+ All Categories
Home > Documents > Khartoum Salafi

Khartoum Salafi

Date post: 15-Nov-2023
Category:
Upload: khangminh22
View: 0 times
Download: 0 times
Share this document with a friend
20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1213 RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA , JANUARI 22-28, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] Soma Uk. 7 Ya ‘Sitakishari’ yasikie tu… Polisi Dar walivyomtesa mtuhumiwa Awali Mahakama ilimwona hana hatia Akadaiwa ana kombati za Al Shabaab “ALIPONIONA tu, alieleza kuwa amenitaja ili nifike nimuone katika hali aliyokuwa nayo, hata akifa ifahamike kuwa amekufa akiwa mikononi mwa Polisi. Kweli jamaa alifariki usiku wa saa nane, siku ile ile niliyoingia mimi.” Maalim amegonga msumari kichwani Papa Francis akitoa agizo kwa JPM… 'Sanamu za Babeli' zaporomoka Z’bar Soma Uk. 9 PAPA Francis SEIF Sharif Hamad. Kutoka kushoto: Bi Ummukhayr Sadri Abdulla, Bi Maryam Said Aboud na Bi Khadija Abubakar Abdulkadir wakiwa kortini Mombasa Machi 30, 2015. Soma Uk. 10 Khartoum Salafi Sawa ‘Mzee Punch’ wa UDSM Alihusika kadhia ya Bint Sadr? Aeleza alivyo wagaragaza MUM! Habari kamili Uk. 3 MUATHIRIKA wa mateso ya Polisi, Ustadh Saidi Michael Danieli. Mapinduzi hayakuwa na maana ya ubaguzi WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mhe. Charles Kitwanga. MKUU wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Jumbe Mangu.
Transcript

ISSN 0856 - 3861 Na. 1213 RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA , JANUARI 22-28, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected]

Soma Uk. 7

Ya ‘Sitakishari’ yasikie tu…Polisi Dar walivyomtesa mtuhumiwaAwali Mahakama ilimwona hana hatiaAkadaiwa ana kombati za Al Shabaab

“ALIPONIONA tu, alieleza kuwa amenitaja ili nifike nimuone katika hali aliyokuwa nayo, hata akifa ifahamike kuwa amekufa akiwa mikononi mwa Polisi. Kweli jamaa alifariki usiku wa saa nane, siku ile ile niliyoingia mimi.”

Maalim amegonga msumari kichwani

Papa Francis akitoa agizo kwa JPM…'Sanamu za Babeli' zaporomoka Z’bar

Soma Uk. 9 PAPA Francis SEIF Sharif Hamad.

Kutoka kushoto: Bi Ummukhayr Sadri Abdulla, Bi Maryam Said Aboud na Bi Khadija Abubakar Abdulkadir wakiwa kortini Mombasa Machi 30, 2015. Soma Uk. 10

Khartoum SalafiSawa ‘Mzee Punch’ wa UDSM Alihusika kadhia ya Bint Sadr?Aeleza alivyo wagaragaza MUM!

Habari kamili Uk. 3

MUATHIRIKA wa mateso ya Polisi, Ustadh Saidi Michael Danieli.

Mapinduzi hayakuwa na maana ya ubaguzi

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mhe. Charles Kitwanga.

MKUU wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Jumbe Mangu.

2 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

Fethullah-Gulen

Jee Unajua?

MASUALA1.Yataje majira manne ya Kiswahili, kwa kizungu Summer, Winter, Spring na Autumn. Jawabu: Kiangazi, Kipupwe, Masika, Vuli.2.Jee sauti inatembea kwa haraka kwenye: Maji, Hewa, Mtungi? Jawabu: Maji3.Wakati wa kiangazi Mchana huwa……. na usiku huwa………? Jawabu: Mrefu, Mdogo4.Wakati wa Kipupwe Mchana huwa ………………. Na Usiku huwa……………? Jawabu: Mdogo, Mrefu5.Nyezo gani kuu inayosababisha kupatikana kwa misimu? Jua, Mwezi, Maji kujaa na kukupwa. Jawabu: Jua6.Jee ni kweli kila Sayari duniani ina miongo sawa? Ndio, Sio. Jawabu: Sio7.Dunia inaizunguka: Jua, Mwezi au Wenyewe? Jawabu: Jua8.Sayari ipi iliokubwa koliko zote kati ya 9? Mars, Venus, Jupiter. Jawabu: Jupiter9.Zitaje Sayari 9 kwa mpangilio kutokea kubwa hadi ilio ndogo. Jawabu: Jupiter, Saturn, Uranus, Neptune, Earth, Venus, Mars, Mercury, Pluto.10.Jee Afrika ni Sayari, Bara au Nchi? Jawabu: Bara.

JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 35

CHEMSHA BONGO: 36Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

MASUALA1.Sayari ipi ilio na baridki kali kabisa?2.Sayari ipi ilio na uzito mkubwa kuliko zote?3.Jua lina asilimia ngapi ya Hydrogen na Helium?4.Umri wa Jua miaka mingapi?5.Masafa ya kutoka duniani hadi mwezini.6.Kwenye Mwezi kuna maisha? Ndio, Sio.7.Mwezi wa Kiislamu hufwata mzunguko wa ……………………………8.Mwezi wa Kizungu hufwata mzunguko wa………………………………9.Matumaini ya maji kupatikana yapo katika Sayari ipi?10.Jua likitoka Magharibi itakuwa nini?

1.Inasadikiwa kuwa lugha ya Kitamil ni kati ya lugha kongwe duniani ikiwa inazungumzwa hadi hivi sasa. Lugha hii ina umri wa zaidi ya mika 500 katika survey iliofanyika miaka 14 iliopita inaonyesha kuwa kuna magazeti 1,863 yanachapishwa kwa lugha ya Kitamil hii ni hoja ilio wazi kuwa ni moja kati ya lugha kongwe na ilio hai: http://www.aina.org/ata/20150809113734.htm2.Awujale Sikiru Kayode Adetona, Mfalme wa Ijebuland huko Nigeria ni mmoja kati ya Masultani waliokaa juu ya viti vyao kwa muda mrefu, tangu kukalia kiti hicho ni miaka 55: http://www.theguardian.com/uk-news/2015/jan/23/top-10-oldest-monarchs-in-the-world3.Asili ya ndizi ni nchi za Kusini mwa bara la Asia, kwa nchi ya Papua New Guinea ilianza kutumika miaka 5000 B.C kabla ya kuzaliwa Mtume Issa (AS): http://blog.mapsofworld.com/2011/08/26/where-do-bananas-come-from/4.Mbatata (Viazi ulaya) vilianza kuonekana kwa mara ya kwanza katika Milima ya Andes iliopo Kusini mwa Bara la Amerika: http://www.livescience.com/32433-where-did-potatoes-come-from.html5.Nchi ya China ndio msafirishaji mkubwa wa Mchele ikifwatiwa na India, Indonesia, Vietnam, Thailand, Bangladesh, Burma, Philippines, Brazil, Japan: http://www.whichcountry.co/top-10-exporters-of-rice/6.Nchi ya Brazil inaongoza uzalishaji wa Machungwa duniani, huzalisha machungwa ya tani 35,735: http://worldknowing.com/top-10-largest-orange-producing-country-in-the-world/7.Nchi ya China inaongoza kwa uzalishaji wa Tikiti maji, huzalisha tani 71,754,604 za Tikiti maji kila mwaka: http://worldknowing.com/top-10-largest-watermelon-producing-countries-in-the-world/8.Nchi ya San Marino ndio yenye watu wake wenye magari mengi? Kwa kila watu 1,000 huwa na magari yapatao 1,262: http://worldknowing.com/top-10-countries-with-most-motor-vehicles-per-capita-in-the-world/9.Kama kupata kibaru ni rahisi nchini Singapore, nchi hio inaongoza kwa kutenegeneza nafasi nyingi za kazi, ikifwatiwa na Hon Kong, Falme za Nchi za Kiarabu, Austria, France, China: http://worldknowing.com/top-10-countries-with-highest-job-opportunities-in-the-world/10.Maeneo yalio safi kabisa yenye kuvutia duniani moja wakpo ni bonde la Neelum liliopo Azad Kashmir, mwaka mzima eneo hilo hunawiri kijani na mito na maziwa yake hayakauki: http://worldknowing.com/top-10-most-beautiful-natural-places-in-pakistan/

“NA haikuwa toba kwa wale ambao wanafanya maovu, mpaka yatakapomdhihirikia mmoja wao mauti anasema hakika nimetubia hivi sasa wala wale ambao wanakufa na hali ya kuwa wao ni makafiri, hao tumewaandalia adhabu yenye kutiwa uchungu”. [AN-NISAA 18]

Kitambo cha kukata tamaa ndicho kitambo cha mwisho katika maisha ya binadamu ambaye haikukubaliwa imani yake. Isipokuwa jambo muhimu ni kuuainisha mwanzo wa kitambo hiki. Mwanzo huu unakuwa katika nyakati ambazo anakata tamaa ndani yake mtu katika

An nisaa: 18vitambo vyake ya mwisho vya kurudi katika maisha ya dunia na kuishi humo, kwa hisia yake ikiwa imekamilika. Na katika mtazamo mwingine, hicho ni kitambo ambacho anakata tamaa ndani yake mtu ambaye anakaribia kufa. Na wamekata tamaa pia wale ambao wamemzunguka pambizoni mwake, kwa maana kuwa wamekata tamaa kuwa atarejea tena kwenye maisha ya dunia.

Ndiyo inakubaliwa imani ya mtu mpaka katika vitambo vyake vya mwisho – muda wa kuwa anazimiliki nguvu zake za kiakili. Iwapo ataweza kuamini. Na hiki ndicho kitambo ambacho alikariri ndani yake Mtume (s.a.w.) kutaka kwake kuamini kwa Ammi yake Aby Twalib. Isipokuwa Abaa Twalib alitaja – ikiwa ni msukumo kutoka nje – kwamba yeye atakufa juu ya dini ya Abd Al-Muttalib. Na tukio jingine linastahiki kusimama juu yake nalo ni tukio la mtoto wa Kiyahudi ambaye ni mgonjwa. Kwa hakika Mtume (s.a.w.) alimtembelea mtoto wa Kiyahudi anayekaribia kufa akamfundisha aseme: “Hapana Mola anayestahiki

kuabudiwa kwa haki, isipokuwa Allah”, yule mtoto akamwangalia baba yake kana kwamba anamtaka ruhusa, mzazi wake akampa ishara ya kukubali, pale pale akaanza mtoto kutangaza imani yake, na kutamka tamko la Shahada. Kwa msingi huo, muda wa kuwa hisia si yenye kutetereka kwa hakika milango ya mbinguni inakuwa wazi kwa ajili ya kuikubaliwa Imani (na toba).

Ndiyo kitambo cha kukata tamaa maana kitambo ambacho haikubali ndani yake imani – ni kile kitambo ambacho hamiliki ndani yake mtu hisia yake na hali ya kuwa yeye yuko karibu kuiacha dunia. Katika hali hiyo, haikubaliki imani yake. Isipokuwa iwapo kitapatikana kinyume, hapo kwa hakika inaangaliwa niya ya mtu kama mbegu ambayo itakuwa katika maisha ya Barzakh – kati ya dunia na akhera – na katika maisha ya kukusanywa itakuwa kubwa na itakuwa ni kichanga cha jaza na malipo yake.

Kwa msingi huo, muda wa kuwa mtu kabla ya kitambo cha kuhudhurikiwa na mauti hajakata tamaa ya kurejea kwenye maisha ya dunia na hakukata tamaa na maisha hayo kwa hakika kuelekea kutoka katika ukafiri na kwenda kwenye imani, kunakuwa ni kwenye kukubaliwa, wakati wote. Ikiwa hali ni kinyume cha hivyo, hilo litakuwa na hukumu tofauti. Maana ni kwamba iwapo kutapatikana kukata tamaa na dunia na yakafunguliwa mapazia ya kuangalia kwenye maisha ya akhera, kwa hakika fursa inakuwa imepotea. Kwa sababu hapana tena nafasi ya kufanya tendo lolote jema. Linapokuwa ni tamko zuri na rehma ya Mwenyezi Mungu inatoa nafasi kwa wale ambao wameyachafua maisha yao ya dunia, kwa maasia na uovu, iwapo wataamini na watatubia na hilo ni kufuatana na aya hii tukufu:

“Waambie waja wangu ambao wamevuka mpaka juu ya nafsi zao msikate tamaa na rehma ya Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu anasamehe madhambi yote”. [AZ-ZUMAR 53]

M P L U T O U N M M M U B K

A N E P T U N E R A F R A K

S S A T U R N D E J U A R I

I M E R C U R Y F I P N A A

K J U P I T E R U P I U J N

A E A R T H V E N U S S U G

J U P I T E R M A R S L A A

M W E Z I E S I O N D I O Z

D A K I K A 8 V J U A S O I

K I P U P W E 1 3 4 V U L I

B J N E P T U N E M W J S 384,400 Km

I C A R T O O N P A O U O 980,00Km

L H E L I U M N U R R A L 111,111,000Km

O R O M E S P A I S L A A 788

N F M W E Z I W O S D N R 88,888

I L O L T O S F Y K G K S 12,345,679

4.5 R O I T E R S A W E E Y 875

M W I S H O W A D U N I A 888,999 Km

A L A S K J U P I T E R 25

N E P T U N E Z S I O 75 35

3 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016

Habari

Ya ‘Sitakishari’ yasikie tu…SAIDI Michael Danieli, anasimulia alivyoteswa akiwa mikononi mwa Polisi, huku akiwa hana hatia.

Aidha, anasimulia pia mwenzake alivyokufa baada ya kupigwa na kuteswa kama namna ya kumlazimisha kukiri kuwa ni gaidi baada ya kukamatwa akituhumiwa kuvamia Kituo Cha Polisi Cha Sitakishari, Ukonga Jijini Dar es Salaam.

Saidi ambaye ni muumini wa Dini ya Kiislamu aliyesilimu mwaka 2012 Jijini Mwanza, anasema alijikuta anajumuishwa katika kadhia hiyo baada ya kutajwa na Muislamu mwenzake, ambaye alikamatwa mwanzoni akihusishwa na tukio hilo.

Kijana Said amedai kuwa alikamatwa mwaka jana na kushushiwa kipigo na askari Polisi, huku akitakiwa kueleza wapi zilipo silaha walizopora katika kituo cha Polisi cha Sitakishari, Ukonga, Jijini Dar es Salaam na kutakiwa kueleza wapi walipo wenzake wengine.

Muathirika huyo wa tukio hilo, kwa sasa yupo uraiani baada ya kuachiwa Desemba 31, 2015, akitokea katika gereza la Segerea kutokana na hali ya afya yake kuzidi kuendelea kuwa mbaya kutokana na athari ya kipigo na mateso.

Akifafanua juu ya afya yake, alisema maradhi yanayomkabili ameyapata baada ya kuingizwa jiti katika sehemu yake ya haja kubwa sambamba na vipigo vya askari Polisi waliomkamata na kumtesa wakati wakimhoji.

Mateso hayo yalimletea athari mbaya ambapo alikuwa akitokwa na mkojo bila mwenyewe kujitambua huku akikohoa na kutapika damu.

“Awali wakati wakinitesa nilijikuta nimerusha ngumi kwa hasira nikijaribu kujitetea na ilimpata askari mmoja mdomoni, hapo sasa ndio niliamsha hasira zao, walinivua nguo zote na walianza kuniingiza jiti sehemu za haja kubwa.”

“Kama haitoshi, mti huo ukawa unasokotwa, kwa kitendo hicho nilipoteza fahamu na nilipokuja kuzinduka nilijikuta nipo wodini katika Hospitali ya Muhimbili.” Alisema Said.

Hata hivyo Polisi walimuondoa hospitalini hapo baada ya kupata fahamu, kisha alirudishwa tena Upanga na kuendeleza mada ile ile wakitaka awaeleze wapi zilipo bunduki walizopora Sitakishari na wenzake wengine wapo wapi.

Bw. Said alisema cha

Na Bakari Mwakangwale

IGP Ernest Jumbe Mangu.kusikitisha zaidi ni kwamba, yule jamaa yake Muislamu aliyemtaja, alifariki usiku wa saa nane, siku ambayo aliingia yeye kutokana na kipigo cha Polisi.

Awali akielezea mkasa huo mzima Said Daniel, alisema alikamatwa Agosti 17, 2015, na moja kwa moja alipelekwa sehemu fulani maeneo ya Upanga, Jijini Dar es Salaam, na kuelezwa kwamba ametajwa na mtu mmoja kuhusika katika tukio la uvamizi wa kituo cha Polisi cha Sitakishari.

Alisema baada ya maelezo hayo alionyeshwa mtu aliyemtaja yeye na alimtambua.

Mtu huyo alikuwa katika hali mbaya na alikuwa hatamaniki kwa kipigo alichopewa.

“Kweli nilipoonyeshwa nilimfahamu, alikuwa akiitwa Khalfan, alikuwa ni jamaa yangu wa karibu sana na aliponiona alieleza kuwa amenitaja tu ili nifike nimuone katika hali aliyokuwa nayo na hata akifa ifahamike kuwa amekufa akiwa mikononi mwa Polisi, kweli jamaa alifariki usiku wa saa nane, siku ile ile niliyoingia mimi.” Alisema Said.

Alisema, pamoja na maelezo ya jamaa yake huyo, ambayo yalikuwa na ishara ya kutohusika katika tukio hilo, bado Polisi walitaka awafahamishe walipo Saleh, Yusuph na Ibra, hata hivyo akasema aliwajibu majina hayo kwake yalikuwa ni mageni kwa maana hawafahamu.

Alisema, waliendelea zaidi kumlazimisha aeleze zilipo bunduki za Sitakishari, ambapo aliwaeleza kuwa kwa ujumla hahusiki katika tukio hilo kwani wakati linatokea alikuwa mahabusu Polisi Chang’ombe, kwa tuhuma za ugaidi.

Alisema, walimtaka awapeleke nyumbani kwake Buguruni kwa ajili ya upekuzi.

Alidai, msafara ulianza ukiwa na king’ora mbele na katika gari aliyopakiwa yeye likiwa limefungwa kitambaa chekundu

na yeye akafungwa kitambaa usoni.

“Tulipofika Buguruni, maeneo nipowaelekeza kuwa ni nyumbani walinifungua kitambaa ili niwaonyeshe nyumbani, nilishangaa kuona askari wakiwa wengi sana huku wakiwa na bunduki kila mmoja.

Alisema, waliingia ndani na kupekuwa kadri walivyoweza kila mahala lakini hawakupata walicho kusudia, lakini walikuta kaptula yenye mabaka ya sare za Jeshi na kofia yake, vyote vya mtoto wa miaka nane, kisha walichukua CD za mawaidha za Sheikh Aboud Rogo.

Alisema, wapojiridhisha waliambiana wanipeleke Mikocheni, alipodai kuwa wenyewe wanapaita ‘Task force’. Hao task force walipigiwa simu na walifika kumchukua.

Akiwa katika hali mbaya ya maumivu makali huku akikohoa na kutapika damu, haja ndogo ikimtoka bila kutambua huku akiwa amefungwa kwa mipira, badala ya Mikocheni waliamua apelekwe katika eneo la tukio Sitakishari Polisi, ili wakamtambue.

Said alisema akiwa hapo Sitakishari, katika mahojiano aliulizwa kama aliwahi kukamatwa na Polisi, yeye aliwajibu kuwa aliwahi akituhumiwa kwa ugaidi kabla ya mwezi wa Ramadhani mwaka jana na aliachiwa siku moja kabla ya sikukuu ya Idd.

Kwa maelezo hayo, alisema walimtaka awatajie askari yeyote anayemfahamu, alimtajia afande Majaliwa, kuwa ndiye aliyekuwa anashughulikia kadhia yake, walimpiga picha kisha walimtumia afande Majaliwa na kumuuliza habari zake kama anamtambua.

Alisema, afande huyo

aliwajibu kuwa anamtambua na kuwafafanulia kwamba Said, wakati wa tukio la Sitakishari, alikuwa Mahabusu ya Polisi Chang’ombe, zaidi ya miezi mitatu na kwamba hahusiki na tukio hilo.

“Pamoja na maelezo hayo ya afande Majaliwa, bado waliendelea kuning’ang’ania na nilikaa hapo Sitakishari kwa muda wa siku nane na baada ya hapo nilipelekwa Buguruni, napo wakaniweka mwezi mmoja, siku moja usiku walinitoa na kunipeleka Mikocheni na kule walinifunga jirani na jenereta, hapo mwili wangu ulikuwa umevimba sana na kunidhihaki kwa kuulinganisha na kiazi kilichoiva.” Alisema Said, aliyewahi kuwa kiongozi wa Kanisa kabla hajasilimu.

Alieleza kuwa akiwa hapo Mikocheni, tuhuma za uvamizi wa Sitakishari zilibadilika, ikaja hoja ya kukutwa na Kombati za Jeshi la Somalia, (kaptula na kofia).

Hata hivyo alidai kuwaeleza kuwa nguo hizo zilikuwa za kijana mdogo aliyekufa kwa kipindupindu, jambo ambalo hawakukubaliana nalo.

Alisema baada ya hapo alipelekwa Mahakamani na katika kuhudhuria kwake hapo Mahakamani, Hakimu aliamuru akatibiwe kutokana na kuchafua mazingira kila alipoingia hapo kwa sababu haja zilikuwa zikitoka bila mwenyewe kujitambua.

Awali waumini wa Msikiti wa Makukura, walifuatilia kadhia yake ili kuweza kumtolea dhamana, lakini waliambiwa kesi yake haina dhamana.

Lakini hali ilivyozidi kuwa mbaya na askari kutoonekana Mahakamani, aliachiwa.

“Ilipofika Desemba 31, 2015, tuliporudishwa tena Mahakamani, sikusomewa hata shitaka maana nilivyofika tu mle ndani, haja ndogo ikawa inatoka kwani hali ya kujizuia haikuwepo tena katika mfumo wa mwili wangu hivyo iliamuliwa nitolewe.

Kwa sasa nina nafuu kiasi, ukilinganisha na awali nilipo kuwa mikononi mwa Polisi na baadae gerezani, kwani naweza hata kutembea maana nilikuwa ni mtu wa kubebwa tu.” Alisema Said.

Alisema, nafuu hiyo ameipata kutoka kwa Waislamu wa Masjid Makukura, waliompeleka Hospitali ya Amana Ilala, baada ya kuachiliwa na Mahakama, ambapo alichoma sindano na kupewa vidonge tiba ambavyo vimesaidia kupunguza maumivu na tatizo lililosababishwa na mateso ya Polisi.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mhe. Charles Kitwanga.

4 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016

Tahariri/Makala

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAHAKAMA ni chombo kilichoanzishwa kwa mujibu wa Katiba na kupewa mamlaka ya kutafsiri sheria na kutoa haki katika jamii kuhusu mashauri mbalimbali ya kijinai au madai. Ni chombo cha kutoa adhabu kwa mkosaji na asiye na hatia aachwe huru.

Mahakama ni chombo ambacho kinatuhusu sote tajiri na masikini. Tunaelezwa kuwa katika mahakama zetu hakuna aliye juu sheria. Hilo limeanishwa pia katika katiba.

Katiba imeruhusu kuanzishwa kwa mahakama katika ngazi mbalimbali kuanzia mahakama ya mwanzo, wilaya, mkoa, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa.

Hata hivyo, pamoja na nia nzuri ya kuwepo mahakama zetu, lakini wapo ambao wamekosa uadilifu na hofu ya Mwenyezi Mungu, wanaozitumia mahakama zetu kinyume na kusudio lake.

Tulilo na hakika nalo ni kwamba wapo watumishi wa mahakama ambao wanatumia nafasi zao katika mahakama kujinufaisha kupitia rushwa. Lakini pia wapo wenye mamlaka, wenye nafasi za juu katika dola na wafanyabiashara wenye fedha, ambao wanatumia fedha na vyeo vyao kuingilia uhuru wa mahakama, ili wadhulumu na kupindisha haki.

Kwa upande mwingine, tunaona baadhi ya sheria zikitumika kuzuia au kuminya haki ya mtu mbele ya mahakama. Kwa mfano Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai anaweza kuamua kuzuia dhamana kwa mtuhumiwa, japo tuhuma zenyewe zinaweza zisiwe na uzito

Majipu katika vyombo vya Dolana Sheria nayo yatumbuliwe

unaoweza kumfanya mtuhumiwa akose haki yake ya dhamana.

Maeneo haya tuliyoyataja ni udhaifu mkubwa ambao umesababisha watuhumiwa wengi kuumia na kupata adhabu zisizokuwa rasmi katika mchakato wa kuendesha kesi zao mahakamani.

Ni vyema ikaeleweka kwamba, msingi mkuu wa amani na utulivu na upendo katika nchi ni kuwepo haki na uadilifu.

Tabia ya baadhi ya watu wenye nguvu, kugeuza mahakama kama hifadhi ya dhuluma na maovu au chuki zao dhidi ya wengine kwa maslahi yao, imeota mizizi hapa nchini.

Tunafahamu wazi kwamba katika baadhi ya mahakama zetu na katika jeshi la polisi kuna mitandao ya rushwa inayoshirikisha wanasheria feki, polisi na mahakimu kukosesha haki.

Mitandao hiyo inaathiri utoaji hukumu, inachangia kuchelewesha kesi kwa makusudi, ulaghai katika kuwatoa watuhumiwa waliopo mahabusu.

Kwa upande mwingine, rushwa hutolewa ili dhamana itolewe na kulazimishwa kumaliza kesi kabla ya hukumu. Wanaoonekana kuwa wagumu kutoa fedha za kinachoitwa “kusukuma mwenendo wa kesi” basi hao kesi zao au za ndugu zao zitakuwa ni za kutajwa na kuahirishwa, alimradi usumbufu ili watie adabu.

Tunaelewa kwamba Rais Magufuli aliahidi kuunda mahakama maalum kwa ajili ya mafisadi na wahujumu uchumi. Hilo ni wazo zuri na pia ameonyesha nia yake safi ya kunusuru maendeleo ya

Watanzania wote.Lakini pia Rais

Magufuli afahamu kuwa umefika wakati sasa serikali, kama ilivyotilia mkazo katika kuwabana mafisadi na wezi serikalini, kuwabana na kuwatia adabu wazembe na wavivu katika ofisi za umma, basi nguvu hiyo ielekezwe katika mahakama zetu na katika vyombo vya dola, ambavyo kimsingi ndivyo vyenye jukumu la kuona haki inatendeka.

Akiingia huko, hatuna shaka kwamba atashuhudia na kustaajabu kwa mengi yanayokwaza haki. Ataona ni namna gani watuhumiwa wanavyoteswa na

kudhalilishwa katika vituo vya polisi, wananyimwa matibabu, wanavyobambikiwa na kubadilishiwa kesi, rushwa inavyonunua haki za watu nk.

Ni muhimu Rais John Pombe Magufuli kufanya haraka kurekebisha mfumo wa utendaji sekta hii muhimu kwa ustawi wa amani na utulivu nchini, ili kukomesha mazoea haya mabaya ya wenye mamlaka na wenye fedha kutumia vibaya vyombo vya muhimu vya dola na kuvigeuza kuwa vya kukandamiza wanyonge.

Kazi kubwa ya mahakama ni kutafsiri sheria za nchi na kutoa haki, lakini imefikia

baadhi ya watu hawana tena imani na utendaji wa mahakama. Na ndio maana yanakuwepo matukio ya wananchi kuchukua sheria mkononi.

Wala hatuhitaji Rais Magufuli aanzishe Tume ya Ukweli na Maridhiano kama ile aliyoianzisha Mzee Nelson Mandela, kutoa nafasi kwa wale waliofanya dhulma wakati wa utawala wa kibaguzi na mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi warudishe imani kwa wale wote waliowadhulumu.

Watanzania wanachotaka kuona ni majipu yakitumbuliwa katika mihimili hiyo ya haki, ili haki ya kweli ipatikane kwa wananchi wote.

SHUKURANI zote anastahiki Mwenyezi Mungu, rehema na amani zimfikie mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kipenzi chetu Mtume (s.a.w).

Miongoni mwa Rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu ambazo zimekuja na Mtume wetu Muhammad (S.A.W), ni kwamba alikuwa hawapeleki watu katika hukumu kwa mara moja kwa ujumla, na wala alikuwa hatii uzito katika hukumu zake. Bali ilikuwa ikianza kwa pole pole.

Haya yamepatikana katika hukumu nyingi na hasa katika kuharamisha (kukataza) kama kuondoa masanamu pembezoni mwa Kaaba (Makka). Na harakati hizo za kuondoa masanamu zilifanywa mara kadhaa na kwa muda maalum na kwamba, hayakutolewa isipokuwa siku ya kuikomba Makka.

Kwa mfano pombe haikukatazwa isipokuwa pole pole kulingana na jinsi ilivyokuwa

Msitie uzito katika kutekeleza maamrisho ya Allah (s.w)

Na Sheikh Mohamed al-Amiri

ikiendelea kusababisha madhara katika jamii na wala haikukatazwa kwa mara moja. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu, “Wanakuuliza juu ya pombe na kamari, sema hayo ni madhambi makubwa na manufaa kwa watu na madhambi yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake”.Al-Bakarat.

“Enyi ambao mlioamini, msiingie katika swala mkiwa mmelewa hadi mjue ambalo mnalisema” Nisaa.

“Enyi ambao mlioamini kwa hakika Pombe na kamari na masanam na kupiga bao (ramli) ni uchafu miongoni mwa matendo ya shetani, jitengeni nayo hakika mtafaulu” Al-Maaidah.

Allah amenitia wepesi katika sheria za faradhi (lazima), kwa hakika mwenye kuzingatia katika sheria za Kiislam atakuta zimejengewa uwepesi, hakika ya uwepesi ndio muongozo wa Mwenyezi Mungu wa Mtume na ni alama ya uwazi miongoni mwa alama za dini hii tukufu.

Katika aya na dalili kwamba dini yetu imejengewa juu ya uwepesi, ni neno lake Mwenyezi Mungu katika Surat Al Bakara “Anataka Mwenyezi Mungu kwenu uwepesi na wala hataki uzito”.

Neno lake “Na tunakuwepesishia kuendelea kwenye wepesi” al-Aalaa na toka kwa Abii Hurairat (R.A) toka kwa Mtume (S.A.W) amesema, “Kwa hakika dini ni nyepesi na hatoitia mtu uzito isipokuwa

itamshinda fanyeni mambo kwa wastani na jisogezeni bashirini ombeni msaada asubuhi na jioni na sehemu ya usiku”.

Bukhari toka kwa Anasi bin Maliki (R.A) toka kwa Mtume (S.A.W) amesema “wepesisheni na wala msitie ugumu wabashirieni na wala msifukuze.

Mtume (S.A.W) alipokuwa anawalingania watu alikuwa akiwaamrisha kuwepesisha basi toka kwa Saidi bin ABII BURDA toka kwa baba yake toka kwa babu yake (R.A) toka kwa Mtume (S.A.W), alimtuma Muadhi na Abaa Mussa kwenda Yemen akasema, “Wepesisheni na wala msitie ugumu na bashirieni na wala msifukuze watu, kubalianeni na wala msihitalifiane (msigombane)” Bukhari na Muslim.

Na ni katika dalili hizi “zinazoamrisha” uwepesi kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na wingi wa thawabu zake, na wingi wa vipawa vyake.

Alikuwa Mtume (S.A.W) ni mfano wa juu katika kuwepesisha na ilikuwa uwepesi ndio dini yake na ni muongozo wake. Basi toka kwa Aisha (R.A) amesema, “hajapatapo kuchaguzwa Mtume (S.A.W) kati ya mambo mawili isipokuwa alichagua lililo jepesi mno...” Amepokea Imamu Bukhari na Muslim.

Bali sheria yenye hekima na kama walivyoelezea wanachuoni, iwe ni nguzo kubwa katika sheria. “Ugumu huvuta uwepesi”.

5 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016Habari za Kimataifa

MKUU wa Chama cha Labour cha nchini Uingereza, Jeremy Corbyn, amemtaka Donald Trump, anayewania kuteuliwa na chama cha Republican kugombea urais nchini Marekani kutembelea Msikiti mjini London, huenda akapata somo.

“Nimeamua kumwalika Donald Trump, atakapotembelea Uingereza, afuatane na mimi hadi katika jimbo langu kwa sababu naona ana matatizo na Wamexico na Waislamu”. Alisema Bw. Corbyn.

Corbyn amesema hayo baada ya kuzuka mjadala katika Bunge la Uingereza wakati wakijadili iwapo Trump aruhusiwe kuingia nchini humo au la.

Mkuu huyo wa chama cha Labour alisema kwa mtazamo wake, haoni haja ya kuzuiwa Donald Trump kuingia nchini humo, na iwapo atambelea Uingereza, anapenda ampeleke Msikiti wa London ili akapate somo.

“Kama unavyojua, mke wangu mimi ni Mmexico na jimbo langu ni jimbo lenye watu wa makabila na tamaduni nyingi tofauti, sasa nitakachofanya ni kumchukua Trump hadi Msikitini katika jimbo langu, ili aweze kuzungumza na watu huo. Alibainisha kiongozi huyo.

Wabunge wa Uingereza walikuwa na mjadala kuhusu kupigwa marufuku au la kwa anayewania nafasi ya kupeperusha bendera ya chama cha republican katika kinyang'anyiro cha urais wa Marekani, Donald Trump kuingia nchini Uingereza.

Mjadala huo uliochukua muda wa saa tatu, ulikuja baada ya karibu nusu milioni ya watu nchini Uingereza kuunga mkono hatua ya kumzuia Trump kuingia Uingereza baada ya Trump kusema kuwa Waislamu wote wazuiwe kuingia marekani ikiwa ni njia ya kupambana na vitendo vya kigaidi.

Hata hivyo Wabunge hao hawakuonyesha shauku kubwa ya kumfungia milango Trump, ili asiingie Uingereza kwani hakuna kura yeyote iliyopigwa mwisho wa mjadala.

Mmoja wa wabunge wa Uingereza ambaye ni Muislamu alisema kauli za Trump ni sumu, huku msemaji wa Idara ya Mambo ya Ndani Jack Dromey, akisema kuwa Trump azuiwe kuingia Uingereza.

Wakati chuki zake zikiwakera Waingereza na kujadiliwa bungeni, Trump ameendelea na kampeni zake, akizungumza katika chuo cha Liberty, chuo binafsi cha kikristo kilicho Lynchburg, Virginia amewaambia wanafunzi wa kikristo kuwa wanapaswa kuungana kuilinda dini yao.

''Tunapaswa kuilinda kwa kuwa kuna mambo yanafanyika, mambo mabaya sana, sijui ni nini lakini hatuungani labda dini

Donald Trump aalikwa Msikitini akajifunze

Ataka Wakristo waungane…

nyingine wanaungana kuzuia, hapa tunayo...ukitazama nchi hii, asilimia 70 mpaka 75 ni Wakristo, watu wengine wanasema hata zaidi ya hiyo, inadhihirisha nguvu tuliyonayo, tunapaswa kuungana'' alieleza Trump katika kampeni yake.

Donald Trump ametumia wito wake wa kutaka Waislamu wazuiwe kuingia Marekani kwa muda kwenye tangazo lake la kwanza la kampeni kwenye televisheni.

Tangazo hilo lilipeperushwa runingani mara ya kwanza Jumatatu.

Tangazo hilo la sekunde 30 linasimuliwa na sauti nzito ya kiume na linaonyesha pia picha za mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton na Rais Barack Obama.

Aidha katika tangazo hilo kuna picha za washambuliaji walioua watu 14 San Bernardino jimbo la California, wapiganaji wa Islamic State, manowari ya Marekani ikifyatua makombora, jumba likilipuliwa na wahamiaji wanaodaiwa kuwa wanavuka mpaka wa Marekani na Mexico.

Tangazo hilo linamalizika kwa Trump kutoa kauli mbiu yake ya kutaka kurejesha tena fahari ya Marekani.

Bw. Trump amesema atatumia karibu dola milioni 2 (£1.4 milioni) kila wiki kwa matangazo ya runinga katika majimbo ya Iowa na New Hampshire. BBC

Aidha Bw. Trumph anatumia pia wazo lake la kutaka ua ujengwe ukuta katika mpaka wa Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji haramu kuingia Marekani.

Anataka ujenzi wa ukuta huo “ulipiwe na Mexico”. BBC/irib

JEREMY Corbyn.

RAIS Kenyatta amesema nchi yake haitawaogopa Al Shabab na kuweka bayana kwamba, Kenya itawashughulikia wahalifu hao waliohusika na shambulizi lililogharimu makumi ya askari wake nchini Somalia na damu ya wanajeshi hao haitopotea bure.

Rais wa Kenya, Uhuru Kunyatta akiri kwamba wanajeshi kadhaa wa Kenya wameuliwa baada ya wanamgambo wa kundi la Al-Shabab Somalia, kushambulia kambi ya jeshi.

Imeelezwa kambi hinyo ni ya Umoja wa Afrika iliyopo katika mji wa El-Adde, unaopatikana takriban kilometa 60 kusini mwa mji mkuu wa eneo la Garbaharey.

Rais Kenyatta alisema nchi yake na washirika wake wataendelea kubaki nchini Somalia kukamilisha mpango uliowapeleka huko.

Wapiganaji wa Al Shabab walivamia lango kuu la kambi hiyo wakiwa na takriban magari manne yakiwa na milipuko na kuwashambulia kwa risasi wanajeshi wa Kenya ambao walikuwepo kambini hapo.

Kwa mujibu wa kundi la Al-Shabab, linadai limewaua wanajeshi 60 wa vikosi vya Kenya.

Lakini Naibu Gavana wa Gedo, Mohamed Hussein Isaak ameiambia VOA kwamba wanajeshi wa Kenya waliouliwa ni kati ya 35 na 40 na vikosi vingine vilifanikiwa kukimbia kutoka kambini hapo.

Aidha Bw. Isaak alisema ndege za kivita za Kenya zilirusha mambomu kwa wapiganaji wa Al Shabab kuzunguka mji wa El-Adde na kuharibu magari mawili yaliyokuwa na silaha.

Mashuhuda wamesema Al-Shabab walipandisha bendera yao baada ya kulitwaa eneo hilo na kushikilia silaha katika magari ya kivita.

Misheni ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia AMISOM imethibitisha tukio hilo japokuwa haikutoa taarifa za kina.

Waziri wa Usalama wa Somalia Abdiqadir Aheikh Ali Dinii, ameshutumu shambulizi hilo katika kambi ya Umoja wa Afrika. VOA.

Kenya yathibitisha wanajeshi wake kuuliwa Somalia

SHEIKH Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dini cha Azhar nchini Misri amesema kuwa kwa mujibu wa siasa za chuo cha Azhar, kinakubali madhehebu yote za Kiislamu.

Sheikh wa Azhar ameyasema hayo katika mwendelezo wa mzungumzo yake ya kila wiki, ambapo wiki hii alilazimika kutetea chuo cha Azhar, kutokana na kile kilichodaiwa kuwa kinafundisha ugaidi na kupinga madhehebu mengine.

Tamko hilo la Sheikh Ahmad Taib, ambaye ni Sheikh Mkuu wa chuo hicho alilitoa baada ya vyombo vya habari vya Misri kutoa taarifa kuwa chuo hicho cha dini, kinafundisha baadhi ya masomo yanayosababisha kueneza ugaidi, hali ambayo imetokea baada ya uongozi wa chuo hicho kukiri na kutangaza kuwa kuna mamia ya wanafunzi kutoka nchi mbalimbali wamejiunga na vyuo vya kigaidi na wameamua kuwafukuza chuoni hapo.

Sheikh huyo alisema tangu chuo cha al Azhar kiasisiwe kina muda wa miaka 1060, katika kipindi hicho chote kimekuwa kikifanya juhudi za kuwa na mwenendo wa wastani, na kujiepusha na kasumba na ushabiki wa madhehebu, ikiwemo kuheshimu madhehebu na wafuasi wa madhehebu nyingine na mpaka hivi sasa juhudi zao ni kuhakikisha kuwa wanawalea wanafunzi wao kwa misingi ya Kiislamu ya kuheshimiana, hivyo Azhar kamwe hakijawahi kuwakafirisha wafuasi wa madhehebu yeyote nyingine.

Aidha alisema hivi sasa wanasikia baadhi ya tuhuma dhidi yao kuwa katika ratiba ya baadhi ya masomo ya chuo wanakuza fikira potovu ya kigaidi, hali ambayo wanafunzi wa chuo hicho wako mbali na tuhuma na mafunzo ya kigaidi, huku akisisitiza kuwa yeye yupo katika chuo hicho zaidi ya nusu karne na hajawahi kuona mafunzo yaliyokuwa na misingi hiyo ya kigaidi.

Sheikh Ahmad Taib alisema siasa ya chuo cha dini cha Azhar kinakubali rasmi madhehebu zute za Kiislamu, na kuwasuka wanafunzi wote kuwa katika mstari huo, huku akibainisha kuwa katika chuo hicho kuna tahakiki nyingi wanazozifanya wanafunzi, zinazohusu madhehebu ya Kishia, tahakiki ambazo hufanya uchunguzi kuhusu nadharia za wanazuoni wa kishia, kwa maana mwenendo wa Azhar ni kutowakafilisha wafuasi wa madhehebu mengine huku wakiamini kuwa kila mtu atakaye tamka shahada mbili kuwa yeye ni Muislamu. ABNA.

Tunakubali madhehebu yote ya Kiislam-Sheikh Mkuu

6 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016Hoja ya Juma Kilaghai

UGONJWA wa moyo, kiharusi, saratani, kisukari na magonjwa mengine ya kimfumo ndiyo sababu kubwa ya vifo duniani. Magonjwa haya yote yana uhusiano wa moja kwa moja na lishe. Takwimu za hivi sasa zinaonyesha kuwa 80% ya vifo vinavyotokana na haya magonjwa, hutokea katika zile nchi zenye vipato vya chini na vile vya kati. Tazama takwimu hapa chini.

Kuna uhusiano gani kati ya chakula na maradhi?

1

NCHI KWA MUJIBU WA KIPATO VIFO VINAVYOTOKANA NA

MAGONJWA YA KIMFUMO ZENYE KIPATO CHA JUU 20% ZENYE KIPATO CHA KATI KINACHOKARIBIANA NA JUU

8%

ZENYE KIPATO CHA KATI KINACHOKARIBIANA NA CHINI

37%

ZENYE KIPATO CHA CHINI 35%

Hali haikuwa hivi siku zote. Huko nyuma, hususan kwenye miaka ya 1950 kurudi nyuma, kuenea kwa maradhi haya katika nchi za kipato cha chini kulikuwa kwa kiwango kidogo sana ukilinganisha na zile nchi za kipato cha juu. Tazama takwimu hapa chini.

Chanzo: www.who.int/chp/chronic_disease_report/en/

1

NCHI 1940 -1950 1950 -1960 1960 -1970 1970 -1980 1980-1990 1990-2000 NCHI ZA KIPATO CHA JUU Ongezeko la

kasi Kilele Kuanza

kushuka

NCHI ZA KIPATO CHA KATI KINACHOKARIBIA JUU

Ongezeko kidogo

Ongezeko la kasi

Kilele kwa baadhi ya nchi

NCHI ZA KIPATO CHA KATI KINACHOKARIBIA CHINI NA NCHI ZA KIPATO CHA CHINI

Viwango vya chini

Ongezeko kidogo

Ongezeko la kasi kwa baadhi ya nchi

Ni kitu gani kimetokea na

kuzisukuma nchi za kipato cha chini kutoka katika nchi zilizokuwa na vifo vichache vinavyotokana na maradhi ya kimfumo, hadi kuwa ndiyo nchi zinazoongoza katika miaka hii?

Katika makala iliyoandikwa na Dylan Neel aliyoipa kichwa cha habari ’The Sugar Dilema’, na kuchapishwa katika jarida la Global Health Review linalochapishwa na Harvad College, mnamo tarehe 24 Octoba, 2012, Dylan anasema. Tunanukuu:

“Uzito wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa dunia umefikia kiwango cha kutisha katika kipindi cha muongo mmoja uliopita. Kwa mara ya kwanza katika historia ya mwanadamu magonjwa haya kwa mfano kisukari, saratani, na ugonjwa wa moyo yamekuwa ni tishio kubwa la kiafya kuliko magonjwa ya kuambukiza, ambapo yanasababisha kiasi cha vifo 35 milioni kila mwaka!.

“Pamoja na kwamba ziko sababu nyingi zinazopelekea katika hali hii, moja ya sababu kubwa na isiyo na ubishi ni

Chanzo: WHO, NMH/MNC

ongezeko kubwa la matumizi ya sukari ya viwandani. … Utandawazi umepelekea vyakula vya sukari kuenea kwa kasi katika nchi zinazoendelea. Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, matumizi ya sukari yameongezeka mara 3 dunia nzima. ….Vyakula vya chapchap (fast food), ice cream, keki, juisi za viawandani na soda mbalimbali ni vyakula

ambavyo vina kiasi kikubwa sana cha sukari za glucose na fructose. Mchanganyiko wa sukari hizi unapoingia mwilini ini huubadilisha bila kuchelewa kuwa mafuta, na hali hii inaweza kupelekea kwenye tatizo la seli za mwili kuigomea insulin kufanya kazi

yake (insulin resistance). Kwa sasa inaaminika kwamba hali hii ndiyo kisababishi namba moja cha unene uliopindukia, ni moja ya visababishi vikuu vya magonjwa ya moyo, kisukari cha ukubwani, na baadhi ya saratani…..”

Jarida la Vascul Pharmacol la April 2014 limechapaisha matokeo ya utafiti uliopewa kichwa cha habari “Vihatarishi vya magonjwa ya moyo na mafuta ya mbegu ya kupikia”

Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa mafuta ya mbegu hayafai kwa matumizi ya kupikia kwa sababu yanapopata joto hubadili muundo wake wa kikemia na kutengeneza kitu ambacho kina madhara makubwa kwa afya ya moyo na mishipa ya damu. Kwa mujibu wa utafiti huu, matumizi ya muda mrefu ya mafuta haya kama kiungo kilichotumika kupikia chakula yamehusishwa na kuongezeka kwa shinikizo la damu, ongezeko la lehemu kwenye mzunguko wa damu, mfuro (inflammation) kwenye mishipa ya damu, na mabadiliko mengine kwenye mfumo wa

mzunguko wa damu, ambapo vyote kwa pamoja vimebainika kuongeza kitisho cha mkakamo wa mishipa ya damu.

Tangu mwaka 1953 kumekuwa na mgogoro mkubwa sana kuhusu mafuta ya kula. Katika mwaka huo Dk. Ancel Keys alichapisha matokeo ya utafiti wake aliouta “The Seven Countries Study”. Dk. Keys alisema kuwa kuna uhusiano wa karibu sana kati ya kiasi cha mafuta koza (saturated fat) yaliyoko kwenye chakula na kiasi cha utando-nta (sludge) kwenye mishipa ya damu. Pamoja na kwamba baadhi ya wanasayansi walimpinga sana Dk Keys kwa madai kwamba kulikuwa na takwimu kutoka mataifa 22 ambazo alichagua kuzifumbia macho na kutoziingiza kwenye matokeo ya utafiti wake kwa sababu hazikuunga mkono kile alichokitaka, hawakusikilizwa. Kuanzia hapo ilianzishwa kampeni kubwa na ya kutisha dhidi ya ulaji wa mafuta koza ikishikiwa bango na vyombo vya habari, madaktari na hata mamlaka za kusimamia masuala ya afya katika nchi mbalimbali. Baadhi ya watu wanadai kuwa kulikuwa na mtu. Kwa mujibu wa watu hawa kampeni hii ilifadhiliwa kwa kiasi kikubwa na wasindikaji wa mafuta ya mbegu.

Kitu cha kushangaza ni kwamba mpaka leo nadharia hii imeota mizizi na inaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na madaktari. Inashangaza kwa sababu akili ya kawaida tu ilitakiwa ihoji juu ya kuwepo kwa ongezeko kubwa la magonjwa ya moyo na mengine ya kimfumo, huku kimsingi mafuta ya kula kwa sasa yakiwa takriban yote ni yale ya mbegu! Akili hiyo hiyo ilitakiwa ihoji: Ni kwa nini magonjwa ya kimfumo katika miaka ya 1950 kurudi nyuma, wakati huo matumizi ya mafuta ya mbegu ukilinganisha na yale koza yakiwa kidogo sana, yalikuwa nayo ni kidogo sana?

Tumalizie kwa kuzungumzia kundi la chakula la protini. Hili ndiyo lile linaloitwa la kujenga mwili! Ukweli wa mambo ni kwamba protini ina majuku mengi mwilini. Baadhi ya majukumu haya ni:

1) Protini huhitajika kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa tishu mbalimbali za mwili kwa mfano nywele, ngozi, misuli, na viungo mbalimbali vya ndani.

2) Protini ni moja ya vyanzo vya niashati ya kuendeshea mwili. Protini iliyozidi mwilini ambayo haihitaji kwa majukumu

muhimu ya ukarabati na ujenzi wa tishu za mwili na majukumu mengine ya lazima ndani ya mwili hugeuzwa kuwa nishati ya kuendeshea mwili. Inapotokea kuwa haihitajiki, na wakati huo huo kuna vyanzo mbadala vya nishati, mathalani wanga, basi protini hiyo iliyozidi hugeuzwa kuwa seli za mafuta ndani ya mwili.

3) Protini inahusika katika uundwaji wa baadhi ya homoni, kwa mfano insulin. Homoni ni kemikali inayozalishwa na mwili kwa ajili ya kuwezesha utendwaji wa majukumu fulani fulani maalumu katika mwili.

4) Protini inahusika katika uundwaji wa vimeng’enya (enzymes) mwilini.

5) Protini huhitajika katika usafirishaji na utunzaji wa molekuli mbalimbali. Kwa mfano, wakati hemoglobin ni protini inayotumika kusafirisha na kusambaza gesi ya oxygen kote mwilini, ferritin ni protini inayotumika kuwezesha madini ya chuma kuhifadhiwa katika ini.

6) Protini huhitajika katika uundwaji wa chembechembe zinazotumika kuulinda mwili dhidi ya maambukizi na maradhi zinazoitwa antibodies. Protini hizi hutambua na kusaidia katika kuwaangamiza maadui mbalimbali walioingia mwilini ikiwa ni pamoja na bakteria na virusi. Protini hizi mara nyingi hufanya kazi pamoja na seli zingine zinazohusishwa na mfumo wa kinga za mwili, kwa mfano chembechembe nyeupe za damu.

Maisha hayawezekani bila ulaji wa protini. Pamoja na umuhimu huu wa protini, protini inaweza kuwa chakula cha hatari pale inapoliwa bila mazingatio. Protini ni chakula kinachozalisha tindikali kwa wingi sana mwilini baada ya kuchakatwa ili kupata nishati na viini lishe vilivyopo.Tindikali hii ni lazima itolewe mwilini la sivyo itaweuweka mwili katika msongo mkubwa wa kifiziolojia na kusababisha seli za mwili kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Wingi wa tindikali kwenye mwili unaaminika kuwa ni chanzo kikuu cha maradhi mengi sana ya kimfumo kama vile saratani, magonjwa ya mifupa na magonjwa ya mzunguko wa damu.

Taarifa nyingi ambazo ni rasmi zinaonyesha kwamba mtu mzima mwanamme ambaye hana mambo mengi ya kuushughulisha mwili wake anahitaji kiasi cha gramu 56

Inaendelea Uk. 7

7 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016Makala

Kuna uhusiano gani kati ya chakula na maradhi? Inatoka Uk. 6tu za protini kwa siku. Aidha taarifa hizo zinaonyesha kuwa kwa upande wa wanawake, mtu mzima ambaye haushughulishi sana mwili wake mahitaji yake ni gramu 46 tu. Hata hivyo baadhi ya wataalamu wanasema viwango hivyo ni vya chini sana na vinaweza visitosheleze mahitaji ya kiafya ya mhusika iwapo ataongeza kiwango cha kuushughulisha mwili wake. Waliomo kwenye kundi hili wanapendekeza kiasi cha gramu 124 za protini kwa mwanamme kwa siku na gramu 102 za protini kwa mwanamke kwa siku.

Kundi la tatu la wataalamu linasema kuwa ukweli wa mambo ni kwamba miili yetu inahitaji kiwango kidogo sana cha protini kuweza kujiendesha kwa ufanisi. Wataalamu hawa wanadai kuwa kuna tafiti zinazoonyesha kuwa mahitaji ya mwili ya protini kwa siku kwa mtu mzima hayatakiwi kuzidi gramu 25. Kwa mujibu wa wataalamu hawa, tafiti hizi zimeonyesha kuwa ulaji ukifikia kiasi cha gramu 47 kwa siku mifupa ya mwili huanza kupoteza madini ya calcium na kuifanya iwe kama chekeche. Dk. M.Ted Morter, Jr., kupitia kitabu chake kinachoitwa Health and Wellness amejenga hoja nzito kuhusiana na suala hili ambako ametoa mifano halisi kuhusiana na madhara ya ulaji wa protini uliopindukia mipaka. Hoja hizi zina mazingatio

makubwa ukizingatia kuwa tamaduni zetu zinawaona watu wenye uwezo mkubwa wa fedha kama ndio watu bora kwenye jamii, na moja ya vipimo muhimu vya uwezo mkubwa wa kifedha katika tamaduni hizi ni kiasi cha protini, hususan nyama, samaki na maziwa kinacholiwa na mhusika na familia yake!

HitimishoKuugua ni kitendo chenye

athari kubwa na mbaya kwenye uchumi. Mtu anayeumwa mara kwa mara uwezo wake wa uzalishaji hupungua na hali hii ina athari hasi kwenye mapato ya familia. Kwa hivi sasa sheria na sera za nchi zinazohusu wafanyakazi zinamtaka mwajiri kulipia gharama za matibabu za mfanyakazi wake pamoja na matibabu ya familia yake. Hii ina maana kuwa pale wafanyakazi na familia zao wanapougua mara kwa mara, uchumi wa mwajiri huathirika, kwanza kutokana na uzalishaji mdogo, na pili kutokana na kulazimika kulipia gharama za matibabu. Mwisho wa siku hata uchumi wa nchi huathirika kutokana na kushuka kwa uzalishaji na pia matumizi ya fedha nyingi katika kuagiza madawa na vifaa tiba.

Hakuna shaka yoyote kuwa uwekezaji katika elimu ya afya kwa wafanyakazi na wananchi kwa ujumla, hususan katika masuala ya lishe, ndiyo suluhisho endelevu na la kudumu kwa afya na uchumi wa wadau wote.

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Zanzibar, ulitia doa sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushabikia ubaguzi wa rangi miongoni mwa raia wa visiwa hivyo. Akizungumza katika Televisheni ya Azam, Jumanne ya wiki hii, Mwanahistoria maarufu Sheikh Mohammed Said, alisema vijana hao wa CCM, wamezitia doa sherehe hizo kwa kusheherekea kwa mtindo wa ubaguzi wa rangi huku Watanzania na Ulimwengu ukishuhudia hali hiyo.

Katika kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika viwanja vya Maisara, Mjini Unguja, waliibuka na bango lenye ujumbe uliosomeka ‘Machotara Hizbu Zanzibar ni nchi ya Waafrika’.

Bango hilo lilipitishwa mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein alipokuwa akipokea matembezi ya Vijana hao waliotembea katika mikoa minne ya Kichama. Sheikh Said alisema kwa ujumla katika historia ya sherehe hizo, Watanzania hawajapata kusheherekea Mapinduzi ya Zanzibar katika hali ya majonzi kama mwaka huu, kukiwa na dalili ya mgawanyiko kutokana na mkwamo wa kisiasa visiwani humo.

“Tunasheherekea sherehe za Mapinduzi tukiwa katika hali ya CCM Zanzibar wakipanda jahazi la ubaguzi wa rangi kupitia Umoja wa Vijana (UVCCM), na kwa kupita mbele ya umma wakionyesha bango la kibaguzi, wakiwabagua Wazanzibari wenzao ambao hawakuzaliwa na ngozi nyeusi, jambo ambalo limezagaa katika mitandao ya kijamii kama moto wa makumbi.” Alisema Sheikh Mohammed.

Sheikh Said alisema hataki kuamini kuwa CCM Zanzibar imefilisika kiasi hicho, kwa kufikia kuiacha hali hiyo ambayo waasisi wa Tanzania waliikemea kwa nguvu zao zote. Akifafanua maana ya ''Hizbu,'' alisema kuwa ni neno la Kiarabu lenye maana ya ''Chama'' na ''Watan,'' likiwa na maana ya ''Taifa.''

Akifafanua zaidi kuonyesha kwamba yaliyofanywa na UVCCM ni kutaka kuiingiza nchi katia ubaguzi wa rangi ambao haukuwepo tangu enzi hizo, alisema historia ya Tanzania katika kupigania uhuru wa Tanganyika walikuwepo Wazungu na Wahindi, ambao walikuwa ni viongozi wa TANU na wakisimama kugombea nafasi za uongozi na wakishinda bila kubaguliwa.

Sheikh Mohammed, aliwatawaja baadhi yao kuwa ni Sophia Mustafa, Ratansey, Amir Jamal, Dereck Bryceson, na zaidi katika Bunge la Tanzania kulikuwa na kila aina ya Wabunge mpaka Makalasinga.

Kwa upande wa Zanzibar imekuwa na Rais Amani Abeid Karume, ambaye baba yake asili yake ni Mnyasa na mama yake ana asili ya Kihindi.

“Hivi ndugu zetu kama Mansour Yusuf Himid na Mahamoud Thabit Kombo na wengi wao akiwemo Mh. Amani Karume (Rais mstaafu) na binti yake Fatma, watajisikiaje kwa kauli kama hizi za ugozi?”

Mapinduzi hayakuwa na maana ya ubaguziMansour, Amani Karume watajisikiajeNa Bakari Mwakangwale

alihoji, Sheikh Mohammed. Hata hivyo Mohammed Said

alitoa tahadhari juu ya hatari ya kuwatumia vijana kama walivyotumiwa na Adolf Hitler kwa kutengeneza ''Storm troopers,'' au ''Brown Shirts,'' kuwatisha wananchi huku akiwataka viongozi kuisoma historia ili wapate mafunzo, nini ilikuwa hatima ya mambo haya.

Awali, Sheikh Mohammed Said, akifanya mahojiano na mtangazaji wa Azam TV, Faraja Sindegea kuhusu historia ya Mapinduzi ya Zanzibar, alisema kumbukumbu nyingi za Mapinduzi ya Zanzibar, zimo katika vifua vya watu na wengi wao wameshatangulia mbele ya haki huku wengi katika hao, kwa njia moja au nyingine walishiriki wakiwa Bara katika kuiangusha Serikali ya Zanzibar.

“Lakini kutokana na mauaji yaliyotokea katika Mapinduzi, baadae wengi wao walifunga midomo na hawakutaka watu wajue kuwa walihusika, mfano ni Ali Mwinyi Tambwe na wengine wengi.” Alitoa mfano Sheikh Said.

Akielezea hali ya baadae ya Zanzibar katika hali ya kisiasa kwa sasa alisema, suala hilo lipo wazi kwamba Wazanzibari wamefanya uchaguzi walioshinda wapewe haki yao na walioshindwa wakubali kushindwa.

“Kwa ufupi ni kuwa, ''The people of Zanzibar have spoken,'' hakuna njia yeyote nyingine ila kwa walioshindwa kukubali kushindwa na maneno ya Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, kuwa kesi yake ipelekwe mahakamani, isingestahiki kutolewa. Itakuwa kichekesho cha mwaka mtu akishindwa uchaguzi dhahiri na anapoelezwa hivyo aseme, ''Nenda mahakamani mimi ni rais halali.''.” Alisema Sheikh Mohammed, huku akinukuu kauli za Mh. Ali Mohammed Shein.

Aidha Bw. Mohammed Said alifanya rejea za Ton Ton Macout wa Papa Doc wa Haiti,

ambae alitumia mbinu za vitisho kwa wananchi wake mfano wa Mazombie wa Zanzibar. Aliwataka viongozi waisome historia ili

wapate mafunzo nini ilikuwa hatima ya mambo haya.

Akizungumzia kuhusu hali ya baadae ya Zanzibar, Sheikh Said alisema hataki kuamini kama uongozi wa juu wa CCM Zanzibar waliwatuma vijana wale kufanya walichofanya na kwamba akili yake inamkatalia kabisa.

“Sitaki kuamini kuwa tumeanza kuwatengeza akina Hendrik Verwoerd na Eugene Terre Blanche weusi katika visiwa vya Zanzibar. Kwa hili CCM Zanzibar inamuiga nani katika hili? Hitler na Manazi na vijana wao waliojulikana kama Stormtroopers ukipenda waite Brown Shirts? Hilo bango mbona litawagusa wengi katika safu ya uongozi wa siasa katika Zanzibar na wengine walipatapo hata kuiongoza nchi? Machotara? Nani huyu chotara?” alihoji.

Alisema ujumbe wa bango liliooneshwa na waandamanaji wa CCM linaonyesha kwamba tumehama kwa Waarabu na sasa tuko kwa Machotara! Lakini akahoji kuwa huyo chotara si ana wajomba, babu, bibi na mama wakubwa na wadogo Waafrika? Na kwamba nini khasa tafsiri ya mambo yale ? Hata hivyo alihitimisha maswali yake kwa watu wasubiri na kwamba wakati utatoa jibu.

Vijana wa CCM wakiwa wameshika bango lenye kuashiria ubaguzi wa rangi visiwani Zanzibar hivi karibuni.

8 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016MakalaSomalia moja

MWISHONI mwa mwaka jana Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Mahiga alifanya ziara ya siku moja nchini Burundi ili kuangalia hali ya huko kuhusu vurugu zinazoripotiwa. Aliporudi alieleza kuridhishwa na “hali ya utulivu” aliyoikuta Burundi. Waziri alisema, “ kulikuwa na utulivu na watu waliendelea na shughuli zao…sikusikia mlio wa risasi na sikuwa na haja ya kusindikizwa na polisi kwenye ziara… labda kama ni mikoani, lakini jiji (Bujumbura) lilikuwa tulivu.”

Mahiga pia alisema serikali ya Burundi ilimhakikishia kwamba inashiriki kikamilifu katika mazungumzo ya kurejesha amani yanayofanyika nchini Uganda. Tanzania na nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pia zinashiriki. Wengine walioalikwa ni pamoja na Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Ulaya (EU), Umoja wa Mataifa (UN) na Marekani.

Ziara hiyo ya Mahiga ilitokana na agizo la Rais John Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa EAC, kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa ulioikumba Burundi kutokana na makundi yanayompinga Rais Pierre Nkurunzinza kuongoza awamu ya tatu baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika Julai mwaka jana. Mie sina hakika iwapo ziara ya siku moja ya Mahiga inatosha kujua iwapo kuna utulivu au machafuko nchini. Pia kama kuna utulivu, kwanini yafanyike mazungumzo ya kurejesha amani? Lakini ndivyo tulivyoelezwa.

Pia ni vizuri tukajiuliza, iweje katika amani ya Burundi inayozungunziwa nchini Uganda waalikwe wajumbe kutoka Ulaya na Marekani? Kuna wasiwasi kuwa mgogoro huu unaweza ukaibua tena mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yaliendelea kuanzia 1993 hadi 2006. Wakati huo wananchi wa Kihutu walio wengi nchini walipambana na jeshi lililokuwa na Watutsi wengi. Matokeo ya mapigano haya ni kupotea kwa roho za

Somalia moja inatutosha…

Na Nizar Visram

Tusitume tena majeshi Burundi

raia 300,000. Hii ndio Burundi ambayo leo inakumbukwa kwa masikitiko makubwa. Mapigano hayo yalimalizika baada ya makubaliano ya Arusha yaliyosainiwa na pande zilizokuwa zinapingana. Walikubaliana kuunda jeshi la pamoja na serikali ya mpito iliyoongozwa na Nkurunziza.

Sasa mgogoro umeanza upya tangu Aprili mwaka jana wakati Rais Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kugombea urais kwa muhula wa tatu ambao yeye anasema ni wa pili. Anadai muhula wa kwanza ni ile serikali ya mpito. Hata hivyo mahakama ilikubaliana naye na kusema kuwa ana haki ya kugombea kwa vile katiba inamruhusu. Wapinzani walipinga na kusema jopo la majaji lililazimishwa kutoa uamuzi huo, hasa kwa vile mmoja wa majaji hao aliamua kutoroka nchini kwa vile alipinga uamuzi huo. Mara moja baadhi ya makamanda wa jeshi walifanya jaribio la kuipindua serikali ya Nkurunziza. Walishindwa na mwezi wa Julai 2015 uchaguzi ukafanyika na Nkurunziza alitangazwa mshindi. Wapinzani wakayakataa matokeo.

Alimradi nchi imekosa utulivu. Shirika la kimataifa la haki za binadamu (Amnesty International) limeripoti kuwa tarehe 11 Disemba mwaka jana majeshi ya serikali yaliwashambulia wananchi katika jiji la Bujumbura. Ripoti hiyo inasema watu wasiopungua 87 waliuawa, wanane wakiwa wanajeshi. Kwa ujumla watu zaidi ya 300 inasemekana wamekufa tangu Nkurunziza kuchaguliwa. Aidha zaidi ya watu 220,000 wamelazimika kuikimbia nchi yao na kwenda nchi za jirani kama Tanzania. Wengine wengi wamegeuka wakimbizi ndani ya nchi yao.

Machafuko kama haya kwa hivyo hayawezi yakawa ya nchi moja peke yake. Ni lazima nchi

za jirani zitahusika kwa namna moja au nyingine. Burundi ni mwanachama wa EAC. Ndio maana jumuiya hiyo imeamua kuingilia kati na kusuluhisha. EAC imemteua Rais Museveni wa Uganda kuzikutanisha pande husika. Mwishoni mwa Disemba 2015 Waziri wa Ulinzi wa Uganda alisema makundi 14 yalitarajiwa kushiriki mjadala jijini Kampala. Ni pamoja na chama tawala, vyama vya upinzani na asasi za kiraia. Mipango imefanywa pia kwa ajili ya mazungumzo mjini Arusha yakifuatiwa na mkutano wa marais wa nchi za EAC chini ya uwenyekiti wa Rais Magufuli.

Kuna watakaouliza iwapo EAC itafanikiwa kuwasuluhisha Warundi wanaozozana. Makubaliano ya Arusha yalitiwa sahihi na pande zote baada ya jitihada kubwa zilizofanywa na Mwalimu Nyerere na viongozi wengine wa Afrika. Yote haya yamesahauliwa na kwa mara nyingine Tanzania na nchi za EAC zinaitisha mikutano ya usuluhisho. Lakini huo ni wajibu wetu. Mgogoro wa Burundi ni dhahiri unazigusa nchi za jirani. Nchi ya kwanza ambayo itaathirika ni Rwanda kwa sababu nchi hizi mbili zinafanana kihistoria, kitamaduni na kikabila. Ndio maana Rais Kagame wa Rwanda aliingilia kati na kumtaka Nkurunzinza asigombee muhula wa tatu. Lakini tatizo ni kuwa Kagame mwenyewe hataki kuachilia kiti cha urais. Atawezaje kumshauri mwenzie?

Nchi ya pili inayohusika moja kwa moja ni Uganda ambako Rais Museveni ameitisha mkutano akiwa msuluhishi. Tangu Julai mwaka jana aliteuliwa na EAC awe msuluhishi. Lakini na Museveni naye anaendelea kukalia kiti. Mnamo 2005 alibadili katiba ili imruhusu kuendelea kukaa madarakani. Hivyo na yeye naye si rahisi

kumshauri Nkurunzinza ag’atuke. Labda Rais Magufuli ataweza kumshauri. Lakini tatizo la Tanzania ni kuwa inaonekana ina kigeugeu. Hapo awali ilimwambia Nkurunzinza aachie kiti. Lakini baadae ikamnyamazia kimya. Kwa vyovyote vile, itabidi EAC iwasuluhishe Warundi kama alivyofanya Mwalimu.

Kuna wanaosema njia pekee ni kutumia majeshi. Hii si rahisi hata kidogo. Tuangalie Somalia jinsi majeshi ya nje yalivyozama katika matope, yakishindwa kujitoa na yakishindwa kuzuia machafuko. Nadhani Somalia moja yatutosha.

Hata hivyo, AU imeamua kutuma majeshi ya usalama yatakayoitwa Kikosi cha Kiafrika cha Kulinda Usalama nchini Burundi (African Prevention and Protection Mission in Burundi au MAPROBU). Wameamua hata jina. Na huo usalama watakaoulinda uko wapi?

Kikosi hiki kitakuwa na wanajeshi 5,000. AU eti imetoa siku nne kwa serikali ya Burundi kukubaliana na uamuzi huu, la sivyo kikosi kitapelekwa bila ya idhini ya serikali. Suali ni je, AU inaweza kutuma majeshi bila ya idhini ya nchi husika? Katiba ya AU kifungu cha 4 (h) inaruhusu AU kuingilia kati kijeshi kama nchi inayokabiliwa na mauaji ya halaiki au uhalifu wa kijeshi au uhalifu dhidi ya mwanadamu. Ni nani wa kuamua iwapo Burundi imeingia katika hali hii? Tumeona Waziri Mahiga akisema kuna utulivu!

Na Nkurunzinza naye ametangaza kuwa anakataa wazo la AU kutuma majeshi yake. Amesema huo utakuwa ni uvamizi wa kijeshi usiokubalika katika nchi huru inayojitawala kama Burundi. Bunge la Burundi nalo limekubaliana naye kwa kukosoa uamuzi wa UN. Bunge liliitaka serikali isikubali nchi kurubuniwa na AU wakati kuna ‘utulivu’ nchini. Wabunge pia walilaani kuingilia kwa nchi za magharibi katika mambo ya ndani ya Burundi.

Hili suala la nchi za Magharibi kujiingiza katika mambo ya Burundi linahitaji maelezo. Burundi ina madini aina ya nikeli (nickel) ambayo inaongoza katika ubora wake duniani. Utajiri huu unamezewa mate na makampuni ya kimataifa ambayo yanataka kuudhibiti. Makampuni ya Marekani yamekuwa yakifanya bidii kudhibiti nikeli ya Burundi lakini serikali ya huko imesaini mkataba na kampuni ya Urusi. Jambo hili limeikasirisha sana Marekani. Ni katika muktadha huu ndipo tunaelewa mbinu za Magharibi kutumia majeshi huko Burundi. Sio kwa kutumia majeshi yao bali kwa kupitia nchi za Kiafrika.

Inaendelea Uk. 18

WAZIRI wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Mahiga

9 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016Makala

KATIKA hatua ambayo kwa uchambuzi wa haraka inaonekana imekosea kiprotokali, au kimantiki, kongozi wa upinzani Visiwani na mgombea urais, Seif Shariff Hamad, amefichua kupeleka barua kwa Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, kuingilia kati suala la kutangazwa matokeo. Kilichosemekana ni kuwa Maalim Seif amemshitaki Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwa Papa Francis, hali ambayo ilikuwa inazua utata wa kihisia na kiprotokali. Ila ukiiangalia barua kwa undani utata huo unapotea.

Barua hiyo ya Novemba 25 mwaka jana ina umuhimu mkubwa kwa jinsi ambavyo suala la mzozo wa matokeo uchaguzi wa urais Zanzibar linatatuliwa na nafasi ya serikali ya Muungano katika suala hilo. Ni kwa kuinua nafasi ya dini na taasisi zake zitumiwe uwezo zilizo nao au ushawishi miongoni mwa wakuu wa nchi, na hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. John Magufuli ambaye ni muumini katika Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, chini ya Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo. Huyu aseme, "nataka, takasika...."

Anachokisema Maalim Seif katika barua hiyo ni kuwa Chama cha Wananchi CUF kimekuwa kikishinda uchaguzi mara zote tangu 1995 lakini matokeo yanabadilishwa, ili CCM iendelee kukaa madarakani. Tofauti ni kuwa safari hii

Maalim amegonga msumari kichwani

Papa Francis akitoa agizo kwa JPM…'Sanamu za Babeli’ zaporomoka Z’bar

Na Anil KijaMAALIM Seif Shariff Hamad

MKUU wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis

Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. John Magufuli

kulikuwa na waangalizi wa kimataifa ambao wamethibitisha kila hatua ya uchaguzi huo kwenda sawa, watu kupiga kura na kura hizo kuhesabiwa, na mtitiriko wa kura kutoka vituoni na majumuisho ya majimbo unaonyesha bayana kuwa CUF imeshinda. Ila kama ilivyo kawaida yao, CCM hawataki. Ndiyo hoja ya Maalim Seif Shariff Hamad kwa Papa Francis.

Kwa maana hiyo Maalim Seif kama Katibu Mkuu wa CUF na mgombea urais ambaye haki zake zinaporwa kwa mara nyingine tena, anamwangukia Papa Francis awatumie watu wake hapa nchini, asiporwe tena ‘Urais’ wake safari hii. Hasa ni mwakilishi wa Papa (aliye na hadhi ya Balozi) na utawala wa Kanisa Katoliki, kwamba asasi hizo zikitilia maanani haki katika suala hilo, litatatuliwa. Ila wakiendelea kujificha katika protokali ya kisheria na udanganyifu wa mazungumzo, halitamalizika.

Licha ya kuwa wasomi na wachambuzi ngazi tofauti hawaoni mantiki ya kiongozi wa kisiasa Muislamu kumshitaki kiongozi mwingine wa kisiasa

pia Muislamu kwa Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, barua hiyo ni kielelezo cha yale ambayo wengi kati ya wanaharakati wa Kiislamu wamesisitiza kwa miaka mingi. Wana ainisha nguvu ya kisiasa ya Kanisa Katoliki katika mfumo uliopo, ambako kitakwimu ni rahisi kuelewa, kwani waumini wa Kanisa Katoliki ni takriban robo tatu ya Wakristo kwa jumla, wakati Bunge la Jamhuri (nje ya wabunge toka Zanzibar) takriban robo tatu jadi ni Wakristo.

Ushawishi wa Kanisa Katoliki hasa ni pale kunakuwa na jambo linalogusa Kanisa moja kwa moja na wafikie tamati fulani kwa kauli moja, kuwa suala kama hilo litarekebishwa na utawala ulioko madarakani, bila kujali dini ya aliyeko madarakani, kuelekea kile kinachotakiwa na Kanisa. Ila kwa masuala mengine ambayo hayalijumuishi Kanisa kwa dhati, sauti au ushawishi ambao unaweza ukatoka huku au kule katika Kanisa hilo au mengine, unaweza usiwe na nguvu za kutosha miongoni mwa watawala. Ndicho anacholenga Maalim.

Anamtahadharisha Papa Francis kuwa katika yale ambayo Kanisa Katoliki linatilia maanani na kuweka msimamo wa pamoja, suala lirekebishwe kwa matakwa yake, nje ya mwelekeo ambao serikali itakuwa imechukua hadi wakati huo, mojawapo liwe ni kutanguliza haki katika uchaguzi wa Rais Zanzibar. Kwa lugha ya haraka, Maaskofu Katoliki wakifikia msimamo wa pamoja kuwa ni budi haki itendeke kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais Zanzibar, hilo litafanyika. Wasipofikia msimamo huo, basi tusije kulaumiana.

Maalim Seif kwa barua hiyo amelifikisha suala hilo liwe ni kati ya taasisi za kidini, suala ambalo kwa wachambuzi wa Katiba na siasa ni kosa au halina mantiki, kwani Kanisa halihusiki katika kufanya maamuzi ya suala hilo. Ila katika hali halisi Maalim Seif hajakosea. Amegonga msumari kichwani. Kuwa endapo Kanisa litatilia maanani suala hilo, lisikilize kilio cha CUF na waangalizi wote wa uchaguzi ndani na nje ya nchi, basi litatatuliwa. Endapo Kanisa Katoliki, huku limepata barua hii na kuitafakari, litapuuzia suala hilo, basi litakuwa limeridhia matokeo yoyote yanayotokana nayo, ikiwa ni pamoja na kubebeshwa zigo la kutotendwa haki Visiwani Zanzibar, ipatishwe taabu kwa dhulma hii. Kuwa limekiuka wajibu wake wa kitaasisi inaoutambua fika.

Ukiangalia kwa mantiki ya maandiko ya Kikristo, barua

DK. Ali Mohamed Shein.

Inaendelea Uk. 14

10 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016

Makala

HIVI sasa zipo ripoti nyingi zinaibuka, zikifichua jinsi uwongo ulivyotumika kuchochea chuki dhidi ya kiongozi wa Libya Muamar Gaddafi na ‘kuhalalisha’ kupigwa, kupinduliwa na kuuliwa kwake. Nakumbuka siku moja tulikuwa tukijadili habari za Libya na rafiki yangu mmoja. Jamaa yangu yule akisema kuwa Gaddafi hana aqida sahihi. Hatawali kwa Kitabu na Sunna, kwa hiyo ni sahihi kabisa kupigwa na NATO. Akisema hayo, wakati huo, taarifa za vyombo vya habari zinafahamisha kuwa makundi ya Salafi katika Libya yameshika silaha wakisaidiwa na Marekani na NATO.

Nilichomwambia jamaa yangu yule ni kuwa Gaddafi anaweza kuwa mbaya, lakini haiwezi kuwa Marekani na NATO wakawa watu wema wa kuwasaidia Salafi wamwondoe Gaddafi ili wapate kusimamisha Kitabu na Sunna. Jamaa yangu yule hakunielewa kabisa. Hata Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice, alipotoa taarifa za uwongo na propaganda katika Baraza la Umoja wa Mataifa (UN) kwamba Gaddafi anawapa wanajeshi wake Viagra na kuwaamuru kusambaa mitaani kubaka wanawake, jamaa yangu yule aliona inawezekana hayo kufanyika kwa vile alishamuhukumu Gaddafi kuwa hana aqida sahihi. (Tazama: Gaddafi 'supplies troops with Viagra to encourage mass rape', claims diplomat).

Yakafanyika yaliyofanyika. Labda sasa ndio anaweza kuona kuwa kumbe Salaf wa Libya walitumika tu kama ‘foot soldiers’ wa ‘proxy war’ ya mabeberu wa NATO. NATO wapo angani na midege yao ya kivita, Salaf wapo ardhini na silaha walizomiminiwa na Marekani. Gaddafi akawa hana pa kukimbilia. Mchezo umemalizika, Kitabu na Sunna hakijasimama Libya.

Katika jumla ya habari zilizotikisa vyombo vya habari mwaka jana,

Na Omar Msangi

KIONGOZI wa zamani wa Libya Muamar Gaddafi.

BALOZI wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice.ni pamoja na ile ya kukamatwa mabinti watatu waliodaiwa kuwa walikuwa njiani kwenda Somalia, kujiunga na Al-Shabaab. Mabinti hao walitajwa kuwa ni Ummul-Khayr Sadri Abdullah, Maryam Said Aboud na Khadija Abubakar Abdulkadir. Mimi ni mmoja wa watu ambao waliguswa sana na kishindo cha habari zile kwa sababu Sadri, baba wa Ummul Khayr, ni rafiki yangu ambaye tuliwahi kuwa pamoja katika uongozi wa Umoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (MSAUD) miaka ya 1980s.

Kwa bahati nakijua Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika Khartoum alichokuwa akisoma Ummul Khayr na dada

yake Sumaiyyah na niliwahi kufanya kozi fupi ya mwezi mmoja katika chuo hicho wakati huo kikiwa Markaz (Islamic Centre). Nilichokuwa na uhakika ni kuwa haiwezi yaliyomkuta Ummul Khayr yakatokana na mtaala wa chuo hicho, bali ni kama ilivyotokea kwa ‘Mberesero’ wa Mazengo, Dodoma. Na kwangu mimi lililokuwa wazi ni kuwa mabinti wale walikuwa ‘trapped’, walikuwa wahanga wa mchezo wa ‘entrapment’. Hata hivyo nikiri kuwa sikuwa nimelifuatilia kwa undani zaidi na kujua kilichokuwa kikiendelea mpaka kurahisisha hizo ‘entrapment’ katika chuo hicho.

Ilikuwa ni mapema

mwezi huu ambapo nilikutana na jina la taasisi moja ambayo taarifa zake zilinistua kidogo. Global Service High Court (GSHC) au Khartoum Salafi, ndio jina la taasisi yenyewe. Nilikutana na jina hili katika mtandao nikiwa katika jitihada za kutafiti juu ya huu uhusiano unaojitokeza baina ya ‘Salafi’ na harakati za mabeberu wanaozivamia na kuzivuruga nchi za Kiislamu. Taarifa za GSHC (Khartoum Salaf) katika ukurasa wao mtandaoni, hawaonyeshi kuwa tofauti na Salafi wengine. Mtizamo ni ule ule, kuwaona wengine wote hawana Aqida sahihi na kwa hiyo wanajipa jukumu la kufundisha ‘Aqida’ maana wanasema kuwa hata Sheikh Nassor Bachu hakufundisha Aqida. Alichofundisha Sheikh Nassor ni Fiqhi ya Jeneza (fiqh tu). Sasa ‘Khartoum Salaf’ inakuja kuendeleza harakati za Sheikh Nassor Bachu kwa kufundisha Aqidah. Mtu unaweza kujiuliza, kama Sheikh Nassor hajafundisha Aqida, kiasi cha mtu kusema kuwa Sheikh Nassor kajishughulisha tu na ‘fiqhi ya jeneza’, hiyo Aqida yenyewe maana yake nini hasa?

Ukisikiliza “over view” ya GSHC hadi mwisho, kinachoelezwa ni kushadidia mifarakano miongoni mwa Waislamu kwa kupandikiza msimamo wa usahihi wa Salafi na wengine wakidaiwa kuwa na aqida mbovu. Wanaeleza walivyowagaragaza walimu waliokuja na ‘aqida mbovu’ kutoka Muslim University of Morogoro (MUM) kwa masomo ya juu (Masters na PhD). Kwa kutokufuata manhaji ya Salafi, walimu hao kutoka MUM walionekana kama watu walio na imani potofu juu ya dini na kwamba ulipofanyika mdahalo walipigwa mwereka wakajikuta hawana hoja. PhD na Masters zao hazikuwasadia mbele ya mabinti wa kisalafi walioiva.

Lakini kilichonitisha zaidi ni mambo matatu.

Inaendelea Uk. 11

Khartoum SalafiSawa ‘Mzee Punch’ wa UDSM Alihusika kadhia ya Bint Sadr?Aeleza alivyo wagaragaza MUM!

11 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 201611 AN-NUURMakala

Inatoka Uk. 10Kwanza kutajwa mtoto wa Sadri kuwa ni katika ‘wanafunzi’ wa ‘Sheikh wa Khartoum Salaf’. Sheikh wa ‘Khartoum Salaf’ anamtaja Bint Sadr kuwa alikuwa katika wanafunzi wake mahiri walioiva katika Manhaj Salaf na waliokuwa na ujasiri wa kupambana kwa hoja na watu wasio katika Manhaj hiyo. Anatamba akisema kuwa japo walikuwa wanafunzi wa ‘Medicine’ (wakisomea Shahada ya Udakitari), lakini aliwapika kisalafi wakaiva.

“Hawa ni wanafunzi wanaosoma medicine. tunawapa ‘self confidence’, haikutokezapo miaka yote tupo hapa kwamba hata wale waliosoma thanawiyati na wanajiita Masalafi, hakuna siku waliyowahi kuradi. Lakini jamaa wakakiona siku hiyo kilichomtoa kanga manyoya. Watoto wa kike hawakukubali …maana aliyekuwa mbele yao kabisa, ni Baratai Sadri. Baratai Sadri natumai wapo mwaka wa pili. Vijana walisimama hawakuchelea kuwa huyu ana PhD huyu alikuwa mwalimu, wakaradi shubuhat. Jamaa walishangaa, walifikiri kwamba wakijadiliana na hawa watoto wa kike mambo yataenda sawa, yakakwama.”

Anasimulia Sheikh wa ‘Khartoum Salaf’ aliyejitaja kwa jina la Mkongwe: Al hidhri Youssouph Serve alivyowaivisha watoto wa kike katika msimamo wa Kisalafi na kuwajenga kujiamini kutetea msimamo huo. Katika kufuatilia habari hizi, nilipata kufahamu kuwa mabinti wa rafiki yangu Sadri ni Ummul Khaiyr ni Summaiyah. Sasa huyu Baratai (yaweza nikawa sikumnukuu vizuri msemaji katika kanda ya video) Sadri, yaweza kuwa ni kufanana kwa majina ya baba zao. Hata hivyo, muhimu hapa ni uwepo wa ‘Khartoum Salaf’ na msimamo inaowajengea wanafunzi. Muhimu zaidi ni kuwepo kwake

Kutoka kushoto: Bi Ummukhayr Sadri Abdulla, Bi Maryam Said Aboud na Bi Khadija Abubakar Abdulkadir wakiwa kortini Mombasa Machi 30, 2015.

Zanzibar kwa sasa. Na inavyoonyesha ‘Khartoum Salaf’ imezamia katika kukamata mabinti na akina mama. Maana hata ilipoingia Zanzibar, imeanza na darsa la akina mama, dauru kwa dauru. Hatua iliyofuata ni kuwaita akina baba kwa hoja kuwa haiwezekani Sheikh kusomesha wake za watu bila kujuana na waume zao. Nini kitafuata hatujui. Lakini maadhali akina baba hao wamejisajili katika fomu maalum walizopewa kupitia kwa wake zao, huenda baada ya muda nao wakasajiliwa katika mtandao wa GSHC kwamba ni memba wa ‘Khartoum Salafi’.

Tunajua yaliyomkuta mmoja wa watoto wa Sadr Abdullah. Ukijaaliya kuwa naye alikuwa mmoja wa waliokuwa wakihudhuria darsa za ‘Khartoum Salafi’, ambapo anajengwa kuwa na msimamo kuwa wengine wote hawana aqida sahihi, picha inayokuja hapa ni kama imesafishwa njia kwa walio na program za ‘entrapment’ na false flag terror attacks’ kumnasa kirahisi.

Hapa sisemi kuwa ‘Khartoum Salaf’ inachochea watu kujiunga na Al Shabaab au IS. La hasha. Hoja hapa ni kuwa, ukimpa mtu somo na

msimamo kuwa ‘Salafi pekee’ ndio wenye aqida sahihi, ndio Waislamu (na kwa maana hiyo wengine wote ni watu wa motoni), mafunzo na msimamo huo unamfanya iwe rahisi kuchotwa. Ni kiasi cha kumwambia tu kuwa wote wanaokuzunguka ni makafiri, hawana Aqida, wenye aqida sahihi pekee ni Al-Shabaab/IS na ukimuonyesha kuwa kuna uwezekano wa kwenda kuishi na wenzake wenye aqida sahihi Mogadishu, ushampata. Nadhani hiki ndio chambo na mtego uliotumika ‘kuwanasa kwa hadaa’ mabinti wale ili kuendeleza (hoax)- ‘mzaha’ wa kitisho cha Al Shabaab.

Jambo la pili lililonivuta kuitafiti zaidi ‘Khartoum Salaf’, ni picha potofu inayojengwa ili kuipa ‘credibility’ GSHC. Katika ukurasa wa mtandao wake, inaoneshwa kana kwamba ‘Khartoum Salaf’ ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika, Khartoum. Maana katika ukurasa huo inatajwa GSHC, kisha yanakuja maandishi International University of Africa, na kuandikwa program zinazoendeshwa chuoni hapo. Ukija kusikiliza maelezo nini ‘Khartoum Salaf’ (Khartoum Salaf Over View) kama

yalivyorekodiwa na kiongozi wake, Mkongwe: Al hidhri Youssouph Serve, ndio unagundua kuwa kumbe ni ‘Masalafi’ wa Kitanzania wanaosoma chuoni hapo na program zao ni nje ya program za chuo. Na wenyewe wanasisitiza kuwa wanawafundisha Aqida wanafunzi wanaokuja kusoma hapo kwa sababu chuo hakifundishi Aqida (sahihi).

Jambo la tatu lililonistua ni kuona kuwa GSHC imetangaza katika mtandao wake kuwa imepata mtaji wa kuanzisha harakati zake Zanzibar kupitia kundi la akina mama walio wakusanya na kuwapa mafunzo mwezi Septemba mwaka jana 2015. Na kwamba darsa zinaendelea awamu kwa awamu.

Mwaka jana nilipata kuelezwa kisa cha kijana mmoja wa jijini Mwanza ambaye katika mwezi wa Ramadhani alikuwa anajifungia chumbani na kufuturu peke yake. Alikuwa akisema kuwa mama yake na wadogo zake hawana Aqida sahihi. Ni makafiri hawezi kufuturu na makafiri. Wapi kayapata hayo? Alikuwa mmoja wa wafuasi wa Masheikh wa ‘Manhaj Salaf’ waliopo Mwanza.

Kwa waliosoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mpaka mwishoni mwa miaka ya 1990s au mwanzoni mwa 2000s wanakumbuka habari za ‘Mzee Punch’. Kwa vituko alivyokuwa akifanya kila mwaka, mwenyewe akidai kuwaadabisha watu waovu, alipewa cheo kwamba yeye ni mwanafunzi asiyemaliza masomo. “Mzee Punch Never Graduate.” Kwamba kila mwaka yupo akipokea wanafunzi wapya na kwenda nao mpaka wanamaliza maisha yao ya chuo. Anabaki.

Sasa inavyoonekana “Khartoum Salaf” (GSHC) ni ‘Mzee Punch’ aliyejichimbia katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika, Khartoum, Sudan akiwasubiri vijana kutoka nchi za Afrika Mashariki, wanaozumguza Kiswahili kuwatia katika utumishi wa GSHC-Khartoum Salaf.

Khartoum Salafi

12 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 201612 Makala

Uzanzibari ni nini hasa?Tujifunze yaliyowakuta WanubiKujitenga imekuwa nuksi, balaa

NILIWAHI kuandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari “Je! Mwafirika ni kwa kuzaliwa Afrika au ni kuwa mtu Mweusi?” Kwa leo nitazungumzia kichwa cha habari hapo juu. Kwanza kabisa, niseme kuwa, hapa duniani kuna njia mbili tu, au miongozo miwili tu ya kumuongoza mwanadamu katika maisha yake. Kwanza ni mwongozo wa Mwenyezi Mungu (swt) na pili ni sheria za shetani ambazo ziko kinyume na Sheria za Mwenyezi Mungu s.w. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akatutahadharisha hivi:

“Enyi mlioamini msifuate nyayo za shetani; na atakayefuata nyayo za shetani (atapotea) kwani yeye huamrisha mambo ya aibu na maovu.” (Qur’an 24:21).

“Ninyi ni wa baba yenu , Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.” (Biblia-Yohana 8;44.)

Kwa bahati nzuri Watanzania tuna dini kuu mbili; ikimaanisha kuwa asilimia nyingi ya Watanzania ni wana dini. Na viongozi wetu wa dini wana pigia debe katika kampeini za uchaguzi, kauli mbiu yao ni kuwa wachaguliwe viongozi wacha Mungu; na wagombea wanajinadi katika majukwaa ya kampeni kuwa wao ni wacha Mungu; sikwambii kitu kuwa wa Zanzibari zaidi ya 99% ni Waislamu na viongozi wao. Na kitabu chao cha dini yao ni kimoja, Qur’an.

Pamoja na viongozi wa serikali ya Tanzania bara wanaoongozwa na vitabu hivyo viwili, Qur’an na Biblia; waliojinadi kuwa ni wacha Mungu, tuwaulize kwa haya yanayoendelea Zanzibar na hata huku bara, wanaongoza kwa muongozo upi kati ya hiyo miwili niliyoitaja hapo juu?

Viongozi wetu wa dini na wa serikali wamekua wakipokea sera za nchi za Magharibi, katika kuongozea nchi zetu; kiasi kwamba, huoni tofauti katika baadhi ya mambo ambayo wakoloni waliyafanya na wanayoendelea kufanya.

Chukulia mfano wa karibu, wa nchi ya Sudani; nchi za Ulaya na Marekeni na Israeli, zimepiga propoganda ya udini na ukabila, kuwa Sudani inatawaliwa na Waarabu wa Kaskazini ambao ni Waislamu. Wanawanyanyasa Waafrika Wakristo wa Kusini; Wana waua na wanachukua mali ya mafuta ya Sudani Kusini na kuwaacha Wasudani Kusini masikini.

Viongozi wa nchi zetu za Afrika, wamemezeshwa kasumba hiyo hadi kukaa vikao vya A.U. Na kuigawa Sudani. Yaliyo na yanayotokea Sudani Kusini inayotawaliwa na Wakristo watu Weusi-Wadubi, tumeyaona! Hata hivyo haionyeshi kuwa viongozi wetu wamejifunza kitu.

Tukija Zanziba, kasumba ni ileile, ya Waarabu na Waafirika. Ndiyo maana katika makala zangu niliata kuuliza “Mwafrika ni mtu aliyezaliwa Afrika au ni mtu Mweusi tu? Na leo pengine niulize, Mzanzibari ni mzawa au ni mtu Mweusi tu?

Kwa elimu iliyopo hapa duniani siku hizi, na elimu waliyonayo wanadamu siku hizi, hasa elimu ya Jiografia ya hii dunia kwa jumla; na elimu ya historia ya wakaazi wa Bara la Afrika; na uhusiano na nchi za Arabuni na za Asia, ni Aibu tena aibu sana, kwa Mtanzania Mweusi kumwona Mtanzania mwenye asili ya Kiarabu au Kiasia kuwa si mwananchi, wakati amezaliwa hapa na baba, babu n.k. walizaliwa hapa.

Afrika haina mpaka na Arabuni na Asia uliotenganishwa na bahari. Mfereji wa Suezi, umefanywa kuchimbwa, ili kuunganisha bahari ya Sham na Mediterranian. Na majina haya ya mabara yamewekwa na mabeberu, ambayo sasa yanatufarakanisha.

Jina Zanzibar lilijulikana miaka mingi kabla ya jina la Tanganyika na jina hilo si la kibantu ni la lugha ya Kiarabu; na hatulifuti na

hatutalifuta katika historia, ila kuna dalili ya kutaka kuwafanya watoto wetu waamini kuwa Zanzibar ni ya watu Weusi tu.

Lakini la msingi ni kuwa Tanganyika kabla ya mwaka 1885 ilijulikana kama ‘Mrima’ wakoloni walipo igawa Afrika mwaka wa1884-85, ndio walio toa jina la Tanganyika, baada ya wale wapelelezi wao waliowatuma kutafuta makoloni, wakijiita Wamissionari na wavumbuzi (majasusi) waliporudisha mrejesho, ndipo kikakaa kikao hicho nchini Berlin Ujerumani Magharibi, wakaigawa

Afrika. Ndiyo maana, watu wanaoishi mipakani mwa kila nchi, ni wa asili ya pande mbili Wamakonde wa Mtwara-Msumbiji, Wanyasa wa Malawi-Tanganyika Wajaluo wa Kenya- Tanganyika, Wamasai wa Kenya-Tanganyika, Wamanyema wa Kongo-Tanganyika-Warundi wa Rwanda-Tanganyika n.k.

Tuwasihi viongozi wetu wa nchi na wa dini, kuwa, wasikubali kutumikia agenda zinazoongozwa na sera za Ibilisi, za kuwabagua watu na kuwagawa matabaka. Waiangalie Sudani ya Kusini na propoganda za Uarabu na Uafrika, Ukristo na Uislamu waliovishwa na kujitenga na wenzao wa Kaskazini na maafa yanayowakuta hadi sasa. Mwenyezi Mungu atuepushe na wafitini wana wa Ibilisi.

(Khatibu Juma Mziray, 0757 013 344.)

Mtoto Hawa/Machwi Kakima mwenye umri wa miaka 13 (pichani kulia)amepotea n y u m b a n i k wa o t a n g u Novemba 30, 2015.

Alikuwa akiishi na mama yake mkubwa Mivinjeni jijini Dar es Salaam.

Yeyote anayejua aliko au kuwa na taarifa zake au kumpata tunaomba apeleke kituo chochote cha Polisi au apige simu namba 0754 025142, 0654 333595, 0712 953871.

Mtoto amepotea

BAADHI ya Mashekh Na Walimu wa chuo cha Kiislam cha Markaz Chang`ombe cha Jijini Dar es salaam, wakiwa katika kongamano maalum la kumbukumbu ya Mazazi ya Mtume (S.A.W) lililoandaliwa na kufanyika katika ukumbi wa chuo hicho hivi karibuni.

13 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016Makala

Tujiimarishe kiuchumiKWA mujibu wa fikra na

mafundisho ya Uislamu, itikadi na imani za

watu ndizo ambazo hutoa muongozo wa namna miamala mbali mbali ya kiuchumi na shughuli zingine za kimaisha zinavyoweza kuendeshwa. Kwa msingi huo, uchumi wa Kiislamu ni lazima uwe na mafungamano ya moja kwa moja na masuala ya kimaadili na kiitikadi. Na ndivyo ilivyo katika uchumi wa Kiislamu kwamba mafungamano yaliyopo ni makubwa kiasi kwamba ni vigumu mno ama ni muhali wakati mwingine kuweza kutenganisha baina ya viwili hivyo. Na eneo hili ndilo linaloleta tofauti kati ya uchumi wa Kiislamu na wa kitwaaghuti. Kutenganisha baina ya viwili hivyo, ni kutengeneza mazingira ambayo yanaweza kupelekea upatikanaji wa chumo lisilokuwa la halali.

Utoaji wa zakah, kwa mfano, una munasaba wa moja kwa moja na masuala ya kiuchumi, lakini kwa hakika vinahesabiwa kuwa ni sehemu ya masuala ya kiibada, na sharti la kukubaliwa mambo hayo mbele ya Mwenyezi Mungu, ni mwanadamu kutia nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Halikadhalika, ibada ya hija haiwezi kutekelezwa, ila mtu awe na uwezo wa mali (fedha) ili kwayo imuwezeshe kulipa nauli sanjari na gharama zingine muhimu. Usimamishaji wa nguzo hizi mbili, zakah na hija una mafungamano ya moja kwa moja na fedha (mali) ambayo kwa hakika hutegemea uchumi.

Hata hivyo, uchumi haupatikani tu, kwa mtu kufanya adhikar kwa wingi, kuleta tasbih, tahlili na mfano wa hayo, bali kwa kufanya kazi, tena kwa bidii. Lakini kama tulivyotangulia kusema kwamba, miiko ya kimaadili haiwezi kuepukika kwa kuwa ni jambo la kiitikadi na kiimani zaidi. Hivyo basi, kazi inayokusudiwa hapa ni ile shughuli yoyote ya halali inayoweza kumuingizia mtu kipato.

Dini ya Uislamu inatambua vyema kazi na bidii inayofanywa na mja kwa ajili ya kuboresha maisha na kukidhi mahitaji yake yeye na familia yake, na kwamba yote haya yakifanywa kwa ajili ya Allah (swt) huhesabika kuwa ni ibada. Kazi na harakati za kutafuta kipato mbali na kuwa sababu ya ustawi na maendeleo ya maisha ya kidunia iwapo itafanyika

kwa nia ya kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu na kufanywa kwa ajili ya malengo aali zaidi, huwa sababu ya kupewa ujira na thawabu huko Akhera. Kwa sababu hiyo Mtume Muhammad (saw) amesema: "Dunia ni shamba la Akhera" kwa maana kwamba, dunia na vilivyomo vinaweza kutayarisha uwanja mzuri wa ustawi wa kiroho wa mwanadamu na kuwa sababu ya kupata makazi mazuri huko Akhera kwa sharti kwamba vitu hivyo vitumiwe kwa njia sahihi. Njia inayozingatia mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kwa mantiki hiyo basi, mfumo wa uchumi wa Kiislamu unafanya bidii za kuimarisha zaidi thamani za kidini na kimaadili katika nafsi ya mwanadamu. Kwa hakika suala hilo ni msingi muhimu na hivyo basi malengo makuu katika mfumo wa uchumi wa Uislamu ikiwa ni pamoja na Kujitegemea Kiuchumi, Uadilifu, Hali Bora ya Maisha ya Jamii, Ustawi wa Kiuchumi na kadhalika vinaarifishwa kwa mujibu wa malengo hayo.

Katika mafundisho ya Uislamu, akhlaki na maadili mema na thamani za kiroho hutawala mienendo ya kiuchumi ya mwanadamu ili kuzuia dhulma, kuchupa mipaka au kukanyaga haki za watu wengine. Harakati zote za kiuchumi za Mwislamu katika mtazamo huo hufanyika kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kutekeleza maamrisho na makatazo yake. Mwanadamu kama huyo hufuatilia faida na maslahi ya kiuchumi yanayooana tu na imani na itikadi zake. Mwanadamu kama huyu hufanya jitihada kadiri ya uwezo wake kuhakikisha kuwa wanadamu wenzake wanafaidika pia na neema za Mwenyezi Mungu.

Mwanadamu anayefaa

katika mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu ni yule anayetambua kuwa, mali na utajiri ni amana aliyopewa na Mwenyezi Mungu ambayo analazimika kuitumia vyema kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya kimaada na kiroho ya jamii. Kwa msingi huo Mwislamu wa kweli hujitambua kuwa anawajibika kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuboresha na kuijenga dunia. Mwenyezi Mungu (swt), anasema katika aya ya 61 ya Suratu Hud kwamba: “Ni Yeye ndiye aliyekuumbeni kutokana na ardhi na akakupeni jukumu la kuijenga..”.

Ikiwa ukweli ndio huo, sisi Waislamu wa Tanzania tuna haja ya kuunganisha nguvu zetu kwa lengo moja tu, ambalo ni uchumi ili kuwezesha kufikiwa kwa malengo mengine ambayo, aghalabu uchumi ndiyo nyenzo pekee ya kuyafanya kwa sahali na aali zaidi. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyekuwa Rais wa awamu ya kwanza Tanzania, alipata kusema maneno machache lakini kimsingi yalilenga dhana hii ya uchumi. Akihutubia Taifa kwa mara ya kwanza akiwa Waziri Mkuu wa Kwanza mnamo mwaka 1961, alisema:

“Mara nyingi sana nimesema nanyi juu ya umaskini, ujinga na maradhi, lakini kwa kweli adui yetu mkubwa ni umasikini. Tukiweza kumshinda adui huyu, tutakuwa tumeweza kupata silaha itakayotuwezesha kuushinda ujinga na maradhi”.

Katika hotuba hii ni wazi kuwa, kulikuwa na changamoto ya uchumi (umasikini), elimu (ujinga) na afya (maradhi). Hivyo, kwa maoni ya Mwalimu ni kwamba, ikiwa kweli unataka kupambana na ujinga na maradhi basi uchumi ndio silaha pekee itakayorahisisha kushinda vita hii. Maneno haya yana ukweli na yafaa kuyafanyia kazi bila kujali ama kuangalia msemaji.

Tutafanikiwa katika hili kama tutaweka pembeni tofauti zetu

na kutengeneza nia, mikakati, program na miradi madhubuti ya kujenga na kwuaimarisha Waislamu kiuchumi.

Kimsingi hatuna sababu ya kuendelea kulalamikia serikali yetu, kulalamikia taasisi zetu za dini ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa vijana wetu kupata elimu, bali tuingie kwenye utendaji na kufanya yote yaliyo ndani ya uwezo wetu kisha Allah atatufanyia tawfiiq katika sehemu iliyobakia. Na kwa kuwa msikiti ni taasisi inayojitegemea kama zilivyo taasisi zingine, hebu tuiwekee mazingira sadifu na nyumbufu ili iweze kukidhi haja za Waislam na jamii kwa ujumla.

Allah Mtukufu katika kitabu chake kitukufu, Qur-an anatutaka tushikamane kwenye kamba yake wala tusifarikiane. [03:103]. Mwenyezi Mungu anatutaka tushikamaneni na Dini yake, wala tusifanye jambo litakaloleta mfarakano baina yetu. Hakika katika kushikamana huku kuna faida nyingi mno ambazo hawanufaiki nazo isipokuwa wenye kushikamana. Nyanja zote za kimaisha kama Uchumi, Siasa, Elimu, Afya na mengineyo yanahitaji msukumo unaotokana na mshikamano thabiti uliopo baina ya wanajamii.

Kupitia mshikamano huibuliwa fikra mbali mbali, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi juu ya wengine. Ni kwa msingi huu ndio unakuta wengine madereva, walimu, madaktari, wakulima na kadhalika. Yote haya hayakuja kwa bahati mbaya. Lakini pamoja na uwepo wa fani tofauti, jambo la msingi na la pekee ambalo litaweza kuleta ustawi tarjali ni mshikamano. Makundi haya yanaishi katika hali ya kutegemeana kwa kiwango kikubwa kabisa.

Pamoja na hayo, changamoto kubwa iliyopo mbele yetu ni umasikini, jambo ambalo endapo hatutafanya jitihada za makusudi kuitatua inaweza kuleta farka baina yetu. Tujenge, tuimarishe na tudumishe mshikamano na tuutumie mshikamano huo katika kujiimarisha kiuchumi. Hata nguzo ya tatu ya Uislamu ambayo ni Zakah, nayo inatulazimu kujiimarisha kiuchumi, vinginevyo tutashindwa kuitekeleza. Hatuna sababu ya kushindwa kutekeleza nguzo hii wakati Mwenyezi Mungu ametupa elimu na wataalamu wa fani mbali mbali tunao.

Wabillah Tawfiiq!!(Juma Jumanne ---- KATESH,

MANYARA.0659 - 789468)

14 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016

MAKALA/MASHAIRI

Inatoka Uk. 9

Maalim amegonga msumari kichwaniya Maalim Seif kwa Papa Francis inaingia akilini, kwani katika Kitabu cha Nabii Isaya sura ya 8 na 9, yako maelezo kuhusiana na mfalme wa Shamu aliyekuwa akimbeza Mungu wa Israeli, akijivunia sanamu zake za Babeli kuwa Mungu wa Ibrahim hana uwezo wa kuiokosoa Israeli katika mikono yake. Nabii akatumwa kwa mfalme wa Yuda wakati huo, akaandika bango, "Mahel Shalal Hash Bazi,' (mama yangu na baba yangu) kwa maana ya mtoto aliyezaliwa leo, kabla hajaweza kusema 'mama yangu na baba yangu' hazina, nyara zote za ufalme wa Shamu zitakuwa mbele ya Mfalme wa Ashuru. Shamu ikapigwa kabla ya kuipigia Yuda. Anayeibeza haki, na ndiyo amri kuu mbele za Mungu, anahitaji bango.

Isitoshe, sura inayofuata (ya tisa) nabii anaelekezwa kumwelezea mfalme kuhusu tishio la mfalme wa Shamu. Anaambiwa kuwa kichwa cha Shamu ni mfalme huyo ambaye andiko linamwita 'mwana wa Remalia,' kuwa akipigwa huyo, nguvu yote ya Shamu inayeyuka. Rais Dk. John Magufuli anaweza pia 'kupigwa' na Kanisa kuwa atende haki katika suala hilo, na kwa vile yeye ni muumini huko, hataweza kupuuza tamko la kina, dhamira halisi la maaskofu kwa hitaji hilo la kutenda haki. Ni mantiki, mazingira halisi uthabiti wa dola.

Kwa maana hiyo pia, endapo Kanisa litakataa kufanya hivyo, lisimwingilie Dk. Magufuli katika kazi zake, litakuwa

kwa hakika limeridhia uharibifu. Unaweza ukasema ni jambo ambalo Mungu ameliweka mbele ya Kanisa, kuwa litambue wajibu wake wa kusisitiza haki katika suala hilo, au kusiwe na haki ambayo Kanisa linaitegemea, ya kufanya shughuli zake bila ya bughudha kutoka upande huu au ule, uwe ni ukinzani wa kidini, kidhehebu au kisiasa. Ni mtego wa Kanisa Katoliki kutambua lina wajibu hapo, au liamue kupuuza.

Kwa njia hiyo unaweza kuona kuwa licha ya kwamba barua ya Maalim Seif kwa Papa Francis inalenga ushawishi wa jumla wa Kanisa Katoliki na nguvu yake hapa nchini, hali hiyo si ya lazima. Ni uhalisia wa kisiasa kuwa matokeo hayatangazwi kwa sababu serikali ya Muungano inawakingia kifua kwa nguvu zote watawala wa Zanzibar, hivyo kuna mantiki pana zaidi. Hata kama Rais Magufuli angekuwa wa dhehebu la Sabato (kuacha hata Pentekoste) ambalo halina ushawishi wa kitaasisi na kidola kama Kanisa Katoliki, bado Maalim Seif angeweza kumwandikia kiongozi wake mkuu kwa mantiki hiyo.

Suala hapa ni kielelezo hicho cha 'mwana wa Remalia,' kuwa bila kujali dhehebu lake na ushawishi wake hapa nchini, kiongozi mkuu wa dini au dhehebu, akiungana na watu wake katika nchi husika, anakuwa na uwezo wa kutosha

kumshawishi mkuu huyo wa nchi ambaye ni muumini wa dhehebu hilo, kutenda haki katika jambo husika. Hivyo kinachotofautisha mazingira ya barua hiyo ni kuwa kuna jadi ya kiitikadi hapa nchini ambayo inatambua kuwa Kanisa Katoliki limekuwa na nafasi maalum kuamua nini kifanyike katika suala gani, ambayo dini nyingine na madhehebu mengine hawana nafasi hiyo. Unaweza kuainisha kimsingi kuwa Maalim Seif aliegemea hapo. Lakini mantiki pana zaidi ni kuwa hata ingekuwa ni dhehebu dogo, inatosha kuwa ni muumini wao, nao wametoa kauli isiyo na utata tena kwa pamoja kwa suala husika, ili atilie maanani walichosema atende inavyopasa kwa hilo. Akikataa kutii, ule usemi utafanya kazi, kuwa "asiyesikia la mkuu, mbele huvunjika guu," na taasisi vile vile, ikipuuza wajibu wake huo itavunjika guu.

MWENYEKITI wa ZEC, Mhe. Jecha Salum Jecha

Kumekucha kumekucha, washairi amkeni, Kumekucha kumekucha, wa Bara na Visiwani,Kumekucha kumekucha, mijini na vijijini,Kumekucha kumekucha, washairi amkeni!

Kumekucha kumekucha, 'shawika jimbi nyikani,Kumekucha kumekucha, naumuni zindukeni,Kumekucha kumekucha, nyenzo zenu chukueni,Kumekucha kumekucha, washairi amkeni!

Kumekucha kumekucha, pamoja njia shikeni,Kumekucha kumekucha, kondeni twakungojeni,Kumekucha kumekucha, si kwingine swahifani,Kumekucha kumekucha, washairi amkeni!

Kumekucha kumekucha, NASAHA twatumaini,Kumekucha kumekucha, za Sunnah na Qur-ani,Kumekucha kumekucha, tupeni kama zamani,Kumekucha kumekucha, washairi amkeni!

Kumekucha kumekucha, twazingoja gazetini, Kumekucha kumekucha, kutoka kwenu jamani, Kumekucha kumekucha, kwalo msijetukhini,Kumekucha kumekucha, washairi amkeni!

Kumekucha kumekucha, rijali na nisiwani,Kumekucha kumekucha, tukosapo tuonyeni,Kumekucha kumekucha, tustakimu safuni,Kumekucha kumekucha, washairi amkeni!

Kumekucha kumekucha, nyote kalamu shikeni,Kumekucha kumekucha, wa sasa na wa zamani, Kumekucha kumekucha, kikoa TUNASIHINI, Kumekucha kumekucha, washairi amkeni!

Kumekucha kumekucha, sipendi kukuchosheni, Kumekucha kumekucha, nimefika ukingoni, Kumekucha kumekucha, kalamu naweka chini, Kumekucha washairi, washairi amkeni! ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

KUMEKUCHA, AMKENI !

Bilhaki inakera, pamoja na kuchukiza,Kukumbatia fikara, za wenye kuwaburuza,Mwaweza dhani busara, kumbe mwajiangamiza,Japo ninyi si chotara, mamluki wa mfumo!

Japo mkazi wa Bara, siwezi damu kulaza,Kuwazindua ni bora, hata mkinipuuza,Mwageuzwaje majura, ndugu zenu kuwabeza?Japo ninyi si chotara, mamluki wa mfumo!

Ya Kaburu ile sera, nanyi mwaihanikiza,Na kuacha yenu sira, utu inoutukuza,Mwageukaje sogora, ya 'ugozi' kutumbwiza?Japo ninyi si chotara, mamluki wa mfumo!

Kutumika si busara, bayana nawaeleza,Hatima yake hasara, nyote itowangamiza,Mwageuzwaje kafara, wenyewe kujimaliza?Japo ninyi si chotara, mamluki wa mfumo!

Hata kama mkifura, ukweli nawaeleza,Acheni ubarakara, kwa vyeo vinowatweza,Mwageukaje tujara, wa nchi yenu kuuza?Japo ninyi si chotara, mamluki wa mfumo!

Si kwamba naona gera, kwa mlipwavyo 'vifeza',Kinitiacho harara, kufanywa ninyi 'vilaza',Mwageuzwaje kachara, kufikiri msoweza?Japo ninyi si chotara, mamluki wa mfumo!

Mmebaki kusowera, katika nuru ya kiza,Kwa nurenu kuigura, kwa wa kizacho mwangaza,Mwageukaje vinara, wa nuru ya kutatiza?Japo ninyi si chotara, mamluki wa mfumo!

Kwa utamu wa ngawira, mwazidi dira poteza,Mwapeperusha bendera, ya wanowapatiliza,Mwageuzwaje bakora, wenyewe kujicharaza?Japo ninyi si chotara, mamluki wa mfumo!

ABUU NYAMKOMOGI-MWANZA.

JAPO NINYI SI CHOTARA!!!

15 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016Safu ya Ben Rijal

SHEIKH Abdalla bin Wazir wa Ndsujini na na Sheikh Muhammadbin Ahmad bin Hassan Al-Muronyn ni Masheikhe wawili wenye kufanana na walifika Zanzibar kustakimu na kujichotea elimu. Unaposoma juu ya Masheikhe hawa wawili itakupa sura kuwa Zanzibar kwa Masheikhe kupambana na watawala yanarudi nyuma sana na wengine waliamua siku hizo katika mwanzo mwanzo wa karne ya 20 kukihama kisiwa na wengine wakaendelea kuhama katika miongo mine ya mwisho wa karne ya 20

Sheikh Abdalla bin Wazir Mdsujini

Sheikh Abdalla bin Wazir ni kati ya wasomi wakubwa w a l i o p a t a k u k u w e p o visiwani Zanzibar na alikuwa gwiji wa kuitafsiri Qu’ran n a k u we z a k u wa v u t i a wengi katika darasa zake. Alipokuwa anadarasisha i l ikuwa hata watu wa aila ya kifalme walikuwa wakihudhuria darsa zake ndipo pale ilipopelekea wakati wa Mfalme Seyyid Ali bin Said kumtukuza na kumtanguliza mbele, akafanywa kuwa kama Mufti wa Zanzibar na kufanywa kuwa Wazir-al-Awkaaf na kutakiwa kuongoza Wakf wa nchi kuwa chini yake na inasemekana aliweza kuweka

Sheikh Abdalla bin Wazir wa Ndsujini na na Sheikh Muhammadbin Ahmad bin Hassan Al-Muronyn -11

msingi mzuri wa Wakf katika visiwa vya Zanzibar na taratibu alizoziweka zikaja kufwatwa kwa muda mrefu.

Sheikh Abdalla bin Wazir aliifanya kazi yake kwa uadilifu na kwa uungwana lakini kulikuwa na baadhi ya watu hawakupendezewa k u o n a a ya f a n ya y o n a kutamani nafasi yake hio kupewa mtu mwengine, na hayo yakaja kukamilika nyakati za za Mfalme Seyyid Hemed bin Thuweyny ambae hakuwa anamuona kama alivyokuwa anatukuzwa na mtangulizi mwenzake, kwa hio Mfalme Seyyid Hemed bin Thuweyny akammpa notisi ya kuondoka na kumfanya kuwa mtu asiotakiwa na kupewa Persona Non Granta kama aliyopewa baadaye Sheikh Hassan bin Ameir. Alirejeshwa visiwa vya Comoro na huko alipokelewa kwa mikono miwili na wakazi wa huko walifurahi ghaya ya

furaha kumpata Sheikhe wa sampuli hio. Juu ya kurejeshwa Comoro alikuwa roho yake yote ipo Unguja kwa namna alivyozowea nakuwaacha wanafunzi wengi ambao aliamini kuwa watakuja kuwa wasomi wakubwa akiwa mmoja ni mwanawe wa kumzaa.

Shikh Abdalla bin Wazir alirudi Unguja bada ya kuaga dunia Mfalme Seyyid Hemed bin Thuweyny. She ikhe huyu a l ikuwa akisikilizana na Sheikhe mwengine mkubwa ambaye nitakuja kumzungumza kwa upana naye ni Sheikh Abdalla Abubakar Bakathir, walijuana Masheikhe hawa wawili na wakapendana na kufunga udugu na hata wakawa wanasoma pamoja na kutalii pamoja.

Katika darsa ake za kutafsiri Qu’ran zilikuwa na kugusia kila fani ya elimu iwe lugha na nahwi yake

na balagha, sarfu, mantiki tarekhe, sira pamoja na ulimwengu ulivyokuwa kwa wakati wake na harakati zake hilo likamfanya kuwa kwa wakati huo alioishi h a k u k u wa n a S h e i k h e aliobobea kuisomesha tafsiri ya Qur’an zaidi yake na alikuwepo Sheikh aliokuwa aki julikana kwa j ina la Sheikh Abdulshakur ambaye akipenda kuwakosoa baadhi ya Mashiekh lakini kwa Sheikh Abdalla bin Wazir alikuwa akisema “Tafsiri chapa kwa Sheikh Abdalla Wazir”

Msikiti wa Chale (Charlie) uliokuwepo hadi leo katika eneo la Mkunazini karibu na kwa Abulrahman M a p e r e m e n d e n d i p o alopokuwa akidarasisha, Msik i t i huu n i mdogo haubebebi za idi ya ya watu 100 lakini darasa zake zikiujaza na wasomaji wengine wakiwa wanakaa nje ya Msikiti.

Juu ya kusomesha kwake wanafunzi wengi watu walipenda mwanawe Sheikh Mohammaed bin Abdaalla bin Wazir ashike makamo yake, lakini Sheikh Mohammed bin Abdalla bin Wazir hakuwa akihudhuria darsa za baba yake kikamilifu na alikuwa akipenda jioni baada ya sala ya Alasiri kwenda kucheza mchezo wa Golf (gofu) wengi wakilaumu kwa kusema mtoto wa Sheikh anacheza Golf bada ya kujitahidi kusoma kuja k u c h u k u a m a k a m o ya

babake. Alipofariki Sheikh Abdalla bin Wazir wanafunzi wake wakaona sasa ule utamu waliouzowea wa darsa uliokamilka umekwisha k w a n i h a w a m u o n i atakayeweza kudarasisha na kufwata nyayo za Sheikhe. Bada ya maziko mwanawe S h e i k h M o h a m m e d bin Abdalla Wazir kwa mshangao wa wengi alisema darsa ipo na itaendelea na yeye ndio atakayedarasisha, ilikuwa kama changamoto na kila mmoja kumuambia mwenzake kuwa Shiekh Mohammed eti anajitia darsa ipo na yeye atadarasisha, baada ya siku 3 kupita huu ulikuwa ni mtindo siku hizo hapa visiwani mtu akifariki husomwa Khitima kwa siku 3, siku 2 za mwanzo watu hupewa tangawizi na siku ya mwisho hutegemea ima hupewa visheti au halua. Zilipomalizika siku 3 Sheikh Mohammed Abadala bin Wazir alifika Msikiti wa Chale na kukuta Msikiti umesheheni hakuna pakutia mguu, akauliza wanafunzi wal iof ika kat ika darsa walipofika na alipoambiwa w a l i p o f i k a a k a a n z a kudarasisha na kupita njia zilezile ambazo babake akizipita na yeye alivyokuwa akikichapa Kiengereza sawa sawa ikawa anayaelezea hata ya magazeti yamesema nini? Wanafunzi wa babake walipigwa na butwaa na kuulizana huyu mtu kasoma

Inaendelea Uk. 16

Miti duniani na maisha yetu - 2KATIKA makala iliopita ilikuwa ni utangulizi juu ya Makala 15 mfululizo yatakayo eleza miti mbalimbali, makala hii ya mwanzo itauzungumzia mti ulio maarufu hasa kwa wakazi wa maeneo ya Pwani sio mwengine ila ni Mnazi. Mswahili anamsemo wake usemao, Kua kama Mbuyu faida kama Mnazi, kwa kuwa Mnazi kila sehemu yake inapatikana faida.

Ubaiti wa Nazi : Ukitaka kutafuta, Sisumbuke nenda pwaniKila kona tazikuta, Mjini na mashambaniZilopangwa kwa matuta, Uchague hadharani

J i n a l a k i t a a l a m u : Cocos nucifera, Familia: Arecaceqacea

Majina ya Mnazi kwa lugha mbalimbali :

Kispani unaitwa Cocotero or Palmera de coco, Kihindi [naariyal], Urdu, Kifaransa Cocotier cultivé au Noix de coco au r Palmier de coco, Kichina [Yēzi], Kijapani [Kokonattsu, Kitaliano Noce di cocco or Palma da cocco, Kireno Coco, Kikorea [kokoneos], Kirusi кокос [kokos], Kiyunani καρύδα [karýda], Kiyahudi, Kijarumani Kokosnusspalme or Kokospalme, Kipoland orzech kokosowy, Kiengereza Coco, Coconut or Coconut palm, Kidachi Kokosboom or Kokosnoot or Kokospalm. Czech Kokosovy`ooech, Filipino Buko, Hawaian Niu, Hindi Khopra, Indonesia Kilapa, Kiswahili Mnazi, Kisomali Qumbe, Tamil Thenggai, Kiveinam Tra'i du*`a, Kiarabu Juzu minal hindi.

Kuonekana kwakeMinazi inaonekana zaidi

katika nchi za tropiki zilizo na joto. Inaelezwa kuwa Mnazi ulifikishwa katika maeneo ya Hawai kutokea

Mnazi wa Kitamli

visiwa vya Polynesia na nazi iliokuwa haijafuliwa inaweza kubakia baharini na kutembea kwa masafa narefu pasina kupoteza ubora wake. Minazi kwa kipindi kirefu ilionekana katika maneo ya visiwa vya Caribbean na katika sehemu za bahari ya Atlantiki na maeneno ya Afrika ya magharibi, inaelezwa kuwa Christopher C o l u m b u s m v u m b u z i alioaminika kuivumbua Marekani ameandika katika maandiko yake kuiona Minazi katika Amerika ya Kusini. Chr is topher Columbus

wazungu wanajivunia sana juu ya umahiri wake na kuweza kuvumbua Bara la Marekani, kunaushahidi unaonyesha kuwa kufika kwake Marekani alisaidiwa na kijana wa Kiafrika ingawa maandiko mengine yanasema alikuwa Chotara wa Kiafrika na Kizungu al iyokuwa akiongoza msafara wake kwa kutumia nyota na hivi sasa ugunduzi uliofanyika na wataalamu wa mabaki kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge c h a h u k o U i e n g e r e z a

Inaendelea Uk. 16

16 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016Safu ya Ben Rijal

Sheikh Abdalla bin Wazir wa Ndsujini na na Sheikh Muhammadbin Ahmad bin Hassan Al-Muronyn -11

Inatoka Uk. 15lini? Wengine wakasema kapewa Ijaza kitu hakiingii akilini kwenye elimu, wengine wakisema kajaaliwa kuelewa kwa zile siku chache alizokuwa akihudhuria darasa. Mwenyewe akawa anayasikia hayo maneno yenye kugongana akaona asiwapatishe dhambi wanafunzi wa babake na sasa wanafunzi wake, akawambia kuwa yeye akicheza Golf kwa kuwa mchezo huo unakufanya uende mwendo mrefu na yeye alikuwa anatatizwa kiafya akaona ndio mchezo unaomfaa, lakini alikuwa kila siku kuanzia saa sita ya usiku hadi sala ya Alfajiri akisomeshwa vitabu mbalimbali na babake pasina watu kujuwa hilo na akijua fika kuwa babake akimtaka ashike makamo yake kwahio akisoma kwa juhudi. Akawaeleza aidha wanafunzi wake namna watu walivyokwenda kumshtaki kwa babayke kuwa huyu kijana kaendekeza mchezo wa Golf hasomi nini kitakuwa pale utapoondoka? Sheikh Abdalla hakuwa na jawabu akicheka tu.

Katika kukicharaza Kiengereza akipenda kufanya mijadala na Mapadri na alikuwa akipenda mijadala yake iwe kwa Kiengereza, akipenda kwenda Kanisa la Kimoto liliopo Mkunazini hata kabla ya kufariki babake, wengine hawakujua akenda kufanya nini , kumbe alikuwa anakwenda kwa mijadala na akiwafahamisha hata wanafunzi wake namna ya kujadiliana na waliokuwa sio Waislamu.

Mola atujaalie na kina sisi tufate nyanyo za Shekih Abdallla bin Wazir na mwanawe Sheikh Mohammed bin Abdalla bin Wazir, Ameen.

Sheikh Muhammad bin Ahmad bin Hassan Al-Murony

Wengi walioishi katika nyakati alizoishi Sheikh Muhammad bin Ahmad bin Hassan Al-Murony wakitatanishwa na namna alivyokuwa na shauku ya kusoma na kutaka kuishi katika ardhi takatifu ya Makka.

Sheikh Muhammad bin Ahmad alikuwa kati ya wanafunzi wa Sheikh Muhydin bin Sheikh na alisoma vitabu vingi kwake na

alipofariki Sheikh Muhydini alihajiri Zanzibar na kuelekea Mombasa kwenda kusoma kwa Sheikh Ali bin Abdalla Mazrui na aakfika hadi Lamu kusoma kwa Sayyid Mansab, baada ya kuelimika ziada kwa Masheikhe hao aliitwa na wenzake kuja kushika makamo ya Sheikh wao Sheikh Muhydin akakubali na kurudi Unguja na kudarasisha katika Msikiti wa Kiponda zamani ni karibu na nyumba ya Sharif Dewji siku hizi tutasema ni pembeni mwa Makapu hawa ni watengenezaji wa vikapu walio maarufu hapo Kiponda. Umahiri wake na upeo wake wa elimu alikuja kupewa Ukadhi katika mwaka wa 1303 AH (1886) aliifanya kazi hio vilivyo lakini hakudumu nayo akaiwacha na kuhamia Makka, kabla ya kuhamia Makka alifika visiwa vya Comoro kisha akenda Afrika ya Kusini huko kote alikwenda kufanya Daawah na aliooondoka Afrika Kusini hakusimama ila alifika Makka.

Jambo mmoja ambalo nimejifunza k a t i k a H i j j a ya n g u n i k u wa unapokwenda Hijja na kuiona Al-Qaba kwa mara ya kwanza moyo wako unabadilika na kukupitia mengi ya kutamani na wewe uwe unaishi pale Makka na kila siku kupata kuwa unatufu. Tunaelezwa waliotangulia walikuwa kila wakisha

kusali huwenda kutufu na kuongeza kufanya hizo Tawaf katika mwezi wa Ramadhan. Wengine wanapoomba dua zao kuyataka hayo hutakabaliwa na ndio Sheikh Muhammad bin Ahmad bin Hassan Al-Murony aliyaomba hayo na kayapata. Sheikhe huyu alikuwa na sifa ya Ucha Mungu wa hali ya juu inaelezwa kuuacha kwake Ukadhi ni kuhofia asije akawa anahukumu sivyo na anaendesha mambo yenginevyo na ndio akuacha na kuelekea Makka.

Sheikh Muhammad bin Ahmad bin Hassan Al-Murony alisomesha wanafunzi wengi ambao baadaye walikuja kuwa mahiri, kati ya wanafunzi wake wakubwa ni Sayyid Mansab ambaye nishamzungumza m a k a l a z a n y u m a a l i o s o m a uchoraji kwa bibi wa Kimishini, Sheikh Jabir bin Saleh babu wa Sheikh Abdalla Saleh Farsy, Sheikh Abdurahman Mwenze Mbamba hao ndio waliokuwa wanafunzi wake wakubwa.

Habari zake Sheikh Sheikh Muhammad bin Ahmad bin Hassan Al-Murony za Makka hazikunukuliwa ila inafahamika kuwa alifia Makka na kuzikwa huko huko, tuamuomba Mola nasisi atujaalie yale mema walioyafanya Masheikhe hawa, Ameen.

Miti duniani na maisha yetu - 2Inatoka Uk. 15wanaelezea kuwa Christopher Columbus mwenyewe alikuwa sio mzungu alikuwa ni Mwafrika (Rejea: http://weeklyworldnews.com/headlines/23529/christopher-columbus-was-black-2/ aidha: http://rense.com/general43/before.htm na http://weeklyworldnews.com/headlines/23529/christopher-columbus-was-black-2/#idc-cover).. Ushahidi mwengine uneeleza kuwa Waafrika kutoka Afrika ya magharibi walikuwa wameshafika Marekani kwa zaidi ya miaka 150 kabla ya Christopher Columbus kufika kwake huko Marekani na wao huwenda ndio waliokwenda na hizo nazi. Chambuzi nyengine za kitaaluma zinasema kuwa Minazi asili yake ni Mashariki ya mbali.

Kuufahamu MnaziWataalamu wa elimu ya mimea

wanafahamisha kukuwepo kwa aina 150 ya minazi ambayo huonekana katika nchi 80 duniani kote. Minazi hukuwa katika maeneo ya Tropiki, inategemea udongo wa mchanga kuweza kukuwa kwa Mnazi, huwa ni vigumu kukuwa kwa Mnazi katika hali ya hali ya baridi, Minazi ipo ilio mirefu na ilio mifupi inajulikana kama kitamli. Minazi mifupi huwa na urefu baina ya mita 6 hadi 18 na ile ilio mirefu hufikia urefu wa mita hata 50. Mnazi hauna matawi lakini huwa na makuti kileleni, Mnazi huwa na mauwa ya jike na dume na hufanya mpango wa uzazi wakibinafsi.

Mnazi uliotimia huzaa kwa mpigo nazi zifikiao 75 na mara chache zao hilo hupungua kwa kuzaa nazi 30 kwa mwaka. Aghlabu uzito wa nazi hufiki kilo 1.5 hadi 2. Takwimu zinaonyesha kwa mwaka duniani kote huzalishwa tani milioni 600 za nazi. Nazi huangushwa na Mkwezi katika maeneo ya kwetu lakini nchini Thailand na kwengineko anayopanda Mnazi na kuziangusha

ni Nyani. Mafuta ya nazi hutumika kwa kupikia, dawa na urembo, walimbwedu wa asili wakimeremeta kutokana na mafuta ya nazi. Sabuni nyingi hutengenezwa kutokana na Nazi. Hivi sasa imepatikana teknolojia ya kutengeneza fanicha kwa kutumia kigogo cha mnazi na fanicha hizo hudumu muda mrefu na zenye kupendeza.

M a k u m b i h u t u m i wa k a m a nishati, Mnazi huishi umri mrefu kama haujadhurika kwa maradhi. Mnazi hufikisha umri wa miaka 100. Makuti ya Mnazi ni mjarabu kwa kuezekea nyumba. Maji ya madafu ni kinywaji cha burdani nchi ya Brazil inaongoza kusafirisha maji ya madafu yalioingizwa kwenye mikebe.

Makuti ya Mnazihutoa vijiti vinavyochomekewa nyama ya mshikaki, aidha fagio za njukuti

hutokana na vijiti vya makuti. Kumbi la kukogea la Mnazi hutoa nongo na kukung;arisha useme Brasso inavyosafisha shaba.

Nchi zinazoongoza uzalishaji wa Nazi duniani

Indonesia ndio inayoshikia usukani wa uzalishaji wa metric tone 18,300,000 sawa na asilimia 38 ya uzalishaji wa nazi zote duniani, ikifwatiwa na Philippines metric tani 15,353,200 sawa na asilimia 30 ya uzalishaji wa nazi zote duniani, India metric tani 11,930,000 asilimia 23.3, Brazil meric tani 2,890,286 asilimia 5.66, Sri Lanka metric tani 2, 513,000 na Tanzania metric tani 370,000.

Faida za Nazi kiafyaWazee wetu wakiitumia nazi

kwenye maakulati yao na afya zao hazikuwa zimeathirika ila hivi karibuni vitisho vya wataalamu

vilizagaa na kututaka tusitumie nazi kwenye vyakula vyetu kwa wingi kwa kuwa nazi ina shahamu nyingi na ina dhara kubwa kiafya. Wazee wetu huko nyuma wakila wali wa nazi, mchuzi wa nazi, samaki wa kupaka wa nazi, ndizi mbichi za nazi, pweza wa nazi isitoshe jioni anakwenda kunywa maji ya madafu barazani na wenzake na afya zao hazikuwa zenye kutetereka.

Wazee wetu wa maneo ya Pwani iwe Matemwe, Wingwi, Bagamoyo, Mikindani, Handeni, Kilwa n.k walikuwa ni watu wenye afya na wakifikia umri wa miaka 80 kwenda juu huku wakiwa bado afya zao zipo madhubuti kwa kutembea, kufanya kazi hata wanapolala usiku na wenzao. Mswahili akiwa mlo wake haujapikwa nazi mzee hununa, daku lisilokuwa la wali wa nazi mwenye nyumba hamaki moto mmoja, kumbe kweli wazee hawajakosea kuipenda nazi sasa tuangalia watalamu wanatuambiaje?

Mafuta ya Nazi yanafaida kubwa sana, mafuta ya nazi ni moja kati ya nyenzo inayotokana na miti yenye shahamu iliokamilika (saturated fat) ina lauric acid ambayo ina sifa ya kupambana na baketeria na virusi, matumizi ya mafuta ya nazi huongeza harakati za kimwili, husaidia kuipa mizani shindikzio la damu, kupungua uzito, huongeza nguvu za mafupa, hurahisisha chakula kusagwa kwenye tumbo, husaidia kujikinga na saratani, huifanya ngozi na nywele kuwa imara, husaidia kuepukana na maradhi ya moyo, huongeza kinga katika mwili (Rejea: http://altmedicine.a b o u t . c o m / o d / c o c o n u t o i l / a /Benefits-Of-Coconut-Oil.htm?utm_t e r m = h e a l t h y % 2 0 c o c o n u t % 2 0o i l & u t m _ c o n t e n t = p 1 - m a i n - 3 -tit le&utm_medium=sem&utm_s o u r c e = g o o g l e & u t m _campaign=adid-117ed24d-5c05-4d2f-823a-ec07b092505f-0-ab_gsb_ocode-

17 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016

HABARI/TANGAZO

Inawatanganzia Waislam wote kuwa imeandaa safari ya Hijja mwaka 2016 sawa na mwaka 1437 Hijria kwa Dola US$ 3,555

Kutakuwa na punguzo la asilimia 16% kuanzia muda huu mpaka Feb 29/2016. Itakuwa Dola $2986 tu.

Kuanzia mwezi Machi 01-2016 mpaka Juni 12-2016 kutakuwa na punguzo la asilimia 6% sawa na Dola $3,341 tu.

MAMBO YATAKAYOGHARAMIWA1. Semina za Hija, 2. Huduma za afya na kuchinja 3.Airport Charge na

ticket za Ndege 4.Nyumba Makkah na Madina 5.Irham na Kuchinja kwa ajili ya Tama-tuu 6.Chakula wakati wote 7.Usafiri na ziara Makkah na Madina 8.Mahema Mina na Arafa.UMRA MWEZI WA RAMADHANI ITAKUWA NI DOLA US $1995

Fomu zinapatikana sehemu zifuatazo:-1.Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es Salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini nyumba Namba 26 mkabala na Showroom ya magari Tell. 0713 730 444, 0773 804 101 ,0785 930 444 au 0773 930 444.2. Ofisi ya Ahlu Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484 982, 0777 413 987.3. Abubakr Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es Salaam, Tel: 0784 453 8384. Abdallah Salehe Mazrui (Hoko) Dar es Salaam, Tel: 0715 724 444 5. Abdallah Hafidh Mazrui, Wete Pemba Tel: 0777 482 6656. Mohammed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba 0777 456 9117. Sheikh Daud Khamis Shekha Tel: 0777 679 6928. Maalim Seif Humoud Hamed (Kijichi Zanzibar) 0777 417 736WAHI KULIPIA1. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Tel: 0713 730444, 0773

804101,0785 930444.2. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484982,

0777 413 987.Maalim Seif Humoud Hamed (Kijichi Zanzibar) Tel: 0777 417 736

TANBIH(a) Atakaemaliza taratibu zote mwanzo ndie

atakayeshughulikiwa mwanzo(b) Ili uwemo katika fungu la kwanza unatakiwa umalize

taratibu zote kabla ya punguzo (c) Kumbuka kikundi cha Ahlul Daawa kwa bei nafuu kuliko

wote na huduma kuliko wengi.Wabillah Tawfiq

Ahlu Daawa Hajj and Travel Agency

WAPO mashujaa waliopigania Uhuru wa Zanzibar, lakini historia haiwataji na wala michango yao haitambuliwi na nchi, akiwemo Aman Thani.

Hayo yamebainihswa na nguli wa Historia nchini Sheikh Mohammed Said, akiyazungumzia Mapinduzi ya Zanzibar, akiwaelezea wale ambao wamefichwa na historia kwa ujumla, akiwemo Aman Thani, ambaye si wengi wanaomfahamu.

Alisema, kwamba amezisoma kumbukumbu za Aman Thani na kueleza umuhimu wa kusomwa nyaraka zake haswa kwa wanafunzi wanaojifunza historia ya siasa za Afrika, hususan historia ya Zanzibar na Mapinduzi yaliyotokea mwaka wa 1964.

Alisema, kumbukumbu zinaonyesha kwamba Aman Thani, ametamka kuhusu Mapinduzi ya Zanzubar kuwa hayakuwa ''Mapinduzi,'' bali mavamizi, huku akitoa changamoto katika moja ya picha maarufu ya Okello, akitaka atokee mtu yeyote awaonyeshe Wazanzibari halisi katika picha ile.

Aman Thani na Mapinduzi ZanzibarNa Bakari Mwakangwale Sheikh Mohammed,

amemtaja Aman Thani ni yeye peke yake katika wafungwa wa kisiasa wa Zanzibar, aliyeweza kueleza kwa kirefu kuhusu jela za mateso zilizoundwa baada ya Mapinduzi na jinsi alivyokabiliana na mtesaji mkuu Hassan Mandera.

Ama kuhusu, John Okello, ambaye amekuwa akitajwa sana katika kumbukumbu nyingi za historia ya Mapinduzi ya Zanzibar, alisema Okello, hakuwa chochote katika Mapinduzi hayo ila alitumiwa zaidi kutoa matangazo ya kuwatisha wananchi.

“Kwa lugha ya wenye Mapinduzi yao ni kuwa, ''Walimvisha blanketi la U-Field Marshall na likamwenea na yeye mwenyewe akaamini khasa kuwa hakika ni ''Field Marshall,''” Amesema Sheikh Mohammed.

Kuhusu ''Blanketi la Okello,'' aliwata watu kurejea katika kitabu cha Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru'' ambapo alimtaja Abdallah Kassim Hanga kuwa ndiye aliyepanga Mapinduzi akishirikiana na Serikali ya Tanganyika, chini ya Mwl. Julius Nyerere.

SHEIKH Abeid Aman Karume.

MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

John Okello (kulia)

18 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016

MAKALA/TANGAZO

SURVEY KWA WASOMAJIUONGOZI wa gazeti la An-Nuur unatoa shukurani kwa Wasomaji wa gazeti hili kukushukuruni kwa dhati kutuitikia na kuwa An-Nuur ni Sauti ya Waislamu.

Gazeti hili linataka kuboresha matoleo yake kwenu wasomaji na ikiwezekana kuongeza kurasa na hayo hayawezekana pasina kupata mashirikiano yenu kwa kutoa maoni yenu juu ya matoleo yetu mbalimbali kipi mnakiona ni vyema kuongezwa na kipi mnaona kipunguzwe na kipi kitolewe.

Survey hii tutaifanya kwa njia tatu nazo ni: (i) Kutumia njia ya Posta, (ii) Barua pepe (e-mail) na (iii) Ujumbe mfupi (SMS). Watakaotuma kwa njia ya Barua pepe na Posta, wajaribu kukopi Jadweli au kufwata njia ya hapo chini ambayo kwa watakaotumia njia ya Ujumbe mfupi.

Majibu kwa ujumbe mfupi

Kwa wale watakaotuma kwa kutumia ujumbe mfupi (SMS) tutaomba

Jadweli ya Survey

Makala Ubora (Points) Chakuongezwa Chakuondolewa 1.Ukarasa wa mwanzo na wa mwisho (Habari) 2. Tahariri. 3. Uchambuzi wa Omar Msangi. 4. Habari za Kimataifa. 5.Hoja za Juma Kilaghai. 6. Makala kwa Jumla. 7. Safu ya Ben Rijal 8. Masheikhe waliopita. 9. Mashairi. 10. Waandishi Msangi Juma Kilaghai Ben Rijal Waalikwa Points: 1. Afadhali, 2. Inatosheleza 3. Nzuri 4. Nzuri sana.

wachukue wakati wao, kwenye Makala tulizoorodhesha aziandikie, kisha afanya hivi: 1.Ukarasa wa mwanzo aupe point tuseme (4) 2. Tahariri (4) 3.Uchambuzi wa Msangi (4) 4. Habari za Kimataifa (2), mpaka mwisho.

Kisha mtumaji wa Survey hii andike hivi tunaweka mfano:

Wasomaji watoe maoni yao wanafikiri kipi kiongezwe na kipi kiondolewe, tumeweka mfano hapo chini.

Chakuongezwa: Barua za wasomaji, Malezi ya watoto, Mashindano kila mwezi na kutolewa zawadi n.k.

Chakuondolewa: Chemsha Bongo, Mashairi n.k.

Njia nyengine itakayorahisisha majibu ya Survey

Msomaji unaweza kutumia njia hii aidha. Andika nambari chini ya anuwani mfano kwenye Makala kisha weka Points, mfano: Makala 1. (4), 2.( 3), 4. (2) n.k. au 1=4, 2=3, 3=4 n.k.

mfano tu)MAKALA1.Ukarasa wa mwanzo na

wa mwisho (Habari)2. Tahariri.3. Uchambuzi wa Omar

Msangi.4. Habari za Kimataifa.5.Hoja za Juma Kilaghai.6. Makala kwa Jumla.7. Safu ya Ben Rijal8. Masheikhe waliopita.9. Mashairi.WAANDISHI1. Msangi2. Juma Kilaghai3. Ben Rijal

4. WaalikwaCHAKUONGEZWA:CHA KUPUNGUZWA:Points: 1. Afadhali, 2.

Inatosheleza 3. Nzuri 4. Nzuri sana.

*Watukufu wasomaji “Survey” hii ni muhimu katika kuliendeleza gazeti letu hili na wewe msomaji ujuwe fika mchango wako adhimu ndio kufanikisha zowezi letu hili.

Anuwani kwa Waandishi weka Nambari na Points mfano Waandishi 1. (2), 2. (4). Au 1=2, 2=4 n.k

Cha kuongezwa: (Hapa utashauri jambo la kuongezwa): Barua za wasomaji, Ukumbi wa Mashairi n.k. (Huu ni mfano tu)

Cha kupunguzwa: (Hapa utashauri kitu gani kipunguzwe) : Chemsha Bongo, Habari za Ulimwengu n.k. (Huu ni

Somalia moja inatutosha…Inatoka Uk. 8Asasi ya kutatua

migogoro ya kimataifa iitwayo International Crisis Group (ICG) imependekeza kwa Marekani na nchi zingine za Magharibi zifadhili kikosi cha Afrika cha kulinda amani huko Burundi. Ndipo Marekani na Umoja wa Ulaya (EU) zimekuwa zikizishawishi nchi za Kiafrika kutuma majeshi huko Burundi. Baraza la Usalama na Amani la AU limekubali pendekezo ambalo linapingwa na nchi za EAC na SADC. Ndipo tunaelewa kwanini suala la Burundi linapozungumzwa na Waafrika mkutano huwa unahudhuriwa na Marekani na EU. Hii haifanyiki huko Burundi tu, bali katika bara zima la Afrika. Ni kwa sababu Marekani na wenzake wa Ulaya (EU) wana maslahi yao ya kiuchumi na kisiasa barani Afrika, na ndio maana wametandaza majeshi yao kote. Mfano ni hiki kikosi

cha Marekani kiitwacho Africom. Madhumuni yao ni kulinda maslahi ya kibeberu, lakini lugha wanayotumia ni kuwasaidia watawala wa Afrika kulinda na kutunza amani katika nchi zao. Na mara nyingi hutumia bendera ya Umoja wa Mataifa (UN) ili kufunika mbinu zao

zisijulikane kwa urahisi.Wanapofanya hivyo

hutumia watawala wa Kiafrika na jumuiya zao kama AU au Ecowas kule Afrika Magharibi. Angalia jinsi nchi za Magharibi zinavyofadhili majeshi ya “kulinda amani” kule Somalia (AMISOM). Na ndivyo ilivyokuwa kule Afrika

Magharibi na DRC. Sasa wanataka kupeleka majeshi Burundi.

Tumeona kuwa Rais Magufuli akiwa mwenyekiti wa marais wa EAC ana jukumu la kushughulikia mgogoro wa Burundi kama nchi mwanachama. Lakini rais wetu anamaliza miezi miwili na hajatoka nje ya nchi. Ameamua kushughulikia majipu yaliyo ndani ya nchi. Sasa anakabiliwa na jipu la Burundi. Wakati huo huo Magufuli anakabiliwa na mgogoro uliozuka visiwani Zanzibar kutokana na kufutwa kwa uchaguzi. Mgogoro huo umechukua sura ya kimataifa kutokana na mabalozi wa magharibi nao kujiingiza.

Mwaka jana wakati Nkurunzinza alipoonyesha nia ya kubaki madarakani, msimamo wa Tanzania ulikuwa kuwa alipaswa

kuheshimu katiba ya nchi na makubaliano ya Arusha. Tulitoa hata risala rasmi mnamo Machi 2015 tukimwambia Nkurunzinza aheshimu kikomo cha urais. Hata hivyo Nkurunzinza hakujali na akagombea uchaguzi. Mara moja Tanzania ikaonekana ikibadili msimamo wake na hata ikatuma waangalizi wa uchaguzi. Mataifa na mashirika mengi kama UN na AU yalikataa kutuma waangalizi ili kuonyesha kuwa hawakubaliani na Nkurunzinza.

Ndio maana si jambo la kushangaza kuwa Tanzania inapinga kuingizwa kwa majeshi ya AU huko Burundi na badala yake inajaribu kusuluhisha kwa njia ya Amani. Labda mara hii tutahitaji tena wazee kama Mwalimu Nyerere au Mzee Mandela ambao walisaidia sana kusuluhisha wakati ule. Je, Magufuli ataweza kuvaa viatu vyao?

(0713 562181, [email protected])

RAIS wa Burundi, Pierre Nkurunzinza.

19 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016

MAKALA/TANGAZO

“MAMLAKA tuliyonayo ni mojawapo ya mafanikio yetu hatutoyaacha yapotee, wala kumruhusu yoyote kufanya uharibifu katika ardhi tukufu”.

B e t h l e h e m u : S h i r i k a la habari la Wafa mnamo tarehe 06/01/2016 limeripoti kuwa,Rais wa Dola ya Palestina Mahmoud Abbas, siku ya Jumatano jioni alitoa wito wa kuitisha mkutano wa kimataifa ili kujadili utekelezaji wa mpango wa amani ya Kiarabu.

M p a n g o u n a o t o k a n a n a k a m a t i m b a l i m b a l i ikiwemo ile ya 5+1, zinazo jishughulisha na utatuzi wa migogoro kadhaa kikanda na kimataifa.

Rais Abbas aliwaambia hayo wakuu na wawakilishi wa waumini Orthodox Ikulu mjini Bethlehemu, katika maadhimisho ya madhehebu ya Mashariki kwa mnasaba wa kuzaliwa Mtakatifu.

Rais ameongeza kusema kuwa, haikubaliki kabisa kuona suala Palestina bado hali japatiwa ufumbuzi , wakati masuala mengine mengi yakipatiwa ufumbuzi kama vile suala la Iran, Libya na Syria, licha ya ukweli kwamba letu ni la muda mrefu zaid kuliko yote hayo.

Hali ni tete na ngumu, japokuwa ufumbuzi wake unaweza usipatikane leo au kesho, lakini inatubidi kushikamana na mafanikio yetu, kwani hii ni nchi yetu na sisi ndio walinzi wake, ni wajibu wetu kuendelea kubaki hapa na kutorudi nyuma katika kudai haki zake kamili.

Alisema: "Tunaendelea kunyoosha mkono wetu kuomba amani, na uwepo wa mazungumzo yanayolenga k u f i k i a h u k o k u p i t i a ufumbuzi wa kuundwa serikali mbili zilizo huru.

I s r a e l i h a i r u h u s i w i k u e n d e l e z a “ u b a g u z i wa rangi "au nchi yenye mifumo miwili.Tunataka dola huru huru na yenye haki kamili kama nchi nyingine duniani,si vingine. "

Kwa upande wa juhudi za kidiplomasia,Rais Abbas amesema bado tunaendelea na jitihada zetu katika Baraza la Usalama na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, si kwa

Rais Abbas atoa wito wa kufanyika mkutano wa kimataifa, kujadili mpango wa amani ya Kiarabu

RAIS wa Dola ya Palestina Mahmoud Abbaslinguine bali ni kwa ajili ya kupata ulinzi wa kimataifa kwa wananchi wetu,pia kusitisha shughuli za ujenzi wa makazi ya walowezi katika ardhi ya Palestina.

Rais Abbas amesisitiza kuwa, makazi hayo ya walowezi yapo kinyume na sheria tangu mwaka 1967 hadi leo, hii ni nchi yetu na lazima walowezi wote waondoke kama ilivyotokea katika Ukanda wa Gaza.

Alipoulizwa yaliyotokea hivi karibuni kuhusu uwepo wa Mamlaka ya kitaifa ya Palestina, Rais Abbas alisema uwepo wa Palestine National Authority (PNA) ni mojawapo ya mafanikio yetu na yataendelea kuwepo, wala mtu yeyote asiwe na ndoto kinyume na hivyo.

Alisisitiza kuwa mamlaka ipo na baadae itakuwa dola huru lenye haki kamili, h a t u t o k u b a l i u b a g u z i w o w o t e a u k u r u h u s u kuendelea kwa hali iliyopo sasa, tumeazimia kutekeleza kila kitu, lakini Israeli haina nia njema hiyo., Tunataka kuishi katika nchi mbili kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967,ambapo Jerusalemu ya Mashariki itakuwa ndio mji mkuu wa Palestina.

Tunaendelea kuiomba Israeli licha ya majanga haya yote tufikie katika lengo letu la kupatikana amani, kupitia mazungumzo,huku nikiwaambia na kutaka kunifahamu vizuri Waisraeli kuwa, sisi hii ni nchi yetu h a t u t o o n d o k a , k a m a mnataka nchi yenye mifumo miwili hilo halikubaliki,

kwani tunataka dola yetu huru yenye haki zote kama zingine duniani.

Ama kuhusu ardhi takatifu Rais Abbas amesisitiza kuwa, ardhi iliyopo imemilikiwa rasmi na watu au taasisi kama makanisa,hivi leo tunaona inatumika kwa makazi zaidi iwe mjini Jerusalem,Bethlehem au Beit Jala. Tunafanya juhudi ili iwe ya watoto,jambo a m b a l o t a y a r i tumeshalianza kulifuatilia kikamilifu.

Hii ni ardhi takatifu hatutairuhusu taasisi au mtu yeyote kuichafua, kwani haya ndio makazi y e t u n d i o m a a n a tunaipigania kwa nguvu zote.Isitoshe huu ni wakfu ambao haufai kuuzwa wala kuuharibu,bali ni haki yetu na watoto wetu ifahamike hivyo kwa wote.

Aliongeza: "Sisi tupo katika kulifuatilia hilo kikamilifu na ndugu zetu wa nchini Jordan, na ni matumaini yetu kwamba k a m a t i ya p a m o j a ya kutatua matatizo kutoka pande mbili husika, na hivi karibuni tunataraji kuona ikishughulikia mustakabali wetu.

Kwa hiyo Rais Abbas katika hotuba yake amesema kuwa,siku hii ya leo na sherehe zote ni zetu wote. Mwaka 2015 ulikuwa na matukio mengi muhimu,yakiwemo makubaliano yasiyo na mfano,yaliyo sainiwa na Papa na Palestina,yakijumuisha

masuala kadhaa ya uhusiano wa pande mbili husika.

Tumefurahi sana kwa kukiri Vatican uwepo wa dola ya Palestina ambayo ni ardhi tukufu.

Sipendi kuzungumzia t o f a u t i z a k i i m a n i z i l i z o p o k a m a v i l e Orthodox,Shia,Sunna,Duruzi na wengine kwani hii ni ardhi yetu wote na kwa hali zote tupo pamoja ndivyo tulivyolelewa,tutabakia hivi milele. Hakuna atakae tutenganisha pia sherehe na maadhimisho yote ni yetu na zina uzito sawa kwetu.

N a p e n d a i e l e we k e wazi kuwa, endapo kama haukupatikana utatuzi wa dola mbili huru basi hapatakuwa na ufumbuzi tena duniani wa matatizo kama ugaidi,matumizi ya nguvu na kadhalika.

Yanayotokea Palestina leo yanaelekea katika mgogoro wa kidini,jambo ambalo ni hatari sana. Ni bora ziachwe sehemu takatifu yakiwemo makanisa ambayo imefikia yanaharibiwa na k u k a t a l i wa u we p o wa wakris to na kupelekea kukwama kwa utatuzi wa

haraka wa mgogoro.Kwa hiyo msimamo wetu

tokea mwanzo ni kufikia amanina hata maandamano yetu ni ya amani, hatutaki madhara kwa ta i fa na wananchi wetu,ili tujenge mustakabali mwema.

T u n a l a a n i s a n a ugaidi,matumizi ya nguvu na kadhalika, mfano halisi wa hilo ni ndugu zetu Wasaudia walipotoa wito wa kuungana kupiga vita ugaidi,tulikuwa wa kwanza kukubali.

Hivyo,umoja wetu wa kitaifa ni muhimu sana na ni wajibu wetu kufanya juhudi katika hilo ili kuwasaidia ndugu zetu wa Gaza,wapate kuishi maisha mazuri.

K u p i t i a s i k u h i i tukufu, tunawaombea wafu na majeruhi wetu,pia mateka wetu zaidi ya elfu 70 wengi wao wakiwa ni watoto warudi nyumbani s a l a m a , h u k u a m a n i ikitawala kati yetu na Israeli.

Contact us: P.O Box 20307, 612 UN Road – Upanga West, Dar es Salaam Tel: 2152813, 2150643 Fax: 2153257 E m a i l : p i c t @ p a l - t z .orgWebsite: www.pal-tz. Org.

20 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 201620 MAKALA AN-NUUR

20

Soma gazeti la AN-NUUR

KWA TSH 800/=kila Ijumaa

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 22-28, 2016

HAIIBA TIMAMU TEA CHAI YA AJABU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA

SHINIKIZO LA DAMU (HYPERTENSION/HIGH BLOOD PRESSURE)

UGONJWA WA MOYO KIHARUSI JONGO (GOUT) MAUMIVU YA VIUNGO (RHEUMATISM) MAUMIVU SUGU YA KICHWA BAWASIR (PILES/HEMORRHOIDS) MAGONJWA YA INI SARATANI MBALIMBALI UOTO/UVIMBE MBALIMBALI KATIKA VIUNGO VYA UZAZI VYA MWANAMKE (FIBROIDS, POLYPS NA CYSTS)

KUSHINDWA KUZUIA MKOJO (URINARY INCONTINENCE)

ATHARI ZA KISUKARI CHA UKUBWANI PUMU UPUNGUFU WA KINGA ZA MWILI KASI YA KUZEEKA MATATIZO YA MFUMO WA MZUNGUKO WA DAMU

MKAKAMO WA NGOZI; UDHAIFU WA MACHO KUPOTEZA KUMBUKUMBU KASI NDOGO YA KUPONA MAJERAHA MAKOVU KWENYE MAPAFU UGONJWA WA NGOZI KUCHUJA RANGI, YAANI, VITILIGO

HAIIBA TIMAMU TEA INAPATIKANA

HERBAL IMPACT

MOSQUE STREET, NO. 1574/144 (MKABALA NA MSIKITI WA SUNNI), KITUMBINI, DAR ES

SALAAM

TUTEMBELEE AU TUPIGIE SIMU NAMBA:

0754281131/0655281131/0686281131/0779281131

PRESHA YANGU IMEKUWA YA KAWAIDA KWA MARA YA KWANZA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 13!

Na. Abdulkarim Saidia

Nimekuwa nikiishi na ugonjwa wa presha ya kupanda kwa takriban miaka 13. Hali ilikuwa ni mbaya mno kiasi kwamba muda mwingi nilisikia kama sauti ya mvumo kwenye masikio. Nimejaribu tiba nyingi sana kupitia hospitali za kisasa na hata zile za tiba mbadala lakini sikupata mafanikio. Miezi michache iliyopita rafiki yangu mmoja alinishauri niende Herbal Impact. Alinipa namba za simu za wahusika na kuniambia kwamba kabla ya kwenda ni vizuri nikaongea nao kwanza. Nilifanya kama alivyonishauri. Herbal Impact walinipa paketi 3 za Timamu Tea na maelekezo ya jinsi ya kutumia. Huwezi kuamini! Ndani ya wiki 2 tu za mwanzo presha ilikuwa imekuwa ya kawaida na hata mvumo masikioni ulikuwa umetoweka!.

https://www.facebook.com/Herbal-Impact-157972014402705/

WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wametakiwa kuisimamia Serikali iweze kuwachukulia hatua watumishi wake wanaokiuka misingi ya Katiba ili kulinda haki za binadamu.

Wito huo umetolewa na Imam wa Masjid Taqwa, Sheikh Juma Ramadhani, katika hotuba yake ya ibada ya swala ya Ijumaa katika Masjid Rahmaan, Msasani Ji j ini Dar es Salaam.

Alisema, Watanzania w a n a m a t u m a i n i makubwa na wabunge wa Bunge hili la Serikali ya awamu ya Tano, kwa k u i s i m a m i a S e r i k a l i ili iweze kuwatendea h a k i r a i a w a k e n a kuwawajibisha wale wote wanao kiuka misingi ya Katiba.

Imamu Ramadhani, a m e y a s e m a h a y o akizungumzia kuwepo

Sheikh awataka Wabunge wasimamie serikali itende hakiNa Bakari Mwakangwale kwa madai na malalamiko

ya muda mrefu kuwa w a p o r a i a a m b a o wametoa malalamiko yao ya kufanyiwa mambo k i n y u me ch a sh e r i a na Katiba na hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa.

Alisema, pamoja na kuwa matendo hayo yalifanyika katika utawala wa awamu ya nne na sasa ni utawala mpya, lakini kanuni na sheria ni zile zile na wahanga hao bado wapo magerezani na wanaotuhumiwa kukiuka Katiba pia bado wapo Serikalini.

Akikumbushia kwa kuwataja raia hao, alisema ni Masheikh kutoka Zanizbar na Waislamu wengine ambao mpaka sasa wapo magerezani kwa tuhuma za ugaidi, ambao miongoni mwao w a l i d a i k u f a n y i w a matendo ya kinyama na Askari Polisi pamoja wale wa usalama wa Taifa.

Alisema, pamoja na

sakata hilo kutinga katika Bunge la Serikali iliyopita ikitakiwa kuunda Tume ya kuchunguza madai ya raia hao (Masheikh na Waislamu), lakini ilipuuzia suala hilo.

Akirejea baadhi ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano

wa Tanzania, Imamu R a m a d h a n , a l i s e m a Katiba imeweka misingi mbalimbali ya utu kwa lengo la kul inda na kuheshimu utu wa raia wake.

Alisema, Katiba hiyo i m e e l e z a k w a m b a , binadamu wote ni sawa na kila mtu anastahiki heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.

Z a i d i a k a s e m a , katiba hiyo pia inasema ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa ama kupewa adhabu zinazomtenza mtu nguvu au kumshurutisha.

Alisema, pamoja na kuwepo kwa maelezo hayo ka t ika Kat iba , ambayo lengo lake ni kumlinda mwananchi, lakini mtuhumiwa wa Ugaidi, Sheikh Salimu Ally, amedai kufanyiwa vitendo vya kinyama na Askari Polisi, wakati a k i h o j i wa b a a d a ya kukamatwa na Serikaili h a i k u c h u k u a h a t u a

yoyote.I m a m u R a m a d h a n

a l i s e m a w a k a t i w a uchaguzi Mkuu, Rais John Magufuli, alijipamba na kupambwa kwa sifa nyingi nzuri, miongozi mwa hizo ni mwadilifu, mwaminifu na mfuatiliaji.

K wa m a a n a h i y o , waislamu wanadhani sasa ni wakati muafaka kwa Rais John Magufuli, kufuatilia na kuwafanyia uadilifu raia hawa waliopo mahabusu.

Alisema, suala la haki duniani hivi sasa limekuwa ni tatizo, ambapo viongozi wengi katika mamlaka z a o v i n y w a v y a o vimetawaliwa na hadaa huku wakisahau kwamba uongozi ni amana na hapa duniani ni mahali pakupita tu.

Imamu Ramadhani, akaitanabahisha Serikali ya Rais Magufuli, akitaka ifahamu kwamba kuna vitu viwili hata siku moja haviwezi kukaa pamoja, navyo ni haki na batwili.

SHEIKH Salimu Ally


Recommended