha kwa njia ya rushwa/au jambo lolote

lile baya, je tunaweza kuzipokea fedha kama hizo? Je tunaweza kuwaendea Waislamu

matajiri na kuwaomba wachangie huduma zetu?

Maswali haya yote yanahitaji uchunguzi wa hali ya juu sana. Wengi wanaoshadidia

upande wa kwamba inawezekana kuchukua fedha kwa wasio waamini wanadai kwamba

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

10

fedha walizo nazo watu sio za kwao. Wanatoa mfano wa Ezra na Nehemia waliopokea

msaada wa mfalme wa Babel ambaye alikuwa mwabudu miungu. Hili ndilo suala la

kimaadili katika harambee!

b) Kutangaza fedha zilizotolewa katika harambee au kama ni msaada wa mtu.

Hii inatokea hasa kama katika changizo umeita MC anayejulikana kabisa. Anahamasisha

watu na watu wanatoa fedha nyingi. Je fedha hizo zitangazwe?

c) Mhubiri kuomba fedha ili aje kufanya kwenye mkutano

Hili nalo siku hizi linasumbua sana jamii za Kikristo. Watumishi mbalimbali wanaomba

fedha kabla ya kufika katika mkutano wa Injili. Waimbaji wengi wa injili siku hizi bila

kuweka chochote kwenye akaunti yake hawezi kwenda kwenye mkutano wa Injili. Je

hayo ni maadili ya Kikristo. Je ni maadili ya kikristo kutoa namba zako za akaunti za

benki kwa umati wa watu? Je ni sawa kwa mtu akitaka kuombewa atoe kwanza fedha

kwa ajili ya huduma hiyo? Haya ni baadhi ya maswali ya msingi ambayo tunahitaji

kujiuliza na kuyatolea majibu sahihi.

Watumishi wa Mungu tunahitaji kuwa makini katika masuala haya ya kimaadili. Lakini

kwa ujumla tunaweza kusema kwamba, mambo yafuatayo katika masuala ya kifedha

katika huduma yanapaswa yafuatwe:-

Angalia nia ya mtoaji ni ipi? Kama ni ya kisiasa zaidi au anataka kumteka

mchungaji/mwinjilisti au anataka kupata sifa fulani ndani ya kanisa hilo? Usipokee fedha

ovyo ovyo maana ni hatari sana!

Kwa wewe unayepokea lazima uwe mwaminifu na muwazi. Kama umepewa fedha kwa

ajili ya kujenga kanisa unapaswa kujenga kanisa tu. Kuna wachungaji wengi wakishapata

misaada ya aina hiyo tayari wanaibadilishia matumizi, wananunua magari nk. Jambo hili

ni hatari sana.

Kuwepo na mrejesho kwa kile ulichotumia. Ni vizuri zaidi kuelezea vizuri kile ambacho

umetumia. Ikiwezekana andika kila kitu, itakusaidia sana maana kuna wafadhili wengine

wanataka kujua kila kitu.

Baada ya kuangalia mambo ambayo ni ya muhimu; epuka mambo yafuatayo:-

Epuka kupotosha ukweli. Kama una mradi utagharimu shilingi laki tano sema laki

tano.

Epuka kuwashawishi watu kutoa hata pale wasipotaka kutoa. Kuna watu

makanisani wanatoa vitu huku wakinugh’nuka mioyoni mwao

Epuka kuwa ombaomba/ Mungu hasemi kwamba tuombe kwa watu.

C. Masuala ya familia na ndoa

Suala la familia na ndoa ni suala ambao linahitaji kujadiliwa kwa undani zaidi. Ndoa ni taasisi

pekee ambayo Mungu huitumia kuendeleza uumbaji wake hapa duniani. Lakini wakati mwingine

ndoa hizi hizi zinakuwa na changamoto nyingi ambazo zinapelekea mambo fulani fulani ambayo

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

11

sio mazuri kutokea katika maisha ya kila siku. Katika sehemu ya familia na ndoa tutaangalia

masuala ya utasa, mitara, talaka na mahusiano.

3.1. Utasa/Ugumba

Utasa katika nchi nyingi za kiafrika ni suala mtambuka. Kwa maana ya kwamba waafrika

wanaamini kwamba watoto ndio urithi wa pekee kabisa. Sasa inapotokea kwamba kuna tatizo la

utasa mambo haya yanakuwa ni shida kubwa. Watu wengi wametoa talaka kwa sababu ya

kutokupata watoto kwa wake zao wa kwanza. Watu wengi wanaamini kwamba ndoa bila kuwa

na mtoto bado haijawa ndoa sahihi bali ni ndoa nusu. Tunahitaji kujifunza na kujua mapenzi ya

Mungu nini katika maisha ya ndoa zetu. Kama tukikaza kwamba lazima tuwe na watoto je

inapotokea hakuna watoto inakuwa ni laana au? Watu wengi wanatembea usiku na mchana

kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kutafuta watoto. Lazima tuwe makini katika

jambo hili. Kuna wachungaji wengi ambao wamejikita katika huduma ya kuombea tu watu wasio

na watoto huku wakikaza kwamba mtu asiyekuwa na watoto ana laana kutoka kwa Mungu na

yeye anaondoa laana hizo.

Chanzo cha utasa/ ugumba

Kabla ya kwenda mbali zaidi hebu tuangalie maana ya utasa na ugumba. Kwa mujibu wa kamusi

ya Kiswahili sanifu (2004:398)7 tasa ni “kiumbe chochote cha kike kisichoweza kuzaa” kwa hiyo

tunapozungumzia tasa tunamaanisha mwanamke asiyeweza kuzaa. Neno ‘mgumba8’ maana yake

ni “mtu aliyefikia umri wa kuzaa lakini akawa hajazaa wala kupata au kutia mimba” kwa hiyo

neno ugumba ni kwa watu wote. Sasa tuangalie kwa ufupi sababu za kuwa mgumba kwa:-

Kwa wanaume

Uhanithi-huyu ni mwanaume asiyekuwa na nguvu za kiume kabisa, yaani ni dhaifu.

Uume wake hauwezi kusimama sawasawa na hivyo hawezi kufanya mapenzi na mke

wake. tatizo hili husababishwa na masuala ya kiafya,kwa mfano kupiga punyeto kwa

muda mrefu na hata masuala ya kisaikolojia. Kama mtu akiwa na tatizo hili tunawashauri

kwenda kupima hospital ili kubaini chanzo cha tatizo.

Swali: wewe kama mchungaji ukiletewa suala la mtu ni kuwa

hanithi utafanyaje ili uweze kunusuru ndoa yao? Utawashauri vipi?

Tatizo katika kutoa mbegu- wanaume wengine hawawezi kuwapa wake zao uja uzito kwa

sababu shahawa/mbezi zao haziwezi kufikia yai la mtoto. Yaani katika kutoa

mbegu/shahawa hazina spidi ya kufikia yai.

Kukosekana kwa mbegu katika shahawa-wanaume wengine hawana mbegu katika

shahawa zao. Wanamwaga shahawa kama kawaida lakini hazina mbegu. Hili nalo ni

tatizo kubwa.

7TUKI (2004). kamusi ya Kiswahili sanifu. Nairobi: Oxford

8 khj

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

12

Kuharibika kwa mbegu za kiume-wakati mwingine mbegu za kiume zinaharibika na kufa

kabisa. Wanaume wengi wanaopenda kuvaa chupi zinazowabana hupatwa na tatizo hili

mapema sana. Maana kwa kawaida mbegu haziwezi kukaa katika joto kali.

Matatizo ya kiroho, wakati mwingine masuala ya kiroho yanaweza kusababisha kuwa

mgumba mwanaume

tafuta sababu za kiroho za ugumba katika maandiko matakatifu

kisha yaelezee kwa undani na chanzo cha matatizo hayo.

Kwa wanawake

Wanawake wengi wanakuwa matasa kwa sababu zifuatazo

Tatizo la homoni za uzazi

Tatizo la tumbo la uzazi/hakuna kizazi

Maambukizi katika uke

Chango la kike

Tatizo kiroho

Namna ya kushughulikia ugumba/utasa

Kila kundi la watu lina namna yake ya kutatua tatizo hili kubwa katika jamii. Jamii

nyingi zisizoamini hukimbilia kwa waganga wa kienyeji na kujikuta wanagawa ngono

kwa kudanganywa ili wapate watoto. Wanaume wengine wanaambiwa mashariti

magumu. Kwa mfano jamaa mmoja alienda kwa mganga wa kienyeji akaambiwa

kwamba alale na mama yake mzazi ndipo kizazi cha mke wake kitafunguka. Kwa ushauri

wangu ni bora:-

Kumwomba Mungu sana na kutambua nini hasa kusudi la ndoa katika maisha yenu.

Kwenda kuwaona wataalamu wa afya ili waone suala hili kitabibu zaidi. Na kama hakuna

tatizo la kitabibu basi ni vizuri kusubiri mpango wa Mungu

Kujifunza namna ya kujua siku ambazo mwanamke anaweza kuchukua mimba au la

Kujua kusudi la Mungu katika uumbaji. Kila kitu kinachokuja duniani kinakuwa na kusudi

la Mungu katika maisha ya mwanadamu. Kwa mtu aliyeokoka si jambo la kulazimisha

upate mtoto wakati Mungu hajaamua kufanya hivyo. Usije ukachanganyikiwa na kuanza

kukimbilia maombezi kila kukicha

3.2. Mitara (ndoa za wake wengi)

Waafrika wengi hawaoni kwamba ni jambo geni kuingia katika ndoa za mitara. Hii ni kutokana

na ukweli kwamba mwanaume wa kiafrika anaweza kuoa mwanamke mwingine wakati wowote

ule bila shida. Hili nalo ni tatizo kwa wakristo wengi. Nakumbuka kanisa moja niliwahi kusali

nilipokuwa kijana mdogo lililoitwa Last Church/Batola mhali (kwa kisukuma) lilikuwa

linahalalisha kabisa kuoa wake zaidi ya mmoja. Mwinjilisti kanisa hilo alikuwa na wake wawili

Ada na Sila. Kuna siku waligombana sana hao wake zake na kubebeana mapanga na hapo hapo

ndipo kikawa chanzo cha familia yetu kuhama kanisa hilo!!

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

13

Mpango wa Mungu haikuwa kwamba mwanadamu aweze kuoa wake wengi, kwani

alipomuumba Adamu alimwomba na Hawa nao walikuwa wawili tu. Hata hivyo kwa sababu ya

anguko la mwanadamu, kwa sababu ya dhambi mwanadamu alijitwalia wake zaidi kwa kadri

alivyotaka. Hebu tuangalie ndoa za mitara katika biblia na madhara yake.

Ndoa ya Lameki Mwanzo 4:19-25

Huyu ndiye mtu wa kwanza kabisa kujitwalia wake wawili. Ukisoma mistari hiyo utaona

kwamba huyu jamaa alikuwa roho ya kisasi kama ya Kaini. Kwa hiyo moja kwa moja makosa

yake yanaelekezwa kwa uasi aliokuwa nao. Matokeo yake yeye mwenyewe anakiri kwamba

anaweza kulipizwa kisasi na Mungu. Hapa tunaona kwamba madhara yake ilikuwa kwenda

kinyume na Mungu.ukoo wa Kaini mara nyingi imeonekana katika maandiko kwamba ni ukoo

wa kigaidi uliokataa kwenda katika sheria ya Mungu.

Ndoa ya Ibrahimu Mwanzo 16-17 na 28-30

Ni dhahiri kwamba Ibrahimu alizaliwa katika familia yenye kushika msimamo wa ndoa za wake

wengi(20:12). Katika ndoa yao Ibrahimu alichelewa sana kupata mtoto wa ahadi, lakini mke

wake Sarah,kwa sababu tayari ndani yake yalikuwepo mawazo ya kuwa na wake wengi kwa

mume wake,alimshauri amchukue Hajiri. Hapa ndipo chanzo cha matatizo ya ndoa hii.

Katika agano jipya hakuna mahali popote ambapo tunakuta kuna mtu alikuwa na wake zaidi ya

mmoja. Lakini tukiangalia maandiko inaonekana kwamba kuna waliokuwa na wake zaidi ya

mmoja. Hebu soma mafungu haya (I Kor 5:1-9) hapa tunaona jamaa ambaye alikuwa ni mzinzi

kiasi cha kulala na mke wa baba yake, je wewe unadhani ni mama yake mzazi? Labda nafikiri

kwamba huyu baba yake alikuwa hawara/nyumba ndogo. Sio hapo ukisoma katika I Tim 3:1ff

utaona sifa za asikofu na shemasi kwamba wawe waume wa mke mmoja. Hii inatudhihilishia

kwamba kulikupo na watu ndani ya kanisa wenye wake zaidi ya mmoja.

Maandiko hakuna sehemu ambapo yameruhusu mwanaume kuoa wake wengi au mwanamke

aolewe na wanaume wengi, kinachofanywa na binadamu ni ugumu wa mioyo yao. Wengine

katika kipindi hiki kwa sababu ya changamoto za ndoa wanaamua kuwa na nyumba ndogo ili

kunusuru maisha yao. Hii ni hatari sana, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na neno la

Mungu.

Kwa kawaida hakuna mtu anayeweza kugawa upendo wake katika sehemu mbili. Na ndiyo

maana ndoa za wake wengi zinakuwa na matatizo mengi sana. Unakuta wanawake hao

hawaelewani kila siku. Kuna mifano mingi katika agano la kale ambayo inaonyesha madhara ya

ndoa za mitara. Ushauri wangu ni kwamba ni lazima tufundishe watu wafuate utaratibu wa

Mungu kwamba ndoa ni ya mke mmoja. Hakuna sababu ya kuoa mke wa pili. Na kuoa mke wa

pili ni kwenda kinyume na neno la Mungu.

Swali: je kama kanisani kwako kuna waumini ambao kabla ya kuokoka walikuwa na

wake zaidi ya mmoja, utawashauri wawaache au utafanyaje? Jadili kwa mapana huku

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

14

ukizingatia maadili ya kikiristo ni pamoja na hekima ya Roho Mtakatifu kufanya kazi

Wewe kama mchungaji umeitwa kwenda kumbatiza mtu aliye na wake zaidi ya mmoja utafanyaje?

3.3. Talaka

Suala la talaka ni suala nyeti sana katika kanisa. Watumishi wengi wanahangaika kutatua

masuala yanayohusiana na talaka. Katika kipindi hiki suala la talaka ni jambo la kawaida

miongoni mwa wapendwa. Hasa kunapokuwa na tatizo ambalo wanandoa wamekosana na jamii

pamoja na kanisa inaliona wazi basi talaka hutolewa.

Nini sababu ya talaka?.

Kwa ujumla kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha talaka kutolewa. Nitajaribu kutaja baadhi

ya hayo matatizo kama ifuatavyo;-

Kukosekana kwa watoto miongoni mwa wanandoa ni sababu kwa Waafrika. Na hasa

lawama zinapelekwa kwa wanawake

Kusalitiana kimapenzi, yaani kama kuna mmoja anatoka nje ya ndoa basi yule mwingine

anaamua kuachana naye

Kulazimishwa na wazazi wa upande mmoja kuachana kwa sababu za kimila na kitamaduni

Mmojawapo wa wanandoa hao kupatwa na magonjwa ya kuambukizwa hasa UKIMWI

Sababu za kiuchumi katika wanandoa. Wengine wanapooana huonekana wakiwa na mali

mara baada ya kuisha mali hizo huachana mara moja

Huko Ulaya wengine wanaona kwamba kama mtu amemchoka mwenzake anaamua

kuachana naye tu bila hata sababu za msingi

Ugomvi wa mara kwa mara ndani ya nyumba hupekea talaka kwa wanandoa hao. Ugomvi

huo unaweza kusababishwa na tabia sugu za wanandoa hao kutokubadilika ili kuendana

pamoja.

Matumizi ya mabavu ndani ya nyumba husababisha talaka miongoni mwa wanandoa. Kwa

mfano kwa waafrika walio wengi kumpiga mwanamke ni jambo la kawaida sana, lakini

kuna wakati inafikia hali ngumu ndipo mwanamke huamua kuondoka na kudai talaka. Ni

mara chache kukuta familia mwanaume anapigwa na mwanamke japo kuna familia za

namna hii nyingi.

Kunyimana kitandani. Nazungumzia hapa ile hali ya kumnyima mwenzi tendo la unyumba

hupelekea talaka miongoni mwa wanandoa. Hii inatokea pale ambapo miongoni mwa

wanandoa anatoa tendo la ndoa kama silaha ya kumwadhibu mume/mke wake. jambo hili

huvunja ndoa nyingi kila siku.

Wivu wa kimapenzi huvunja ndoa nyingi, unaweza kukuta miongoni mwa wanandoa

anakuwa na wivu kiasi kwamba hataki kumwona mwenzi wake anaongea na mtu mwingine.

Mfano unakuta baba akimwona mke wake ana mtu mwingine wa kiume basi moja kwa moja

anasema kwamba huyu anakutongoza na hivyo kudai talaka kwa haraka sana.

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

15

Ndoa za mitara huvunja ndoa ya kwanza. Mara nyingine kwa wapenzi ambao

hawakukusudia kuwa ndoa yao itakuwa ya wake wengi wakiona kwamba kuna mwanamke

mwingine ameletwa ndani mara moja hudai talaka.

Ulevi wa kupindukia, hili mara nyingi linatokea hasa ikiwa mmojawapo wa wanandoa hao

akiwa mlevi kupindukia na mwingine hana tabia za ulevi ikifikia hatua fulani mmoja

anachoka kumvumilia mwenzake kwa ajili ya ulevi wake basi huamua kuvunja ndoa

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanasababisha ndoa nyingi kuvunjika. Kwa mfano

matumizi mabaya ya simu yanavunja ndoa za watu. Nakumbuka kijana mmoja alikosea

akatuma massage ya mapenzi katika simu ya mke wa mtu, ujumbe huo ulileta mtafaruku

ndani ya ndoa hiyo. Pia matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile facebook na twitter

yanasababisha kuvunjika ndoa. Pale ambapo mmoja wa wanandoa anasahau ku-log out

kama alikuwa ameingia mtandaoni na mtu mwingine mbaya akiingia kwenye akaunti yake

na kuweka picha mbaya itampa shida kubwa sana.

Watoto wa kambo huvunja baadhi ya ndoa za watu. Hii inatokea pale ambao mmoja wa

wanandoa hao alikuwa na mtoto wakati wa kuolewa, watoto wa aina hiyo wakati mwingine

huleta matatizo makubwa ya kuchonganisha wanandoa hao

Hizi ni sababu chache tu miongoni mwa sababu nyingi zinazosababisha kuvunjika kwa ndoa. Na

kumbuka kwamba kila ndoa ina sababu yake ya pekee ambayo haifanani na nyingine

inayopelekea kuvunjika kwa ndoa hiyo.

Fungu la kwanza ambalo linazungumza juu ya talaka kwa mara ya kwanza ni katika

Kumbukumbu la Torati 24:1-5 mahali ambapo tunaona kwamba Musa aliwaelekeza watu namna

ambavyo wanaweza kuwapa talaka wake zao. Lakini jambo hili Yesu alisema kwamba sababu za

Musa kuruhusu talaka ilikuwa ni ugumu wa mioyo ya watu

Mitazamo mbalimbali kuhusu talaka

Kuna wanaosema hakuna kutoa talaka kabisa katika maisha ya mwanadamu. Soma

Warumi 7:2-3,I kor 7:39, Mal 2:16

Kuna wanaosema kuwa ni ruksa kutoa talaka lakini usioe tena. Hawa nao wanasimama

na mafungu mbalimbali, mfano. Math 19:9 wanafafanua kwa namna ya pekee sana

Kuna wale wanakubali kwamba kama mwanamke/mwanaume umemkamatisha kwenye

uzinzi unaachana naye mara moja. Nao wanasimama na fungu hili la Math 19:9 na Kumb

24:1-5 wakifasiri neno OVU kuwa ni uzinzi

Kila kundi la watu wana msimamo wao juu ya suala hili lakini cha kuzingatia ni kwamba

tunahitaji kumwomba Mungu hekima ya pekee katika kujadili suala la talaka makanisani

huku tukijua mambo yafuatayo:-

Ndoa ya kikristo imekusudiwa kuwa ni ya milele. Mal 2:16

Kuna wakati inaweza kutokea talaka. Math 19:8

Talaka ni hatari sana kwa wanandoa

Hatuwezi kujumuisha moja kwa moja masuala ya talaka lazima yaangaliwe kwa

undani zaidi

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

16

Kuna matumaini ya ziada baada ya talaka na kuoa tena, kwa maana ya kwamba hilo

si suluhisho la maisha ya mwanadamu

Kabla ya kufanya uamuzi wa haraka wa kuvunja ndoa yako, fikiria. Mara nyingi

talaka haimalizi mahangaiko ya maisha. Badala yake, inatatua tatizo moja, na

kutokeza lingine. Katika kitabu chake, The Good Enough Teen, Dakt. Brad Sachs

anaonya hivi: “Wenzi wa ndoa wanaotalikiana huwazia kwamba kufanya hivyo

kutafaa kabisa, yaani, talaka yao itawaondolea kabisa huzuni na ugomvi mkali, na

badala yake wapate utulivu mwanana. Lakini kutarajia hilo ni sawa tu na kutarajia

kuwa na ndoa kamilifu, haiwezekani.” Hivyo, ni muhimu kuwa na habari kamili na

kuona talaka kihalisi.

Talaka huweka majeraha yasiyokoma mpaka kaburini

Nini madhara ya talaka kwa maisha ya wanandoa?

Huharibu afya ya kiroho

Huharibu afya ya kimwili

Kuchanganyikiwa miongoni mwa wanandoa

Watoto kukosa malezi ya wazazi wote wawili

Matatizo ya kifedha. Daniella, anayeishi Italia, alikuwa katika ndoa kwa miaka

12 alipogundua kwamba mume wake alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na

mfanyakazi mwenzake. Daniella anasema hivi: “Nilipogundua jambo hilo,

mwanamke huyo alikuwa na mimba ya miezi sita.”

Kuna matatizo ya kifedha.hebu ona mfamo huu baada ya kutengana kwa muda,

Daniella aliamua kumtaliki mume wake. “Nilijaribu kuiokoa ndoa yangu,” anasema,

“lakini mume wangu hakuacha kuwa na uhusiano nje ya ndoa.” Daniella anahisi

kwamba alifanya uamuzi unaofaa. Lakini anasema hivi: “Mara tu tulipotengana, hali

yangu ya kiuchumi ikawa mbaya. Nyakati nyingine nilikosa hata mlo wa jioni.

Nilikunywa tu maziwa.”9

Swali:1 je kama miongoni mwa washirika wako amepatikana na ugonjwa wa UKIMWI ilhali mwenzi

wake hana, utaamuaje suala la kuzuia talaka isitolewe?

swali 2. Hebu tuchukulie kwamba umemkamata mume/mke wako ana kwa ana (ready handed) akiwa

katika kifua cha kahaba utavumilia kuishi naye au utampa talaka?

Swali 3.wewe kama mwanadamu umewahi kufumaniwa? Ulimalizaje mgogoro huo nyumbani kwako?

D. MATUMIZI YA VILEO

Matumizi ya vileo ni jambo la kawaida kwa watu wengi, wakristo na wasio wakristo. Ni jambo

ambalo ni la muda mrefu hata kabla ya histori ya binadamu kuanza kurekodiwa katika

maandishi.

9 http://www.jw.org/sw/machapisho/magazeti/g201002/mambo-manne-kuhusu-talaka/

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

17

Kinaachofanya unywaji wa pombe/divai uwe ni wa kawaida ni kwa namna ambavyo

inatengenezwa. Pombe/divai nyingi inatengenezwa kutokana na nafaka, kwa mfano mtama

huweza kutengeneza aina mbalimbali ya vileo. Kwa mfano kwa wasukuma mtama huweza

kutengeneza pombe iitwayo ‘gongo’ au ‘mapuya’ au ‘mataputapu’ nk. Pia nafaka za mahindi

hutengeneza pombe. Lakini zamani za siku hizi nimesikia kwamba watu hutengeneza hata

pombe kwa kutumia kinyesi cha wanyama na wanadamu. Hii ni katika kuhakikisha kwamba

wanaongeza ukali katika vileo hivyo.

Maendeleo ya viwanda yamehamasisha unywaji wa pombe za kawaida na pombe kali kwa

kutengeneza vileo hivyo kwa njia ya kisasa kabisa. Hapa Tanzania, kampuni ya bia inatengeneza

aina mbalimbali ya bia kwa mfano Safari lagar, Serengeti larga, tusker lagar. Bia hizi zote utafiti

unaonyesha kwamba sio kali sana. lakini nimewahi shuhudia mtu amekunywa bia mbili aina ya

‘Ze bingwa’ na kuishiwa nguvu kabisa. Kuna vinywaji vingine vinatoka nje ya nchi kama vile

whisky ambayo ina 50% ya kileo. Daniel Jakes nk. Hata konyaji ni kileo kikali sana .

Kileo katika maandiko matakatifu

Kileo kinaonekana kutajwa katika maandiko kwa namna mbalimbali na kuonyesha umuhimu

wake kwa watumiaji.

Divai inatajwa kama dawa ya tumbo kwa anayesumbuliwa na tumbo na kwa ushauri wa

daktari anaweza kutumia. I Tim 5:23

Yesu alitengeneza divai kwenye arusi ya kana ya Galilaya na watu wakanywa na kulewa.

Yoh 2:1-11

Divai inatumika kuponya vidonda/majeraha ya vidonda. Lk 10:31

Divai inasaidia kupoteza mawazo ya umasikini. Mith 31:7

Divai hufurahisha moyo wa mwanadamu. Zaburi 104:15

Divai ilitumika katika sadaka kwa Bwana. Hes. 15:5-7

Japokuwa divai/pombe imeongelewa kwa mlengo chanya katika mafungu haya lakini pia

tukumbuke kwamba kwa upande mwingine imeongelewa kwa mlengo hasi. Yaani kwamba

ina madhara kwa maisha ya wanadamu. Mfano mafungu haya yanaonyesha hivyo, Kumb

21:20 IKor 6:7-9 nk

Mkristo na kunywa pombe.

Swali hili limekuwa ni swali la siku nyingi na kila siku wakristo wengi wanapingana katika

hili. Kwa baadhi ya madhehebu ya Kikristo yanaruhusu kunywa pombe ila usilewe tu. Lakini

kwa upande mwingine wengine wanasema kwamba kunywa pombe ni dhambi kubwa mbele

za Bwana. Hku wengine wakidai kwamba kunywa pombe ni tabia mbaya tu ila siyo dhambi.

Hebu tujaribu kuangalia hoja za kila upande unavyodai.

a) Misingi ya mkristo kunywa pombe

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

18

Biblia haikatazi unywaji wa pombe bali inakataza ulevi wa pombe. Ndiyo maana katika I

Tim 3:3 ‘si mtu wa kuzoelea ulevi’ kuzoelea ni kitenzi cha ‘kuzoea’ maana yake kuendekeza

tabia ya kufanya hivyo. Na hapa Paul anatoa sifa za kiongozi wa kiroho. Kumbe wakiristo

wengine wasio viongozi wanaweza kunywa pombe.

Biblia imeagiza mkristo aweze kujitawala sio kuacha kunywa pombe, hivyo basi kama

mkristo anaweza kunywa bia moja na akalala bila kumbughudhi mtu basi anaweza

kunywa ili mradi tu atawale hali yake.

Biblia inatambua kwamba pombe inaweza kutumika kama dawa, basi si mbaya

kunywa pombe kwa ajili ya afya10

.

Si kila mtu anayekunywa pombe anakuwa mlevi. Na biblia imekataza ulevi sio

unywaji wa pombe.

Kukataa kunywa pombe unaweza kujitenga na jamii. Kwa mfano kuna jamii zingine

kama ukienda kwenye sherehe lazima uzimue kidogo ndipo uonekane unashirikiana

nao.

Unapokunywa pombe unatuliza akili yako na hivyo kukufanya siku nyingine ukitaka

kufanya kazi ufanye kwa bidii kubwa

Suala la kunywa pombe halihusiani na masuala ya uzima wa milele. Kwa kuwa mtu

amempokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake basi amehesabiwa haki

na ana uzima wa milele. Hivyo si dhambi kunywa pombe.

b) Misingi ya mkristo kutokunywa pombe

Biblia inaonya juu ya matokeo ya matumizi ya pombe

Mtu aliyeweka nadhiri haruhusiwi kunywa kileo. hES 6:2-3

Makuhani hawakuruhusiwa kunywa vileo. LAW 10:9

Wafalme hawakupaswa kunywa vileo katika falme zao. MIT 31:4

Kileo hupotosha watumishi wa Mungu wanaojaribu kunywa. ISA 28:7

Si vizuri mtu aliyekusudiwa kuwa mkuu kutumia kileo. LK 1:15

Kunywa pombe kwa mkristo ni kuonyesha na kuendelea kuishi maisha ya zamani. 1PET

4:3-4

Pombe huleta magomvi katika nyumba za watu

Ulevi huua idadi kubwa ya watu. Nadhani hata wewe umeshuhudia watu ambao wamekufa

kwa sababu ya pombe

Pombe huvunja ndoa nyingi sana

Hakuna anayeanza kunywa pombe na kusema kwamba hatakuwa mlevi bali hustukia mlevi

tu

10 Mtu mmoja anaitwa nabii Tito (Nabii wa pombe- a prophet of beer) ni nabii anayehubiri watu kunywa pombe akitumia

maandiko matakatifu ya Biblia na kudai kuwa Biblia inaruhusu kunywa pombe.Hufanya mahubiri yake maeneo ya posta mpya

hapa jijini Dar es Salaam.

Nabii Titto yeye anadai kuwa ameoteshwa na mungu kuwa watu wanywe pombe kwani ni tiba sahihi tosha kwa magonjwa

mbalimbali na si pombe tu mpaka sigara. Dini yake aliyoianzisha inarushu watu kuoa wake wengi,kuvuta sigara na kunywa

pombe.Huyu ndiye nabii Tito (a prophet of beer)

Maadili ya Kikristo/ mch. Daniel John Seni/ Calvin Theological College DSM-Tanzania

19

Matokeo ya ulevi ni mabaya mno. Mfano kwa habari ya Lutu kulala na watoto wke wakati

wa ulevi na Nuhu wakati wa ulevi alilaani mjukuu wake Kanaani.

Kila mlevi unayemwona alianza kama mnywaji halafu polepole akawa mlevi mkubwa.

Tanbihi: ushauri kuhusu pombe

kwa kuwa hoja zinazopinga kunywa pombe ni nyingi sana, kwa ushauri wangu

usijaribu kunywa pombe hata siku moja. Usijaribu hata kutaka kujua ladha yake

ikoje. Achana na misemo ya wataalam soda ni hatari kuliko bia kwa afya!! Eti uache

kunywa soda ugeukie kunywa bia ni hatari sana.

------------------------------------------Mwisho--------------------------------------------------

Mch: Daniel John Seni

S.L.P 32807/[email protected]/ 0786684062 na 0769080629

Dar es salaam

Ni mchungaji wa kanisa la Shekinah Presbyterian Church Tanzania

Ni mwandishi wa kitabu cha ‘uwezekano wa mkristo kupagawa na pepo’moja ya

vitabu muhimu sana kwako na hupaswi kukikosa


Recommended