+ All Categories
Home > Documents > Uhaini wa Baba

Uhaini wa Baba

Date post: 01-Dec-2023
Category:
Upload: udsm
View: 0 times
Download: 0 times
Share this document with a friend
24
Uhaini wa Baba 1 SEHEMU YA KWANZA. (Shoma aliamuka asubuhi na mapema kama kawaida yake ili ajiandae kwenda shuleni, hapakuwa na saa katika chumba chake, kwa hiyo alikuwa amezoea kuamuka kwa kukisia tu. Lakini jana yake Shoma alifanya kazi nyingi hivyo alichoka na kujikuta anachelewa kuamka. Mara alisikia sauti ya mwalimu na wanafunzi) MWALIMU: Mchaka mchaka!!! WANAFUNZI: Chinja!! MWALIMU: Aliselema!! WANAFUNZI: Alija!! MWALIMU: Hiyuu hiyu!! WANAFUNZI: Hiyu!! MWALIMU: Haiiiiiii!!! WANAFUNZI: Waaaaaaaaa!!! MWALIMU: Chilemba iyuu chile! WANAFUNZI: Oo nchilu! (sauti hizo zilimsitua Shoma, maana haikuwa kawaida kukimbia asubuhi kama jeshi la mgambo, mara alitoka nje ghafula baada ya kuvaa nguo kwa haraka na kukimbia kujiunga kundi la wanafunzi hao, hapo hapo kabla hajajiunga alikutana na jicho la Mwalimu) MWALIMU: Wee kifaranga! We!! Kwa nini umechelewa? Unafikiri hii shule ni ya bibi yako, haraka jiandae kula bakora. SHOMA: Mwalimu sikujua kwamba utaratibu umebadilika!(maana alikuwa na siku kama nne hivi hajaenda shule) MWALIMU: Utaratibu upi we! Hebu chanja chini upate zako tano tuendelee na mwendo wetu! SHOMA: Mwalimu samahani nimekosa! MWALIMU: Ukirudia tena utatembelea magoti yako! Haya ingia msitarini.(waliendelea na mchakamchaka wao mpaka waliporudi shuleni mida ya saa kumi na mbili asubuhi) MWALIMU ONESIMO: (baada ya kujipanga msitarini, anaanza kutoa matangazo ya jumla ili kila mwanafunzi ajiandae kwa hayo) kesho kila mwanafunzi aje na jembe, ukuni mmoja na dumu la maji! Oke? WANAFUNZI: Ndiyo mwalimu!
Transcript

Uhaini wa Baba

1

SEHEMU YA KWANZA.

(Shoma aliamuka asubuhi na mapema kama kawaida yake ili ajiandae kwenda shuleni,

hapakuwa na saa katika chumba chake, kwa hiyo alikuwa amezoea kuamuka kwa kukisia tu.

Lakini jana yake Shoma alifanya kazi nyingi hivyo alichoka na kujikuta anachelewa kuamka.

Mara alisikia sauti ya mwalimu na wanafunzi)

MWALIMU: Mchaka mchaka!!!

WANAFUNZI: Chinja!!

MWALIMU: Aliselema!!

WANAFUNZI: Alija!!

MWALIMU: Hiyuu hiyu!!

WANAFUNZI: Hiyu!!

MWALIMU: Haiiiiiii!!!

WANAFUNZI: Waaaaaaaaa!!!

MWALIMU: Chilemba iyuu chile!

WANAFUNZI: Oo nchilu!

(sauti hizo zilimsitua Shoma, maana haikuwa kawaida kukimbia asubuhi kama jeshi la mgambo,

mara alitoka nje ghafula baada ya kuvaa nguo kwa haraka na kukimbia kujiunga kundi la

wanafunzi hao, hapo hapo kabla hajajiunga alikutana na jicho la Mwalimu)

MWALIMU: Wee kifaranga! We!! Kwa nini umechelewa? Unafikiri hii shule ni ya bibi yako,

haraka jiandae kula bakora.

SHOMA: Mwalimu sikujua kwamba utaratibu umebadilika!(maana alikuwa na siku kama nne

hivi hajaenda shule)

MWALIMU: Utaratibu upi we! Hebu chanja chini upate zako tano tuendelee na mwendo wetu!

SHOMA: Mwalimu samahani nimekosa!

MWALIMU: Ukirudia tena utatembelea magoti yako! Haya ingia msitarini.(waliendelea na

mchakamchaka wao mpaka waliporudi shuleni mida ya saa kumi na mbili asubuhi)

MWALIMU ONESIMO: (baada ya kujipanga msitarini, anaanza kutoa matangazo ya jumla ili

kila mwanafunzi ajiandae kwa hayo) kesho kila mwanafunzi aje na jembe, ukuni mmoja na dumu

la maji! Oke?

WANAFUNZI: Ndiyo mwalimu!

Uhaini wa Baba

2

(Shoma akiwa anaendelea na masomo yake kama kawaida, lakini baba yake Mzee Mabula ana

mpango wa kumwachisha masomo ili aolewe, hapa ni nyumbani kwa mzee Maduhu)

MZEE MADUHU: Mimi nadhani rafiki yangu mimi na wewe tuwe kitu kimoja tu maana

tulikotoka ni mbali sana au unaonaje?

MZEE MABULA: Mimi na wewe hatuwezi kutengana hata kidogo kwa kuwa tulikotoka ni mbali

kweli.

MZEE MADUHU: Nataka niuimarishe zaidi urafiki wetu, hata watoto wetu wa kiume na wa kike

nao wawe marafiki!

MZEE MABULA: Hilo ni wazo la busara sana rafiki yangu, mimi nadhani tuwe tunafanya vikao

vya pamoja na watoto wetu ili wajue kabisa kwamba sisi hatuwezi kuachana.

MZEE MADUHU: achana na mambo ya vikao, Mwanangu Malemo anataka kuoa, nami naona

haitakuwa vyema kwamba aende mbali kutafuta wasichana, bali nataka aoe karibu na eneo hili tu!

Unajua rafiki yangu mabinti siku hizi wameharibika! Huyu bado!

MZEE MABULA: (huku akitikisa kichwa chake kwa kukubali) sawa kabisa rafiki yangu, ni kweli

kabisa siku hizi wasichana walio wengi hawafai kabisa, wengi wao wana ugonjwa huu mgeni

(anaendelea) siku hizi naona wasichana wengi wamekuwa wahuni kabisa, wanavaa visuluari vya

kubana, kama sio uhuni nini? Ole wako mwanao aoe kisichana kinachovaa suluri atakoma!

MZEE MADUHU: mmm! sasa unanisaidiaje (ananyamaza sekunde kadhaa) Sasa unaonaje kama

Malemo akimuoa Shoma?

MZEE MABULA: Wewe leta ng’ombe tu!

MZEE MADUHU: Ndugu yangu ng’ombe wote wamekufa kwa sababu ya ugonjwa wa madundo,

yaani kichaa cha ng”ombe kimewaramba karibia wote na wamebaki ng’ombe hamsini tu na

ndiyo maana nataka angalau kijana wangu aoe tu ili ninusuru mali yangu!

MZEE MABULA: Sasa kama ni hivyo, leta hao ng’ombe hamsini na uongeze pesa kidogo tu,

kama shilingi mia nane hivi!

MZEE MADUHU: Aaa! Rafiki yangu punguza bwana! Kwani mwanao yuko salama?

MZEE MABULA: Salama kivipi? Mwanangu hana ugonjwa wowote!

MZEE MADUHU: namaanisha bado ni bikra? Maana mwanangu nataka awe wa kwanza

kabisaaa!

MZEE MABULA: Aaa! Mimi nimemlinda mwanangu, yuko salama! Hakuna mwanaume

ambaye amewahi gusa hapo!

MZEE MADUHU: Basi mimi nitatoa ng’ombe hamsini na shilingi mia nane, lakini rafiki yangu

nenda kwanza ukamuulize Shoma kwani naogopa anaweza kuleta longolongo na kusababisha

matatizo katika familia yangu.

MZEE MABULA: Usiwe na shaka, mwanao ameshapata kitoto kichanga!

Uhaini wa Baba

3

MZEE MADUHU: Haya nitakuja kesho asubuhi na mapema, ila naomba nipate jibu la uhakika.

MZEE MABULA: Je leo haunywi?

MZEE MADUHU: Leo siwezi kwenda kwa Ng”wana Bukandile kwa sababu ananidai chupa

mbili za gongo, hivyo leo nimejipa likizo mwenyewe!

MZEE MABULA: Haya mzee wangu, kwa heri!

(Asubuhi na mapema mzee Maduhu alienda kwa mzee Mabula kwa ajili ya kumalizia

mazungumzo yao ya siku iliyopita. Hapa ni nyumbani kwa mzee Mabula)

NG”WANA BUGANGA: (Mzee Maduhu aingia) karibu sana shemeji yangu!

MZEE MADUHU: Habari yako shemeji!

MZEE MABULA: Karibu sana rafiki yangu! Mbona unaanza kusalimia wanawake kwanza!

Kwa kawaida tunaanza kusalimia wanaume kwanza!

MZEE MADUHU: Acha utani wako mzee wangu!

NG”WANA BUGANGA: Shemeji habari yako! Achana na huyu rafiki yako!

MZEE MADUHU: Namfahamu huyu jamaa!

NG”WANA BUGANGA: (huku akiwa anabeba ndoo) sasa shemeji ngoja niwaache kidogo

nifuate maji, si unajua kwamba maji katika mtaa wetu ni ya shida sana, kisima kinakauka mara

kwa mara hivyo ni lazima niwahi

MZEE MADUHU: haina taabu shem wewe wahi, utatukuta tu

MZEE MABULA: (aongea polepole) afadhali ameondoka ili tujadili ule mpango wetu

MZEE MADUHU: Ehe, niambie je ulimwambia Shoma na mama yake juu ya suala hili?

MZEE MABULA: Mimi nafikiri haina haja ya kumuuliza yeye nitakachokifanya ni kwamba,

nitaenda kwa mwalimu mkuu, bwana Onesimo na kumpa chochote ili akubali na asifuatilie

jambo hili.

MZEE MADUHU: Kumbe rafiki yangu una akili,( huku akitikisa kichwa chake) ndiyo maana

tulikuweka kuwa mwenyekiti wetu katika CCWT (Alimaanisha Chama Cha Walevi Tindabulligi)

kweli ukimwambia Shoma pengine hawezi kukubali jambo hili, hivyo cha kufanya kama

ulivyoamua wewe nyamaza tu na nenda kwa mwalimu mkuu ukaongee naye kama anakubali

ieleweke mara moja!! (mara Ng”wana Buganga aingia kwa haraka na hivyo mzee Maduhu

abadililisha mazungumzo yao)eeeee!!! Mimi naona kwamba leo twende tukanywe kiasi kidogo tu

maana mimi najisikia vibaya sana, jana niliharisha!!! (amkaribisha shemeji yake) karibu sana

shemeji yangu, naona umewahi sana, je leo hakukuwa na watu wengi? Au watu wamekuhurumia

kwa sababu una mgeni nyumbani kwako?

NG”WANA BUGANGA: Ni kawaida tu shemeji kama mtu akiwahi haina shida anapata!

Uhaini wa Baba

4

MZEE MADUHU: Shemeji mimi naondoka!!!

NG”WANA BUGANGA: Mbona mapema shem? Subiri tunataka tuwashe moto (alikuwa

anamjaribu tu ili aone kama atakubali au la)

MZEE MADUHU: Asante shemeji yangu, wewe pika tu kwa ajili ya wanao na mzee wako!!!

Nyumbani kwa mzee Mabula

MZEE MABULA: Ng”wana Buganga!

NG”WANA BUGANGA: abee! Sema baba angu! Maana wewe ndiye baba wa watoto wangu!

MZEE MABULA: Nataka Shoma aolewe na mtoto wa mzee Maduhu anayeitwa Malemo,

nadhani itakuwa vizuri sana!

NG”WANA BUGANDA: (huku akiwa amemkazia macho) Niondolee kichaa chako hapa! Mbona

unaleta utani ambao sio mzuri?

MZEE MABULA: Sio utani, na wakati wowote naweza kupokea ng”ombe na fedha zangu! Nami

ninakupa taarifa tu sio kwamba labda nakuuliza ushauri, maana tayari nimeshaamua kabisa!

NG”WANA BUGANGA: Nasema sikubaliani na jambo hili hata kidogo, kumbuka mume wangu

kwamba Shoma anasoma, je utawaambia nini waalimu? Utaiambia nini serikali? Shoma bado

mtoto wa serikali.

MZEE MABULA: Hilo sio suala lako, wewe mambo yote niachie mimi!

NG”WANA BUGANGA: Mimi sikubaliani kabisa na suala hili.

(Nyumbani kwa MZEE MADUHU, mambo sio mazuri, mama yake na Malemo yuko moto, hataki

mwanae aoe katika umri mdogo)

MZEE MADUHU: Ng”wana Makune, nataka Malemo aoe ndani ya wiki hii, maana hata wewe

unaona jinsi ng”ombe wanavyokufa, na ninadhani kwamba itakuwa ni bora kuweza kuzihidhi

kwa kumpatiea mtoto wetu mke! Na tayari nimeshapata mke kwa rafiki yangu yaani Shoma

ndiye atakuwa mke wa Malemo ndani ya juma hili!

NG”WANA MAKUNE: Je leo umelewa sana,? mbona huachi kunywa pombe zako? Kila

ukinywa unakuja na jipya, juzi ulisema unataka uuze lile shamba la eka mbili linalopakana na

shamba mzee Mabilika, leo unataka mtoto wetu aoe kwa Ng”wana Buganga!! Hivi mbona

unakuwa na tabia za namna hiyo!! Haya mimi, tabia hiyo siiwezi vinginevyo beba virago

uondoke kwangu!!!

MZEE MADUHU (Huku akiwa anachukua fimbo) hivi we mwanamke, hapa ni kwako? Nani

Uhaini wa Baba

5

kamleta mwenzake? Si ulinikuta na kila kitu kabisa katika faimilia hii na ulichopata wewe labda

ni hawa watoto wako kumi na mbili na huyu wa mwisho ndio nataka aoe, kumbuka wale wengine

wako makwao, tena ukome na ukomae tabia ya kunifokea mimi!

NG”WANA MAKUNE: (huku anakimbia) nakwambia nimekataa kabisa! Haiwezekani hata

kidogo!!

MZEE MADUHU: Haya tutaona mshindi ni nani

NG”WANA MAKUNE: Nakwambia ushindwa na ulegeee!!!!!

MZEE MADUHU: ulegee mwenyewe, mimi niko imara kama gogo!!

Nyumbani kwa mzee MABULA mambo yanaendelea kuwa magumu na mara baada ya Mzee

Mabula kuona kwamba haeleweki kwa mke wake, akaamua kwenda shuleni ambako Shoma

alikuwa anasoma ili kuongea na waalimu aone kama kuna uwezekano wa kumwachisha masomo!

Hinyo mabula aliondoka moja kwa moja mpaka shuleni huko NTOBO.

MZEE MABULA: Haloo!!!!!................hodiiiiii!!!!!!!!!!!!...................hodiiiiii!!!

MWALIMU 1: Karibu mzee, sema una shida gani? Au umekuja kuomba ruhusa kwa ajili ya

mwanao Shoma Mabula? Ruhusa za mara kwa mara hazitakiwi hata kidogo!! Do you hear mzee?

MZEE MABULA: Asante sana mwalimu kwa kuona kwamba ruhusa za mara kwa mara hazifai,

ni kweli na mimi naona hivyo, hivyo naomba leo Shoma apate ruhusa ya moja kwa moja asije

tena shuleni maana nimechoka sana kuja hapa mara kwa mara kuomba ruhusa! Una akili wewe

mwalimu!!!

MWALIMU 1: wewe mzee mwache mwanao aje kila siku shuleni, sasa wanajiandaa na mtihani

wa darasa la nne!! Who do you think you are?

MZEE MABULA: Unauliza ninayo masinki mangapi? Ninayo mawili, moja liko bafuni na

lingine liko jikoni, wayataka ya nini? Na kwa taarifa yako Shoma ameshaolewa tayari!!

MWALIMU 2: Huyu mzee kalewa? Hebu ondoka hapa sisi twende madarasani kufundisha au if

possible go to that office! Headteacher!!

MZEE MABULA: Lekanaga nu nene! Wapi? Ina maana kichwa changu hakina akili mpaka

niende kufundishwa? Wewe mwalimu namna gani? Do dont please you!!( Mara anaondoka na

kwenda katika ofisi ya mwalimu mkuu juu ya mwanae Shoma)

MR ONESIMO: Samahani mzee wangu kwa sasa nina majukumu mengi sana, nahitajika

wilayani kupeleka taarifa ya wanafunzi! Mimi naona kwamba uje tu nyumbani leo jioni!

MZEE MABULA: (wakatoka nje na kuanza kuongea kidogo) Asante sana mwalimu!! Na wewe

unaonekana kwamba utanisaidia sana hii shida yangu!!

Uhaini wa Baba

6

MR ONESIMO: Ninataka kusahau mzee, naomba wakati utakapokuja uje na mbuzi wawili na

shilingi elfu tano tu kwa ajili ya kusawazisha mambo yako!!

MZEE MABULA: hiyo haina shida kabisa! Na ndiyo maana wewe napenda utendaji wako wa

kazi!! Na ndiyo maana na serikali walikuweka kuwa mkuu wa shule hii

(Mzee Mabula aenda nyumbani kwenda kumweleza mke wake!! Sasa ,mambo yameiva Shoma

akiwa na umri wa miaka kumi na nne na kijana Malemo mwenye umri wa miaka kumi na

mitano!!! Hapa ni nyumbani kwa mzee Mabula)

MZEE MABULA: Sasa Mama Shoma mambo yameiva, nimeongea na mwalimu na tayari

ameshapokea mbuzi wawili na shilingi elfu tano leo jioni na sasa no problem kabisa

NG”WANA MAKUNE: hivi kumbe kweli ulikuwa umekusudia, haya amua mwenyewe lakini

mwanao atakuja akukumbuke baadaye

MZEE MABULA: Kunikumbuka ni lazima kwa maana mimi ni baba yake

NG”WANA BUGANGA: Mume wangu tafadhali fikiria sana juu ya jambo hii!! Wewe hukusoma

japo ulijifunza kiingereza kidogo kwa rafiki yako Wiliam na kiingereza chenyewe ni cha

kubabaisha babaisha tu, na mimi mkeo kabisa, sikukanyaga umande wa asubuhi, Siya naye

alibeba mimba akiwa darasa la saba, na hatuna mvulana wa kusoma hapa!! Nilitegemea angalau

Shoma amalize darasa la saba na aendelee sekondari, lakini sasa unamkatisha masomo yake!

Wewe mwanaume fikiri sana!(mara Ng”wana Bunganga anaanza kulia kwa sauti kubwa!! Na

wakati huo huo Shoma na Siya walikuwa ndani wakisikiliza maongezi yao)

SHOMA: mama kwa nini unalia?

NG”WANA BUGANGA: Mwanangu uolewe sasa? Nani atasoma katika mji huu?

SHOMA: Mimi mama bado!! Nani kakwambia habari hizo? Kwanza mimi bado mdogo na pia

bado ninasoma!! Wewe mama nyamaza usilie jamani!!!

SIYA: Na wewe mama umekosa kitu cha kulilia, wakati nilipobeba mimba hukutoa hata tone la

chozi, leo kusikia habari hizi ndiyo imekuwa kilio!! Mwache aolewe tu! Unaonekana

kumpendelea Shoma! Mwache!! Mwache!! Mwache tu aolewe!!!

NG”WANA BUGANGA: Baba yenu kasema ataolewa na Malemo mtoto wa mzee Maduhu na

tayari ameshapokea mahari ng”ombe hamsini na shilingi mia nane, na tayari Shoma ameshafutwa

jina lake pale shuleni!

SHOMA: Mimi mama hapana!!! Hapana! Hapana! Hapana! Hapana! Na tena sitaki kusikia

maneno hayo!!!

MZEE MABULA: Wewe mtoto nyamaza kimya! Unafikiri ulijizaa mwenyewe, nina haki ya

kukufanya nionavyo mimi!! Wewe (amnyoshea kidole) nyamaza shwiiiiii!!

(Mara sauti toka nje yasikika kama mtu anagonga, mzee Mabula amwambia mke wake asiseme

kwamba yupo,naye akimbia kujificha chumbani kwake)

Uhaini wa Baba

7

NG”WANA BUGANGA: Karibu, karibu, karibu sana shemeji!!!

MZEE MADUHU: habari za hapa shemeji yangu?

NG”WANA BUGANGA: Nzuri sana shem, habari za nyumbani kwenu shem

MZEE MADUHU: Rafiki yangu yupo

NG”WANA BUGANGA: Hayupo! Maana amesema kama akija mtu tumwambie kwamba mzee

Mabula hayupo

MZEE MADUHU: Mimi nilikuja tu kumuulizia kama ana nafasi twende tukaburudike mahali

Fulani, lakini kwa sababu hayupo, wacha niende zangu mwenyewe! Tena afadhali, kuvuja kwa

pakacha nafuu ya mchukuzi!!!

MZEE MABULA: (mara baada ya kusikia maneno hayo) nipooooo!!!!

MZEE MADUHU: mhola!, mhola!,mhola!, namhala!!!

MZEE MABULA: Ngoja nivae kofia mzee wangu!!

MZEE MADUHU: kofia yenyewe kama mwewe anataka kula watoto wa nguruwe!!!

MZEE MABULA: acha utani wako bwana!! Twende!

MZEE MADUHU: Shemeji kwa heri sisi tunaenda!!!

NG”WANA BUGANGA: haya shemeji yangu!!! Umurudishe mume wangu salama!!!!

(Mara wanaondoka kwa haraka!! Mara baada ya kuondoka, pale nyumba kwa mzee Mabula)

SEHEMU YA PILI

SIYA: Mama!! Mama!! Mtoto wangu anaumwa!! Kichwa chake kama cha kaa la moto!! Hebu

njoo umwone!!

NG”WANA BUGANGA: (analalamika sana) shida ya kijiji hiki ndiyo hii, sasa nimepata mjukuu,

wanataka kumkwangua ooo! Jamani Mungu wangu nifanyeje?

SIYA: Mama nipe shillingi mia tano niende hospital tu!!

NG”WANA BUGANGA: Chukua pale mezani, nenda haraka ila usikubali wamchome sindano!!

Sindano ni hatari sana kama kuna mkono wa mtu ujue!! Eee unajuaaaaaaa!!!!!!!!!

SIYA: Sawa mama nimeelewa!!

NG”WANA BUGANGA: mmmmmmmm!!!.........hebu rudi kidogo!

SIYA: (anageuka kwa haraka) mama nini tena??

NG”WANA BUGANGA: mimi naona tumpeleke kwa mganga wa kienyeji, yeye atajua ni nani

hasa aliyefanya jambo hili, huko hospitalini siamini kabisa!!

SIYA: Sawa mama, lakini kwanza tuanzie hospitalini!!!!

NG”WANA BUGANGA: mmmmmmm!!!!....au tumpeleke kwenye maombi katika kanisa la

Bupiji naamini kabisa kwamba Yule pasta ana upako wa ajabu na ninajua kabisa kwamba mara tu

atakapoweka mikono juu ya mtoto huyu atapona!!

Uhaini wa Baba

8

SIYA: haya mama twende kanisani pamoja na wewe!

(Mara waondoka na kwenda kanisani na kumkuta mchungaji wa kanisa la Bupiji akiwa ameketi

kusubiri watu walio na shida mbalimbali ikiwa ni pamoja na wagonjwa.)

MCHUNGAJI: Karibuni wapendwa katika Bwana! Bwana Yesu asifiwe!

NG”WANA BUGANGA,SHOMA,SIYA: Ameeeeen!!!! (Siya akamwangalia pasta, kisha

akapaza sauti)pasta sisi tuna tatizo mtoto wetu ni mganjwa sana!!

MCHUNGAJI: anaumwa nini?

SIYA: Amechemka sana kama kaa la moto!!

MCHUNGAJI: Amini Mungu atamponya tu!!!

NG”WANA BUGANGA, SHOMA, SIYA: tunaamini baba mchungaji!

MCHUNGAJI: Twendeni madhabahuni, maana hapo ndipo palipo na upako! (mara wanaingia

kwa haraka ndani ya kanisa! Madhabahu imepambwa kwa vitambaa vya rangi nyekundu na

nyeupe! Mbele yake kuna msalaba picha ya mtu amebeba kondoo! mbele yake kuna maji ambayo

yanasemekana kuwa ni maji ya baraka na yanatumika kwa uponyaji! Nao wote wanaingia!, mara

mchungaji akamaka) Msishangae shangae hapa!

SIYA: Sawa baba mchungaji!!!

MCHUNGAJI: Je mnamwamini Yesu ninyi nyote?

SIYA&SHOMA: Ndiyo baba mchungaji!!!

MCHUNGAJI: fumbeni macho nimwombee mtoto huyu!! (wakati huo macho yake ameyaelekeza

juu, akaanza kusema maneno ambayo yalikuwa hayaeleweki kwa sauti kubwa, alifanya hivyo kwa

muda wa dakika kumi na mbili, lakini mtoto alikuwa bado hajapona) mmmmh! Yes Lord!

Ooyaah! Mtoto anaitwa nani?

SIYA: anaitwa Buganga (jina la babu yake kizaa mama)

MCHUNGAJI: aaaaa! Ndiyo maana hajapona bado! Sogea hata! (anaonekana amekasirika

sana) jina gani hili? Majina mengine sio mazuri, yana roho za mababu na mabibi, jina linaweza

kusababisha magonjwa katika maisha ya mtu yeyote, maana majina mengine yametambikiwa na

wazee wetu walikuwa na dini za kipagani, dini za kijinga, kipumbavu, kishetani kabisa! hivyo

jina hili lazima abadilishwe. Haya chagueni kati ya majina haya: Emanuel, Ezekiel, Daudi,

Daniel na Mathayo.

SIYA: (Kwa sauti kuu) Emanuel!!

MCHUNGAJI: hapo sawa! Achana na majina ya mababu (atwaa maji yale ya uponyaji na kuanza

kumnyunyizia mtoto huyo huku akitoa sauti kubwa) Baba ninakushukuru kwa ajili ya watu hawa!

Naomba umponye mtoto wao sasa hivi! Mungu umesema katika neno lako kwamba kwa kupigwa

kwa Yesu sisi tumepona, kwa hiyo Mungu naomba urejeshe uponyaji wako mahali hapa katika

Uhaini wa Baba

9

jina takatifu la Yesu! Semeni wote amen!!!!!!

SIYA, NG”WANA BUGANGA&SHOMA: Ameeeeeni!!!

SIYA: Lakini mchungaji bado hajapona mwanangu nifanyaje? Naona hakuna mabadiliko kabisa

tangu ulivyoanza kuomba mpaka sasa bado tu hali inazidi kuwa mbaya!!

MCHUNGAJI: unaonekana una upungufu wa imani!

SIYA: ninayo imani mchungaji! Tatizo ni hali ya mwanangu kuwa mbaya zaidi! Tatizo ni nini

baba mchungaji?

MCHUNGAJI: (anakuwa kama amepagawa na mashetani) Mtoto wako ana mapepo elfu kumi

na mbili na mia mbili na hamsini. Mapepo haya amepewa na wachawi wa hapo kijijini kwenu!

Kinachotakiwa hapa ni kwamba toeni sadaka kwanza shilingi elfu hamsini nami nitafunga kwa

maombi kwa ajili ya mtoto wenu na pia nitakuja mwenyewe nyumbani kwenu ili nikague vizuri,

maana Mungu ananiambia kwamba kuna vitu ambavyo wachawi wameweka kwenu na hivyo

lazima nije mwenyewe kuomba hapo hapo! Na pia nahitaji kuacha upako katika nyumba yenu ili

kuwe na baraka tele!!! Na kama mapepo haya hayaondolewi, huyu mtoto atakufa ndani ya siku

mbili!! Hili ni neno la kinabiii! Msiogope kwani mimi ni mtume na nabii na pia ni mchungaji!!

Sawa?

SIYA: Sawa baba mchungaji, lakini sasa hatuna hela tuna shilingi mia tano tu ambayo ndiyo

tulitaka kumpeleka mtoto huyu hospitalini ili akatibiwe lakini mama alishauri tuje kwako

mchungaji, tusaidie watu wako!!

MCHUNGAJI: Msijaribu kabisa kumpeleka huko, kwani mapepo huwezi kuyapa asprini! Ni

hatari sana wanangu! Cha muhimu mimi naomba sasa hivi tu hiyo shilingi mia tano na ile

iliyobakia mtaleta baada ya kupokea muujiza wenu!! Amini mimi ni mtumishi wa Mungu aliye

juu! Msiwaamini madaktari hata kidogo kwani wale ni waongo na hawana uhusiano wa karibu na

Mungu!

SIYA: (anaongea polepole) Mbona baba mchungaji sikuelewi, nina wasi wasi na wewe!

SHOMA: usisema maneno hayo kwa mtumishi wa Mungu!!! Atakulaani!

NG”WANA BUGANGA: (amwambia Siya) wewe humwogopi hata Mungu jamani! Huyu ni

mtume na nabii kabisa! Tayari ameshatabiri juu ya mtoto wako na sasa unataka kuleta tena

maneno gani hayo?

SIYA: (Kwa sauti kubwa) Mimi simwamini kama kweli ni mtumishi wa Mungu! Mwanangu hana

mapepo hata kidogo! Labda malaria imepanda tu, mie naenda hospital!!! Sawaaa!!! (mara

aondoka kanisani kwa haraka! Shoma naye anafuata kwa nyuma kwa kutaka kumzuia asiondoke,

mama yake ameshika tama na kushangaa kwa kitendo ambacho mwanae Siya amekifanya kwa

huyo mtumishi wa Mungu baadaye wote waondoka..Shoma na mama yake wanarudi nyumbani

lakini Siya anaenda moja kwa moja hospitalini. Huko Hospitalini anakutana na daktari)

Uhaini wa Baba

10

DAKTARI: Hali hii imeanza lini?

SIYA: Jana!!

DAKTARI: Mbona hamkuja jana hiyo hiyo?

SIYA: Tulimpeleka kwenye maombi!

DAKTARI: sasa imekuwaje ukaja huku?

SIYA: sijaona mafanikio!

DAKTARI:((achukua vipimo kwa ajili ya mtoto na kwenda maabara na mara baada ya kurudi)

okay, mtoto wako ana malaria tatu, sasa ilikuwa imepanda! Umefanya jambo la maana kuwahi

kuja hapa! Hivyo nitakupa hivi vidonge, mpe usiku kipande hiki na asubuhi mpe kipande

kitakachobakia! Na kama unaona hali bado sio nzuri basi umlete tena! Lakini najua atapona tu!

SIYA: asante sana daktari! Je nadaiwa shilingi ngapi?

DAKTARI: hospitali hii inatoa huduma bure kwa watoto chini ya miaka mitano hivyo usiwe na

wasiwasi nenda tu!!

SIYA: Basi daktari pokea hii zawadi ya shilingi mia tano!!

DAKTARI: Tumia tu hiyo hela, najua umetoka mbali sana kilometa ishirini sio karibu, hivyo

tumia! Na asante kwa moyo wa kushukuru!

SIYA: Haya asante sana daktari! Na kwa heri!!

*** *** ***

(Siya alirudi nyumbani akiwa amechoka sana lakini alikuwa na furaha kwa sababu ya mtoto

wake amepona! Na mara alipofika nyumbani alikuta mazungumzo juu ya ndoa ya Shoma huku

baba yake mzee Mabula akitaka ifanyike kwa haraka sana)

MZEE MABULA: Na wewe mwanamke nimeshagundua mpango wako! Unataka mwanangu

abebe mimba kama huyu dada yake na kisha sijui utakuja useme nini? Kipindi kile Siya

alipobeba mimba sikusema neno lolote, lakini kumbuka safari hii tutamaliza vibaya we

mwanamke! Na hili ndilo tatizo la wanawake ukiwaendekeza sana wanakudharau. Inaonekana

kwamba huna adabu hata kidogo kumbishia mumeo!! Au hata mama yako hakukufundisha hili?

Je hata mnakosali huko kwa mchungaji wenu hamfundishwi kuwatii waume zetu? Maana

nilikuruhusu uende kanisani ili angalau uweze kunitii!

NG”WANA BUGANGA: Haya mimi nasema tu kwamba fanya ulivyokusudia ila utakumbana na

mkono wa serikali

MZEE MABULA: kelele za panzi hazimzuii ng”ombe kula majani! Kwa hiyo unataka kunitisha?

Niondolee balaa hilo we mwanamke! Niondolee mkosi wako we mwanamke! Kwanza nikiamua

nawaponda wote na ninawafukuza hapa kwangu? Unasikiaaaa eee? Ukinichosa sana naoa

Uhaini wa Baba

11

mwanamke mwingine!

NG”WANA BUGANGA: Ondoka mwenyewe uniachie wanangu!!! (Baada ya mazungumzo hayo,

mara mzee maduhu anaingia ndani)

MZEE MADUHU: Hodi! Hodi! Hodi!

NG”WANA BUGANGA: Karibu shemeji mpaka ndani, habari za siku nyingi shem.

MZEE MADUHU: Nzuri kiasi, maana familia yangu ilikumbwa na malaria kali sana lakini sasa

wanaendelea vizuri, vipi hapa?

NG”WANA BUGANGA: Pole sana shemeji hata sisi ilitukumba hiyo malaria, lakini sasa naona

mtoto amepona kabisa!

MZEE MABULA: Karibu rafiki yangu!!

MZEE MADUHU: Je uko tayari?

MZEE MABULA: Mimi niko okee! Haya twende zenu, unakumbuka kwamba leo ni zamu yako

kununua eeeehh!!

MZEE MADUHU: Haina shida! (huku akimwangalia Ng’wana Buganga) Shemeji kwa heri!!!

Mara baada ya kuondoka kwao, Ng”wana Buganga anabuni mbinu mpya ya kumnusuru Shoma

asiolewe)

NG”WANA BUGANGA: Shoma!! Shomaaaaaa!!

SHOMA: Abeee! Mama ninakuja! (huku anakimbia haraka sana)

NG”WANA BUGANGA: Uikuwa wapi? Mbona nakuita mara zote hizi kimya tu!

SHOMA: Nilikuwa naosha vyombo!

NG”WANA BUGANGA: Sasa nataka nikwambie jambo la muhimu sana na lazima ulifanye.

Sawa?

SHOMA: sawa mama nitafanya!!

NG”WANA BUGANGA: Leo baba yako akirrudi nitamwambia unaumwa sana, huwezi hata

kuongea, mimi nitakulinda mwanangu maana sitaki kwamba uolewe, nataka usome mwanangu!

Sawa mwanangu?

SHOMA: Na kama baba akija na kunishika shika na kugundua kwamba mimi siumwi si itakuwa

shida mama?

NG”WANA BUGANGA: Maliza wasiwasi, hawezi kukushika shika, desturi zetu haziruhusu

mwanaume kumshika binti yake!!

SHOMA: Kweli mama?

NG”WANA BUGANGA: Au kama vipi nitamwambia kwamba joto lako limepanda na uko uchi

hivyo hataweza kuja na kukuangalia hata kidogo

SHOMA: Akisema anipeleke hospitali nitasemaje?

Uhaini wa Baba

12

NG”WANA BUGANGA: Hana akili hiyo ya kukupeleka hospital!

SHOMA: Akitaka kunipeleka kwenye maombi kwa mchungaji itakuwaje?

NG”WANA BUGANGA: Usiwe na wasiwasi leo hii nitaenda kwa mganga wa kienyeji wa pale

Malwilo, nitamweleza kila kitu ili kama akienda mambo yasijichanganye na ninajua kwamba

hawa waganga wa kienyeji ni waongo tu, hivyo nitampa chochote! Na pia nitaenda kwa

mchungaji wa kanisa la Bupiji sijui wengine wanaliita Bupanga ili kama akitaka kukupeleka

huko akagonge mwamba, si unajua tena kwamba siku hizi hata haya makanisa wachungaji wake

wanaganga njaa tu, wewe unadhani Yule ni mchungaji kweli? Kwani kuna tofauti gani kati yake

na mganga wa kienyeji? Siku ile tulienda katuambia habari za wachawi!! Wewe huoni kwamba

hawa watu wana uhusiano wa karibu sana?

SHOMA:((Huku akiwa na wasiwasi kabisa) haya mama lakini mmmmmmhhh!!!

(Ng”wana Buganga aondoka na kwenda moja kwa moja kwa mganga wa kienyeji na kwa

mchungaji wa kanisa la be open)

MGANGA: uuuu! Waaa! Karibu mama wewe ndiye uliyenisumbua usiku kucha sijalala, je

unataka nini mama?

NG”WANA BUGANGA: Kuna mtoto ataletwa hapa anaitwa Shoma, baba yake anaitwa mzee

Mabula na mimi ni mama yake naitwa Ng”wana Buganga, sasa wakija waambie haya!!

MGANGA: Ehe wakija niwaambiaje:

NG”WANA BUGANGA: Waambie Shoma ni mgojwa sana, na anatakiwa aondolewe kijijini

kwenu na apelekwe katika kijiji cha Ntobo huko wazazi wake hawaruhusiwi kwenda kumuona

kwa muda wa miaka minane Katika eneo hili kuna wachawi ambao wanataka kumchukua mtoto

wenu.

MGANGA: kama ni hivyo tu! Nitawaongezea na ya kwangu!!

NG”WANA BUGANGA: wasisitize wasikose kumpeleka!

MGANGA: wacha niwaangalie kwamba wako wako wapi? (mara akaa chini na kuanza kutoa

maneno yasiyoeleweka) ooooo!!uuuuu!!!s shwiiiiiiiiiiiiii!!!!!!(mara akaanza kuimba wimbo)

ikoba ng’ana lihaile bujingi jingi, ikoba ng’ana lihaile bujingi jingi, ilelo iyi nalya!

NG”WANA BUGANGA: Kwa heri! (aenda moja kwa moja kwa mchungaji na kumweleza

maneno yale yale aliyomwambia mganga wa kienyeji)

Uhaini wa Baba

13

SEHEMU YA TATU

(Huko nyumbani kwa Mzee Mabula kazi ipo sasa)

MZEE MABULA: Ng”wana Bugangaaaaaaa!!!!!!!!!!!

NG”WANA BUGANGA: Sema baba!!

MZEE MABULA: Shoma yuko wapi? Maana kesho Malemo anatarajia kuja hapa kuchukua mke

wake?

NG”WANA BUGANGA: Samahani! Nilitaka kukuelezea kwamba Shoma ni mgonjwa sana na

hawezi kutembea wala kuongea! Mwili wake ni wa moto kama nini yaani!!

MZEE MABULA: Kwa nini hamkuniambia asubuhi! Ameugua tangu lini? Huu naona ni wivu

wa watu wa Tindabuligi tu. Aaaahhhhhh!!!!!!

NG”WANA BUGANGA: Lini mume wangu ningekwambia habari za mtoto huyu? Kila siku

unaamka kama mtu kaacha kamba mtoni, wewe na pombe, pombe na wewe ningekuona wapi

ukiwa na akili timamu nikwambie?

MZEE MABULA: Umeshampeleka kwa mganga?

NG”WANA BUGANGA: Lini nimpeleke? Nimeamkia kufuata maji, baadaye nikaenda kuokota

kuni na sasa tayari ni jioni! Labda nakushauri tumpeleke hospitali huko Sakasaka?

MZEE MABULA: OO mwanangu atafia njiani Sakasaka ni mbali sana, na hata hivyo

haiwezekani kabisa kumpeleka hospitali kwa sababu najua hawa ni wachawi tu!! Hebu mleteni

hapa nimuone kwanza!!

NG”WANA BUGANGA: Joto limepanda sana, hivyo nimemvulisha nguo zote ili angalau aweze

kupoa.

MZEE MABULA: Oo jamani wivu wa namna gani huu majirani zangu, kusikia tu kwamba

nimepata ng”ombe hamsini imekuwa kero, jamani hebu mwacheni mwanangu! Najua kwamba

mtu wa mbali hawezi kuja kumroga mwanangu.

NG”WANA BUGANGA: Wacha tuone leo anaendeleaje, na kama hali hii ikiendelea basi

tutampeleka hosptalini

MZEE MABULA: Sitaki kabisa kusikia habari za kwenda hospital,na leo hii naenda kwa mganga

ili kwenda kumwangalia ni nani huyu mchawi mbaya sana!!

NG”WANA BUGANGA: Na mimi ni lazima tuongozane pamoja, maana hali yake ni mbaya sana

kwa sasa!!

MZEE MABULA: Wewe mwanamke sitaki kabisa kuona uso wako huko, maana nyie

wanawake ndio wachawi wakubwa hapa kijijini. Na kama mtoto wangu akifa, naanza na wewe

kabla sijaita sungusungu kuwashambulia wanawake vikongwe wote hapa kijijini!

Uhaini wa Baba

14

NG”WANA BUGANGA: Sawa baba nenda na yule unayetaka kwenda naye! Au kamwambie

rafiki yako mzee Maduhu akusindikize!

MZEE MABULA: Siya, Siyaaaaa!!

SIYA: abeeee!

MZEE MABULA: Mchukue Shoma polepole kwenye baiskeli na tuongozane kwa mganga wa

pale Malwilo.

SIYA: Ndiyo baba ngoja nimwamshe!! (aita kwa sauti ya chini) Shoma inuka twende (Shoma

ainuka kwa shida kwa ajili ya uchovu kwa kuwa anajua kabisa kwamba yeye ni mzima lakini kwa

sasa anajisingizia tu na anajiuliza sana kwamba itakuwaje kama baba yake atagundua mchezo

wao)

MZEE MABULA: Mnaongea nini humo, hebu fanyeni harakaaaa!!!

(Basi wakachukua baisikeli ambayo haikuwa hata na pedali, wakaanza kusukuma, huku Shoma

amekaa kwenye kiti cha nyuma kwa ulegevu, wanaenda moja kwa moja mpaka Malwilo, mji ulio

umbali wa kilometa kumi toka kwao nao wakamkuta mganga wa kienyeji akiwasubiri kwa hamu

sana)

***kwa mganga***

MGANGA: Wewe umenisumbua sana usiku wa leo, sikuweza kulala kabisa!! Kabla ya mambo

yote toa kwanza makanyagio!!

MZEE MABULA: Makanyagio ni nini?

MGANGA: Makanyagio maana yake ni kwamba ukifika kwangu, ile tu kukannyaga eneo la

kiwanja changu unahitaji kutoa pesa! Na hiyo ni tofauti na huduma utakayopewa ambayo itabidi

uilipie

MZEE MABULA: Kiasi gani haya makanyagio?

MGANGA: Ni shilingi mia mbili bila chenji!

MZEE MABULA:(anachukua hela ambayo alikuwa ameipata baada ya kuuza tumbaku, nayo

ilikuwa imeng”ang”ania kwenye mfuko wa nyuma wa suluari yake) haya hii hapa!!

MGANGA: Kaa chiniiii!!! Uwiiiiiii shwaaaa!!weeee!! wewe ni mzee Mabula, na mtoto wako ni

Siya na Shoma lakini bado sijaambiwa jina la mkeo! Ngoja kidogo

MZEE MABULA: (anaitikia kwa matumaini kwa maana mganga tayari ameshajua majina yao

na ni kweli ni majina yao, hivyo tayari ameshaweka imani yake kwa mganga Yule) ehe!!!!

MGANGA: weeeeee!!swiiiiiii!!! shuuuuu!!!! Ruuuuuu!!!! Zwiiiiiii!!! Bila shaka mkeo anaitwa

Ng”wana Buganga na huyu binti yako anayeumwa anaitwa Shoma!!

MZEE MABULA: Ekizakitili!!!!!!!!

MGANGA: Nakuuliza ni kweli hizi habari nilizokwambia mzee wangu!! Mbona mgumu

Uhaini wa Baba

15

kuelewa.

MZEE MABULA:Samahani nilidhani unajua lugha zote, mie tayari nshakuwambia kwamba ni

kweli.

MGANGA: Swiiiii!!!braaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!shweeeeeeeeeee!!!!...shika kisu hiki mzee

wangu!!

MZEE MABULA: Ni cha moto mzee wangu

MGANGA: Vumilia tu!

MZEE MABULA: aaaaa…mimi ntakiachia tuone maana naungua

mwenzio…iiiiiiiiiiiiiiishiiiiiiiiiii…………

MGANGA: Ukiona kisu ni cha moto ujue mambo yako ni hatarii sana lakini ni afadhali umekuja

mapema ili upate suluhisho la mambo yako.

MZEE MABULA: Sawa mzee wangu!

MGANGA: Sasa sikiliza! Mtoto huyu ni mgonjwa kwelikweli, lakini mababu zangu

wananiambia kwamba Shoma apelekwe akaishi na bibi yake huko Ntobo kwa muda

usiopungua miaka minane!! Wewe huruhusiwi kumpeleka kule, wala mama yake labda angalau

huyu mwanao binti mrembo anaweza kumsindikiza naye anahitaji kurudi haraka baaada ya

kumfikisha!!

MZEE MABULA: Una maana gani kusema binti mrembo we mganga? Huyu ni mwanangu wa

kuzaa! Usinivunjie heshima.

MGANGA: Samahani mzee wangu, sisi tulishazoea mabinti wengi wanakuja hapa wanatafuta

kuoelewa, wengine wanataka wapendwe na wake waume zao, lakini wale ambao huwa ninafaidi

ni wale wanaokuja anataka kupata mtoto, wa namna hiyo lazima nilale naye tu ili kumjaribu

kama anaweza kuzaa au la, hayo ndiyo malipo yetu!

MZEE MABULA: Achana na maneno hayo! Hebu sema kweli, Eeee miaka minane?

MGANGA: wakati ninapomalizia kusema maneno haya wewe unatakiwa uwe umeshatema hela

hapo chini na uende nyumbani! Mwache huyu binti ampeleke Shoma waende Ntoba! Ni hatari

mzee wangu, angalia utazika mwanao hivi hivi!!!

MZEE MABULA: Kabla sijatoa hela nataka kujua ni nani amemroga mwanangu!! Maana

haiwezekani kabisa kuchomeana utambi hivi hivi, niko tayari usiku huu kwenda kumaliza watu

mie mwana wa Masele!!

MGANGA: Kikulacho ki nguoni mwako mzee! Okoa maisha ya mwanao, ondoka upesi

MZEE MABULA: Jina jingine anaitwa nani?

MGANGA: umdhaniaye siye ndiye!!

MZEE MABULA: Loo!!! Hayo majina hakuna hata moja kijijini kwetu, wacha kwanza niokoe

maisha ya mwanangu!! Haya kwa heri

Uhaini wa Baba

16

MGANGA: Mzee usiangalie kulia wala kushoto wala nyuma angalia mbele tu, na hii ni lazima

iwe siri watu wakijua watamfuata huko!

MZEE MABULA: Sawaaaaaaaaaaa!!!

Uhaini wa Baba

17

SEHEMU YA NNE

Aenda moja kwa moja nyumbani na kumweleza mke wake na Siya na Shoma walienda Ntoba.

Mama yake aanza mpango wa kumtafutia shule

** ** **

(Mzee Mabula akiwa nyumbani kwake baada ya kutoka kwa mganga wa kienyeji)

NG”WANA BUGANGA: Ehe binti yako anaendeleaje huko?

MZEE MABULA: (ana huzuni) atibiwe wapi!! Mtoto karogwa na nimeambiwa ni lazima

nimpeleke kwa bibi yake kule Ntobo, na kule haruhusiwi mtu yeyote kwenda huko!

NG”WANA BUGANGA: Mwanangu jamani wamemroga! Uuuu, mganga kasema nani kamroga?

(akifurahi moyoni mwake)

MZEE MABULA: Jina lake ni refu sana siwezi kulitaja zima zima ngoja kwanza nikumbuke

kidogo.

NG”WANA BUGANGA: Hebu mseme huyo mpuuzi.

MZEE MABULA: Sasa namkumbuka, eee….jina lake niii…Kikulaaa..nimeshau, lakini nguoni

ipo.

NG”WANA BUGANGA: mmmmh! Muuza nguo yule aweza kuwa ni mchawi kweli! Mimi

siamini kabisa, maana nilidhani ni wale mabibi kizee wenye macho mekundu.

MZEE MABULA: Achana nalo hilo wala usilifuatilie hata kidogo!

(Baada ya siku kadha wa kadha kupita, Mzee Maduhu alimtembelea rafiki yake ili kujua ni lini

hasa mwanae Malemo aende akachukue mke wake)

MZEE MADUHU: hodi mpaka ndani!

MZEE MABULA: Karibu mpaka ndani, hapa ni kwako.

NG”WANA BUGANGA: (huku akiona aibu kumwita shemeji) karibu sana sheeemmmeji yangu.

MZEE MADUHU: Habari za hapa?

MZEE MABULA&N.BUGANGA: Nzuri kiasi

MZEE MADUHU: kwa nini nzuri kiasi? Je mnaumwa?

MZEE MABULA: (akumbuka maneno ya mganga wa kienyeji kwamba hatakiwi kumwambia

mtu yeyote habari ya familia yao) huo ni utani tu rafiki yangu sisi ni wazima kabisa, ila tatizo ni

kwamba kulikuwa na mlevi alianguka na kufa jana katika maeneo haya ya karibu na kwetu, sasa

mimi nilienda kutoa ushahidi wa upatikanaji wa maiti yake, lakini hata hivyo nimeshayamaliza

kabisa!

MZEE MADUHU: habari za ukimya?

MZEE MABULA: Twende nje tukaongee kwa maana si vizuri kabisa kuongea mambo ya

Uhaini wa Baba

18

kikubwa mbele ya wanawake!

MZEE MADUHU: Ni kweli bwana, maana hawa huwa hawana siri kabisa! Hata kineno kidogo

mpaka kisambazwe kwa majirani wote!

MZEE MABULA: Umelijua leo hili?

MZEE MADUHU: Ni tangu zamani maana hata Ng”wana Makune huwa sina tabia ya

kumwambia maneno yangu ya siri maana hawa ni hatari sana! Mwanamke, mwanamke hana siri

kabisa!

MZEE MABULA: (wakiwa pale nje ya mazungumzo yao yaliendelea)Sasa rafiki yangu nataka

nikuume sikio.

MZEE MADUHU: Nena rafiki yangu!

MZEE MABULA: Hii ni siri ambayo wewe hautakiwi hata kumwambia mkeo, maana hata mke

wangu hajui kabisa na ndiyo maaana nilikwambi tutoke nje.

MZEE MADUHU: usiwe na wasiwasi wewe sema tu, mimi sio mwanamke bwanaaa!!!!!

MZEE MABULA: Aisee mwanangu Shoma wamemroga kabisa, ni mgonjwa sana na hapa

nyumbani hayupo, yuko mahala Fulani

MZEE MADUHU:(huku akimkazia macho) sema kweli!!!!

MZEE MABULA: aliugua tangu mwezi uliopita lakini sasa sijui anaendeleaje.

MZEE MADUHU: (akigongagonga chini kwa fimbo yake) Sasa ng”ombe zangu inakuwaje?

MZEE MABULA: yaani wewe rafiki yangu unafikiri juu ya ng”ombe tu, badala ya kumhurumia

mwanangu? Mwanangu amekanyaga mizizi mwenzio!!

MZEE MADUHU: Nani kamtega?

MZEE MABULA: kuna mtu anaitwa eti nguoni!

MZEE MADUHU: wa wapi mshenzi huyu?

MZEE MABULA: nimejaribu kufuatilia kwa makini jina hili sijalipata katika kijiji chetu, labda

ni wa kutoka maeneo ya mbali kidogo.

MZEE MADUHU: Pole rafiki yangu lakini itakuwaje juu ya ndoa?

MZEE MABULA: Pale sina la kusema kabisa, labda nikusikilize wewe una ushauri gani juu ya

jambo hili.

MZEE MADUHU: mie naona jambo hili tuahirishe tu

MZEE MABULA: Daa! Mungu wangu, nimenyang”anywa tonge mdomoni! Mungu aepushie

mbali balaa hili katika familia yangu! (huku akitetemeka)Kwanza Siya alipata ujauzito akiwa

masomoni hawezi hata kuolewa, na Shoma naye ametaka kuolewa wamemlisha majani ya kunde,

je mimi nifanyeje jamani!

MZEE MADUHU: sasa rafiki yangu naona kwanza nikuache ufikiri vizuri juu ya suala hili, mimi

naona ni zito kidogo! Jaribu kujadili na mke wako japo sio vizuri sana kuwauliza wanawake

Uhaini wa Baba

19

lakini wakati mwingine ni watu wazuri kwa ushauri.

MZEE MABULA: Asante rafiki yangu tutaonana kesho!! Kumbuka ndugu yangu kwamba hii ni

siri, usijaribu kabisa kumwambia mtu yeyote juu ya hili!

Uhaini wa Baba

20

SEHEMU YA MWISHO

(sehemu hii Shoma akiwa kule Ntobo kwa bibi yake, mama yake alimtafutia shule ya msingi

akaendelea na masomo yake vizuri, alifaulu kuanzia darasa la nne mpaka darasa la saba

aliendelea kuongoza namba moja, matokeo ya darasa la saba yalipotoka alifaulu kwenda

sekondari, waalimu wakampenda, wanakijiji wakazidi kunena juu yake,Shoma akachaguliwa

shule ya Bwilu girls, shoma akiwa shuleni)

MKUU WA SHULE: Wewe ni mwanafunzi mzuri sana, unajitahidi kimasomo. Napenda

uendelee hivyo bila kuacha! Conglatulation!

SHOMA: Asante mwalimu wangu!

MKUU WA SHULE: kumbuka shule yetu ni nzuri sana lakini pia kuna sheria za kufuata, kama

ukikosa sheria mja tu, utafukuzwa shule

SHOMA: Sawa mwalimu, Mungu anisaidie tu.

MKUU WA SHULE: Take care!

SHOMA: Yes sir.

MKUU WA SHULE: Make sure that you score above 90%

SHOMA: Yes sir

MKUU WA SHULE: Shomaa! Please I think rembeeeeee…….ok! just go to the dormitory!

SHOMA: Yes sir

(Baada ya kumaliza kidato cha kwanza, Shoma alifaulu vizuri sana,wakati wa likizo alikosa nauli,

na aliamua kwenda kukaa kwa mchungaji wa kanisa ambao alikuwa akishiriki alipokuwa

shuleni, maana mama mchungaji alionekana kumpenda sana Shoma, hivyo aliamua kukaa hapo

kwa muda wote wa likizo, lakini kwa bahati mbaya sana hata pale kwa mchungaji maisha

yalikuwa magumu. Kila siku mchungaji alilalamika)

MCHUNGAJI JERE: (Akiwaambia familia yake, na siya akiwa amekaa hapo) Bwana Yesu

Asifiwe sana! Namshukuru Mungu kwa ajili ya familia yangu, kwa sababu ameendelea kutulinda

na kutupa hekima na maarifa, na sasa ninashukuru kwa sababu familia yetu tumeongezeka,

Shoma naye yupo hapa, binti mzuri, mwimbaji mzuri na mcha Mungu! Hili ni jambo la kujivunia!

FAMILIA: Ameni!

MCHUNGAJI JERE: Mnajua namna maisha yanavyozidi kuwa magumu, sioni mwelekeo wa

kupata fedha! Watu siku hizi wamekuwa wajanja hata kutoa sadaka hawatoi, wiki iliyopita

sadaka ilikuwa shilingi mia mbili tu, sasa mia mbili tutaifanyia kazi gani? Mimi naona tuanze

kugawana majukumu ili mambo yaende vizuri. Biblia inasema asiyefanya kazi na asile. Hivyo

leo naenda kugawa kazi kwa kila mmoja wenu,

FAMILIA: Haya Baba Mchungaji!

MCHUNGAJI JERE: Wewe mama mchungaji uanze biashara ya unga! Maana yupo mchungaji

Uhaini wa Baba

21

mwenzangu, mke wake ameanza kuuza tu unga muda mfupi tu sasa wana prado. Na ukiwakuta

kanisani wanasema Mungu amewabariki sana tu!

MAMA MCHUNGAJI: Mmm! Baba huu unga wa Azam au?

MCHUNGAJI JERE: Wewe bado upo gizani, tuendeleee! Magdalene!

MAGDALENE: Bee baba

MCHUNGAJI: Wewe kazi yako ni kutafuta vijana wa kiume wenye hela, wakikutongoza

usiwakatae, ila hakikisha wamekuhonga hela nyingi! Ili mradi familia iishi. Hata biblia inasema

kila mmoja atakula kwa jasho lake mwenyewe, hilo ndilo jasho lako

MAGDALENE: Sawa baba!

MCHUNGAJI JERE: Zamu yaaaa!!( anajifanya kama amesahau jina) Shoma! Wewe Shoma,

kazi yako inafanana fanana na ya Magdalena ila wewe utafute wanaume wakubwa wakubwa ,

wenye hela zao! Hao ndio watakuwa nguzo kwa familia hii! Hapo mambo yataenda tu!

SHOMA: Nikiwapata huko nje niwaambie unawaita?

MCHUNGAJI JERE: Hapana, wewe malizana nao huko huko! (huku akiwa na wasi wasi sana

moyoni mwake) lakini naomba iwe siri kubwa!

(kila mmoja alianza kutekeleza wajibu wake, mama mchungaji aliletewa cocaine na mume wake,

Magdalene alipabadilisha nyumbani kuwa pango la wanyang’anyi: Shoma ndo usiseme kabisa,

baada ya muda wa miezi miwili tayari alikuwa ameshalala na wengi: waume za watu 12

wachungaji 7 akiwepo Mchungaji Jere, Mashehe 4 na wazee wenye umri wa miaka 78 walikuwa

tayari 12 , mawaziri na wabunge nao walilala nao. Sasa wakachoka na kazi hiyo. Hela

wamepata nyingi sana sasa wakaona inatosha wakati ule alishauriana na Magdalena kwamba

waache sasa hiyo kazi.)

SHOMA: Naona rafiki yangu hii kazi tuache sasa! Maana moyoni mwangu sina amani!

Nimemkumbuka mama yangu na baba yangu! Zaidi ya hayo fedha tulizo nazo sasa zinatutosha!

Mimi sitapeleka tena fedha kwa baba mchungaji maana inatosha

MAGDALENA: Mmm baba akisikia jambo hilo itakuwa hatari sana, maana anataka anunue gari

lingine kwa hela hiyo hiyo halafu leo wewe unaleta mchezo!

SHOMA: Hapana mimi nimekusudia kuacha kabisa, tena ikiwezekana kuanzia sasa nimeachana

na kazi hii ya ukahaba! Sikutegemea kama baba mchungaji angeweza kunifundisha mambo haya!

Sikutegemea kama wachungaji wengine wangelala na mimi! Lakini haya yote nimeyapata kwa

sababu ya baba yangu mzazi! Nilikuja kusoma lakini sasa sikumbuki hata mbili mara mbili!

Lakini nakumbuka shairi moja tu (Akaanza kuimba kwa kubahatisha bahatisha )Sikiri mimi

masikini, uvivu wangu……aaaa hata huu siukumbuki hata kidogo!

MAGDALENA: Achana na mambo ya shule mtoto! Wewe bado unakumbuka ya shuleni tu?

(wakiwa wamekaa pale pembeni kibarazani kulikuwa na redio, mara wakasikia taarifa ya habari

Uhaini wa Baba

22

ya saa 6:00 mchana ya RFA)

RADIO: wanawake kumi na mbili akiwepo mama mchungaji wa kanisa moja hapa mkoani

wamekamatwa wakiwa na madawa ya kulevya aina ya cocaine yenye thamani ya shilingi milioni

mia nane, taarifa za awali zinasema kwamba wanawake hao wamekuwa wakiuza unga huo kwa

siri na mpaka leo siri yao imegundulika, ambapo wote wamekamatwa na vigogo wengine saba

ambao inasemekana wamekuwa wafadhili wao bado wanatafutwa na polisi. Taarifa zaidi

zinasema kuwa vigogo wanaowafadhili wanawake hao ni pamoja na mawaziri, wabunge na

watumishi wengine wa umma ambao kwa sasa majina yao yanahifadhiwa. Unaendelea kusikiliza

taarifa ya habari kutoka hapa RAF…

SHOMA: Sikiaaaaaa!!!! Acha makelele! Ehe! Mama amekamatwa pia? Mama amekamatwa pia?

Mama amekamatwa piaaaaaaaaaaa? Redio nakuuliza mama amekatwa pia?

MAGDALENA: Mambo yamechacha!! Mimi mama nilimwambia kwamba aachane na ile kazi!

lakini baba alikataa kabisa!

SHOMA: Ni kweli nadhani hata mimi bora wangeacha biashara hiyo! Lakini watu husema mtu

akila nyama ya mtu hawezi kuacha!

MAGDALENA: Baba alipoenda Jumapili kanisani aliwaambia waumini wake kwamba

amebarikiwa sana. Aliwaonesha magari yote aliyonunua, Toyota Prado VX72, Hyundai, Hammer,

Range Rover na hata ile nyumba aliyojenga huko ziwani amewaambia Mungu amembariki sana!

Mmmmm! Jamani baba haogopi dhambi! Yaani anahubiri watu wasiibe, wasifanye umalaya!

Lakini ipo siku huyu Mungu kama kweli yupo maana siamini sasa kama yupo kweli, maana kama

angekuwepo asingeruhusu mambo haya anayoyafanya baba na mama!

SHOMA: Hehehehee! Unawaangalia tu baba na mama yako, mbona wewe hujiangalii! Hivi haya

matendo tunayoyafanya ni ya kibinaadamu kweli? Nakumbuka wiki iliyopita yule waziri alikuwa

amemwacha mke wake kabisa akaja kulala na mimi! Hebu fikiria rafiki yangu! Mimi nilipokuja

kwenu nilimwamini kabisa baba yako kuwa ni mtumishi wa Mungu lakini matokeo yake ndiyo

haya! Ameshindwa kuwa baba yangu wa kiroho! Nilimwamini kama baba wa kiroho, lakini haya

yote yametoka wapi? Aaa jamani baba! Uhaini wa baba! Ila ipo siku! Nikisalimika katika hili!

Sitarudia tena!

MAGDALENA: Mbona unaongea pumba? Maneno gani hayo? Wewe unawaamini watumishi

wa Mungu wote? Japo ni baba yangu simwamini! Sijui itakuwaje kama mama amekamatwa?

SHOMA: (Wakiwa wamekaa hapo, akawa anaangalia angalia barabarani, mara gari moja

likapita hapo) Mbona nimeona kama gari la polisi limepita?

MAGDALENA: Woga wako tu! Ina maana kama polisi wakija hapa utakimbia?

SHOMA: ndiyo! Mmm! Hivi hii siyo namba ya polisi PT 20876?

MAGDALENA: Ni kweli lakini hayatuhusu, kama yeye kakamatwa,ni yeye,maana tulipeana

Uhaini wa Baba

23

majukumu kila mtu afanye ya kwake! Kama wao wamekamatwa watajua wenyewe!

SHOMA: aaa! Tuwe makini sana! Umalaya sio jambo zuri! Tutakamatwa!

MAGDALENA: wewe binti bado mtoto kweli! hebu ngoja nikusimulie hadithi: kuna baba

mmoja alimhisi mke wake anatoka nje ya ndoa!

SHOMA: ehe!

MAGDALENA: Tatizo alikuwa hamjui Yule aliyekuwa anamtongoza mkewe,hivyo akaamua

kwenda kwa wacheza drafi mtaani! Mara alipofika hapo alichomoa panga lake na kuanza kulinoa

huku akisema maneno haya kwa sauti “Yule ambaye anazini na mke wangu ataniona leo ataniona,

lazima kieleweke”

SHOMA: Endelea, stori nzuri!

MAGDALENA: Alipokuwa akiendelea kulinoa panga lake, watu kama saba hivi wakatimka

mbioo!!!! Akaendelea kulinoa panga tena! Akashangaa watu wanne tena wamekimbia, tena hao

walikurupuka kwa haraka sana! Mwishoni walibaki watu wawili tuuu!

SHOMA: Hahahahahahahahhahahahaaaaa! Usinivunje mbavu, ehe ilikuwaje sasa?

MAGDALENA: Unafikiri kuna kilichoendelea tena! Tayari alikuwa ameshajua ni akina nani

wanaomtongoza mke wake!

SHOMA: Hiyo kali, nimeikubali kabisa!

MAGDALENA: Unaelewa hadithi hii?

SHOMA: Hapana! Nini maana yake?

MAGDALENA: Kama polisi wakija hapa, wewe utakimbia kwa sababu unajijua kwamba ni

mharifu!

SHOMA: Yaani kama wakikamatwa wote na kufungwa, aaaaaa! Yaani nakwambia mimi narudi

nyumbani kwetu Tindabuligi! Siendi kwa bibi wala kwa nani! Tayari nina miaka kumi na mbili

sijawaona wazazi.

MAGDALENA: Nenda kapime kwanza magonjwa ndipo uende ili usiwapelekee watu

magonjwa! Au ndo njia za kusogeza maiti rafiki? Maana siku hizi kuna ujanja bibie mtu akiumwa

sana anasogea nyumbani ili kuepusha usafirishaji wa mwili wa marehemu.

SHOMA: Hilo tu, nitaenda tena leo hii hii! (mara Shoma akaenda kupima mwili mzima akitaka

kujua hali ya afya yake)

****(Hospitalini)***

SHOMA: ngo ngo ngo!!!!

DAKTARI BINGWA: Karibu!

SHOMA: Shikamoo!

Uhaini wa Baba

24

DAKTARI BINGWA: Marahaba! Pole sana! Nikusaidie nini?

SHOMA: Nataka kupima afya yangu!

DAKTARI BINGWA: Kwani una tatizo la afya?

SHOMA: Hapana, ila nataka tu kuwa na uhakika na afya yangu!

DAKTARI BINGWA: Kweli ni jambo zuri sana kupima afya yako! Watu wengi wanaogopa

sana. Nakupongeza kwa uamzi wako mzuri!

SHOMA: (Huku akiwa anatetemeka) asante dokta.

DAKTARI BINGWA: Jina lako nani?

SHOMA : Shoma Mabula

DAKTARI BINGWA: Unaishi wapi na una umri wa miaka mingapi?

SHOMA BINGWA: Naishi maeneo ya hapa karibu tu, na nina miaka kumi na saba

DAKTARI BINGWA: (anachukua vipimo vifuatavyo; damu, mkojo, tumbo, kinyesi na sehemu

zingine zote muhimu, mara anaondoka na kuelekea maabara kwa ajili ya vipimo ) nisubilie binti!

SHOMA: (huku akiwa na wasiwasi sana, mara anakaa mara anasimama, kijasho chembamba

kinamtoka, mara mashuzi, mara kikohozi cha kizee, mara apige miayo maana dokta alitumia

muda mrefu sana kama masaa manne hivi. Alipokuwa amekaa palikuwa hapakaliki) mmm!

Mbona amechelewa sana? Au mambo yamegoma nini? Lakini sana kama yakiwa

yamegoma,kwani ya kwake? Si aniletee tu? (mara anasikia nyayo za daktari akirudi, naye

akajifanya kana kwamba hakusikia)

DAKTARI BINGWA: (huku akiwa ana furaha, akiwa ametoa meno nje )Ah! Pole sana Shoma!

SHOMA: Nini tena dokta? Ninajua ni tatizo la baba yangu? Alinilazimisha niolewe nikiwa

mdogo sana! Nikakimbilia kwa bibi, baadaye nimekuja huku kimasomo na nimejikuta nikiingia

katika vitendo vibaya vya ngono!

DAKTARI BINGWA: samahani Shoma, mbona unaongea maneno kama hayo? Pole kwa sababu

nimechelewa sana! Ujue nimejaribu kufanya marudio ya vipimo vyako ili kuhakikisha kabisa!

SHOMA: (huku akijivuta polepole mpaka chini) sasa mbona husemi? Najua ni tatizo la baba

yangu! Isingekuwa yeye nisingekuwa hapa!

DAKTARI BINGWA: mbona sikuelewi binti? Toa majibu mwenyewe! Haya acha nikwambie!!

Majibu yako yanaonyesha kwaaa!! Kwaaa!!! Kweli huna ugonjwa wowote isipokuwa una

malaria tatu tu! Nenda nunua dawa aina ya chloroquine au doxycycline dose utapota haraka sana!

SHOMA BINGWA: Waaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!! Narudi nyumbani!!! Narudi Tindabuligi!

Narudi kwa mama! Naenda kuanza tena darasa la kwanza!! Maana huu ulikuwa ni uhaini wa

baba yang utu!!! (watu wote walikuwa pale hospitalini walianza kushangaa maneno ya Shoma)

***MWISHO****.


Recommended